Kauli hii ya CHADEMA imenishangaza!!

Mkuu Akili,

Ni vizuri tunapotazama hili jambo tuamini kwamba utaratibu wa kikanuni na katiba ya chama katika uteuzi wa mgombea urais ulifuatwa.
Nataka nikuhakikishie kwamba hakuna mtu aliyenunuliwa kumpendekeza Dr. Slaa kuwa mgombea, utakumbuka kuwa hadi dakika za mwisho kabisa chadema haikuwa na mgombea uraisi na Dr. Slaa alikuwa amechukua fomu za kuwania ubunge Karatu, na ukumbuke kwamba kulikuwa na mazungumzo kati ya vyama vya upinzani kuona uwezekano wa kuungana na kuwa na mgombea mmoja, lakini hadi dakika za mwisho ikaonekana isingewezekana kuwa na mgombea mmoja kwakuwa vyama bado vilihitaji kukubaliana namna ya kugawana na majimbo zoezi ambalo lilishindikana, pia ilichangiwa na vyama kutoaminiana.

Kwa maoni yangu, labda kinachohitajika kwa sasa ni kuboresha utaratibu huu wa kamati kuu kufanya utafiti wa jina la mgombea anayefaa kukiwakilisha chama. Uwekwe utaratibu wa wazi na sifa za mgombea na mchakato wake uwe wazi kwa wanachama wote, ingawa bado kamati kuu itakuwa na jukjumu la kutafiti majina ya waliojitokeza ama hata nje ya hao waliojitokeza.

mkuu MM, shukrani sana kwa maelezo mazuri na ya kina..................... naona nikubaliane na wewe hapo kwenye bold kuwwa ni vyema huo utaratibu ukaboreshwa zaidi ili kuondoa kila aina ya swali ama utata juu ya namna ya kumpata flag bearer ndani ya chadema................. hilo litaimarisha imani ya wanachama na hata wasio wanachama juu ya demokrasia ndani ya chama................

uwe na siku njema mkuu.....................
 
Sijakuelewa mkuu ila kwa uelewa wangu mdogo nimegundua kuwa wewe ni kibaraka wa Magamba!
Inawezekana Kigarama asiwe kibaraka wa Maghambas bali anataka kujua baadhi ya mambo:-
1. Tofauti ya CCM na CHADEMA kwenye uchaguzi wa viongozi ni kwamba CCM wanateuwa wagombea bali CHADEMA wanachagua wagombea kwa kura kidemokrasia.
2. CCM wanakumbatia wezi wa mali za umma na wawekezaji feki wakidhulumu mali zetu Watanganyika; CHADEMA wanapigana kukomboa mali zilzo ibwa na kupambana na ufisadi kwa nguvu zote bali CCM wanalinda na kutetea mafisadi na wezi kuanzia kwenye chama hadi serikalini.
3. CCM ni watawala wa nchi yetu ya Tanzania CHADEMA ni chama cha siasa kisicho na mandate ya utawala wowote bali kinaelimisha wananchi kuhusu dhuluma zinazofanywa na vibaraka wa chama tawala.
4. Viongozi wengi wa CCM wamepata utajiri kwa njia za wizi wa mali za taifa letu, waliomo kwenye CDM wenye mali wamesota kuzipata!!! Tofauti ni nyingi bila shaka umefunguka sasa na kuelewa!!!!
 
Kigarama umejenga hoja nzito, nnakuhakikishia ni asilimia mbili tu ya wana JF ambao watakuelewa.
Wewe mwanamke balaa, umetumia kigezo gani cha kuwahukumu wana JF na uelewa wao? Tatizo la nyie mijitu mnao fanya kazi usalama wa ccm mnajifanya mnaakili kuliko mtanzania yeyote, kumbe ni mazuzu wa kutupwa.
 
