Katika hili nashindwa kumuelewa mke wangu

Katika hili nashindwa kumuelewa mke wangu

Panda gari ya staff ili umpe ahueni mkeo maana ukilazimisha haitapendeza ukizingatia ananyonyesha.
 
Yeye kuwa mtoa wazo si ishu kwakuwa nae pia alikuwamo ndani ya izo safari(asubuh,jioni)....ivi sasa Ni lazima usimpe lift kwakuwa hayupo kwenye nenda rudi zenu,.
ushari ni wewe kutompa lift kwa kutomwambia chochote huyo bint,mpite tu siku ya kwanza ya pili,...ataelewa tu.maana ukisema ususe kutotumia gari la family itakuwa umeleta picha mpya kwa mkeo.
 
Tumia gari ya wife kila siku ondoka saa kumi usiku na kurudi saa 5 usiku.
Ukifanya hivyo week moja mdada atajiongeza...duuh mdada nae kabadili lift kuwa sehem ya maisha yake
 
Hapo kazi ipo. Maana mazoea ambayo mliyatengeneza na huyo dada ni ngumu kuanza kumuacha. Ila inabid ufike mahali uamue kati ya kumsikiliza mkeo au kuendelea kumbeba huyo dada
 
Pia mkuu komaa ununue gari lako uwe complete kichwa cha familia...haya masuala ya kujifanya mwili mmoja mnakaa chini mnapanga bajeti afu mke anasema hela yako baby tumalizie paa la nyumba hii ya kwangu ninunue gari itusevu usafiri...hakikisha siku zote ww unaanza ..
Hahaaaa kidding for lovers
 
Na huyo dada kwa nini nae anasubiri subiri lifti ya mume wa mtu? Na wewe mume wa mtu, mkeo ameshasema hataki unachongangania nini?
 
Wadau,
Sina haja ya kuunganisha wanawake wote katika suala ninalopitia. Kwa ujumla ninaishi vizuri kabisa na mke wangu mpendwa ambaye tumeoana mwaka 2014. Tulibahatika kujenga na kuhamia nyumbani kwetu mwaka jana. Kwa bahati nzuri ambayo sasa imekuwa mbaya tulijenga urafiki na familia ya jirani na kwetu, mke wangu na dada wa nyumba ya jirani wakawa marafiki wakubwa.
Hali hii ilipelekea hata kuwa tunatoka wote asubuhi kwa gari ya mke wangu na kurudi pamoja pia muda wa jioni kwa kuwa wote tunafanya kazi katika maeneo jirani. Sasa mke wangu mpenzi amejifungua na sasa yupo ''maternity leave''. Jumatatu ikabidi nitoke mwenyewe na dada wa jirani ambaye huwa tunampa lift asubuhi na jioni. Sasa niliporudi usiku huo wa jumatatu wife akaniambia hataki nimpe lift tena dada wa jirani, nikauliza kwa nini? Akajibu hataki tu; niliwaza usiku ule na kuamua kuendelea kumpa lift huyu dada kwa kuwa wazo la kumpa lift lilikuwa la wife mwenyewe na kwangu ni ngumu sana kumpita huyu dada ambaye ameshazoea kuwa anapanda gari hii ukizingatia kuwa ni wife mwenyewe aliyemkaribisha. Nilipoamka jumanne nikamkuta huyu dada ananisubiri nje, nikampa lift kama kawaida na jioni pia nikarudi naye nyumbani pamoja.
Sasa mke wangu baada ya kuona hivyo, usiku wa jumanne akaniambia nikubali moja, kuendesha gari yake bila kumpa lift dada wa jirani au niende kazini kwa gari ya staff?! Hii kauli ya kutamka kuwa gari ni yake ilinipa mawazo sana kwa kuwa mke wangu huyu mpendwa hajawahi kuwa mtu anayeonyesha ubinafsi, tumekuwa na ndoa nzuri yenye amani na upendo wa hali juu.
Ndipo nikauliza ana tatizo gani na huyu dada? bado alinijibu kuwa hataki tu.
Nikampigia simu dereva wa staff bus kuwa anipitie asubuhi, na kuwakuwa basi huwa halijai kwa kuwa staff tunaoishi huko ni wachache na huyu dada alikuwa nje muda basi lilipofika kunichukua naye pia akapanda kwenye staff bus.
Niliporudi home wife amenuna na hataki kuongea, nashindwa kuelewa tatizo lake kwa huyu dada ni nini hasa?
Kiukweli naishi maisha yenye kuheshimu ndoa na kumpenda mke wangu kwa kiwango cha juu kabisa.

Waungwana, kama hivi ndivyo wanawake wanavyoweza kuwa na maamuzi yasio na chembe ya aibu napata shida sana kumuelewa mke wangu.
Kajifungua sasa anaogopa kipind cha kumsubiria had akae sawa ndio akupatie haki yako ya Ndoa unaweza chepuka hakuna kingine hapo. Nenda kamuulize halafu utaleta mrejesho hapa hana kingine huyo
 
Reading between the lines...... ni HIVI

Issue kubwa hapa sio kwamba unataka kukaidi ushauri wa mke wako bali unakataka wife ambaye ndiye alianza kumkaribisha mdada lift ndio atoe agizo la kumpiga stop.

SULUHISHO: Kwa vyovyote vile usimwambie binti kuwa kuanzia leo wife kasema nisikupe lift. Majirani huwa hawafanyi hivyo. Cha kufanya ni kutumia diplomasia. Kwa sababu una usafiri mbadala wa kwenda ofisini. Basi tumia huo. Tizama hili katika hali chanya zaidi. Utakuwa unasave gharama za mafuta na vile vile utakuwa umempa ahueni mke wako. Ndoa wakati mwingine nikuchukuliana na kubebeana ubaya lakini kubebeana huko kusizidi uwezo.

DIPLOMASIA: Mwambie yule dada kuanzia sasa utakuwa unapanda gari la ofisini kwa sababu mke wako ambaye ni mzazi anaweza kupata dharura na akataka kulitumia gari.

ANGALIZO: Kwa sababu umeshajenga nyumba ni muda mwafaka sasa ukajitahidi kununua kausafiri kako ili usipate matatizo kama haya.
 
mkuu pole,ila wanawake mara nyingi huwa hawatabariki na wakati mwingine inakuhitaji akili ya ziada ili kufinika kombe mwanaharam apite.
mosi, mwambie mkeo hilo la lift amwambie yeye huyo jirani mana yeye ndio aliekuja na wazo la kumpa lift, hivyo wazo la kutengua pia afanye yeye. asikuangushie jumba bovu.
pili, gari la mkeo (huo ndio ukweli,japo mchungu...) kwa sasa acha kulitumia . tumia usafiri wa ofisini na suala la huyo dada kupanda gari la ofisi pia sitisha na ili jumba bovu lisikuangukie mwambie dereva wa hilo gari la ofisi amwambie huyo dada kuwa anampa lift mara ya mwisho ila hairuhusiwi kupanda asie mfanyakazi.
tatu, kaa na wanawake kiakili. ukicheza kidogo tu utawagombanisha hao wanawake na ndoa utaitoa doa lakini pia uadui wa wanawake haudumu kama ulivyo urafiki wao, wanaweza kuja kurudia ushoga wao halafu ukaumbuka mtu mzima. jirani akikuuliza mwambie gari lina hitilafu....hii ni kwa sasa wakati ukisubiri mkeo atafte namna ya kumwambia.
mwisho, kuwa makini na wanawake....mali yao mara nyingi ni yao ila ya kwako ni yenu wote. kwa hiyo cheza kwa step hata kama ni mkeo wa ndoa ila tumia akili,wanawake wa kileo si sawa na mama au bibi zetu walivyokuwa.
 
