Mwambie huyo msukuma aliyeanzisha uzi... Yan kuna vilaza hii nchi jaman dah... Kijana na misuli yako unakuwa na mawazo mgando kiasi hiki?Una uhakika mkuu? Mbona sisi tulisoma huko na kupasua vibaya mno.
Nilienda A - Level shule ya serikali mchepuo wa Sayansi, PCB. Mwalimu wa Physics alikuwa ndiye headmaster, mwalimu wa biology alikuwa msaidizi wa headmaster (na hawa wote walikuwa busy mambo ya utawala). Chemistry, tulikuwa tunaazmishwa mwalimu kutoka shule binafsi.
LAKINI kila anapopata muda headmaster anakuja kupiga pindi hata usiku ... Practical zote alitufundisha, the same to second master. Morale yao ilikuwa juu..!
Mwisho wa siku tukatoka na kwenda chuo.
Tatizo linajulikana, serikali imekuwa mtesaji wa watumishi wake ... Sio kwenye elimu, pote huko huduma hazina morale.
Na hapo karibia Shule 80. Ni za Kanisa Katolikikatika shule mia bora za matokeo shule za serikali ni saba tu
Profesa Ndalichako walimu wa serikali wanalala sana Mimi advance nimesoma serikali walimu wengi wa serikali ni wavivu kufundisha na awana morali pia wakuu wa shule wanashindwa kuwasimamia walimu
Mkuu hii shule ulioopo ni International au maana sio kwa pesa hizo....Mimi nipo shule moja ya binafsi, Moshi, tupo bize Sana na watoto!
Kila sekunde ina kazi kwa mwl na mwanafunzi!
Kila ijumaa nasaini elf 50 ya remedial, salary yangu 1m , kila baada ya miaka 2 nachukua gratuity isiyopungua 5m.
Serikali ikifanya vivo mbona hata mimi nitahamia !
Serikalini hata kwenda markings tu, yunabaniwa!
hahahaa una hakika hao wa shule za serikali nao wanakijua kimalikia?aah wapi,tusidanganyane shida watanzania hatutaki kuita spade eti kijiko kikubwa hebu nenda hizo shule binafsi mazingira tu utaona tofauti kubwa sana watu wamewekeza eti.Hata hao wanaofundisha private nao wanatumia kizungu hicho hicho.... ila private wanafaulu, Gvt wanafeli. Ishu kubwa hapa ni motisha kwa waalimu...
Ueleze na changamoto zilizopo huko serikalini ndo utakuwa umemsaidia MH Waziri wa Elimu.katika shule mia bora za matokeo shule za serikali ni saba tu
Profesa Ndalichako walimu wa serikali wanalala sana Mimi advance nimesoma serikali walimu wengi wa serikali ni wavivu kufundisha na awana morali pia wakuu wa shule wanashindwa kuwasimamia walimu
Mkuu umeongea vyema sana,sina shaka na utaalamu wako.......Hongera sana!!Wala sihitaji nikujuwe,nimejadili hoja yako,ingependeza kama ungetumia hiyo Elimu unayojisifu kuwa nayo kutoa mchango wako wa nini kifanyike ili Ku "rescue situations",huo ndiyo usomi,kuja na takwimu tu kuwa kati ya Shule 100 bora Shule za serikali ni 7 tu haiwezi kuleta tija katika kizazi hiki chenye wazazi wanaohimizwa wafyatue watoto tu kwa sababu Elimu ni bure.
Elimu ni moja ya hitaji la msingi la mtoto,kama yalivyo mahitaji mengine,msimamizi mkuu wa Elimu ya mtoto ni Mzazi mwenyewe.Kama Mzazi hatawekeza muda wake katika kufuatilia maendeleo ya mwanaye darasani,akaishia kumtelekeza mwanaye kwa walimu na yeye asishiriki kwa namna yeyote ile kufuatilia na kuwezesha ufanisi wa mtoto wake darasani,Mwalimu hata afanyeje,bado mwanafunzi husika hawezi kuleta matokeo bora.
Shule kama Kidete Sec.hata upeleke walimu magwiji wa taaluma ya ualimu,bado haiwezi kufanya vizuri.Haiwezekani Shule yenye watoto wahuni,waliokosa malezi bora ya wazazi,watoto wanaozurula katika fukwe za bahari pale Mjimwema badala ya kuwa darasani,watoto wanaojificha kwenye vichaka vilivyoko pembezoni mwa bahari na kufanya uchafu,kisha wanadandia malori ya mchanga/kokoto na kurudi kwao uwategemee wafanye vizuri darasani.
Wengi wa wanafunzi tulionao darasani siku hizi hawana sifa stahiki za kuwepo darasani,wamefika hapo kwa msaada wa mfumo mbovu wa Mitihani yetu ya darasa la VII,tangu tulipoamua kuifanya Mitihani ya VII iwe ya kuchagua,tuliua vipaji vya watoto wetu na kuasisi Taifa lisilokuwa na uwezo wa kutumia vipawa katika kufikiri,tukazalisha "kizazi cha kubet", sasa watoto waliochaguliwa kujiunga sekondari kupitia Mitihani ya " kubet"(multiple choice),unatarajia waweje darasani?
Haiwezekani serikali ihamishe Attendance registers za Shule ya msingi Maweni,Mjimwema,Ungindoni,Kibugumo,Mikwambe na Mizimbini na kuzihamishia Kidete Sekondari,kisha utarajie watoto hao waliopelekwa Kidete bila sifa stahiki waweze kufanya vizuri.
Tuache kucheza na Elimu ya watoto wetu kwa kutafuta umaarufu wa kisiasa,tuwaache wataalamu waziendeshe Shule kitaalamu,serikali ijikite katika kuziwezesha Shule kwa kuzipatia vitendea Kazi na walimu wa kutosha,iboreshe mazingira ya upatikanaji wa Elimu,na iache kuhamisha Attendance registers toka Shule za msingi na kuzipeleka sekondari,katika hali ya kawaida haiwezekani darasa zima likafaulu,wapewe nafasi wale tu wenye uwezo,tujikite zaidi katika ubora badala ya wingi,tukifanya hivyo serikali itakuwa na wanafunzi wachache wenye uwezo mzuri,na itawasomesha vizuri,vinginevyo tukiendekeza siasa katika mambo ya msingi,tutaendelea kufanya vibaya kila uchwao.
Hiyo ni nzuri ila mi huwa siungi mkono mwanangu kumpeleka boarding akiwa Class I anaeza kuwa na taaluma nzuri sana ila kimaadili akawa tofauti sana!!Ni kweli kabisa Mkuu. Hicho cha kwangu kiko boarding since Class I. Likizo anakuja na rundo la homeworks masomo yote na ni lazima azimalize. Hizo volumes za vitabu tunazowanunulia sio mchezo most of them za Kenya na chache za hapa. Katika level yake ya Class V tayari ana uwezo wa ku-solve maswali makali ya mathematics ambayo ndiyo hasa yanatumika katika mitihani ya kuingia F.I katika shule za maana hapa nchini - Feza, Marian, St. Francis, Loyola, St. Joseph, and the like.
Juzi hapa likizo ya Desemba alitukalisha kitako na mama yake kutuelezea story (homework) about "persuasion". Ilikuwa ni academic story ya kama pages tatu hivi ambayo alitakiwa kuielewa, kutoa title, na kuweza kuielezea kwa ufasaha, na kujibu maswali - kwa sisi wa zamani it was so funny. Wakenya wakiwa good marketers tunabaki kukodoa mimacho; haikuja by surprise bali wanajengewa misingi imara tangu utotoni.
Tatizo sio lugha ndugu. mbona hicho kiswaz chenuewe watoto wanafeliTatizo ni "Kithungu" masomo yanafundishwa Kimalikia wakati walimu na wanafunzi hawaijui hiyo lugha!?
What do we expect?
Nashauri Shule zote (Form 1-6) waweke wakalimani
Ni kweli Kiongozi ila sio kila shule unaweza kuthubutu kufanya hivyo. Unaangalia na maadili ya shule yenyewe; lazima ufanye kautafiti kidogo. Muhimu iwe na hofu ya Mungu wa kweli maana miungu ipo mingi, miongoni mwa vigezo vingine.Hiyo ni nzuri ila mi huwa siungi mkono mwanangu kumpeleka boarding akiwa Class I anaeza kuwa na taaluma nzuri sana ila kimaadili akawa tofauti sana!!
Ni kweli kabisa ila mi naogopa sana,shule inaweza kuwa na maadili ila watoto wenyewe wakaharibiana......au mtoto anakuja nyumbani hajui hata kufagia uwanja!!Ni kweli Kiongozi ila sio kila shule unaweza kuthubutu kufanya hivyo. Unaangalia na maadili ya shule yenyewe; lazima ufanye kautafiti kidogo. Muhimu iwe na hofu ya Mungu wa kweli maana miungu ipo mingi, miongoni mwa vigezo vingine.
Ha ha ha! Kweli ni kichekesho. Kwa matokeo yaliyotoka juzi, kwa mzazi anayejali future ya mwanae, imani kwa shule za serikali ndio hivyo tena imekwisha. Ku-overhaul mfumo wa shule za umma ukae vizuri will take not less than 10 years.Nilicheka sana baada ya kuona baadhi ya vyombo vya habari vikiripoti kua shule binafsi zinaelekea kukosa wanafunzi eti kwa sababu serikali ya awamu ya tano imeboresha shule za uma.twafaa
Umenena ya moyoni ubarikiwe.Ha ha ha! Kweli ni kichekesho. Kwa matokeo yaliyotoka juzi, kwa mzazi anayejali future ya mwanae, imani kwa shule za serikali ndio hivyo tena imekwisha. Ku-overhaul mfumo wa shule za umma ukae vizuri will take not less than 10 years.
Ndalichako atapita; Magufuli terms zake zitaisha ila mfumo ulivyoharibika hautaweza ku-stabilze ndani ya muda wao. Kimzaha mzaha, elimu imekwenda "kaburini" pamoja na wadau kupiga kelele enzi na enzi lakini ndio hivyo nani awasikilize "vyura wapigao kelele"? Tembo atakunywa maji, atashiba, na kwenda zake; vyura watakaokufa watakuwa wamekufa; hatajali wala hana haja ya kujua nyuma huko kaacha maiti ngapi za vyura.