Wewe mwanamke balaa, umetumia kigezo gani cha kuwahukumu wana JF na uelewa wao? Tatizo la nyie mijitu mnao fanya kazi usalama wa ccm mnajifanya mnaakili kuliko mtanzania yeyote, kumbe ni mazuzu wa kutupwa.
Hujamwelewa kabisa FF, rudi usome mabandiko ya huko nyuma!!
 
Mwita Maranya, Akili Kichwani na Mkandara nawashukuru sana kwa kujikita kujadili hoja hii tofauti na wengine wenu ambao walijikita kunijadili mimi. Kabla ya kutoa ufafanuzi labda niseme wazi mimi si kati ya wale wanaoogopa kuitwa majina, na wale wanaopachika wenzao majina ni watu hatari zaidi ya wale waliopachikwa majina hayo. Waingereza wana msemo wao unaosema "ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya" na jina baya JF ni CCM au Magamba na jina la "ukombozi" ni CHADEMA au magwanda.

Wapuuzi wasiotaka kuzisumbua mbongo zao huziona hoja kwa jicho la CCM au CHADEMA, wanazishabikia kwa kauli mbiu za Magamba ua Magwanda. Mimi ni mzalendo ninayeipenda nchi yangu na pia ni mdau wa Demokrasia. Kuna mabandiko humu nimewalaumu CCM na mengine nimewalumu CDM. Hebu tujadili mada hii iliyopo mbele yetu bila ya kuleta ushabiki wa kijinga jinga. Wakati CDM wanapitisha katiba yao pale PTA Hall mwaka 2006 mimi nilikuwepo na tuliwashauri wairekebishe lakini wakapuuza.

Leo hii kwenye vikao vyao vya ndani wanataka kuunda kamati ya kuirekebisha. Mimi msimamo wangu ni wa kisheria tu, kama Slaa ni Katibu wa Kamati iliyompendekeza na kamati hiyo inatakiwa kufanya utafiti na kupendekeza jina la mgombea Urais kwa nini hapa tusiseme kwamba kuna mgongano wa Kimaslahi. Tunapomkataza Rais kufanya biashara akiwa Ikulu kwani huwa tunamaanisha kwamba Rais hana fedha za kuanzishia miradi akiwa Ikulu?

Sina chuki na DK. Slaa, na ninajua kuna watu humu ni washabiki wakubwa wa Slaa. Lakini mfumo mzima ninavyouona mimi ni mfumo ambao mwisho wa siku utatujengea tabaka la wasio gusika ndani ya chama. Kwanini nasema ni kinyume cha Katiba, sababu yangu kuu Kamati Kuu ambayo inadai ilimpendekeza Slaa kuwa mgombea kwa kuwa CDM ilikosa mgombea ni Kamati hiyo hiyo ambayo ilitakiwa itayarishe utaratibu wa kupata mgombea lakini haikufanya hivyo.

Kwa hiyo kama Slaa aliteuliwa kwa sababu CDM ilikuwa haina mgombea ni lini Kamati Kuu ilifanya utafiti wakati tunaambiwa kumbe hata fomu ya kugombea Ubunge kwenye Jimbo la Karatu Slaa alishachukua? Slaa ni Katibu wa Kamati Kuu, wakati anakwenda kuchukua fomu za kugombea ubunge wa Karatu ailikuwa hana taarifa kwamba Kamati Kuu inafanya utafiti na utafiti huo unamtaja yeye kama ndiye anayefaa kuwa mgombea wa nafasi ya Urais?
 
Mkandara hii ndiyo hoja yangu na wala siwalaumu CDM, ndiyo maana nimesema kwamba kauli yao imenishangaza na wala haijanichukiza au kunikwaza. Imenshangaza kwa kuwa sisi wengine tunataka CDM kiwe chama mfano wa Demokrasia nchini, lakini kwa kauli hii nakiona chenyewe kinaogopa kutenda kidemokrasia..

