Katika hili nashindwa kumuelewa mke wangu

Wadau,
Sina haja ya kuunganisha wanawake wote katika suala ninalopitia. Kwa ujumla ninaishi vizuri kabisa na mke wangu mpendwa ambaye tumeoana mwaka 2014. Tulibahatika kujenga na kuhamia nyumbani kwetu mwaka jana. Kwa bahati nzuri ambayo sasa imekuwa mbaya tulijenga urafiki na familia ya jirani na kwetu, mke wangu na dada wa nyumba ya jirani wakawa marafiki wakubwa.
Hali hii ilipelekea hata kuwa tunatoka wote asubuhi kwa gari ya mke wangu na kurudi pamoja pia muda wa jioni kwa kuwa wote tunafanya kazi katika maeneo jirani. Sasa mke wangu mpenzi amejifungua na sasa yupo ''maternity leave''. Jumatatu ikabidi nitoke mwenyewe na dada wa jirani ambaye huwa tunampa lift asubuhi na jioni. Sasa niliporudi usiku huo wa jumatatu wife akaniambia hataki nimpe lift tena dada wa jirani, nikauliza kwa nini? Akajibu hataki tu; niliwaza usiku ule na kuamua kuendelea kumpa lift huyu dada kwa kuwa wazo la kumpa lift lilikuwa la wife mwenyewe na kwangu ni ngumu sana kumpita huyu dada ambaye ameshazoea kuwa anapanda gari hii ukizingatia kuwa ni wife mwenyewe aliyemkaribisha. Nilipoamka jumanne nikamkuta huyu dada ananisubiri nje, nikampa lift kama kawaida na jioni pia nikarudi naye nyumbani pamoja.
Sasa mke wangu baada ya kuona hivyo, usiku wa jumanne akaniambia nikubali moja, kuendesha gari yake bila kumpa lift dada wa jirani au niende kazini kwa gari ya staff?! Hii kauli ya kutamka kuwa gari ni yake ilinipa mawazo sana kwa kuwa mke wangu huyu mpendwa hajawahi kuwa mtu anayeonyesha ubinafsi, tumekuwa na ndoa nzuri yenye amani na upendo wa hali juu.
Ndipo nikauliza ana tatizo gani na huyu dada? bado alinijibu kuwa hataki tu.
Nikampigia simu dereva wa staff bus kuwa anipitie asubuhi, na kuwakuwa basi huwa halijai kwa kuwa staff tunaoishi huko ni wachache na huyu dada alikuwa nje muda basi lilipofika kunichukua naye pia akapanda kwenye staff bus.
Niliporudi home wife amenuna na hataki kuongea, nashindwa kuelewa tatizo lake kwa huyu dada ni nini hasa?
Kiukweli naishi maisha yenye kuheshimu ndoa na kumpenda mke wangu kwa kiwango cha juu kabisa.

Waungwana, kama hivi ndivyo wanawake wanavyoweza kuwa na maamuzi yasio na chembe ya aibu napata shida sana kumuelewa mke wangu.
Ungemrudishia Mpira mwenyewe kuwa akamwambia kuanzia sasa haitaji kumuona anapanda gari yake badala ya kukuangushia jumba bovu wewe.
 
Ndo vizuri sasa haoni kama wife anakupenda sana maana anajua ni ngumu sisi wanaume kukwepa majaribu kama hayo cha msingi u one namna gani hautawagombanisha na huyo mdada kama vipi kubali gari la staff
Mimi binafsi naona wife yuko sahihi sana na wala Hakuna matata wewe tu hapo jiongeze ni vipi utafanya wife aridhike na hasa kipindi HICHI ambacho sisi sote tunakupa hongera kwa kupata mtoto
Hongera sana
 
Katika mazingira kama haya, be on your wife's side.

