Katika shule bora 100, shule za seriakli ni 7 tu

Katika shule bora 100, shule za seriakli ni 7 tu

katika shule mia bora za matokeo shule za serikali ni saba tu
Profesa Ndalichako walimu wa serikali wanalala sana Mimi advance nimesoma serikali walimu wengi wa serikali ni wavivu kufundisha na awana morali pia wakuu wa shule wanashindwa kuwasimamia walimu
Tusimtafute mchawi watanzania mchawi wetu ni CCM na siasa zao uchwara za kutojali maslahi ya Walimu
 
Ndugu Dudus tatizo lingekuwa ni lugha pekee basi wanafunzi wote wangekuwa wanapata "A" kwenye Kiswahili. Nikitazama matokeo hata Kiswahili ni majanga. Tatizo ni kubwa zaidi ya lugha.
Kiongozi; nimesema lugha inachangia around 25%; kuna factors nyingine pia. Tukubali tusikubali lugha ni miongoni mwa matatizo sugu yanayochangia performance ngazi ya sekondari pengine hata level za juu zaidi. Pamoja na kwamba hata iweje failures hawakosekani hata hivyo Kiswahili this time ndilo somo liloongoza kwa ufaulu zaidi. Hata kama mtihani ungekuwa na swali moja tu la "wewe ni nani" bado zeros zingepatikana.
 
mtoto wa grade 2 anajua HIV/AIDS na anakuelezea vizuri tu , tayari anajua conditionals I & II si mchezo kaka katoto miaka sita tu kanajua kutumia Had to , have to yaani kwa kweli acha tu wapige ada juu they deserve . watoto wako busy muda wote kila siku home works 3--4
Ni kweli kabisa Mkuu. Hicho cha kwangu kiko boarding since Class I. Likizo anakuja na rundo la homeworks masomo yote na ni lazima azimalize. Hizo volumes za vitabu tunazowanunulia sio mchezo most of them za Kenya na chache za hapa. Katika level yake ya Class V tayari ana uwezo wa ku-solve maswali makali ya mathematics ambayo ndiyo hasa yanatumika katika mitihani ya kuingia F.I katika shule za maana hapa nchini - Feza, Marian, St. Francis, Loyola, St. Joseph, and the like.

Juzi hapa likizo ya Desemba alitukalisha kitako na mama yake kutuelezea story (homework) about "persuasion". Ilikuwa ni academic story ya kama pages tatu hivi ambayo alitakiwa kuielewa, kutoa title, na kuweza kuielezea kwa ufasaha, na kujibu maswali - kwa sisi wa zamani it was so funny. Wakenya wakiwa good marketers tunabaki kukodoa mimacho; haikuja by surprise bali wanajengewa misingi imara tangu utotoni.
 
Serikali isicheze na walimu.... watatutengenezea taifa la watu mbumbumbu.... ndali nae apunguze ubabe na amri za shuluti.... atafute kiini cha tatizo hili....
Ndalichako yuko bize kudhibiti shule binafsi. Anasahau kwamba kudhibiti huko kunafanya pia mambo mazuri yasitokee.
Serikali iimarishe na kuboresha shule zake, iache kuchezea elimu. Tujiulize "ni viongozi wangapi wa serikali watoto wao wanasoma shule za serikali?"
Unategemea nani atazijali hizi shule za serikali.
Hizi shule zimebaki kuwa ni za wazazi wasio na uwezo wa kuwapeleka watoto shule binafsi.
Waziri au mbunge atampelekaje mtoto wake Shule ya Kibugumo?
Ukweli utatuweka huru.
 
katika shule mia bora za matokeo shule za serikali ni saba tu
Profesa Ndalichako walimu wa serikali wanalala sana Mimi advance nimesoma serikali walimu wengi wa serikali ni wavivu kufundisha na awana morali pia wakuu wa shule wanashindwa kuwasimamia walimu
Kwa hiyo uliwaona wakilala na je kipindi hicho wanafunzi walifeli kama walivyofeli mwaka huu? Okay nenda uchukue Buku 7
 
katika shule mia bora za matokeo shule za serikali ni saba tu
Profesa Ndalichako walimu wa serikali wanalala sana Mimi advance nimesoma serikali walimu wengi wa serikali ni wavivu kufundisha na awana morali pia wakuu wa shule wanashindwa kuwasimamia walimu
Jifunzeni kutoka kwa private schools. Nao siyo kukaa kulalamika tu. Mazingira yenyew mabovu ubabe tu.
SIKU MKIACHA SIASA KWENYE ELIMU, NDIPO SHULE ZA SERIKALI ZITAFANYA VIZURI
 
katika shule mia bora za matokeo shule za serikali ni saba tu. Profesa Ndalichako walimu wa serikali wanalala sana Mimi advance nimesoma serikali walimu wengi wa serikali ni wavivu kufundisha na awana morali pia wakuu wa shule wanashindwa kuwasimamia walimu

Walimi katika shule za serikali wamekata tamaa, hawako motivated wamo kazini kwa nifanyeje lakin si kwa kuipenda kazi na kutaman kuifanya kwa bidii na maarifga yao yote
 
katika shule mia bora za matokeo shule za serikali ni saba tu
Profesa Ndalichako walimu wa serikali wanalala sana Mimi advance nimesoma serikali walimu wengi wa serikali ni wavivu kufundisha na awana morali pia wakuu wa shule wanashindwa kuwasimamia walimu

Mmemawalipa satahiki zao??Je mazingira ya kufundishia yakoje??
 