Maana ya uteuzi ni kuchagua kutoka miongoni mwa vingi, na kama utasoma kwenye vifungu vya katiba nilivyonukuu utaona Kamati Kuu haipaswi kuteua bali kazi hiyo inafanywa na Baraza kuu na Mkutano Mkuu. Maana yake Kamati kuu inatakiwa kwenye mkutano wa Baraza kuu ipeleke majina ya wagombea ambayo nayo yatapelekwa kwenye mkutano mkuu kwa uteuzi wa mgombea wa Urais

Hapa kwenye Kamati kuu ndiyo nataka watu waombe kugombea, kamati Kuu ifanye utafiti wake kuhusu sifa zao na majina hayo yapelekwe kwenye Baraza Kuu na Mkutano Mkuu ambao ndiyo wenye kauli ya mwisho uteue jina moja la mtu atakayefaa kuwa mgombea. Mwaka 2010 tuliambiwa Slaa Kaombwa na Kamati Kuu kugombea kwa hiyo ina maana kama mwanachama mwingine alitaka kugombea angesita kwa sababu kwa asili tu kamati Kuu ingekuwa inahukumu kesi inayoihusu yenyewe!!

Hii hofu ya uchaguzi kwenye vyama vyetu ndiyo inayoleta tabu kwenye siasa za Kiafrika, na kwa kiasi fulani inapalilia siasa za "Patronage"kwenye jamii nzima. Hata Slaa mwenyewe kwani hana madhaifu yake kama binadamu? Mimi naona uwanja uwachwe wazi chama kitengenze kanuni na kuteua watu safi wenye uwezo wa kuzisimamia kikamilifu kanuni hizo. wanaotaka kugombea urais wajitose watu wawapime na kisha uchaguzi wa kuteua mmoja ufanyike!!

Kama tunaogopa kufanya chaguzi kwenye vyama vyetu kuna haja gani ya kutaka uchaguzi dhidi ya vyama vingine? kuhusu Obama si kwamba Demokratik wengine wameambiwa wasigombee ila mazingira tu yanawalazimisha wasigombee lakini HAWAKATAZWI kugombea.

Hapa ndipo umuhimu wa mgombea binafsi unapoonekana!!
WATU na MAZINGIRA ---weka juu ya yote haya!
Mkuu wangu tunarudi kule kule kuzungumzia mfumo wa CCM.. CCM ndio wanatumia mkutano mkuu kufanya uteuzi wa wagombea Urais na kuanza mchujo baada ya kamati kuu kuchuja vile vile..Mfano Malecela hakufika hata ktk mchujo wa Mkutano mkuu..Na sababu zake zipo isipokuwa zikitumiwa vibaya ndio tunayapata yalomtokea Malecela. Binafsi sidhani kama mkutano mkuu ndio sehemu nzuri ya uteuzi kwa sababu hawa wote bado ni wanasiasa sio wawekezaji, sio wafanyabiashara, sio wakulima wala Wafanyakazi (Wazalishaji) ambao ndio wenye jukumu la kumteua mgombea

Kwa CCM, nafikiri sababu ya kwanza kamati kuu kufanya Uteuzi wa majina ni kuondokana na Mapandikizi au watu ambao wameingia chama kwa sababu zao binafsi..Mathlan, tuchukulie Lowassa amekuja jiunga Chadema na chama hakitaki kabisa Lowassa agembee urais kwa sababu wanajua hakuja kuongoza nchi bali kufanya mashindano na CCM (kumbuka kesi na madai Ya JK 2005) Ni njia ipi halali ambayo chama inaweza kutumia kuondokana na Mapandikizi kama hawa ikiwa wewe unapendekeza haki ya mtu yeyote kugombea Urais?..

