Katika hili nashindwa kumuelewa mke wangu

Katika hili nashindwa kumuelewa mke wangu

Wadau,
Sina haja ya kuunganisha wanawake wote katika suala ninalopitia. Kwa ujumla ninaishi vizuri kabisa na mke wangu mpendwa ambaye tumeoana mwaka 2014. Tulibahatika kujenga na kuhamia nyumbani kwetu mwaka jana. Kwa bahati nzuri ambayo sasa imekuwa mbaya tulijenga urafiki na familia ya jirani na kwetu, mke wangu na dada wa nyumba ya jirani wakawa marafiki wakubwa.
Hali hii ilipelekea hata kuwa tunatoka wote asubuhi kwa gari ya mke wangu na kurudi pamoja pia muda wa jioni kwa kuwa wote tunafanya kazi katika maeneo jirani. Sasa mke wangu mpenzi amejifungua na sasa yupo ''maternity leave''. Jumatatu ikabidi nitoke mwenyewe na dada wa jirani ambaye huwa tunampa lift asubuhi na jioni. Sasa niliporudi usiku huo wa jumatatu wife akaniambia hataki nimpe lift tena dada wa jirani, nikauliza kwa nini? Akajibu hataki tu; niliwaza usiku ule na kuamua kuendelea kumpa lift huyu dada kwa kuwa wazo la kumpa lift lilikuwa la wife mwenyewe na kwangu ni ngumu sana kumpita huyu dada ambaye ameshazoea kuwa anapanda gari hii ukizingatia kuwa ni wife mwenyewe aliyemkaribisha. Nilipoamka jumanne nikamkuta huyu dada ananisubiri nje, nikampa lift kama kawaida na jioni pia nikarudi naye nyumbani pamoja.
Sasa mke wangu baada ya kuona hivyo, usiku wa jumanne akaniambia nikubali moja, kuendesha gari yake bila kumpa lift dada wa jirani au niende kazini kwa gari ya staff?! Hii kauli ya kutamka kuwa gari ni yake ilinipa mawazo sana kwa kuwa mke wangu huyu mpendwa hajawahi kuwa mtu anayeonyesha ubinafsi, tumekuwa na ndoa nzuri yenye amani na upendo wa hali juu.
Ndipo nikauliza ana tatizo gani na huyu dada? bado alinijibu kuwa hataki tu.
Nikampigia simu dereva wa staff bus kuwa anipitie asubuhi, na kuwakuwa basi huwa halijai kwa kuwa staff tunaoishi huko ni wachache na huyu dada alikuwa nje muda basi lilipofika kunichukua naye pia akapanda kwenye staff bus.
Niliporudi home wife amenuna na hataki kuongea, nashindwa kuelewa tatizo lake kwa huyu dada ni nini hasa?
Kiukweli naishi maisha yenye kuheshimu ndoa na kumpenda mke wangu kwa kiwango cha juu kabisa.

Waungwana, kama hivi ndivyo wanawake wanavyoweza kuwa na maamuzi yasio na chembe ya aibu napata shida sana kumuelewa mke wangu.
Mkuu, Sikiliza amri ya mama mtoto wako................. You have spent alot of MONEY ktk ndoa yenu..!!
Ujue kuwa sasa MAMLAKA ya familia ni ya Mkeo (wife) ili uishi kwa AMANI na furaha sikiliza ushauri wake!!
Ok, hata kama utapata hasira au kufikiria vingine its useless..kwani hii ni hulka za wanawake wote.....popote uendapo utayakuta tu!!
Kila la kheri Mr OFFICIAL
 
kumbe kuna wakati watu wanakuwa ma great thinkers wanaigizaga tu kujitoa akili kama bongo movie. wadau wanachangia positively kujenga ndoa yako mwenzako hapendi uwe na huyo dada wanawake sisi ni nyoka atakutega hutaamin atavyoisambaratisha ndoa yako kaa mbali na huyo dada mpende mkeooo
 
Hebu jaribu kuvaa viatu vyake huyo mkeo....iko hivi; kila siku umezoea kumpa lift kwenye gari yako jirani/ mshkaji wako (rafiki yako mwanaume) lakini umepata likizo au safari, gari yako kabaki nayo mkeo na jiranj/ rafiki/mshkaji wako bado anataka aendelee kupata lift kwa mkeo ikiwa wewe haupo, tena asubuhi na jioni, je! na wewe hutopata wasiwasi rafiki/mshkaji/jirani yako wa kiume kuwa na mkeo kila siku asubuhi na jioni?

Mkeo anawaogopa walimwengu na visa vyao na sio wewe!
 
mbona mtihani mwepesi sana huo mkuu... rudisha mpira kwa kipa tu mchukue asubuh mwambie twende ukamwambie mwenyewe kua hutak apande gar yake..... akikataa bas na wewe kua mwanaume acha kwenda na gar ya mkeo panda staff bus akitokea kupewa lift huyo dada mruhusu apande akilalamika mwambie akamwambie mwenywe maana kama kumkarbisha alimleta mwenywe bas hata kumfukuza mwambie amfukuze mwenywe full stop......
 
unataka kukosana na mkeo kisa dem wa jirani?? shame on you chief,
haitaji kukupa sababu kwa sababu si lazima huyo dada kutumia asset zenu ikiwemo gari

hata staff buss nalo kanuna... sasa afanyaje??
 
