Katika hili nashindwa kumuelewa mke wangu

JIRANI NAE MBISHI KHAAA KAMA KAAMBIWA FAMILY CAR NI YA STAFF,,SIKU MOJA AJIONGEZE TU NA DALADALA
 
Wadau,
Sina haja ya kuunganisha wanawake wote katika suala ninalopitia. Kwa ujumla ninaishi vizuri kabisa na mke wangu mpendwa ambaye tumeoana mwaka 2014. Tulibahatika kujenga na kuhamia nyumbani kwetu mwaka jana. Kwa bahati nzuri ambayo sasa imekuwa mbaya tulijenga urafiki na familia ya jirani na kwetu, mke wangu na dada wa nyumba ya jirani wakawa marafiki wakubwa.
Hali hii ilipelekea hata kuwa tunatoka wote asubuhi kwa gari ya mke wangu na kurudi pamoja pia muda wa jioni kwa kuwa wote tunafanya kazi katika maeneo jirani. Sasa mke wangu mpenzi amejifungua na sasa yupo ''maternity leave''. Jumatatu ikabidi nitoke mwenyewe na dada wa jirani ambaye huwa tunampa lift asubuhi na jioni. Sasa niliporudi usiku huo wa jumatatu wife akaniambia hataki nimpe lift tena dada wa jirani, nikauliza kwa nini? Akajibu hataki tu; niliwaza usiku ule na kuamua kuendelea kumpa lift huyu dada kwa kuwa wazo la kumpa lift lilikuwa la wife mwenyewe na kwangu ni ngumu sana kumpita huyu dada ambaye ameshazoea kuwa anapanda gari hii ukizingatia kuwa ni wife mwenyewe aliyemkaribisha. Nilipoamka jumanne nikamkuta huyu dada ananisubiri nje, nikampa lift kama kawaida na jioni pia nikarudi naye nyumbani pamoja.
Sasa mke wangu baada ya kuona hivyo, usiku wa jumanne akaniambia nikubali moja, kuendesha gari yake bila kumpa lift dada wa jirani au niende kazini kwa gari ya staff?! Hii kauli ya kutamka kuwa gari ni yake ilinipa mawazo sana kwa kuwa mke wangu huyu mpendwa hajawahi kuwa mtu anayeonyesha ubinafsi, tumekuwa na ndoa nzuri yenye amani na upendo wa hali juu.
Ndipo nikauliza ana tatizo gani na huyu dada? bado alinijibu kuwa hataki tu.
Nikampigia simu dereva wa staff bus kuwa anipitie asubuhi, na kuwakuwa basi huwa halijai kwa kuwa staff tunaoishi huko ni wachache na huyu dada alikuwa nje muda basi lilipofika kunichukua naye pia akapanda kwenye staff bus.
Niliporudi home wife amenuna na hataki kuongea, nashindwa kuelewa tatizo lake kwa huyu dada ni nini hasa?
Kiukweli naishi maisha yenye kuheshimu ndoa na kumpenda mke wangu kwa kiwango cha juu kabisa.

Waungwana, kama hivi ndivyo wanawake wanavyoweza kuwa na maamuzi yasio na chembe ya aibu napata shida sana kumuelewa mke wangu.
KWAN KUNA TATIZO GANI UKIMSIKILIZA MKEO ???,,MLIAPA WEWE NA MKEO KTK NDOA YENU NA SII WEWE NA JIRANI,,THINK TWICE BRO

JIFANYE UNAMTETEA JIRANI WAKAT HUO HUO UNACHOCHEA KUNI KTK NDOA YAKO,,,,,HAKUNA URAFIKI KAT YA ME NA KE

MKEI ANAJUA UFUSKA UNAOFANYIKA KTK MAGARI IPO SIKU MTAJIKUTA MNAMALIZANA NA JIRANI KTK GARI

MSIKILIZE MKEO AKWAMBIACHO VINGINEVYO PANDA STAFF BUS KWA KULINDA NDOA YAKO ILIYO CHANGA NA MTOTO WAKO
 
Huyu kaka nae ni wakushangaza, ameamua kupanda staff bus bado tena anamkaribisha na jirani kwenye gari ya office.Kifupi hataki tena dada jirani asumbuke na swala la usafiri.

