Kauli hii ya CHADEMA imenishangaza!!

Njia zote mbili ni vizuri zikatumika
Kujitolea au kufuatwa na kundi la watu katika jumuia inayohitaji huyo kiongozi
Wakati njia ya kujitolea ina uwezekano mkubwa zaidi wa kuwa na agenda binafsi lakini kuna kundi la watu makini ambao ni viongozi wazuri wazuri ingawa hawjitokezi kugombea,na mara chache viongozi wa namna hiyo huwa na agenda binafsi
 
Kama demokrasia inaheshimiwa basi mtu akionekana anafaa hapendekezwi bali ANASHAURIWA. Na ili mchakato uwe fair basi anashauriwa katika personal level siyo officially eg. Mbowe anaweza kumuita Zitto nyumbani kwake akamshauri agombee nafasi fulani kwa sababu anaamini kuwa anafaa na hilo likabaki kati ya Mbowe na Zitto.

Huu utaratibu wa kupendekezana ni utaratibu unaokumbatia insiders and status quo. Na utaratibu huu unakandamiza uwezekano wa kugundua watu wapya wenye vipaji vya kuongoza.

Kwa mtindo huo mtanzania anayeishi nje ya nchi hawezi kuwa kiongozi kupitia chama chenye utaratibu huo. Nani atampendekeza? nani anamjua? lakini ukimruhusu kugombea akaweka sera zake hadharani watu wanaweza kugundua kuwa anafaa na wakamchagua.

kati ya watu wote waliochangia mpaka sasa ni Zemarcopolo pekee ndiye aliyenielewa, Dada yangu FaizaFoxy yeye kaishia njiani sijui kama amenielewa au la! Kwanza mwanzoni kabisa niliweka wazi kwamba kwenye huu uzi hakutakikani ushabiki wa kivyama au upuuzi wa "kumjua" mtu wakati kwa hali halisi humjui. Wengi humu ndani hawajisumbui hata kuisoma hiyo katiba ya CHADEMA ingawa iko kwenye soft copy.

Katiba ya CHADEMA inataja waziwazi ni vyombo gani hasa vinahusika na uteuzi wa mgombea wa nafasi ya Urais na vyombo hivyo ni Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, nje ya hapo ni uvunjaji wa Katiba yenyewe na ni siasa za Kihuni zaidi ya zile zinazofanyika CCM! Kama kuna mtu anadhani kuna mwanachama mwenzake anafaa kwa nafasi ya Urais basi aende akamshawishi agombee lakini si watu wachache tu wao wachukue jukumu la "kuteua" mtu eti kwa kuwa wanadhani anafaa kuwa mgombea.

Tupo watanzania zaidi ya milioni 40, haiwezekani watu wengine wao ndiyo wawe na "akili" za kujua mahitaji ya watu wote wa nchi hii bila ya USHIRIKISHAJI. Hoja yangu kama kweli tunaamini CCM inaviza Demokrasia basi tusiiruhusu CHADEMA nayo ivize Demokrasia yetu changa inayokua!

Uteuzi wa Slaa kuwa mgombea wa CHADEMA hata kama ulileta msisimko kiasi gani kwenye siasa zetu si aina nzuri ya kupata mgombea ya kujivunia. Kwa sababu kugombea ni haki ya kikatiba kwa kila mwanachama. Haiwezekani watu wachache wafunge milango na kusema "sisi tunamjua atakayetufaa na atakayewafaa watanzania". Ni vizuri kama kuna mtu anadhaniwa anafaa basi ni lazima kuna watu pia wanadhani hafai nao wanaye mtu "wao" anayefaa na ni vizuri kuwashindanisha hawa wawili ili anayefaa zaidi achaguliwe. Anayefaa si lazima awe yule unayedhani wewe anafaa!!

Huu ujinga wa kudhani kwamba kila anayeikosoa CHADEMA ni CCM utatotoka lini??
 
Tumbo joto linawasumbua nyie Magamba,na 2015 bado mpaka uharo uwatoke,kwanza hoja yako haina mashiko kijana rudi kwenye katiba ya CDM kajifunze namna taratibu za CDM zilivyo jinsi ya kupata viongozi sio nyie CC ya watu wachache wakisema flani awe hivi na inakua hvyo sie CDM hatupo hivyo so pole yako wewe Magamba
Lawrence najua unataka kuwasisimua watu lakini kama hujaielewa hoja huwezi kuchangia!! Mtu anayejifanya kujua dawa wakati ugonjwa hajaujua ni tapeli!
 
