Katika hili nashindwa kumuelewa mke wangu

Katika hili nashindwa kumuelewa mke wangu

ahsante kwa kisa chako, japo uhitaji msaada, lakini jua kuwa mwanamke iwe vyovyote uyazoee haya:
-nyumba yangu,
- gari yangu
- watoto wangu
- wangu
- wangu, kila kitu changu ni changu,
usiumie kichwa ndio wake zetu hao
Pia jaribu kuelewa kuwa mkeo anaposema "nimeamua tu" ujue ana maanisha.....
Mwanaume utatumiaje Gari la Mkeo? Kwa maelezo yake aliyenunua ni mke. Mnunulie Gari mkeo hata kadi ya gari ikiwa na jina lake hatapga kelele kivile
 
Hakuna tatizo zaidi ya wivu na nivema ukaeuka anayokukataza.kwani waweza fikiri mzaha.
 
Mke yuko sahihi hawa watu wa lift njiani wabaya sana mimi ilinitokea hiyo kwa rafiki yake wife kabisa baada ya wife kusafiri akahamia seat ya mbele na kuanza kufanya manjonjo yale aliyokua anaona wife anafanya. Ni vyema huyo dada awe anapanda wife akiwepo lakini mkiwa 2 hapana hata mimi namuunga mkono shemeji yetu
 
Watu ni majirani kama akitaka kumtongoza atamtongoza tu wala haina haja ya kusubiri lifti. Si ajabu hata namba za simu walishabadilishana.
Yap inawezekana but sometimes inabidi tu kumridhisha mtu
 
Chunguza kwa umakini. Inawezekana mkeo na jirani yako wana katabia flan ambako. Sasa mkeo yupo bench anahisi unaweza kugundua mambo yao. Wanawake wana siri nyingi sana. Wanajuana wenyewe..
 
Tena mkewe nae utakuta ndo anam-cheat mumewe Heaven Sent

Kabisa hili ndio linaweza kuwepo nyuma ya pazia! Official Scandal ....sikutii woga but man u gotta check this!

Mmh kwa nini Umewaza hivyo?

Heaven.... waovu wana weakness kubwa kuu wakati wote wanajistukia na kujiona wao kuwa hatarini na kwa uzoefu nilionao hii inaweza kutumika kuondoa attention kwa cheat inayofanywa naye kuja kwako wewe.....ilinitokea huko nyuma na mwenzangu nami nikawa najitaabisha kujisafi na kumwaminisha kuwa mambo nishwari na nikaacha kabisa kufikiri vinginevyo mpaka baadaye sana .....ni akili waliyopewa binadamu yaani kwa kuwa yeye ni mkosaji anashift attention kwako na wewe unakuwa busy kujitetea na kumplease asikufikirie tofauti...... kumbe looooh
 
Jamani Mimi niko tofauti kidogo, wana JF Mimi napenda sana kuwa peke yangu kwenye gari nahisi nakuwa comfortable sana
Kuna watu ukimpa lift siku 1 anazoea gari mpaka kero, utasikia Mara punguza radio, ongeza sauti kidogo, Mara mbona huendeshi sana wewe endesha bana
Arrrgh Arregh ilimradi tabu tu lol msiniseme mmbinafsi ni walimwengu wanabadili vitu vya wenzao kuwa haki yao ya msingi lol
 
let me guess ........ulizaliwa peke yako? kwa sie wengine tumeshare mpaka nguo na binadamu wenzetu
la umetokea familia masikini sana sasa leo kamkebe kako unaona kama wenzio wanafaidi pasipo kulitolea jasho eeh?
then namalizia ..........labda kwa kuwa wewe ni dereva wa hapo dar es salaam; tukatizao mikoani twajua faida ya kuwa na mwenzako safarini!

na hapo kwenye bold hii tabia haishii kwenye hako kamkebe kako .iko hadi sebuleni kwako ..........wageni hawaruhusiwi kushika remote ya tv yako ama kufungua friji kutoa kinywaji ....................puuuh!
 