Kuna watu hawanaga aibu mmojawapo dada jirani.Hivi awezi ona aibu siku zingine akawa anaondoka mapema awai daladala na kuacha gari la watu.
WISE WORDS JIRAN MBISHI ANATAKA KUVUNJA NDOA YA MTU, BY THE WAY WANAWAKE WANAJUANA KWA NYAKU NYAKU, MKE YUKO SAHIHI

TAHADHARI NI MUHIMU
 
Katika mazingira kama haya, be on your wife's side.

Ila issue ya kumwambia, aifanye mwenyewe e. Unaweza ukamwambia wewe baada ya miezi miwili urafiki wao ukarudi na hatimaye ukaonekana mtu mbaya kabisa
Uko right mke angetakiwa ampigie rafiki yake simu kwamba kuanzia leo usipande gari yetu. Pili kwa nini mke ghafla gari imekuwa yake peke yake? Je na mume akidai nyumba kama ametoa pesa yeye?
 
Naomba nikuulize Mkuu,Ivi kweli kama ingekua ni wewe ungekubali mkeo apande gari ya rafiki yako wakati wewe uko nyumbani na ukawa na amani kabisaa? au huna wivu na chako? isitoshe huyo ni mwanamke na wanawake wana 7senses sio SIX lol huenda amehisi kitu au amesikia kitu,sasa unasusia gari kisa unataka kumpa lift Jarani tena mwanamke,mie namuelewa na hasa wewe mwanamme ndio ungesema mwambie shogako
sitompa lift mpaka utakapokua wewe kwenye gari full stop...
Issue ni kwamba huyo mke angemuita huyo rafiki yake na kumuambia ukweli kwamba bwanaa wee mi ndiyo hivi tena hivyo siwezi kukuruhusu na mume wangu nikiwa sipo maana lolote laweza kutokea, tena ahakikishe akimwambia hayo na mumewe yupo , aweke na utani kidogo but msg itakuwa imemfikia. Lakini hili la kumzushia mwenzio zigo la lawama na kujenga uadui ghafla, tena na majirani siyo sawa.
 
Thanks man,

wazo zuri nitalifanyia kazi
Mbona kitu kidogo sana, usifanye ligi, tafuta namna ya kumkwepa huyo dada kiaina. Anza kupanda daladala atakuwa na amani nawe. Kumbuka mkeo kwa sasa ananyonyesha, sio vizuri akanyonyesha huku anamihasira.
 
Mi nashauri omba ruhusa kama siku tatu hivi ofisini ili ubaki nyumbani. Katika siku hizo kaeni kimya jirani atasubiri weee mpaka achoke. Akioni hutoki atapiga simu au ataamua kuondoka. Na siku ya pili hivyo na siku ya tatu hivyo. Baada ya hapo panda daladala kama siku tatu hivi kimyakimya bila kumtaarifu jirani. Kifupi, jiweke mbali na jirani ila salaam ni muhim, afanye mazoea kwa mkeo sio kwako. Baada ya hapo natumaini jirani ataanza kujiongeza kwenda kazini sio lazima asubiri gari lenu au basi la ofisi
 
Uko right mke angetakiwa ampigie rafiki yake simu kwamba kuanzia leo usipande gari yetu. Pili kwa nini mke ghafla gari imekuwa yake peke yake? Je na mume akidai nyumba kama ametoa pesa yeye?

Hilo ni la muhimu, mke afanye mwenyewe kwa maana ni rafiki yake. Hili la pili inaweza kuwa kwa sababu ya hasira japo hatuwezi jua inawezejana ka-ubinafsi kameanza kuchipuka
 