Nilichosoma mimi na kuelewa ni hivi:-
Utaratibu wa Chadema ni kwamba mgombea Urais hutokana na mapendekezo ya wajumbe au wanachama (when, where, how and why haya sijui) lakini hakuna kitu mtu kuamua tu kugombea Urais kama ilivyoelezwa na gazeti la mwananchi kuanza vurugu za kugombea urais ndani ya chama..Ni muhimu mgombea utokane na Mapendekezo ya wanachama na upo utaratibu wake - Na utaratibu huu lazima kuenziwa!

umeelewa!
 
Njia zote mbili ni vizuri zikatumika
Kujitolea au kufuatwa na kundi la watu katika jumuia inayohitaji huyo kiongozi
Wakati njia ya kujitolea ina uwezekano mkubwa zaidi wa kuwa na agenda binafsi lakini kuna kundi la watu makini ambao ni viongozi wazuri wazuri ingawa hawjitokezi kugombea,na mara chache viongozi wa namna hiyo huwa na agenda binafsi
Hao viongozi wazuri si wataeleza uzuri wao na watu wakawapima dhidi ya viongozi wabaya. Kama tunaona njia hii ya kuteua mtu kuwa mgombea bila kushirikisha watu ni sahihi, basi hata hao watakaoteuliwa na vyama nao pia kuwe na watu wa kutuambia mwisho wa siku nani ni Rais wetu bila ya kufanya uchaguzi!!
 
hiyo kauli imetolewa wapi??................... ni tomato au chili source??......................

lakini sio siri,..................... hoja yako ni nzito................ nakumbuka kumsoma mwanaJF fulani (huenda ni mimi) aliyehoji uhalali na usahihi wa mchakato uliompata na kumthibitidha dr Slaa 2010.................. lakini hakuna majibu sahihi yaliyotolewa................ kwa vyovyote vile kama huu ndio utaratibu rasmi wa chadema kupata wagombea wake, basio ni utaratibu mbaya na unaoweza kuzaa usultani.............. hebu tuendelee kuwasubiri wenye nyetinyeti waje watudadavulie......................
 
Kama umevaa viatu vyako vya ushabiki wa chama chako vivue!!

"Hivyo kinachopewa umuhimu ni utumishi kwa umma, kwa ajili ya maendeleo ya watu na si mbio za kusaka vyeo. Ni vyema hii dhana ya mtu kufuatwa na kuombwa, mara anapoonekana kuwa anafaa kuongoza, kulingana na mahitaji ya watu na sifa za nafasi hiyo, kama ambavyo imekuwa ikifanyika ndani ya CHADEMA, ikaenziwa na kufanywa kuwa ni namna bora ya kupata viongozi".

Hivi katiba ya CHADEMA inasemaje kuhusu jinsi ya kupata wagombea kwenye nafasi mbalimbali za uongozi? Hivi ni kina nani wanaochagua wa kumpendekeza, na wao ni kina nani kawapa madaraka ya "kumtambua" anayefaa na kufaa huko kunachukuliwaje kama ndiyo mahitaji ya wakati na ni vipi wanachama wa kawaida wanahusishwa kwenye "kumtambua" anayefaa'

Mwaka 2010 ilikuwa Slaa tuliambiwa maneno meengi kuhalalisha Kamati kuu Kumchagua Slaa. Hapa sizungumzii kufaa au kutokufaa kwa mgombea, nazungumzia upana wa Demokrasia kwa maana halisi ya kushirikisha watu kwenye kufanya maamuzi yanayowahusu wao. CHADEMA inapinga "kuteuana teuana" lakini kwa maelezo yao haya inayoonyesha kwamba na wao pia wanaamini kuna watu ndani ya CHADEMA "wanajua" mahitaji ya wanachama na wananchi kwa ujumla!