Ndipo kanuni zinapoingia, Chama hakiwezi kutoa haki sawa kwa kila mtu anayetaka kugombea Urais - haiwezekani..Qualifications zinazotakiwa kwa kugombea Urais na malengo hutokana na ajira yenyewe.. Na sio kwamba watu wanabaguliwa hapana isipokuwa kanuni zinazingatia umuhimu wa Uanachama na yale ya kuongoza nchi kwa kutumia tiketi ya chama. Bila kuwepo kanuni hizi Lowassa anaweza kabisa kwenda kugombea Urais Chadema au NCCR kwa sababu tu kuna mshindano ya nguvu za kiutawala CCM.. Hapa tunakuwa hatuwakilishi wanachama bali tunawakilisha matakwa na tamaa za mgombea..

Swala la viongozi wa KIamati kuu walichaguliwa na nani?..nadhani hapa unakwenda nje ya mjadala maana uchaguzi wa viongozi wa Kamati kuu hauhusiani bali hawa ni walinzi ni kaa board of Directors ktk shirika la Umma. Hawa kazi yao ni uhai wa chama na utararibu wa kumchagua mwenyekiti unatokana na Itikadi kwanza, pamoja na malengo ya chama ndani ya chama na sio kila mtu anaruhusiwa kugombea vile vile.

Swala la Zitto mimi nililitazama tofauti kabisa maana namjua Zitto ni Mhafidhina mwenzangu kwa maana ya kuamini ktk Freemarket na kazi ya serikali ni kulinda maslahi ya wananchi wake sio kufanya biashara lakini kutokana na hali halisi ya nchi yetu huduma muhimu kama Afya, Elimu navikubali kutolewa bure nikizingatia umaskini wa wananchi na ukubwa wa Population iliyopo ktk umaskini..Kwa mtazamo kama wangu ama wa Zitto hatutakiwi kuwa Wenyeviti wa Chadema kwa sababu tunatofautiana mengi sana na itikadi za CDM.. Kusema kweli binafsi nipo CDM kwa sababu ndicho chama kilicho karibu zaidi na mtazamo wangu kisiasa lakini siwezi kuongoza kiitikadi kwa sababu nitaleta vurugu tupu..

Kwa hiyo nadhani tuendelee kutafuta njia mbadala ya KUPENDEKEZA wagombea urais kwa sababu binafsi sikubaliani na ile kila mtu achukue form kisha mkutano mkuu waanze kuchuja majina huku wamekwisha lishwa sumu tayari na kuwaengua baadhi ya watu kutokana na kuahidiwa vyeo.. Wakati Siasa za Marekani wagombea urais hutoa ahadi na hupendekezwa na wanachama kupitia makundi ya sehemu za Uzalishaji, mfano Vyama vya ushirika, wawekezaji wa ndani na Mashirika binafsi, sisi wagombea wetu hupendekezwa na wanachama Wanasiasa ktk mkutano mkuu.. Hawa wajumbe wa mkutano mkuu sii wazalishaji, sio wakulima wala wafanyakazi, sii wajasiriamali wala waajiriwa ktk nyanja za uzalishaji hivyo wanapompitisha kiongozi humpitisha kwa malengo ya kisiasa zaidi ya kutazama Maazimio ya mgombea ktk kukuza uchumi. Marekani mjumbe yeyote kama huyu hupelekwa nje kukukutana na wananchi na kuwapa pendekezo lake kama alivyofanya juzi McCain akimfagilia Romney.

Kwa hiyo bado sana siasa zetu zinalenga kuridhisha vyama badala ya kuridhisha wananchi na DR.Slaa kwa mara ya kwanza amechaguliwa kuwa mgombea kutokana na Wananchi kuridhika. kamati kuu ilipelekewa jina hilo na kulipendekeza kwa wajumbe ambao kusema kweli hawakuwa na hila lakini nachosema mimi it's much much better kuwa na mgombea anayetokana na chaguo la wananchi. Je, tunaweza fanya kama Marekani?.. Bila shaka lakini kwa fedha gani tulonayo kuwafanya wagombea watembee majimbo makubwa ya uchaguzi kufanya mihadhara, mikutano na kadhalika ili kumpata mgombea mmoja!.. Hizo fedha na umaskini huu sii ndio tutafilisika kabisa au tutegemee kina Rostam kuja kutumia mwanya wa kujitafutia sifa!..

