Katika kitabu chake cha "My life, My Purpose" Marehemu Mzee Mkapa alikiri kuzushiwa kifo akiwa madarakani

Course Coordinator

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
1,683
3,070
Haya mambo ya kuzushiana ugonjwa na vifo hayajaanza leo, yalikuwepo enzi na enzi. Kuzushiana vifo sio jambo geni katika Ulimwengu huu, kuna mlolongo wa matukio mengi ya watu mashuhuri na watu maarufu waliowahi kuzushiwa kuumwa au vifo.

Sababu mojawapo hutokana ama na siasa zenye chuki na uadui ama usiri wa taarifa pale ambapo wahusika wanaposhindwa kutoa taarifa sahihi kwa wakati.

Mfano wiki hizi mbili kumetokea taarifa kuwa MWENYEKITI WA CHADEMA NDUGU FREEMAN MBOWE na MKURUGENZI wa Habari na itikadi wa CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO(CHADEMA) kuwa wamefariki. Kwa vile ile ni taharuki na inagusa mioyo ya watu, wahusika walijitokeza na kuujulisha umma kuwa wao ni wazima wa afya.

Lakini hivi karibuni kumeibuka taarifa za alipo Rais wetu na afya yake ikoje, hizo tuziache.

Marehemu mzee Mkapa Rais wa awamu tatu nae alipata kuugua na kwenda kutibiwa nje, sasa chama chake cha Mapinduzi kilikataza serikali isitoe taarifa ya Mzee Mkapa kama ni mgonjwa hii ilipelekea taharuki kwa sababu ya usiri ule wa kuumwa kwake, hivyo wapinzani wakachukua advantage ile kuwa Mzee Mkapa amefariki.

Mzee Mkapa alitaka umma ujulishwe ila CCM chini ya Makamu Mwenyekiti Philip Mangula walikataa, kuzushiwa ugonjwa au kifo kunaweza tokana na sababu mbalimbali za kutaka ama kujitakia.

IMG_20210314_044824.jpg
Tuwaombee wagonjwa wale wote wanaumwa na wale wasioumwa waendelee kupata afya njema.

Jumapili njema ya leo.
 
Kama watu hawayaamini maneno bayana ya PM last Friday, hata Bulldozer akitoea leo kwenda kukagua miradi ya maendeleo kule ^Magomeni^ & ^Kariakoo^ still bado waleeee wazabizabina watasema siye, huenda ni mambo ya AI & robotiks :) :) :) ^Dunia ina mambo^ ~ Sam Mangwana
 
Ilifahamika Mkapa alikuwa anaumwa. Tatizo sasa hivi ni kwamba hatujamwona JPM tokea February 24th. Na kama haumwi, ni muhimu aondolee nchi hofu kwa kusalimia wananchi wake kwa hotuba ya live
 
Kwa watawala mara nyungi uzushi ndiyo hugeuka kuwa ukweli. Ya Meles na Mwanawasa yalianza kama uzushi lkn baada ya mwezi mmoja yakawa kweli.

Hata hili la sasa lina 99.9% za kutimilika.
 
Back
Top Bottom