Tofauti yao na CCM ni nini?
Wee Kigarama, unaleta ukosoaji wa Chadema humu jf?!. Haya endelea...ila usije kulalamika!. Sisi wenzako tumeshajifunza kwa upande wangu mimi, nimeona bora niikumbatie CCM mgombea awe Lowassa!. CCM ina utaratibu mzuri sana wa kupata viongozi, hakuna rushwa, mizengwe wala upendeleo, wao wanatumia public opinion ya members, ndi maana sasa tunafanya kazi kubwa ya ku shape public opinion ili wakati ukifika ni jina la Lowassa tuu ndio libaki midomoni mwa public opinion!.
 
Kwa namna nilivyomuelewa Kigarama, ni kama vile anaona kunakuwa na ufinyu wa demokrasia kwa utaratibu huo wa kumuomba mtu agombee nafasi kutokana na mahitaji ya wananchi na chama. Nadhani hii inatokana na mazoea tuliyokuwa tunashuhudia kwa ccm, na kwa sehemu kubwa watanzania wengi wameathiriwa na kila kinachofanywa na ccm as if ndiyo guidelines.

Kwa upande wa chadema katika nafasi ya uraisi, kutokana na uzito na unyeti wa nafasi hiyo kwa Taifa na kwa kuzingatia uzoefu wa hapo kabla na nje ya chama kumekuwa na approach tofauti ambayo kwakweli 2010 imeonyesha mafanikio makubwa sana. Wanachama wenyewe kuanzia ngazi ya chini hupata fursa ya kumpendekeza mwanachama wanayedhani anafaa kuwania nafasi ya raisi kupitia chadema na hatimaye kamati kuu huratibu maoni ya wanachama na kufanya uteuzi. Utaratibu wa kila mtu anapojisikia anawania urais si mara zote hutoa viongozi mahiri na makini wanaokidhi matakwa ya jamii.

Kwa nafasi nyengine za ubunge, udiwani na serikali za mitaa na vijiji mwanachama yeyote anajitokeza kuchukua fomu na ngazi husika ya uongozi wa chama huchuja na kuteua mgombea.

mkuu MM hapo kwenye bold............................ nakumbuka 2010 wakati wa preliminaries za chadema nilikuwa dar na nilifuatilia kwa karibu sana mchakato wwa kumpata dr Slaa....................... naomba nikumbushwe ni lini wanachama wa kawaida ("kutokea ngazi za chini" kama ulivyoita) walipata fursa ya kumpendekeza..................... mi sikuwahi kusikia fursa hiyo ikitolewa, nilichosikia ni kuwa kamati kuu "imemuomba" agombee....................... hebu tufafanulie kidogo hapo tuliopitwa na newz .........................
 
7.7.10 Kazi za Mkutano Mkuu wa Taifa ni:-
(a) Kuchagua Mwenyekiti wa Chama Taifa na Makamu wake wawili
(b) Kujadili taarifa za Baraza Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa utekelezaji.
(c) Kuteua mgombea wa Uraisi na mgombea wenza wake kwa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na mgombea Urais wa Zanzibar.

(d) Kujadili na kuridhia Itikadi, falsafa na sera za Chama kisha kuweka mikakati na
miongozo ya utekelezaji.
(e) Kujadili na kuridhia programu ya Chama kwa kuzingatia mapendekezo ya Baraza
Kuu.
(f) Kuzingatia na kutoa maamuzi juu ya rufaa na masuala ya kinidhamu
yanayowakilishwa na Baraza kuu.
(g) Kupokea na kujadili taarifa ya Bodi ya wadhamini wa Chama juu ya mali na
rasilimali za Chama
(h) Kuidhinisha Ilani (Manifesto) ya Chama kwa uchaguzi mkuu.
(i) Kuthibitisha mapendekezo ya kuunda tume maalum kama yalivyowalishwa na
Baraza Kuu.
(j) Kujadili na kufanyia maamuzi agenda nyingine yeyote iliyoletwa kwake na Baraza
Kuu.
(k) Kujadili na kuthibitisha mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba ya Chama.

7.7.13 Kazi za Baraza Kuu zitakuwa:-
(a) Kupendekeza wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kuwasilisha mapendekezo yake katika
mkutano mkuu kwa uamuzi.

