Kauli hii ya CHADEMA imenishangaza!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli hii ya CHADEMA imenishangaza!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Jan 12, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama umevaa viatu vyako vya ushabiki wa chama chako vivue!!

  "Hivyo kinachopewa umuhimu ni utumishi kwa umma, kwa ajili ya maendeleo ya watu na si mbio za kusaka vyeo. Ni vyema hii dhana ya mtu kufuatwa na kuombwa, mara anapoonekana kuwa anafaa kuongoza, kulingana na mahitaji ya watu na sifa za nafasi hiyo, kama ambavyo imekuwa ikifanyika ndani ya CHADEMA, ikaenziwa na kufanywa kuwa ni namna bora ya kupata viongozi".

  Hivi katiba ya CHADEMA inasemaje kuhusu jinsi ya kupata wagombea kwenye nafasi mbalimbali za uongozi? Hivi ni kina nani wanaochagua wa kumpendekeza, na wao ni kina nani kawapa madaraka ya "kumtambua" anayefaa na kufaa huko kunachukuliwaje kama ndiyo mahitaji ya wakati na ni vipi wanachama wa kawaida wanahusishwa kwenye "kumtambua" anayefaa'

  Mwaka 2010 ilikuwa Slaa tuliambiwa maneno meengi kuhalalisha Kamati kuu Kumchagua Slaa. Hapa sizungumzii kufaa au kutokufaa kwa mgombea, nazungumzia upana wa Demokrasia kwa maana halisi ya kushirikisha watu kwenye kufanya maamuzi yanayowahusu wao. CHADEMA inapinga "kuteuana teuana" lakini kwa maelezo yao haya inayoonyesha kwamba na wao pia wanaamini kuna watu ndani ya CHADEMA "wanajua" mahitaji ya wanachama na wananchi kwa ujumla!

  Tofauti yao na CCM ni nini?
   
 2. M

  Mussa Mussa Senior Member

  #2
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sijaona hoja ya msingi ya kujadili hapo la sivyo ukekuwa umesoma katiba ya chama husika na kuona mapungufu yaliyojitokeza katika kuteua wagombea na kuyaweka wazi hapa ningekuwa na mchango. Tafuta evidence ndugu yangu ili tusaidiane.
   
 3. k

  kicha JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 532
  Trophy Points: 180
  mkuu umejenga hoja makini ila wacha niskie kwa wahusika kuweza kuskia kitu
   
 4. l

  leloson Member

  #4
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hoja ni ipi hapa, au unakua kama viongoz wacuf wanaokimbia hoja za hamad na kubak wanapiga talalila
   
 5. GIUSEPPE

  GIUSEPPE JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 4,487
  Likes Received: 4,491
  Trophy Points: 280
  SASA nawewe unataka uteuliwe wewe?
   
 6. J

  JALUO Senior Member

  #6
  Jan 12, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  umefulia brazaaaa..huna hoja..sijui ata wapi pakuanza kujadili
   
 7. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #7
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sasa unataka tujadili nini?
   
 8. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mmh sioni cha kujadili,yaani heading na maelezo tofauti kabisa,ebu kajipange urudi tena mkuu
   
 9. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  sijaelewa unataka nini kifanyike wakati hata hiyo katiba yao hujaisoma
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Jan 12, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nilichosoma mimi na kuelewa ni hivi:-
  Utaratibu wa Chadema ni kwamba mgombea Urais hutokana na mapendekezo ya wajumbe au wanachama (when, where, how and why haya sijui) lakini hakuna kitu mtu kuamua tu kugombea Urais kama ilivyoelezwa na gazeti la mwananchi kuanza vurugu za kugombea urais ndani ya chama..Ni muhimu mgombea utokane na Mapendekezo ya wanachama na upo utaratibu wake - Na utaratibu huu lazima kuenziwa!
   
 11. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sijakuelewa mkuu ila kwa uelewa wangu mdogo nimegundua kuwa wewe ni kibaraka wa Magamba!
   
 12. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2012
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kauli hii ni nzuri tu kama huitafsiri kiunazi.

  Nakumbuka nikiwa UDSM, kitivyo cha uhandisi mwaka 1993 - 1997 tuliamua kutumia staili hii baada kugundua kuwa wagombea wengi ni waongo na sana sana wanakuwa na agenda zao tofauti na wanachokieleza kwenye campaign.

  Baada ya Mtungirehi kumaliza urais wake kwa matatizo mengi, yakizidishwa na makamu wake bwana Maswi Chacha, ambaye sasa ni Katibu mkuu wizara ya mafisadi pale nishati na madini ambaye ilikuja fahamika kuwa alikuwa pandikizi, wanachuo wa kitivo cha uhandisi tuliamua kutafuta mtu ambaye angefaa kuongeza serikali ya wanafunzi.

  Tulitumia utaratibu wa kupendekeza na kutoa sababu kwenye mkutano uliofanyi engineering kuanzia kama saa moja jioni mpaka around saa tano usiku.

  Watu wote waliojipendekeza wenyewe walionekana hawana sifa baada wanajumuiya kueleza udhaifu wao openly kwenye mkutano huo, huu wapenda kuchaguliwa wakiwekwa karibu na idara ya CPE chini ya ulinzi. Mmoja wapo wa wagombea hao alikuwa ni bwana Malima ambaye kwa uwazi kabisa baada ya kuitwa kuelezwa kuwa tulimdisqualify, alitumia kuwa ngoja akapate maoni ya washauri wake akina Dr. Lamwai, Prof. Barege na wengine wa NCCR-Mageuzi. Katika kuthibitisha kuwa hawakufaa, baadhi ya marafiki zake wa karibu wakatoa siri openly kwenye huo mkutano kwamba nia yake ilikuwa ni kuendesha bar ya DARUSO.