Jifunzeni kutoka kwa private schools. Nao siyo kukaa kulalamika tu. Mazingira yenyew mabovu ubabe tu.
SIKU MKIACHA SIASA KWENYE ELIMU, NDIPO SHULE ZA SERIKALI ZITAFANYA VIZURI

Bora umemwambia.Wanapanda kunde wanategemea maharage
 
1. Walimu wamechoka kufanywa daraja la watu kutokea.
2. Serikali ya JPM haina kabisa mpango na walimu.
3. Kama kuna sehemu wameharibu ni pale waliposema wakuu wa shule wawe ni wale wenye degree na kuendelea. Yani bado tunadhani elimu zetu bila uzoefu wa kazi ndo kila kitu. Walimu wengi wenye degree ndiyo hawa "walimu wa kisasa"
 
katika shule mia bora za matokeo shule za serikali ni saba tu
Profesa Ndalichako walimu wa serikali wanalala sana Mimi advance nimesoma serikali walimu wengi wa serikali ni wavivu kufundisha na awana morali pia wakuu wa shule wanashindwa kuwasimamia walimu
unijui sikujui bora ukae kimya

Sasa wewe umeleta hoja ijadiliwe, kabla ya kuanza mjadala member mwenzio kakuambia umeleta hoja ambayo inaning'inia mno, kitu ambacho ni cha kweli na wala siyo tusi hata kidogo...

Binafsi naiona hoja yako ni nzuri sana kwa mjadala, lakini ni kweli kabisa kwa upande mmoja ina mapungufu ya kimantiki ktk uwasilishaji wake.

Umeshangaa vyema kuwa ktk shule bora 100 kitaifa ni kwa nini za serikali/umma ziwe 7 kati ya hizo na zinazobaki zote 93 zitoke ktk sekta binafsi...

Ukaanza kulivuruga bandiko lako wewe mwenyewe kwa kutoa hitimisho kuwa, sababu ni shule za serikali/umma kuwa
na WALIMU WAVIVU (nadhani ulimaanisha, wasiojituma ktk kazi yao) na WALIMU WAKUU/WAKUU WA SHULE wasio na uwezo bila hata kufafanua uwezo gani kwa sbb walimu walioko ktk shule za binafsi na zile za serikali wote wamezalishwa na vyuo hivi hivi vilivyopo nchini....

Hiki ndicho kinachokufanya ushambuliwe na wachangiaji wengi na wewe kukosa uvumilivu na kutoa majibu ya mkato na kuudhi ambayo yatakufanya usipate michango ya maana ktk hoja nzuri sana uliyoianzisha...

Mwisho basi, ingekuwa vyema sana kama hoja yako usingeitolea hitimisho wewe mwenyewe kwa sbb kwa vyovyote vile hizo sababu mbili za UVIVU WA WALIMU na UWEZO MDOGO WA W/WAKUU haziwezi kuwa sababu pekee za shule za serikali/umma kuburuzwa na shule za binafsi japo zaweza kuwa moja ya sababu nyingi ambazo wana JF wenzako wanaweza kusaidia kuzitoa....

Kumbuka kuwa humu ndani ya jukwaa hili wapo wataalamu wa mambo ya elimu, walimu, wachambuzi wa sera na kila aina ya wataalamu wa fani mbalimbali ambapo ukiweka wazo ama hoja yako vizuri, utanufaika kupata michango mizuri sana na kuwa shule kwako na sisi wengine pia!!

Haikuwa busara kumjibu member mwenzio kama ulivyojibu hapo kwa sababu, vyovyote iwavyo hakuna mtu mwenye shida ya kumjua ama kutomjua mwenzie humu, na akikaa kimya kama ulivyomwambia hapo juu na wengine wakakaa kimya, lengo lako la kuanzisha mjadala linakuwa halina maana. Ni bora wewe ndiye ungekaa kimya na wazo lako!!
 
Msipende kuangalua upande mmoja je mshahara wa mwalumu wa serekali na private ni sawa hapo ndo utajua kwa nini morali ni ndoho kwa walimu wetu wa serikali
Mimi nipo shule moja ya binafsi, Moshi, tupo bize Sana na watoto!
Kila sekunde ina kazi kwa mwl na mwanafunzi!
Kila ijumaa nasaini elf 50 ya remedial, salary yangu 1m , kila baada ya miaka 2 nachukua gratuity isiyopungua 5m.
Serikali ikifanya vivo mbona hata mimi nitahamia !
Serikalini hata kwenda markings tu, yunabaniwa!
 
Ili uwe na shule bora lazima uwekeze kwanza kwa walimu bora wenye motisha na wasimamizi wa shule wenye weledi, vifaa vya kufundishia na miundombinu ya madarasa/library/mabweni etc. Na nimevipanga kwa kuzingatia vipaumbele. Bila kuzingatia hayo tutaendelea kushuhudia shule maarufu na kongwe za serikali zikifanya vibaya mwaka hadi mwaka wakati shule changa za binafsi sikitawala chati za juu. Kwa wale wanaolaumu lugha ya kiingereza wajue kuwa nayo inafundishika tena kwa urahisi tu ikiwa kuna waalimu weledi.
 
katika shule mia bora za matokeo shule za serikali ni saba tu
Profesa Ndalichako walimu wa serikali wanalala sana Mimi advance nimesoma serikali walimu wengi wa serikali ni wavivu kufundisha na awana morali pia wakuu wa shule wanashindwa kuwasimamia walimu
Kwa hiyo unatakaje sasa????
 
Pendekezo - shule za binafsi zifutwe kama tulivyokusudia ili zetu ziwemo kwenye namba za juu .

Dawa ni hiyo tu , wenye shule binafsi wanajifanya wajanja wakati sera tunatunga sisi ; serikali ina mkono mrefu .
Nina imani unatania tu! Ila ukiangalia amri na maelekezo yanayotoka kwa shule binafsi sasa hivi naamini ndiko tunakoelekea.
 
Kuna matatizo mengi yanayomfanya mwanafunzi ashindwe kuperfom vizuri kama,
1-umbali mrefu wa makazi mpaka shuleni
2-siasa za madiwani na wanasiasa wengine hasa shule za kata,unakuta kila siku wanakuja kuleta ujingaujinga
3- vitabu vyao ni uozo mtupu eti Oxford, havijajitosheleza vya kutosha
4- mazingira magumu ya kazi kwa walimu ni tatizo kubwa kwa waalimu unakuta wanashindwa kuwapa kile kinachotakiwa kwa wanafunzi
5- motisha kwa waalimu shida hata increment tabu wakati hali ya maisha inakuwa ngumu kwanini asiwe bodaboda
6- kutenganisha siasa na mambo ya maana
Ndio maana private wanatushinda kila siku na siasa uchwara zao
 
Una uhakika mkuu? Mbona sisi tulisoma huko na kupasua vibaya mno.

Nilienda A - Level shule ya serikali mchepuo wa Sayansi, PCB. Mwalimu wa Physics alikuwa ndiye headmaster, mwalimu wa biology alikuwa msaidizi wa headmaster (na hawa wote walikuwa busy mambo ya utawala). Chemistry, tulikuwa tunaazmishwa mwalimu kutoka shule binafsi.

LAKINI kila anapopata muda headmaster anakuja kupiga pindi hata usiku ... Practical zote alitufundisha, the same to second master. Morale yao ilikuwa juu..!

Mwisho wa siku tukatoka na kwenda chuo.

Tatizo linajulikana, serikali imekuwa mtesaji wa watumishi wake ... Sio kwenye elimu, pote huko huduma hazina morale.

Partially nakuunga mkono.

Tofauti ya miaka ile na leo sirikali imeajili waalimu ambao wengi ni failures. Waliofeli wengi ndo hukimbilia kusoma ualimu hasa wa shule za msingi na sekondari. Matokeo yake tunayaona sasa.

Alafu ukiongezea na mfumuko wa shule za kata na uhaba wa waalimu wenye viwango nilivyotaja hapo juu matokeo yake ndo majanga haya tunayoyashuhudia sasa hivi.

Twafaaaaa
 
Ndalichako yuko bize kudhibiti shule binafsi. Anasahau kwamba kudhibiti huko kunafanya pia mambo mazuri yasitokee.
Serikali iimarishe na kuboresha shule zake, iache kuchezea elimu. Tujiulize "ni viongozi wangapi wa serikali watoto wao wanasoma shule za serikali?"
Unategemea nani atazijali hizi shule za serikali.
Hizi shule zimebaki kuwa ni za wazazi wasio na uwezo wa kuwapeleka watoto shule binafsi.
Waziri au mbunge atampelekaje mtoto wake Shule ya Kibugumo?
Ukweli utatuweka huru.
Hawa wengi ukweli hawautaki na ndo tatizo kubwa la watz....
 
Back
Top Bottom