(b) Kumchagua Katibu Mkuu miongoni mwa majina mawili yatakayopendekezwa na
Mwenyekiti Taifa.
(c) Kuwachagua manaibu katibu wakuu miongoni mwa majina mawili mawili kwa kila
naibu yatakayopendekezwa na Mwenyekiti Taifa.
(d) Kuchagua wajumbe wa nane kuingia kwenye Kamati Kuu. Kwa uwiano ufuatao:-
• Wanaume watatu na wanawake watatu kutoka Tanzania Bara na angalau mmoja
awe mlemavu
• Mwanaume na Mwanamke mmoja kutoka Tanzania Zanzibar
(e) Kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya rufaa za uchaguzi na za kinidhamu kutoka ngazi
za chini.
(f) Kujadili mikakati ya uendeshaji wa shughuli za Chama kwa kipindi kati ya mkutano
mkuu na mkuu mkutano na kuifanyia maamuzi panapostahili.
(g) Kuthibitisha mikakati na rasilimali za kuendesha kampeni za wagombea wa Chama
katika chaguzi za serikali hususani uchaguzi Mkuu na uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
(h) Kuandaa ratiba na maelekezo ya uchaguzi wa kichama kwa mujibu wa Katiba na
Kanuni za Chama .
(i) Kutunga na kuzifanyia marekebisho kanuni za kuendesha shughuli za Chama.
(j) Kujadili taarifa za Kamati Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa utekelezaji.
(k) Kusimamia utendaji kazi wa Kamati Kuu.
(l) Kupendekeza kwa Mkutano Mkuu masuala yote ya Katiba ya Chama na mabadiliko
yake.
(m) Kujadili rasimu ya Ilani (Manifesto) ya uchaguzi kwa Uchaguzi Mkuu na uchaguzi
wa Serikali za Mitaa kuwasilisha mapendekezo yake kwa mkutano Mkuu kwa
maamuzi.
(n) Kusimamia chaguzi za Chama ngazi za Jimbo/Wilaya.
(o) Kuteua wadhamini wa Chama.
(p) Kusimamia utekelezaji na uzingatiaji wa maadili ya Chama.
(q) Kuthibitisha kanuni za uendeshaji Chama na miongozo ya Mabaraza ya Vijana,
Wanawake na Wazee.
(r) Kumwachisha ujumbe wa Baraza Kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume na
Katiba, kanuni na maadili ya Chama ama hatakidhi matakwa ya kuteuliwa kwake.
(s) Kuthibitisha wa majimbo ya chama

7.7.16 Kazi za Kamati Kuu zitakuwa:-
(a) Kufanya utafiti wa wagombea na wa Uraisi na Mgombea Mwenza na kuwasilisha
ripoti zake kwa Baraza kuu kwa ajili ya mapendekezo yake kwa Mkutano Mkuu.

(b) Kuteua Wakurugenzi wa Idara Kuu za Chama Makao Makuu
(c) Kuteua Makatibu wa Wilaya na Mikoa
(d) Kuthibitisha uteuzi wa Sekretarieti za Wilaya.
(e) Kutoa mapendekezo kwa Baraza Kuu juu ya rufaa za uchaguzi na kinidhamu.
(f) Kuandaa na kutoa Mapendekezo kwa Baraza Kuu, Mikakati ya kuendesha shughuli
za Chama kwa kila mwaka na kwa kipindi cha miaka mitano.
(g) Kuandaa na kutoa mapendekezo kwa baraza Kuu , Mikakati ya kupata mahitaji ya
raslimali za kuendesha kampeni za wagombea wa Chama katika chaguzi za kiserikali.
(h) Kuandaa na kutoa mapendekezo kwa Baraza kuu ratiba na maelekezo ya uchaguzi wa
kichama.
(i) Kupitia na kutoa kwa Baraza Kuu mapendekezo ya haja ya kuzifanyia marekebisho
au maboresho Kanuni za Chama ama Katiba ya Chama.
(j) Kujadili taarifa za Sekretarieti ya Kamati Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa
utekelezaji.
(k) Kusimamia utendaji kazi wa Sekretarieti ya Kamati Kuu
(l) Kufanya mapitio ya Sera za Chama na kutoa mapendekezo kwa Baraza Kuu kwa
kuzingatia matokeo ya Utafiti uliofanywa na Sekretarieti ya Kamati Kuu.
(m) Kusimamia utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Baraza Kuu na Mkutano
Mkuu.
(n) Kuwa kiungo na kudumisha mahusiano mema kati ya Chama na vyama vingine vya
siasa nchini, Afrika Mashariki na nchi nyingine.
(o) Kuthibitisha ajira za watumishi wakuu wa Chama ngazi ya Taifa.
(p) Kuteua kamati au tume za kushughulikia masuala maalum ya kichama kwa muda
maalumu.
(q) Kuteua wakaguzi wa mahesabu ya Chama kwa kila mwaka
(r) Kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge na Baraza la wawakilishi
Zanzibar
(s) Kuandaa agenda za Baraza Kuu na Mapendekezo ya agenda za Mkutano Mkuu.
(t) Kufanya uamuzi juu ya mpendekezo ya kufukuza Mwanachama.
(u) Kuandaa hoja za kupelekwa Bungeni na Wabunge wa Chama
(v) Kumwachisha ujumbe wa Kamati Kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume na
katiba, kanuni na maadili au kushindwa kukidhi matakwa ya kuteuliwa kwake.
(w) Kuratibu utendaji wa ofisi ndogo ya Makao Makuu Zanzibar.
(x) Kusimamia utendaji kazi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee.
(y) Kuteua wajumbe maalum wawili kuingia Kamati ya Utendaji ya Jimbo/Wilaya
 