Somehow, somewhere ipo njia mbadala lakini muhimu sana tutazame WATU tunao deal nao (wananchi kwa ujumla) na ktk MAZINGIRA haya ya umaskini wa hali na mali..Huu ni mtihani mkubwa sana kumshawishi maskini amchague kiongozi ambaye anaitazama Tanzania miaka 20 mbele wakati yeye ana njaa na anataka mtu atakayeweka kipande cha mkate mezani leo..
 
Mkuu Mkandara ahsante sana kwa maelezo yako yaliyojitosheleza, naamini Kigarama atakuwa amekusoma.

Lazima tuangalie mazingira yetu sio ku copy na ku paste kila kinachofanyika ulaya na marekani. Nimesema hapo awali kwamba kwa umasikini wa watanzania wanaoweza kuuza kura kwa ubwabwa ni hatari sana kwa demokrasia na ustawi wa vyama vya siasa hasa vya upinzani.

Mkuu Kigarama umehoji kuhusu wajumbe wa kamati kuu, naona bado una walakini na uteuzi wa Dr. Slaa kwakuwa ni katibu wa kamati hiyo. Sijui hapa unataka kusema kwamba huna imani na kamati kuu ama mimi sikuelewi. Je ni chombo gani unachokiamini katika chama? Na unadhani kamati kuu ipatikane kwa utaratibu gani?
 
Kigarama,
Kama Dr. Slaa alijua kwamba jina lake ndilo limependekezwa kugombea uraisi, kwanini tena alichukua fomu za kugombea ubunge? Hili ni jambo ambalo liko dhahiri kwamba Slaa hakuwa amejiandaa kuwania uraisi, na nimekukumbusha kwamba kulikuwa na matarajio ya vyama vya upinzani kuunganisha nguvu na kuwa na mgombea mmoja, sasa baada ya mpango huo kukwama ndipo kamati kuu ikalazimika kutafuta mtu anayefaa kubeba bendera ya chama katika muda mfupi uliokuwa umebaki.

Katika hili nadhani kamati kuu inahitaji kupongezwa kwa kumpendekeza mtu aliyeleta changamoto kubwa sana katika siasa za nchi hii na hasa uchaguzi mkuu uliopita.

Kuhusu katiba ya chama kama unavyofahamu kuna kamati maalum ya kuipitia na kuja na mapendekezo ya kuiboresha. Ukiwa mwanademokrasia unayekitakia mema chama unaweza kutumia fursa hiyo kuwasilisha maoni yako ili kuona kwamba katiba ya chadema inakuwa bora kabisa na kuondoa loop holes unazoziona.
 
mkuu MM, shukrani sana kwa maelezo mazuri na ya kina..................... naona nikubaliane na wewe hapo kwenye bold kuwwa ni vyema huo utaratibu ukaboreshwa zaidi ili kuondoa kila aina ya swali ama utata juu ya namna ya kumpata flag bearer ndani ya chadema................. hilo litaimarisha imani ya wanachama na hata wasio wanachama juu ya demokrasia ndani ya chama................

uwe na siku njema mkuu.....................


Mkuu Akili,

Tuko pamoja mkuu, kujenga chama hadi kufikia level ya juu ya ukomavu kidemokrasia ni process ambayo inahitaji muda kwani kadri unapopitia hali fulani ndipo unagundua madhaifu na kuyarekebisha.
 
huyu ametumwa na nape
Fuatilia Posts na threads zangu tangu nijiunge utajua nina msimamo gani. mimi huwa naikosoa CDM kwa sababu najua humu ndani watu wanaogopa kuikosoa kwa hofu ya kupachikwa majina kama ujinga ulioandika hapo juu. Huyu Nape ana uwezo wa kunishawishi mimi niipigie debe CCM!!? Waswahili wana msemo wao usemao "asifuye mvua, imemnyea" kuna watu wanadhani kwa sababu wao ni rahisi kununuliwa, basi na wenzao watanunuliwa vile vile.
 