Ila issue ya kumwambia, aifanye mwenyewe. Unaweza ukamwambia wewe baada ya miezi miwili urafiki wao ukarudi na hatimaye ukaonekana mtu mbaya kabisa
 
ahsante kwa kisa chako, japo uhitaji msaada, lakini jua kuwa mwanamke iwe vyovyote uyazoee haya:
-nyumba yangu,
- gari yangu
- watoto wangu
- wangu
- wangu, kila kitu changu ni changu,
usiumie kichwa ndio wake zetu hao
Pia jaribu kuelewa kuwa mkeo anaposema "nimeamua tu" ujue ana maanisha.....
 
Wadau,
Sina haja ya kuunganisha wanawake wote katika suala ninalopitia. Kwa ujumla ninaishi vizuri kabisa na mke wangu mpendwa ambaye tumeoana mwaka 2014. Tulibahatika kujenga na kuhamia nyumbani kwetu mwaka jana. Kwa bahati nzuri ambayo sasa imekuwa mbaya tulijenga urafiki na familia ya jirani na kwetu, mke wangu na dada wa nyumba ya jirani wakawa marafiki wakubwa.
Hali hii ilipelekea hata kuwa tunatoka wote asubuhi kwa gari ya mke wangu na kurudi pamoja pia muda wa jioni kwa kuwa wote tunafanya kazi katika maeneo jirani. Sasa mke wangu mpenzi amejifungua na sasa yupo ''maternity leave''. Jumatatu ikabidi nitoke mwenyewe na dada wa jirani ambaye huwa tunampa lift asubuhi na jioni. Sasa niliporudi usiku huo wa jumatatu wife akaniambia hataki nimpe lift tena dada wa jirani, nikauliza kwa nini? Akajibu hataki tu; niliwaza usiku ule na kuamua kuendelea kumpa lift huyu dada kwa kuwa wazo la kumpa lift lilikuwa la wife mwenyewe na kwangu ni ngumu sana kumpita huyu dada ambaye ameshazoea kuwa anapanda gari hii ukizingatia kuwa ni wife mwenyewe aliyemkaribisha. Nilipoamka jumanne nikamkuta huyu dada ananisubiri nje, nikampa lift kama kawaida na jioni pia nikarudi naye nyumbani pamoja.
Sasa mke wangu baada ya kuona hivyo, usiku wa jumanne akaniambia nikubali moja, kuendesha gari yake bila kumpa lift dada wa jirani au niende kazini kwa gari ya staff?! Hii kauli ya kutamka kuwa gari ni yake ilinipa mawazo sana kwa kuwa mke wangu huyu mpendwa hajawahi kuwa mtu anayeonyesha ubinafsi, tumekuwa na ndoa nzuri yenye amani na upendo wa hali juu.
Ndipo nikauliza ana tatizo gani na huyu dada? bado alinijibu kuwa hataki tu.
Nikampigia simu dereva wa staff bus kuwa anipitie asubuhi, na kuwakuwa basi huwa halijai kwa kuwa staff tunaoishi huko ni wachache na huyu dada alikuwa nje muda basi lilipofika kunichukua naye pia akapanda kwenye staff bus.
Niliporudi home wife amenuna na hataki kuongea, nashindwa kuelewa tatizo lake kwa huyu dada ni nini hasa?
Kiukweli naishi maisha yenye kuheshimu ndoa na kumpenda mke wangu kwa kiwango cha juu kabisa.

Waungwana, kama hivi ndivyo wanawake wanavyoweza kuwa na maamuzi yasio na chembe ya aibu napata shida sana kumuelewa mke wangu.

"hataki tu" sio kweli jiongeze hapo kwanza hali yake lazima awe na hasira,pia anahisi utachepuka na jirani hivo anaogopa na hawezi sema direct hiyo sababu anaogopa utammaindi kwa kukugrade hivo au kukuona hivo wkati wazo lake,....hivo mbane aseme sababu ila usimbane sana ...af utaona hawezi nyoosha maelezo......muambie usiponipa sababu itakuwa ngumu kuacha ghafla......ukitamka ya unahisi ntacheouka atapata gia ya kukubana kuwa ndio ulichokuwa unalenga...we kumbuka akili za mwnamke siku zote ni ovy kwenye mapenz au mahusiano hafikirii ye anafaya tuu sau kuamua tuu basi tu ilimradi
mtu wa kisirani, pia ni wivu tayari anaona kamaukienda mtaenda kuchepuka...hanaogopa kukuambia direct kuwa anahisi tamsaiti ndio maana anasema hataki tu.....taki tu."
"hataki tu."
 