Wee Kigarama, unaleta ukosoaji wa Chadema humu jf?!. Haya endelea...ila usije kulalamika!. Sisi wenzako tumeshajifunza kwa upande wangu mimi, nimeona bora niikumbatie CCM mgombea awe Lowassa!. CCM ina utaratibu mzuri sana wa kupata viongozi, hakuna rushwa, mizengwe wala upendeleo, wao wanatumia public opinion ya members, ndi maana sasa tunafanya kazi kubwa ya ku shape public opinion ili wakati ukifika ni jina la Lowassa tuu ndio libaki midomoni mwa public opinion!.

wee kanjanja............................. we na hilo li bahasha lako la lowasa, inatosha sasa....................... its too much kwa "mtoto wa kiume"...................... hapa yanajadiliwa ya chadema mara na wewe unaanza kuleta habari za wanja ulompakia huyo lowasa wako!!....................... khaaaah!!.........................
 
5.2 Haki za MwanaChama
Kila mwanachama ana haki ya:-
5.2.1 Kuchagua viongozi wa Chama wa ngazi anayohusika kwa mujibu wa katiba.
5.2.2 Kuchaguliwa kuongoza na kuwakilisha Chama katika ngazi yoyote kwa kuzingatia
masharti yaliyowekwa ya sifa za uongozi.

5.2.3 Kushiriki vikao vya Chama vinavyomhusu na kutoa mawazo yake kwa uhuru kwa
kuzingatia taratibu za vikao.
5.2.4 Kujitetea, kusikilizwa na kukata rufaa anaposhitakiwa ama kuchukuliwa hatua za
kinidhamu kichama.

Wale wanaojua sheria wanasema "haki inatolewa kwa mkono huu na inachukuliwa kwa mkono mwingine" Kwa maana nyingine hayo masharti ni yale yanayotajwa kwenye kifungu 7.7.16 ambacho kinaipa Kamati Kuu haki ya "kutafiti" na baadaye kupeleka jina la "aliyetafitiwa" kwenye kikao cha Baraza Kuu kwa kupendekezwa kwa Mkutano Mkuu.

Hivi Demokrasia ndani ya CHADEMA imekomaa sana kuliko kwenye vyama kama Demokrat na Republik au Conservative au labour paty vya uingereza na Marekani? Kwa nini kusiwekwe utaratibu wa kila mwanachama kugombea na kisha mkutano mkuu wachague wanayempenda kuliko mkutano mkuu kupelekewa jina na Kamati pamoja na Baraza Kuu? Haya si mambo ya enzi zile za chama kimoja ambapo kulikuwa na picha ya mtu na kivuli?
 
kati ya watu wote waliochangia mpaka sasa ni Zemarcopolo pekee ndiye aliyenielewa, Dada yangu FaizaFoxy yeye kaishia njiani sijui kama amenielewa au la! Kwanza mwanzoni kabisa niliweka wazi kwamba kwenye huu uzi hakutakikani ushabiki wa kivyama au upuuzi wa "kumjua" mtu wakati kwa hali halisi humjui. Wengi humu ndani hawajisumbui hata kuisoma hiyo katiba ya CHADEMA ingawa iko kwenye soft copy.