Mkandara na Mwita Maranya, mimi dhana ninayoipinga ndiyo nyie mnayoishabikia. Kuna dhana nyuma ya utetezi wenu ambayo mimi ndiyo ninaipinga. Zitto amesema hoja inayotumiwa na madikteta kugandamiza haki za wengine ni ile ya kusema hakuna "uhuru bila mipaka" lakini zito anasema "Uhuru ni uhuru tu, uhuru hauna mipaka". Kwenye hoja hii nyie mnasema hakuna "demokrasia isiyo na utaratibu" mimi nasema "demokrasia ni demokrasia, haina utaratibu"

Nyie mnaamini watu wa kwenye kamati Kuu ni "makini" sana kiasi kwamba hawawezi kuvurugwa kwa hoja ya kutafuta mgombea, lakini mnaamini hoja hiyo hiyo ikipelekwa kwa wanachama wa Mkutano Mkuu watavurugwa. Kwanza mimi si muumini wa mikutano "mikuu" na wala kwenye post zangu zijasema kwamba nataka mgombea apigiwe kura na mkutano mkuu wa CHADEMA. Ninachosema Kamati kuu ifanye utafiti wa majina ya wagombea walioomba wenyewe kugombea na siyo kamati kuu kumuomba mtu agombee baada ya kamati kuu yenyewe kufanya tafiti zake kimya kimya!
 
Kigarama,
Nadhani tunafika mwisho wa mjadala huu kwa upande wangu. Kama unaamini kwamba hakuna uhuru usio na mipaka basi napata shida kuelewa ni demokrasia gani hiyo unayoipigia chapuo. Na pengine nitahitaji unifahamishe hiyo demokrasia ya uhuru bila mipaka, katika dunia hii ni wapi wanai practice.

Kama kweli unaamini uhuru ni uhuru tu hakuna mipaka, basi huenda unaamini kuwa hakuna sababu wala umuhimu wa kuwa na katiba, sheria na kanuni si katika kuendesha vyama vya siasa tu bali hata nchi, na sijui kama nchi ya namna hiyo itaweza kutawalika.

Zitto ni kiongozi wangu na ninaheshimu mawazo yake lakini yeye si msahafu ama malaika kwamba kila anachotaka lazima kiwe. Mambo ya uendeshaji wa chama yanafuata katiba, sheria, kanuni na taratibu zilizopo. Na kwa nafasi yake anaweza kupeleka mapendekezo yake katika chama akishauri namna ya kuiboresha demokrasia ya chadema kuwa uhuru usio na mipaka. Na hapa ninapata mwanga kidogo ni kwanini unaitilia mashaka kamati kuu.
 
Kigarama umejenga hoja nzito, nnakuhakikishia ni asilimia mbili tu ya wana JF ambao watakuelewa.