Wazo lakumpa lift Dada lilikua la wife na lakutokumpa Lift Dada ni lawife pia, msikilizi mkeo
 
Naomba nikuulize Mkuu,Ivi kweli kama ingekua ni wewe ungekubali mkeo apande gari ya rafiki yako wakati wewe uko nyumbani na ukawa na amani kabisaa? au huna wivu na chako? isitoshe huyo ni mwanamke na wanawake wana 7senses sio SIX lol huenda amehisi kitu au amesikia kitu,sasa unasusia gari kisa unataka kumpa lift Jarani tena mwanamke,mie namuelewa na hasa wewe mwanamme ndio ungesema mwambie shogako
sitompa lift mpaka utakapokua wewe kwenye gari full stop...
 
Mkeo anashindwa tu jinsi ya kukwambia kuwa unaweza kuishia kuchepuka na huyo rafiki ake since muda wote huu mtakuwa nyie wawili tu. Muelewe tu mkeo, panda zako staff bus

Kuna time Unatengeneza mazingira ayo ya mtu kuchepuka....kwa maneno tu mwanaume naye anaanza jengea hisia....kuna siri kati yao apo ambayo mwanamke anaona mmewe ataambiwa kutokana na ukaribu
 
Wakati anajenga urafiki na huyo mdada alikuwa mjamzito na sasa ameshajifungua na anaona kwa mazingira yaliyopo anahisi utachepuka naye huyo dada kwa kipindi hiki ambacho mkeo yupo nyumbani. Inabidi utumie akili ya ziada katika kulitafakari hili ilihali usilete mgongano kati yao.
 
Hapo Fanya Anavyotaka Tu Koz SheFeels Insecure Around That Woman.
Afu Unakuta Yeye Ndo Pioneer Wa Huo Urafiki Na Kumpa Lifti.
Kuhusu VYANGU, YANGU, LANGU, WANGU, PANGU, KWANGU Mmmhhh No Comment
 
Mkeo anashindwa tu jinsi ya kukwambia kuwa unaweza kuishia kuchepuka na huyo rafiki ake since muda wote huu mtakuwa nyie wawili tu. Muelewe tu mkeo, panda zako staff bus
anajitoa ufahama anaelewa sana wife anamaanisha nini indirectly aacha ukaribu na huyo dada kakatazwa asipandae nae gari moja kamkaribisha gari ya wife mwishowe ataambiwa achague kati ya wife na huyo dada ndo anakoelekea huko ( thinking aloud)
 
Kuna time Unatengeneza mazingira ayo ya mtu kuchepuka....kwa maneno tu mwanaume naye anaanza jengea hisia....kuna siri kati yao apo ambayo mwanamke anaona mmewe ataambiwa kutokana na ukaribu
Ujue kuna Vitu ni vidogo sana, ila vikipuuziwa vinaweza vikaharibu kila kitu. Kama mke kuna kitu anaficha ni sawa tu coz hakuna marefu yasiyo na ncha. Afu unadhani kumwambia mtu siri ni hadi muonane, mtu akitaka kukupa siri atatafuta tu mbinu. Yeye aendelee tu kupanda staff bus, mke akimaliza likizo wataendelea na style yao ya kupeana lift. Mbona maisha simple sana hapo,
 
anajitoa ufahama anaelewa sana wife anamaanisha nini indirectly aacha ukaribu na huyo dada kakatazwa asipandae nae gari moja kamkaribisha gari ya wife mwishowe ataambiwa achague kati ya wife na huyo dada ndo anakoelekea huko ( thinking aloud)
Hahaha kumbe na wewe zako hizo, chagua kati ya mimi na fulani lol, Ujikute sasa kachaguliwa mwenzio teh. Ila huko ndo itakapoelekea kama mwanaume atalazimisha kumpa lift huyo dada jirani, apande tu staff bus jamani
 
hahah akichaguliwa mwenzangu nawashoot wote wakaendelee kupeana lift in hell huko
huyo dada nae hajiongezi kwani zamani alikuwa anaendaga vipi kazini?? tatizo shem wetu nae anatafuta matatizo ya kujitakia kakatazwa huku na kwenye staff bus anamkaribisha ofisi ziko.majirani mwisho wataanza kupitiana lunch time. mpaka maternity leave iishe watu washa bond sana tu
 
  • Thanks
Reactions: nao

Mmh na wakati utakuwa busy kulia umekuwa rejected lol

Mmh watu tumetofautiana, mdada labda yeye anaona kawaida ndo maana hana hata habari hadi kwenye staff bus. Issue ni wao wahusika kujiongeza maana ndoa ni yao
 
anaona sawa tu yani ingekuwa mimi nishamface mume si anajifanya kichwa ngumu
 
hahahahaha ni shiiida mr anaona bora amplease stranger. then wife aendeelee kukereka
Ujue wanaume ni watu wakuchukulia vitu easy ( wanaona wanawake ni watu ambao tupo emotional muda wote), so mume hapo yeye anaona hakuna shida yoyote, haelewi concern ya mkewe. Kumbe mke anamuepusha na majaribu kabla hayajamkuta
 
ubinafsi tu, ukikubali akuongoze ndo utaharibikiwa zaidi na atakuwa akikupa masharti kama hayo, kama gari ipo panda mwachie gari yake kama asemavyo, kikiwa chako wewe chenu ila chake ni chake
 
Back
Top Bottom