Katika katiba mpya tuweke kipengere cha kuwabana wahuni katika uzito wa kura na maamuzi yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katika katiba mpya tuweke kipengere cha kuwabana wahuni katika uzito wa kura na maamuzi yao

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Godwine, Dec 28, 2011.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kutokana na ongezeko la wahuni wengi nchini imefika wakati kutafute mfumo wa kuhesabu kura kulingana na hekima za watu. Haiwezekani kura ya kila mtu kuhesabiwa kama ni moja, inabidi ifike wakati tuchambue hekima za watu na uwezo wao kuwe na mtu akipiga kura inahesabiwa na uzito wa kuanzia 5 na mwingine akipiga kura lakini ni muhuni tu basi kura yake tuihesabu kama ni nusu yani 0.5,

  kama katiba mpya ikiweka wazi mchakato huu na ukafanyiwa upembuzi yakinifu na kuweka madaraja ya watu na kuingiza katika vitambulisho vyao vya kupigia kura na vya utaifa tutafika wakati Viongozi watakuwa wakichaguliwa kwa maslahi ya taifa na si ushabiki wa wahuni.

  KWENYE KATIBA MPYA LAZIMA TUTOFAUTISHE UZITO WA MAAMUZI NA UZITO WA KURA YA KILA MMOJA WA WANANCHI KULINGANA NA HEKIMA NA MAARIFA YAKE LA SIVYO HIPO SIKU WAHUNI NDIO WATATUCHAGULIA RAIS
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  Unaweza kuwa na hoja, lakini ngumu kuitekeleza. Kwanza tuwe na definition ya mhuni/uhuni. Pili hekima haitokani na elimu, utajiri, outstanding performances (kama mastaa etc). Nasema hivyo kwa sababu position ya mtu katika jamii inatokana na vitu vitatu;
  1. Education
  2. Economic status
  3. Outstanding performances- -matendo yaliyotukuka katika jamii- including mastaa mbali mbali
  Ni vigumu kuvipima hivyo (inawezekana kuna vingine) kwa watu wote
   
 3. G

  Godwine JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Natambua ya kuwa ni ngumu kuamua lakini tuaweza wananchi wenyewe kukaa chini na kuweka vigezo vya kutambua nani ni muhuni na nani mwenye hekima na nani anatakiwa kupata kiwango gani ndio maana katika taifa la Marekani mbali na kuwa na kura za kawaida bado kuna kura za super deligate zanye uzito mkubwa na kila watu mashuhuri katika kila jimbo wanakuwa na uwezo wa kutumia kura hizi kwa manufaa ya taifa.

  kwa mfano baadhi ya vigezo vya kutambua uadilifu au uhuni ni

  1. kumbukumbu zako za uaminifu katika shughuli za umma

  2. makosa ya jinai na ufisadi uliowahi kulifanyia taifa

  3.uwezo wako binafsi wa kupambanua mambo IQ

  ​NA VIGEZO VINGINE KATIKA JAMII YETU LA SIVYO SIKU MOJA WAHUNI WATACHAGUA KIONGOZI AMBAYE NI MUHUNI MWENZAO
   
Loading...