Kupendekezwa badala ya kuomba hakupunguzi dhana ya demokrasia. Kwa upande mmoja kunaongeza demokrasia. Unapoomba kuwa mgombea wa Urais au nafasi nyingine yeyote ni wewe pekee yako na baadhi ya wapambe wako ndiyo wanaokuwa wamekupendekeza (kwa kifupi ni kuwa wewe mwenyewe, kama mtu mmoja umejipendekeza). Jina lako linapopendekezwa na kikao au jamii fulani, mapendekezo huwa ni ya watu wengi kuliko mtu anayeomba mwenyewe. Kwangu mimi, pamoja na uhuru na haki ya mtu kugombea, jina lako linapopendekezwa, kuna upana mkubwa zaidi wa demokrasia kuliko kujipendekeza (kuomba wewe mwenyewe). Lakini kwa upande mwingine, wajumbe wa kamati ya mapendekezo wanakuwa huru zaidi, (hasa wakiwa makini) katika kumtafuta mtu ambaye wanadhani anafaa bila ya kuwa na ushawishi wa moja kwa moja wa mwombaji. Wanaoomba huunda kamati za wapambe ambao mara nyingi hata bila ya kuzingatia uwezo wa mgombea wao, kazi yao kubwa ni kumtetea na kuona mgombea wao anashinda. Sababu nyingine ni kuwa utaratibu wa kupendekezwa unapunguza sana msukumo wa matumizi ya rushwa na matumizi makubwa ya fedha, kama nafasi hiyo ikiombwa. Mfumo wa kupendekeza pia hutumiwa na chama cha FRELIMO kule Msumbiji, na kila mara umewasaidia kupata viongozi wazuri. Msisahau kuwa Chisano ambaye ni kiongozi mstaafu mmojawapo wa washindi wa wa Tuzo ya uongozi bora katika Afrika alikuwa ni matunda ya mfumo huu.

CCM mfumo huu hauwafai kabisa. Sababu kubwa ya mfumo huu kutokuwafaa CCM ni kuwa hata katika kamati hizo za kutoa mapendekezo kama vile Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu, wajumbe wengi ni kundi la waovu. Kwa hiyo CCM ikitumia mfumo huu wa CHADEMA watawateua waovu wenzao kuwa wagombea. Kwa upande wa CHADEMA, mfumo huu utawasaidia sana kumpata mgombea anayefaa maana wajumbe wa Baraza Kuu wanaaminika na wameonekana wazi kusimamia maadili na kuwa na dhamira thabiti ya kuwapata viongozi bora. CHADEMA inachotakiwa kufanya ni kuulinda mfumo huu kwa umakini mkubwa ili katika kupendekeza kusiwepo kabisa ushawishi wa anayependekezwa. Atakayeonekana kutaka au kufanya jitihada na mbinu za kutaka kupendekezwa, basi hiyo iwe ni 'disqualification'.
 
"Hivyo kinachopewa umuhimu ni utumishi kwa umma, kwa ajili ya maendeleo ya watu na si mbio za kusaka vyeo. Ni vyema hii dhana ya mtu kufuatwa na kuombwa, mara anapoonekana kuwa anafaa kuongoza, kulingana na mahitaji ya watu na sifa za nafasi hiyo, kama ambavyo imekuwa ikifanyika ndani ya CHADEMA, ikaenziwa na kufanywa kuwa ni namna bora ya kupata viongozi".

CHADEMA ilivyomchukua Shibuda kutoka CCM bila hata kumpitisha kwenye kumpiga msasa wa kuelewa sera za chama, ikampitisha kugombea ubunge, ilikuwa inatafuta utumishi wa umma au viti vya ubunge vingi tu?
 
Kigarama,
Nadhani tunafika mwisho wa mjadala huu kwa upande wangu. Kama unaamini kwamba hakuna uhuru usio na mipaka basi napata shida kuelewa ni demokrasia gani hiyo unayoipigia chapuo. Na pengine nitahitaji unifahamishe hiyo demokrasia ya uhuru bila mipaka, katika dunia hii ni wapi wanai practice.

Kama kweli unaamini uhuru ni uhuru tu hakuna mipaka, basi huenda unaamini kuwa hakuna sababu wala umuhimu wa kuwa na katiba, sheria na kanuni si katika kuendesha vyama vya siasa tu bali hata nchi, na sijui kama nchi ya namna hiyo itaweza kutawalika.

Zitto ni kiongozi wangu na ninaheshimu mawazo yake lakini yeye si msahafu ama malaika kwamba kila anachotaka lazima kiwe. Mambo ya uendeshaji wa chama yanafuata katiba, sheria, kanuni na taratibu zilizopo. Na kwa nafasi yake anaweza kupeleka mapendekezo yake katika chama akishauri namna ya kuiboresha demokrasia ya chadema kuwa uhuru usio na mipaka. Na hapa ninapata mwanga kidogo ni kwanini unaitilia mashaka kamati kuu.