Katiba ya CHADEMA inataja waziwazi ni vyombo gani hasa vinahusika na uteuzi wa mgombea wa nafasi ya Urais na vyombo hivyo ni Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, nje ya hapo ni uvunjaji wa Katiba yenyewe na ni siasa za Kihuni zaidi ya zile zinazofanyika CCM! Kama kuna mtu anadhani kuna mwanachama mwenzake anafaa kwa nafasi ya Urais basi aende akamshawishi agombee lakini si watu wachache tu wao wachukue jukumu la "kuteua" mtu eti kwa kuwa wanadhani anafaa kuwa mgombea.

Tupo watanzania zaidi ya milioni 40, haiwezekani watu wengine wao ndiyo wawe na "akili" za kujua mahitaji ya watu wote wa nchi hii bila ya USHIRIKISHAJI. Hoja yangu kama kweli tunaamini CCM inaviza Demokrasia basi tusiiruhusu CHADEMA nayo ivize Demokrasia yetu changa inayokua!

Uteuzi wa Slaa kuwa mgombea wa CHADEMA hata kama ulileta msisimko kiasi gani kwenye siasa zetu si aina nzuri ya kupata mgombea ya kujivunia. Kwa sababu kugombea ni haki ya kikatiba kwa kila mwanachama. Haiwezekani watu wachache wafunge milango na kusema "sisi tunamjua atakayetufaa na atakayewafaa watanzania". Ni vizuri kama kuna mtu anadhaniwa anafaa basi ni lazima kuna watu pia wanadhani hafai nao wanaye mtu "wao" anayefaa na ni vizuri kuwashindanisha hawa wawili ili anayefaa zaidi achaguliwe. Anayefaa si lazima awe yule unayedhani wewe anafaa!!

Huu ujinga wa kudhani kwamba kila anayeikosoa CHADEMA ni CCM utatotoka lini??
Mkuu bado nadhani unachanganya maswala hapa. Kuna KUPENDEKEZA MAJINA ya wagombea na kuna UTEUZI wa WAGOMBEA, mimi naona umerukia katiba na kuchukua uteuzi unafanyika vipi badala ya kutazama mapendekezo. Kwa maana kwamba vikao vya chama vinafanya uteuzi lakini sivyo vinavyopendekeza majina ya wagombea na mgombea hawezi kujinadi kabla hajapitia hatua za kupendekezwa.. Kama nimeelewa vizuri, maelezo yanafafanua kwamba CDM hakuna kitu kujipendekeza au kujinadi! - ndivyo nilivyoelewa mimi.

Pengine tungejiuliza Dr.Slaa alipendekezwa vipi hadi kuwa mgombea kisha tukatazama utaratibu uliofanyika na tukaanza kukosoa makosa kama yapo. Au tungepata majina ya watu wengine waliopendekezwa na walipendekezwa vipi halafu ndio tunakuja kujadili lakini sio kuruka hatua hii na kuanza kuzungumzia Uteuzi..

Mimi nilichosoma na kuelewa ni kwamba haya yalikuwa majibu ya chama kuhusiana na madai ya gazeti ambalo limeonyesha viongozi wa Chadema wakianza kupigana vikumbo ktk kinyang'anyiro cha Urais mwaka 2015. Na wamejibiwa vizuri tu kwamba, hakuna kitu kama hivyo maana majina hayapatikani hivyo isipokuwa kuna utaratibu wake..Na huo utaratibu unatakiwa kuenziwa!..
 
mkuu MM hapo kwenye bold............................ nakumbuka 2010 wakati wa preliminaries za chadema nilikuwa dar na nilifuatilia kwa karibu sana mchakato wwa kumpata dr Slaa....................... naomba nikumbushwe ni lini wanachama wa kawaida ("kutokea ngazi za chini" kama ulivyoita) walipata fursa ya kumpendekeza..................... mi sikuwahi kusikia fursa hiyo ikitolewa, nilichosikia ni kuwa kamati kuu "imemuomba" agombee....................... hebu tufafanulie kidogo hapo tuliopitwa na newz .........................