Wadau,
Sina haja ya kuunganisha wanawake wote katika suala ninalopitia. Kwa ujumla ninaishi vizuri kabisa na mke wangu mpendwa ambaye tumeoana mwaka 2014. Tulibahatika kujenga na kuhamia nyumbani kwetu mwaka jana. Kwa bahati nzuri ambayo sasa imekuwa mbaya tulijenga urafiki na familia ya jirani na kwetu, mke wangu na dada wa nyumba ya jirani wakawa marafiki wakubwa.
Hali hii ilipelekea hata kuwa tunatoka wote asubuhi kwa gari ya mke wangu na kurudi pamoja pia muda wa jioni kwa kuwa wote tunafanya kazi katika maeneo jirani. Sasa mke wangu mpenzi amejifungua na sasa yupo ''maternity leave''. Jumatatu ikabidi nitoke mwenyewe na dada wa jirani ambaye huwa tunampa lift asubuhi na jioni. Sasa niliporudi usiku huo wa jumatatu wife akaniambia hataki nimpe lift tena dada wa jirani, nikauliza kwa nini? Akajibu hataki tu; niliwaza usiku ule na kuamua kuendelea kumpa lift huyu dada kwa kuwa wazo la kumpa lift lilikuwa la wife mwenyewe na kwangu ni ngumu sana kumpita huyu dada ambaye ameshazoea kuwa anapanda gari hii ukizingatia kuwa ni wife mwenyewe aliyemkaribisha. Nilipoamka jumanne nikamkuta huyu dada ananisubiri nje, nikampa lift kama kawaida na jioni pia nikarudi naye nyumbani pamoja.
Sasa mke wangu baada ya kuona hivyo, usiku wa jumanne akaniambia nikubali moja, kuendesha gari yake bila kumpa lift dada wa jirani au niende kazini kwa gari ya staff?! Hii kauli ya kutamka kuwa gari ni yake ilinipa mawazo sana kwa kuwa mke wangu huyu mpendwa hajawahi kuwa mtu anayeonyesha ubinafsi, tumekuwa na ndoa nzuri yenye amani na upendo wa hali juu.
Ndipo nikauliza ana tatizo gani na huyu dada? bado alinijibu kuwa hataki tu.
Nikampigia simu dereva wa staff bus kuwa anipitie asubuhi, na kuwakuwa basi huwa halijai kwa kuwa staff tunaoishi huko ni wachache na huyu dada alikuwa nje muda basi lilipofika kunichukua naye pia akapanda kwenye staff bus.
Niliporudi home wife amenuna na hataki kuongea, nashindwa kuelewa tatizo lake kwa huyu dada ni nini hasa?
Kiukweli naishi maisha yenye kuheshimu ndoa na kumpenda mke wangu kwa kiwango cha juu kabisa.

Waungwana, kama hivi ndivyo wanawake wanavyoweza kuwa na maamuzi yasio na chembe ya aibu napata shida sana kumuelewa mke wangu.
Kaka mkubalie mkeo na mweleze huyo dada kuwa mkeo amekataa asipande gari tenu ili asiwe anakusubiri
 
Naomba nikuulize Mkuu,Ivi kweli kama ingekua ni wewe ungekubali mkeo apande gari ya rafiki yako wakati wewe uko nyumbani na ukawa na amani kabisaa? au huna wivu na chako? isitoshe huyo ni mwanamke na wanawake wana 7senses sio SIX lol huenda amehisi kitu au amesikia kitu,sasa unasusia gari kisa unataka kumpa lift Jarani tena mwanamke,mie namuelewa na hasa wewe mwanamme ndio ungesema mwambie shogako
sitompa lift mpaka utakapokua wewe kwenye gari full stop...
Hivi kuna shida gani mkeo/mumeo kumpa lifti rafiki yako?! Inabidi ifike mahali tubadili namna ya kufikiri na tujaribu kuwaamini waume/wake zetu.
 
Kabisa hili ndio linaweza kuwepo nyuma ya pazia! Official Scandal ....sikutii woga but man u gotta check this!

Heaven.... waovu wana weakness kubwa kuu wakati wote wanajistukia na kujiona wao kuwa hatarini na kwa uzoefu nilionao hii inaweza kutumika kuondoa attention kwa cheat inayofanywa naye kuja kwako wewe.....ilinitokea huko nyuma na mwenzangu nami nikawa najitaabisha kujisafi na kumwaminisha kuwa mambo nishwari na nikaacha kabisa kufikiri vinginevyo mpaka baadaye sana .....ni akili waliyopewa binadamu yaani kwa kuwa yeye ni mkosaji anashift attention kwako na wewe unakuwa busy kujitetea na kumplease asikufikirie tofauti...... kumbe looooh
Ukichokiongea nakukubaliana nacho kabisa, ila kwa huyu mke wa mtoa mada issue ipo tofauti kidogo. Mbona siku zote hakumzuia huyo rafiki ake, ameona tu sass hivi mumewe na huyo rafiki yake watakuwa huru zaidi, lolote laweza kutokea. Analinda tu mali yake jamani
 
ulinzi hapo hakuna .tabia ni hulka Heaven, wa kumega atamega tu hata iweje!
 
Aah lakini kuna mazingira yanaweza yakakudumbukiza kwenye kuchepuka kwa urahisi
umejitetea kama mwanasiasa wa bongo! ........Penzi ni hisia zinazokua kwa kupaliliwa ukinambia ilitokea tu ......like how?, hiyo kitu inakuwa pre conceived then unafuatia huo utumbukiaji teh teh teh teh teh
 
Weee nyie sio kwa kurubunika, muache dada wa watu alinde ndoa yake
 
Back
Top Bottom