Mipaka ninayoizungumzia hapa si sheria au kanuni za kuendesha mambo, bali mipaka inayozungumziwa hapa ni sheria na kanuni za kibaguzi. Unajua sheria na kanuni ni vitu vinavyotungwa na watu kwa maslahi yao kwa wakati huo. Afrika kusini kulikuwa na sheria na kanuni zilizokuwa zinatokana na Katiba iliyotungwa na makaburu kulinda ukaburu wao. Hata makaburu walikuwa wanaambia kina Mandela "kwenye hili mmevunja katiba". Katiba hii ya CDM ilipitishwa kwa masaa mawili pale PTA Hall pamoja na kanuni zake za Mabaraza. "Ubora" wake mimi naujua na kila mara naisoma na kuniacha nimeshika tama!!

Kamati Kuu ni watu na kwa kuwa ni watu nao pia wana maslahi yao. Ni Kamati Kuu hii hii ambayo inaundwa na kundi kubwa la watu waliokuwa NCCR ambayo mpaka sasa,imeshindwa kuunda majimbo kwa mujibu wa katiba tangu katiba hiyo ipitishwe 13/8/2006. Kamati kuu wakati ule ilitumia kila njia kuhakikisha Katiba hii iliyopo sasa inapitishwa "haraka haraka" bila ya mjadala wa kina kwa masaa mawili tu! katiba ya chama inajadiliwa kwa masaa mawili !!?

Hoja yangu ya kuvunjwa kwa katiba iko pale pale kwamba Kamati Kuu haikutakiwa kupeleka jina kwenye Baraza kuu bali ilitakiwa kupeleka majina, na majina hayapatikani kama kamati Kuu haijaweka utaratibu wa kuyapata, na hofu ya kamati kuu kupata majina mengi ya wagombea inatoka wapi? Kwa nini wao wafikiri kwamba wao pekee wana ujuzi wa"kujua" nani anayefaa kuwa mgombea Urais wakati Katiba inasema kila mwanachama ana haki ya kugombea. Kugombea hakuzuii mtu kutafitiwa!! Uwekwe utaratibu watu walete majina yao na uwekwe utaratibu wa watu hao kuhojiwa kwa nini wanataka kuwa wagombea Urais na wapigiwe kura ya kuamua nani anafaa zaidi na majina yao yapelekwe kwenye Baraza Kuu na Mkutano Mkuu kwa maamuzi. Katiba ya CDM ndivyo inavyosema na Kamati Kuu haina Mamlaka ya kuteua Mgombea. Period!!
 
CHADEMA ilivyomchukua Shibuda kutoka CCM bila hata kumpitisha kwenye kumpiga msasa wa kuelewa sera za chama, ikampitisha kugombea ubunge, ilikuwa inatafuta utumishi wa umma au viti vya ubunge vingi tu?

Kiranga,

Huenda hujaielewa hiyo phrase in relation to Shibuda kujiunga chadema. Shibuda hakuombwa na chadema kugombea ubunge bali yeye mwenyewe baada ya kuona ccm wamemtupa, ndipo akaamua ku cross border kuja chadema kwakuwa aliamini kwamba bado wapiga kura wake wanamhitaji na ccm hawakumtendea haki kumuengua.

Na kama ungekuwa umesoma vizuri tangu awali ungeona kwamba huu utaratibu unaojadiliwa hapa ni kwa nafasi ya mgombea uraisi na mgombea mwenza. Ambao kwa mujibu wa katiba ya chadema, kamati kuu imepewa mamlaka ya kufanya utafiti na kupendekeza kwa baraza kuu majina ya watu wanaofaa kubeba bendera ya chama.
 
Back
Top Bottom