Wadau,
Sina haja ya kuunganisha wanawake wote katika suala ninalopitia. Kwa ujumla ninaishi vizuri kabisa na mke wangu mpendwa ambaye tumeoana mwaka 2014. Tulibahatika kujenga na kuhamia nyumbani kwetu mwaka jana. Kwa bahati nzuri ambayo sasa imekuwa mbaya tulijenga urafiki na familia ya jirani na kwetu, mke wangu na dada wa nyumba ya jirani wakawa marafiki wakubwa.
Hali hii ilipelekea hata kuwa tunatoka wote asubuhi kwa gari ya mke wangu na kurudi pamoja pia muda wa jioni kwa kuwa wote tunafanya kazi katika maeneo jirani. Sasa mke wangu mpenzi amejifungua na sasa yupo ''maternity leave''. Jumatatu ikabidi nitoke mwenyewe na dada wa jirani ambaye huwa tunampa lift asubuhi na jioni. Sasa niliporudi usiku huo wa jumatatu wife akaniambia hataki nimpe lift tena dada wa jirani, nikauliza kwa nini? Akajibu hataki tu; niliwaza usiku ule na kuamua kuendelea kumpa lift huyu dada kwa kuwa wazo la kumpa lift lilikuwa la wife mwenyewe na kwangu ni ngumu sana kumpita huyu dada ambaye ameshazoea kuwa anapanda gari hii ukizingatia kuwa ni wife mwenyewe aliyemkaribisha. Nilipoamka jumanne nikamkuta huyu dada ananisubiri nje, nikampa lift kama kawaida na jioni pia nikarudi naye nyumbani pamoja.
Sasa mke wangu baada ya kuona hivyo, usiku wa jumanne akaniambia nikubali moja, kuendesha gari yake bila kumpa lift dada wa jirani au niende kazini kwa gari ya staff?! Hii kauli ya kutamka kuwa gari ni yake ilinipa mawazo sana kwa kuwa mke wangu huyu mpendwa hajawahi kuwa mtu anayeonyesha ubinafsi, tumekuwa na ndoa nzuri yenye amani na upendo wa hali juu.
Ndipo nikauliza ana tatizo gani na huyu dada? bado alinijibu kuwa hataki tu.
Nikampigia simu dereva wa staff bus kuwa anipitie asubuhi, na kuwakuwa basi huwa halijai kwa kuwa staff tunaoishi huko ni wachache na huyu dada alikuwa nje muda basi lilipofika kunichukua naye pia akapanda kwenye staff bus.
Niliporudi home wife amenuna na hataki kuongea, nashindwa kuelewa tatizo lake kwa huyu dada ni nini hasa?
Kiukweli naishi maisha yenye kuheshimu ndoa na kumpenda mke wangu kwa kiwango cha juu kabisa.

Waungwana, kama hivi ndivyo wanawake wanavyoweza kuwa na maamuzi yasio na chembe ya aibu napata shida sana kumuelewa mke wangu.
Usitake ugomvi na mkeo.... wewe damka mapema kabla ya huyo dada wa jirani wala usitumie gar ya mkeo tena....Kapandie staff bas mbali na kwao......!Binadamu tuna visiran vya ajabu sana...!
 
Kk mwambie yeye ndo amzuie huyo dada kama huwezi basi mweleze tu live...its ur call
 
Hakuna namna baki kwenye uamuz wa mke wako kwan huyo ni rafiki yake yy cyo ww sasa sioni shda huwez jua pengine Kuna vitu anavijua kuhusu huyo mwanamke ndyo maana anakuepusha naye
 
Wadau,
Sina haja ya kuunganisha wanawake wote katika suala ninalopitia. Kwa ujumla ninaishi vizuri kabisa na mke wangu mpendwa ambaye tumeoana mwaka 2014. Tulibahatika kujenga na kuhamia nyumbani kwetu mwaka jana. Kwa bahati nzuri ambayo sasa imekuwa mbaya tulijenga urafiki na familia ya jirani na kwetu, mke wangu na dada wa nyumba ya jirani wakawa marafiki wakubwa.
Hali hii ilipelekea hata kuwa tunatoka wote asubuhi kwa gari ya mke wangu na kurudi pamoja pia muda wa jioni kwa kuwa wote tunafanya kazi katika maeneo jirani. Sasa mke wangu mpenzi amejifungua na sasa yupo ''maternity leave''. Jumatatu ikabidi nitoke mwenyewe na dada wa jirani ambaye huwa tunampa lift asubuhi na jioni. Sasa niliporudi usiku huo wa jumatatu wife akaniambia hataki nimpe lift tena dada wa jirani, nikauliza kwa nini? Akajibu hataki tu; niliwaza usiku ule na kuamua kuendelea kumpa lift huyu dada kwa kuwa wazo la kumpa lift lilikuwa la wife mwenyewe na kwangu ni ngumu sana kumpita huyu dada ambaye ameshazoea kuwa anapanda gari hii ukizingatia kuwa ni wife mwenyewe aliyemkaribisha. Nilipoamka jumanne nikamkuta huyu dada ananisubiri nje, nikampa lift kama kawaida na jioni pia nikarudi naye nyumbani pamoja.
Sasa mke wangu baada ya kuona hivyo, usiku wa jumanne akaniambia nikubali moja, kuendesha gari yake bila kumpa lift dada wa jirani au niende kazini kwa gari ya staff?! Hii kauli ya kutamka kuwa gari ni yake ilinipa mawazo sana kwa kuwa mke wangu huyu mpendwa hajawahi kuwa mtu anayeonyesha ubinafsi, tumekuwa na ndoa nzuri yenye amani na upendo wa hali juu.
Ndipo nikauliza ana tatizo gani na huyu dada? bado alinijibu kuwa hataki tu.
Nikampigia simu dereva wa staff bus kuwa anipitie asubuhi, na kuwakuwa basi huwa halijai kwa kuwa staff tunaoishi huko ni wachache na huyu dada alikuwa nje muda basi lilipofika kunichukua naye pia akapanda kwenye staff bus.
Niliporudi home wife amenuna na hataki kuongea, nashindwa kuelewa tatizo lake kwa huyu dada ni nini hasa?
Kiukweli naishi maisha yenye kuheshimu ndoa na kumpenda mke wangu kwa kiwango cha juu kabisa.

Waungwana, kama hivi ndivyo wanawake wanavyoweza kuwa na maamuzi yasio na chembe ya aibu napata shida sana kumuelewa mke wangu.
Mi nahisi umeshindwa tu kumsoma mkeo yeye anachomaanisha hapo ni kwamba hataki wewe ba huyo dada muwe pamoja peke yenu vishawishi vingi na huyo jirani nae hana adabu ningekuwa mimi kama upo peke yako mkeo hayupo hiyo lifti ni mwiko sipandi na yeye anashindwa kujiongeza maana kuna wadada wengine full mitego ya maksudi kabisaaa kwa waume za watu unajiona umevaa kimino halafu bado utajikalisha siti ya mbele msikilize mkeo she is just jealous lakini hataki kusema moja kwa moja tena as u said ametoka kujifungua I think that's the time most women wanakua insecure na how they look kama kanenepa etc so wewe msikilize mkeo tu hamna namna
 
Wadau,
Sina haja ya kuunganisha wanawake wote katika suala ninalopitia. Kwa ujumla ninaishi vizuri kabisa na mke wangu mpendwa ambaye tumeoana mwaka 2014. Tulibahatika kujenga na kuhamia nyumbani kwetu mwaka jana. Kwa bahati nzuri ambayo sasa imekuwa mbaya tulijenga urafiki na familia ya jirani na kwetu, mke wangu na dada wa nyumba ya jirani wakawa marafiki wakubwa.
Hali hii ilipelekea hata kuwa tunatoka wote asubuhi kwa gari ya mke wangu na kurudi pamoja pia muda wa jioni kwa kuwa wote tunafanya kazi katika maeneo jirani. Sasa mke wangu mpenzi amejifungua na sasa yupo ''maternity leave''. Jumatatu ikabidi nitoke mwenyewe na dada wa jirani ambaye huwa tunampa lift asubuhi na jioni. Sasa niliporudi usiku huo wa jumatatu wife akaniambia hataki nimpe lift tena dada wa jirani, nikauliza kwa nini? Akajibu hataki tu; niliwaza usiku ule na kuamua kuendelea kumpa lift huyu dada kwa kuwa wazo la kumpa lift lilikuwa la wife mwenyewe na kwangu ni ngumu sana kumpita huyu dada ambaye ameshazoea kuwa anapanda gari hii ukizingatia kuwa ni wife mwenyewe aliyemkaribisha. Nilipoamka jumanne nikamkuta huyu dada ananisubiri nje, nikampa lift kama kawaida na jioni pia nikarudi naye nyumbani pamoja.
Sasa mke wangu baada ya kuona hivyo, usiku wa jumanne akaniambia nikubali moja, kuendesha gari yake bila kumpa lift dada wa jirani au niende kazini kwa gari ya staff?! Hii kauli ya kutamka kuwa gari ni yake ilinipa mawazo sana kwa kuwa mke wangu huyu mpendwa hajawahi kuwa mtu anayeonyesha ubinafsi, tumekuwa na ndoa nzuri yenye amani na upendo wa hali juu.
Ndipo nikauliza ana tatizo gani na huyu dada? bado alinijibu kuwa hataki tu.
Nikampigia simu dereva wa staff bus kuwa anipitie asubuhi, na kuwakuwa basi huwa halijai kwa kuwa staff tunaoishi huko ni wachache na huyu dada alikuwa nje muda basi lilipofika kunichukua naye pia akapanda kwenye staff bus.
Niliporudi home wife amenuna na hataki kuongea, nashindwa kuelewa tatizo lake kwa huyu dada ni nini hasa?
Kiukweli naishi maisha yenye kuheshimu ndoa na kumpenda mke wangu kwa kiwango cha juu kabisa.