Mkuu,
Kuna viongozi wa chama kuanzia ngazi ya msingi, tawi, kata, jimbo/wilaya, mkoa hadi Taifa.
Hawa ni wawakilishi halali wa wanachama na ndio walishiriki kutoa mapendekezo/maoni kuhusu mgombea uraisi.
 
njaa ikizidi sana unaweza kujikuta unatafuta vitufe vya key board au cm yako bila kujijua.
 
Mkuu bado nadhani unachanganya maswala hapa. Kuna KUPENDEKEZA MAJINA ya wagombea na kuna UTEUZI wa WAGOMBEA, mimi naona umerukia katiba na kuchukua uteuzi unafanyika vipi badala ya kutazama mapendekezo. Kwa maana kwamba vikao vya chama vinafanya uteuzi lakini sivyo vinavyopendekeza majina ya waghombea na mgombea hawezi kujinadi kabla hajapitia hatuya za kupendekezwa.. Katika CDM hakuna kujipendekeza! ndivyo nilivyoelewa mimi.

Pengine tungejiuliza Dr.Slaa alipendekezwa vipi hadi kuwa mgombea kisha tukatazama utaratibu uliofanyika na tukaanza kukosoa makosa kama yapo. Au tungepata majina ya watu wengine waliopendekezwa na walipendekezwa vipi halafu ndio tunakuja kujadili lakini sio kuruka hatua hii na kuanza kuzungumzia Uteuzi..

Mimi nilichosoma na kuelewa ni kwamba haya yalikuwa majibu ya chama kuhusiana na madai ya gazeti ambalo limeonyesha viongozi wa Chadema wakianza kupigana vikumbo ktk kinyang'anyiro cha Urais mwaka 2015. Na wamejibiwa vizuri tu kwamba, hakuna kitu kama hivyo maana majina hayapatikani hivyo isipokuwa kuna utaratibu wake..Na huo utaratibu unatakiwa kuenziwa!..
Angalia kifungu nilichonukuu na hicho ndicho kinachonitia mimi wasi wasi. Ukisoma kwa makini ni kwamba "utaratibu" unaotakiwa kuenziwa si ule wa kikatiba bali ni ule uliotumika kumpata Slaa kama mgombea.

Mwaka 2010 baada ya Kamati Kuu 'kumwomba" Slaa awe mgombea, kwa kutumia rasirimali za chama Slaa akazunguka nchi nzima kusema "ameombwa' na Kamati Kuu kugombea. Kwa mazingira kama hayo unadhani kuna nafasi ya mtu mwingine kutamani kugombea wakati tayari kamati Kuu inaye tayari mgombea wake?

Sifa ziwekwe wazi wanaotaka kugombea wajipime na kama wanakidhi vigezo na masharti yaliyowekwa basi washindanishwe!! Siyo "watafiti" waseme huyu "anafaa' bila ya kusema anafaa kuliko nani!!
 
njaa ikizidi sana unaweza kujikuta unatafuta vitufe vya key board au cm yako bila kujijua.
"heri wenye njaa na kiu ya maarifa kwa maana ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia ni wao"
 
Kigarama,
Nadhani tatizo lako ni tafsiri ya demokrasia na kwa jinsi ulivyoandika hapo naamini kwako demokrasia halisi ni kuacha milango wazi kwa kila mtu anayejisikia, achukue fomu kuwania uraisi. Ndio maana nikasema labda tumezoea mfumo wa kiccm hadi kudhani kwamba ndio demokrasia na kusahau kwamba demokrasia inatafsiriwa kwa namna nyingi tofauti.

Kwa mujibu wa katiba ya chadema kama ambavyo umei quote, kamati kuu imepewa mamlaka kikatiba kufanya utafiti juu ya wagombea wa nafasi ya mgombea uraisi na mgombea mwenza. Na kwa mwaka jana utafiti huo uliwashirikisha wanachama(viongozi wa chama) kuanzia ngazi za chini na ndipo kamati kuu ilipata pa kuanzia kabla ya kupanua wigo kwa kwenda kwa wadau wengine na chaguo la watu umeliona.

Kwakuwa kazi iliyofanywa na kamati kuu ni kwa mujibu wa katiba, basi nakushauri ukubaliane na ukweli huo.
 
Back
Top Bottom