Katika shule bora 100, shule za seriakli ni 7 tu

Katika shule bora 100, shule za seriakli ni 7 tu

This is a very serious issue; lina-contribute more than 25% ya matokeo mabovu shule za Serikali. Mtoto aliyeanzia English medium tangu vidudu huwezi kumfananisha na aliyetokea Kiswahili medium wanapoingia F.I. Nina kibinti changu kiko Class V; hizo nondo wanazopewa ni balaa; kuanzia Mathematics, English, etc. For sure it is great; acha tu watupige hizo ada ni halali yao na naomba Serikali isiingilie kabisa hili suala kwa shule binafsi kama walivyotaka kufanya. Waboreshe zao tutapeleka watoto huko.
mtoto wa grade 2 anajua HIV/AIDS na anakuelezea vizuri tu , tayari anajua conditionals I & II si mchezo kaka katoto miaka sita tu kanajua kutumia Had to , have to yaani kwa kweli acha tu wapige ada juu they deserve . watoto wako busy muda wote kila siku home works 3--4
 
This is a very serious issue; lina-contribute more than 25% ya matokeo mabovu shule za Serikali. Mtoto aliyeanzia English medium tangu vidudu huwezi kumfananisha na aliyetokea Kiswahili medium wanapoingia F.I. Nina kibinti changu kiko Class V; hizo nondo wanazopewa ni balaa; kuanzia Mathematics, English, etc. For sure it is great; acha tu watupige hizo ada ni halali yao na naomba Serikali isiingilie kabisa hili suala kwa shule binafsi kama walivyotaka kufanya. Waboreshe zao tutapeleka watoto huko.
Ndugu Dudus tatizo lingekuwa ni lugha pekee basi wanafunzi wote wangekuwa wanapata "A" kwenye Kiswahili. Nikitazama matokeo hata Kiswahili ni majanga. Tatizo ni kubwa zaidi ya lugha.
 
unijui sikujui bora ukae kimya



Wala sihitaji nikujuwe,nimejadili hoja yako,ingependeza kama ungetumia hiyo Elimu unayojisifu kuwa nayo kutoa mchango wako wa nini kifanyike ili Ku "rescue situations",huo ndiyo usomi,kuja na takwimu tu kuwa kati ya Shule 100 bora Shule za serikali ni 7 tu haiwezi kuleta tija katika kizazi hiki chenye wazazi wanaohimizwa wafyatue watoto tu kwa sababu Elimu ni bure.

Elimu ni moja ya hitaji la msingi la mtoto,kama yalivyo mahitaji mengine,msimamizi mkuu wa Elimu ya mtoto ni Mzazi mwenyewe.Kama Mzazi hatawekeza muda wake katika kufuatilia maendeleo ya mwanaye darasani,akaishia kumtelekeza mwanaye kwa walimu na yeye asishiriki kwa namna yeyote ile kufuatilia na kuwezesha ufanisi wa mtoto wake darasani,Mwalimu hata afanyeje,bado mwanafunzi husika hawezi kuleta matokeo bora.

Shule kama Kidete Sec.hata upeleke walimu magwiji wa taaluma ya ualimu,bado haiwezi kufanya vizuri.Haiwezekani Shule yenye watoto wahuni,waliokosa malezi bora ya wazazi,watoto wanaozurula katika fukwe za bahari pale Mjimwema badala ya kuwa darasani,watoto wanaojificha kwenye vichaka vilivyoko pembezoni mwa bahari na kufanya uchafu,kisha wanadandia malori ya mchanga/kokoto na kurudi kwao uwategemee wafanye vizuri darasani.

Wengi wa wanafunzi tulionao darasani siku hizi hawana sifa stahiki za kuwepo darasani,wamefika hapo kwa msaada wa mfumo mbovu wa Mitihani yetu ya darasa la VII,tangu tulipoamua kuifanya Mitihani ya VII iwe ya kuchagua,tuliua vipaji vya watoto wetu na kuasisi Taifa lisilokuwa na uwezo wa kutumia vipawa katika kufikiri,tukazalisha "kizazi cha kubet", sasa watoto waliochaguliwa kujiunga sekondari kupitia Mitihani ya " kubet"(multiple choice),unatarajia waweje darasani?

Haiwezekani serikali ihamishe Attendance registers za Shule ya msingi Maweni,Mjimwema,Ungindoni,Kibugumo,Mikwambe na Mizimbini na kuzihamishia Kidete Sekondari,kisha utarajie watoto hao waliopelekwa Kidete bila sifa stahiki waweze kufanya vizuri.