Brother this thing called womens acha kabisa!
Dk 2 mbele kisirani from no where na ndio matatizo yanapoanziaga
Sijajua kwanini hataki ila labda hajiamini baada ya kuzaa anadhani feelings zitaanza kuhamia kwa jirani, ila vema umueleweshe tu vizuri na mpe assurance ya usalama wa ndoa yake!
 
Hekima, Ujenga Nyumba. Heri Mtu Yule Ajaaye Hekima Kichwani Pake. Mtu Huyo Atakuwa Kama Mwangaza Uzukao Asubui. Chemi Chemi za Uzima Zita Bubujika Kinywani Mwake Siku Zote. Na Siku Zote Hata Amua Jambo Kwa Gadhabu, Bali Hekima yake Itakuwa Lulu Juu ya Maamuzi yenye Busara na Adili.

Tafakari. Mithali Hii na Umwombe Mungu Akuruzukie Hekima yake, itakayo Kupa Maarifa ya Kuishi na Sweet, Wako kwa Amani Ndugu.
 
Mkeo hakutendei Haki, katika dunia ya leo mtu humkatazi kufanya jambo bali unampa sababu ya kutokufanya jambo.

Hata mimi ningesita kufanya anavyotaka mkeo maana kabla ya kuchukua hatua/maamuzi ni vizuri ukawa na taarifa sahihi ili uwe ktk nafasi nzuri ya kufanya maamuzi sahihi.

Muombe akupe sababu na kama inawezekana anzisha "udukuzi" kwa huyo dada huenda Kuna jambo analijua juu ya mkeo na mkeo hataki ujue.
 
unataka kukosana na mkeo kisa dem wa jirani?? shame on you chief,
haitaji kukupa sababu kwa sababu si lazima huyo dada kutumia asset zenu ikiwemo gari
 
Mkeo hakutendei Haki, katika dunia ya leo mtu humkatazi kufanya jambo bali unampa sababu ya kutokufanya jambo.

Hata mimi ningesita kufanya anavyotaka mkeo maana kabla ya kuchukua hatua/maamuzi ni vizuri ukawa na taarifa sahihi ili uwe ktk nafasi nzuri ya kufanya maamuzi sahihi.

Muombe akupe sababu na kama inawezekana anzisha "udukuzi" kwa huyo dada huenda Kuna jambo analijua juu ya mkeo na mkeo hataki ujue.

Umewaza vile ambavyo nilikua nawaza yawezekana mkeo kuna kitu anakuficha
 
Inawezekana huyo Jirani anajua mambo mengi ya mkeo Kwahiyo kitendo cha kuwa nae karibu bila yeye kuwepo anaweza kutoboa hiyo Siri!
Mwambie yeye akamwambie huyo shoga yake kuwa hatakiwi kupanda hiyo gari asikuchumie dhambi na Chuki Kwa Kigezo cha mke!

Au ikibidi mwambie huyo Jirani kuwa mkeo hataki upande nae gari......utashangaa utakayosikia....
 
Endelea kutumia gari la staff mpaka either amalize martenity au yeye mwenyewe amweleze huyo dada kuliona gari lake kama defender la polisi.
 
Mi mazoea hayo ili iwejee,mi sitaki mwanamke yeyote awe na mazoea hayo,nae mpewa lifti hata hajiongezi kageuza gari la kwao ,mazoea gani hayo ya kua na mme wangu karibu vile ,namshangaa mke wako kumzoesha kumpa lifti mi hata lifti asingepata angeipata nikiwa ndani ya gari peke yangu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom