Shule za serikali nyingi zinatiisha huruma. Huwa najiuliza unakimbiliaje kufuta ada hali ya kuwa miundombinu ya shule ni duni sana tena saana!!
Maabara na vifaa shida, maktaba ni tabu,madawati tatizo,madarasa hayatoshi na hayajakamilika, umeme na maji utata,vyoo Vya mashaka,chakula hakuna,michezo na vifaa vyake bado...yaani list hainamwisho!! Kubwa zaidi walimu wananyimwa stahili zao,wengi wamejaa madeni wanaishi kwenye vivyumba kwa shida na hata mlo niwatabu. Haya mambo yanahitaji kiongozi makini asiyejali sifa binafsi!! Unahangaikia madege huku shule hazina vyakula,vyoo wala madawati?? Vitimbi