Tuache kucheza na Elimu ya watoto wetu kwa kutafuta umaarufu wa kisiasa,tuwaache wataalamu waziendeshe Shule kitaalamu,serikali ijikite katika kuziwezesha Shule kwa kuzipatia vitendea Kazi na walimu wa kutosha,iboreshe mazingira ya upatikanaji wa Elimu,na iache kuhamisha Attendance registers toka Shule za msingi na kuzipeleka sekondari,katika hali ya kawaida haiwezekani darasa zima likafaulu,wapewe nafasi wale tu wenye uwezo,tujikite zaidi katika ubora badala ya wingi,tukifanya hivyo serikali itakuwa na wanafunzi wachache wenye uwezo mzuri,na itawasomesha vizuri,vinginevyo tukiendekeza siasa katika mambo ya msingi,tutaendelea kufanya vibaya kila uchwao.
 
Serikali isicheze na walimu.... watatutengenezea taifa la watu mbumbumbu.... ndali nae apunguze ubabe na amri za shuluti.... atafute kiini cha tatizo hili....
 
Kiingereza sio tatizo mfano masomo ya sayansi na hesabu ni maswali ya kufikiria na sehemu kubwa ni kukuriri na watoto wengi huwa wanaelewa walichoulizwa ila majibu ndio hawajui hata kama utamuuliza swali hilo hilo kwa kiswahili bado hatolijibu kwani waliofeli wote somo la kiswahili wamefaulu?
 
Kwasasa serikali hamna remedial classess yaan baaada ya mda wa kaz walimu wanalud hom kujitafutia japo ka lizik..wakat private hakiananee ili apate wateja lazima watoto wapasue so anakesha kuwafundisha na walim wanapewa mshahara mnono na malupulupu ya kutosha hafikilii kenda kuendesha boda boda baada ya kazi
 
Tatizo kubwa ni kwamba serikali yetu inapenda mambo mazuri ambayo hawako tayari kuyagharimikia, mathalani walimu hawana motivation, motivation waliyonayo ni vitisho kila uchao,stahiki zao hawalipwi unakuta mwalimu anadai malimbikizo huu mwaka wa kumi,hakuna vifaa vya kufundishia,hakuna vitabu halafu unategemea mwisho wa mwaka upate matokeo mazuri.
 
Unamkata mfanyakazi 15% ya mkopo huku akiwa na mshahara wa Ths. 350,000.00 baada ya mikopo benki anabaki na Tshs. 200,000.00 .Unatarajia akufundishie Watanzania walalahoi ,mmmmmh serikali itasubiri sana.
 
katika shule mia bora za matokeo shule za serikali ni saba tu
Profesa Ndalichako walimu wa serikali wanalala sana Mimi advance nimesoma serikali walimu wengi wa serikali ni wavivu kufundisha na awana morali pia wakuu wa shule wanashindwa kuwasimamia walimu
Hizo shule bora za binafsi si ndio miongoni mwao zina-scarn wanafunzi na kufawanyisha mitihani wale tu wenye understanding capacity ya juu? Sasa tusubiri baada ya agizo jipya la serikali.
 
Tatizo ni "Kithungu" masomo yanafundishwa Kimalikia wakati walimu na wanafunzi hawaijui hiyo lugha!?
What do we expect?

Nashauri Shule zote (Form 1-6) waweke wakalimani
Sikubaliani na wewe asilimia mia mkuu, shule za private secondary kuna wananfunzi wanaokwenda pale wakiwa wametoka kwenye shule za msingi za kayumba na wakifika pale wanafaulu kwa Div. one, mifano ninayo mingi tena ndani ya famili..tatizo ni serikali kudharau walimu na walimu kuamua kukomoa wanafunzi, waliposema elimu bure hakuna hata tuition ambayo mwalimu alikuwa anapata kipato cha ziada walifikiria tu kumkomoa mwalimu, sasa haya ndio matunda yake, wawalipe haki zao wawasimamie nao watawajibika ipasavyo.
 
Mambo mazuri ni gharama ....m spin mnavyotaka lakini bila kuboresha maslai ya walimu na miondo mbinu ya mashule ..tutaendelea kujikongoja tuu hivi na kutupiana lawama kila majibu ya mitihani ya taifa inapotoka......mfano mpaka leo hii kuna vitabu bado havijatolewa walimu wanafundishia uzoefu tuu...well ndio bongo kulalama tuu siku ziende!
 
Pendekezo - shule za binafsi zifutwe kama tulivyokusudia ili zetu ziwemo kwenye namba za juu .

Dawa ni hiyo tu , wenye shule binafsi wanajifanya wajanja wakati sera tunatunga sisi ; serikali ina mkono mrefu .
 
Shule saba nyingi sana,next time walimu kazeni kidogo angalau iwe moja au iwe bila bila kabisa.
 
Usiwalinganishe walimu wa private na walimu wa serikali, kwanza mshahara na mazingira mazuri
 
Back
Top Bottom