  Tukamwambia nenda na ukawaongoze hao hao waliokutuma siyo sisi na kutangaza kuwatenga mabwenini na darasani. Mwingi alikuwa jamaa mmoja wa kihaya ambaye aliwahi kuwa speaker wa bunge wa DARUSO kwa muda. Mwishoni walinywea na kuwa pamoja nasi.

  Kwa kauli moja tulimpendekeza Engineer Sweke ambaye aliungwa mkono na wanakitivo wengi sana. Kwa nguvu moja tulipiga campaign na akashinda upresident.

  Katika miaka yangu minne ya UDSM, huyu ndiye aliyekuwa rais pekee aliye maliza kipindi chake cha urais, kwani hapo awali wengine wote walishindwa kumalizia vipindi vyao kwa sababu kuu ya kusideline na utawala wa chuo pamoja serikali.

  Kwa hiyo, si vibaya kama kuna mtu una muona anafaa kuwa kiongozi na ukawashauri wenzio, imradi pasiwe na hidden agenda.

  Kwa hiyo naomba watu wasipinge kila kitu bali kitafakari kwa mapana na marefu yake yote.

  Nawasilisha.
   
 13. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mbona hujaijadili hy hoja?
   
 14. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #14
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,454
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Kwani Mkwe.re alijipendeka mwenyewe au kuna watu walianza kumpigia chapuo Mapemaaa???
   
 15. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  ...kigarama kwa fikra zako utachanganyikiwa bure! we mwana wa ccm je cdm yakukunaje? sisi wanachama halisi tumeridhika na uteuzi wako we walia na cdm kwanini? achana nasi tujenge chama makini.
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wewe ni mmoja wapo hujaelewa na hauko kwenye hizo asilimia 2
   
 17. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  kama wewe umemuelewa mbona hujachangia hoja?
   
 18. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mimi nimekuelewa vyema ni nini unataka kutueleza lkn kuna mambo ya kuzingatia unapozungumzia DEMO/KRASIA. Kaka Demokrasia ni neno la Kigiriki Democratus ambapo demo ni majority na cratus ni rule or power. Kinachotafsirika leo kuwa demokrasia hapa kwetu ni nje kidogo ya dhana ya kilichokuwa kinazungumziwa na Wayunani (ambao ndio waanzilishi wa dhana yenyewe) lkn tukirudi kwenye objectives, utaona kuwa kinachomatter ni willingness ya waongozwaji kuongozwa na huyo aliyechaguliwa. Demokrasia haimaanishi kila mmoja wetu awe mpendekezaji. Demokrasia haimaanishi kuwa kila mmoja ampendekeze mtu wake. Tukifanya hivyo, kila tunaweza tuwe na nominees 67,000 na sijui tutaamua vipi ikiwa kila mtu ana watu wae wa5 wanaomuunga mkono. Kama unataka kuikosoa CDM juu ya kwa nini watu fulani wanapendekeza nani awe nani, basi sidhani kama unaweza ukanipa mfano wa chama chochote hapa Africa ambapo nominees wake wanachaguliwa na wanachama wote.

  Hayo unayoyadai yafanywe na CHADEMA ili tu wewe uone kuwa demokrasia ipo (kwa kukukumbusha tu) hata serikali imeshindwa kufanya yenyewe. Kama serikali hupitiza bakuli kuomba fedha za kugharamia uchaguzi mkuu, CDM itatoa wapi fedha za kufanya voting ya Wanachama wake nchi nzima? Labda CUF itaweza, manake ipo Unguja na Pemba tu huku tumikoa twa pwani nako tukifuatia kwa mbali kwenye maeneo yaliyo karibu na misikiti.
   
 19. ATUGLORY

  ATUGLORY Senior Member

  #19
  Jan 12, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  weka source ya data iliyokupa ukweli kwamba ni asilimia mbili tu ya wanaJF ambao hawajamuelewa' vinginevyo no research no data no talk' yaana kama huna data za uhakika kusubstantiate maneno yako jiepushe na generalized statements kama 'nakuhakikishia' na utatundea haki ukinyamaza, msahafu mmoja unasema kwamba hata mjinga akinyamaza kwake hiyo ni hekima.
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Jan 12, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Majina ya wagombea wote wa CCM ktk kiti cha Urais walijitokeza wenyewe hata kama wewe ungetaka kugombea maadam unayo kadi ungegombea... Jambo zuri sana kwa demokrasia lakini tatizo linakuja ktk uchujaji yaani kundi la watu wanawachuja bila kujua mapendekezo ya wanachama ni yapi... hakuna mtu anajua Kagoda au Malecela angeweza vipi kupata kura za wanachama kama sii kukwamishwa..

  Sasa Chadema inasema wao wana utaratibu ambao majina yanapendekezwa na wanachama, sasa iwe kupitia wenyeviti wa majimbo, wilaya, mikoa au kupitia ofisi zao za chama na majina hayo ndio huwakilishwa na kuanza mchakato..

  Tofauti zake ni kwamba mgombea wa CCM anapendekezwa na CC kugombea urais wakati mgombea wa Chadema anapendekezwa na wanachama..
   
Loading...