Waungwana, kama hivi ndivyo wanawake wanavyoweza kuwa na maamuzi yasio na chembe ya aibu napata shida sana kumuelewa mke wangu.
Ndugu acha kukoma msikilize mkeo kwa manufa ya ndoa yako huyo jirani asiwe sababu ya ndoa yako kupata doa panda gari la staff utakuwa umetengana na huyo jirani usiwe mbishi nyenyekea kwa maslahi ya ndoa yako
 
Mkuu kwanza hongera kwa kupata mtoto na mke ambaye manaishi kwa kuheshimiana,
Mkuu maswala mengine lazima usimame kama mwanaume swala la mkeo kutaka wewe kutompa lift mtu ambaye yeye ni rafiki yake litakuwa kuvunja urafiki wao,.. kama anataka amwite na amweleze hilo swala peke yake.
My take home with you endelea kupanda staff bus, itasaidia kuonyesha msimamo wako kama mwanaume na pia kumbuka kuendesha gari ni garama nitumie hiyo chance Ku save money kwa ajilo ya mtoto wetu..
 
mwenye matatizo kumbe ni wewe. Unashindwa vp kumwambia huyo jirani ili ulinde ndoa yako? W/wake wakiwa wajawazito wanakuwa na matatizo ya kisaikolojia ukimweleza hivyo jirani atakuelewa tu

Usimdharau mkeo (tena mjamzito) kwa ajili ya wapita njia bana hebu jiongeze kidogo hao majirani achana nao hata kama mkeo ndio alikutambulisha. Pia kuna msemo usimdharau mkeo kabla hujachimbiwa kaburi. Hilo suala la kusema gari lake ni hasira tu za kipindi cha ujauzito mtembelee mtu mzima atakueleza vizuri kipindi hiki uwe karibu sana na mkeo usimsumbue kisaikolojia. Karibu sana kwenye maisha ya ndoa
 
Hapo sasa nini ambacho humuelewi mkeo? Yaani hapo kila kitu kipo wazi, anafanya hivyo kulinda ndoa yake, sema tu labda style anayo tumia ndio sio ya hekima , kwani angeweza kukuchana live tu kwanini hataki uambatane na huyo dada jirani kila wakati , kwani mahusiano ya mapenzi yanaanzaga kimazoea zoea na watu hivyo na kwakua mkeo ni mzazi hivyo anajua pengine utapooza hamu kwa dada .
 
we ulitaka awe na aibu gani ktk maamuzi hayo! ndoa ngapi zimeingiliwa kwa sababu ya mazingira kama haya....we kama bado wataka kumpa lifti huyo dada basi ongea nae ukweli ili awe anatangulia unaenda kumchukua kwa mbele. au vinginevyo acha tu kumpa lifti,
 
Mkuu hongereni kwa kupata mtoto. Nakubaliana na mkeo, acha kumpa lift mwanamke mwingine tena asubuhi na jioni. Jamani tusiwe vipofu ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu ya marafiki dizaini hii. Mwanzo anakuwa rafiki mzuri lakin anakuja kugeuka shetani aliyekubuhu. Hivi unaona shida gani kuacha kumpa lift huyo dada? Ni kwa sabubu tu ya ujirani ama na vihisia fulani vimeanza kukunyemelea. Yaani hadi gari la ofsi nalo anapanda bila haya?!!! Hata kama gari lingekuwa lako na sio la mkeo, bado mkeo anahaki kumzuia huyo jirani. Nina uhakika kauli ya kwamba gari ni lake ilikuja kwa sababu ya hasira, itakuwa ulikuwa unabisha kwamba lazima umpe lift jirani ndo maana mkeo akatamka kwa hasira. Ni kama vile alitaka kukwambia kama unampenda sana huyo jirani basi mpakize kwenye gari lako sio alilotolea jasho yeye. Nakubaliana na wadau walioshauri kuanza kuondoka home mapema kabla huyo jiran yako hajatoka ndani kama unaona aibu kumwambia. Ndoa yako ni muhimu kuliko huyo jirani mkuu. Na huyo jirani naye hana mme kwanini awe nuksi kwenye ndoa za watu? Kama mkeo amenunua gari kwanini huyo jirani naye asinunue yake, hawez basi apande daladala. Itakuwa ajabu kama utaendelea kununiana na mkeo aliyekuzalia kichanga tu hivi punde, eti unaogopa kumuudhi jirani!!!!!
 
Back
Top Bottom