Kwanza umekosea sana kupanda gari ya staff imemfanya mkeo ajihisi kama umemzarau ingawa na wewe umefanya kijeuli kumuonesha kuwa hutegemei gari yake ingawa in real sense ni yenu wote, chakufanya jirani asiharibu ndoa mweleze ukweli kama nae ni muelewa ataheshimu na jua kuwa mkeo anakupenda na anakusaidia katika kile ambacho hata wewe unaamini kiwa ni kuheshimu ndoa yako kwa kukuepusha na vishawishi.
 
ushauri wangu ni tofauti.utabase kwenye hiyo yangu, wangu,changu,usitumie tena gari lake kwenda kazini tena.hii ni hata kama ataendesha yeye baada ya kupona wewe iwe ni staff basi tu.Ni kabinafsi kama walivyo wengi wao.
 
n
Kwanza umekosea sana kupanda gari ya staff imemfanya mkeo ajihisi kama umemzarau ingawa na wewe umefanya kijeuli kumuonesha kuwa hutegemei gari yake ingawa in real sense ni yenu wote, chakufanya jirani asiharibu ndoa mweleze ukweli kama nae ni muelewa ataheshimu na jua kuwa mkeo anakupenda na anakusaidia katika kile ambacho hata wewe unaamini kiwa ni kuheshimu ndoa yako kwa kukuepusha na vishawishi.
ingelikuwa mimi hiyo gari ndio ingekuwa mwanzo na mwisho kujihusisha nayo,hakika ingekuwa basi hata nikizidiwa nibebwe na bajaji au teksi.
 
Hapo wewe ndio una tatizo kubwa kuliko mkeo. Huna nia ya kumkwepa huyo dada kwasababu unaonekana umevutika. Mkeo hataki ukaribu naye, amekupa option ya staff bus akijua utakuwa naye mbali lakini bado unampandisha kwenye hilo bus! Hebu jiongeze, wanaume tunatumia kichwa kuendesha mambo sio moyo banaa
 
Ujue wanaweza tu wakamwambia huyo mdada kuwa, kwa kuwa now mke amejifungua wanaona ni vyema gari libaki home, kwa ajili ya mtoto, mama na mizunguko yao mingine. Sasa kama dada naye ataendelea kupanda staff bus tena eeh
Huyu kaka nae ni wakushangaza, ameamua kupanda staff bus bado tena anamkaribisha na jirani kwenye gari ya office.Kifupi hataki tena dada jirani asumbuke na swala la usafiri.

Kuna watu hawanaga aibu mmojawapo dada jirani.Hivi awezi ona aibu siku zingine akawa anaondoka mapema awai daladala na kuacha gari la watu.
 
Naona ushauri ni mmoja tuu kuwa yeye ndo amuambie rafiki yake kwa kuwa hayupo basi asubiri mpaka amalize maternity yake ndio utaratibu utaendelea..
I mean yeye ndo atetee ndoa yake waziwazi
 
Wadau,
Sina haja ya kuunganisha wanawake wote katika suala ninalopitia. Kwa ujumla ninaishi vizuri kabisa na mke wangu mpendwa ambaye tumeoana mwaka 2014. Tulibahatika kujenga na kuhamia nyumbani kwetu mwaka jana. Kwa bahati nzuri ambayo sasa imekuwa mbaya tulijenga urafiki na familia ya jirani na kwetu, mke wangu na dada wa nyumba ya jirani wakawa marafiki wakubwa.
Hali hii ilipelekea hata kuwa tunatoka wote asubuhi kwa gari ya mke wangu na kurudi pamoja pia muda wa jioni kwa kuwa wote tunafanya kazi katika maeneo jirani. Sasa mke wangu mpenzi amejifungua na sasa yupo ''maternity leave''. Jumatatu ikabidi nitoke mwenyewe na dada wa jirani ambaye huwa tunampa lift asubuhi na jioni. Sasa niliporudi usiku huo wa jumatatu wife akaniambia hataki nimpe lift tena dada wa jirani, nikauliza kwa nini? Akajibu hataki tu; niliwaza usiku ule na kuamua kuendelea kumpa lift huyu dada kwa kuwa wazo la kumpa lift lilikuwa la wife mwenyewe na kwangu ni ngumu sana kumpita huyu dada ambaye ameshazoea kuwa anapanda gari hii ukizingatia kuwa ni wife mwenyewe aliyemkaribisha. Nilipoamka jumanne nikamkuta huyu dada ananisubiri nje, nikampa lift kama kawaida na jioni pia nikarudi naye nyumbani pamoja.
Sasa mke wangu baada ya kuona hivyo, usiku wa jumanne akaniambia nikubali moja, kuendesha gari yake bila kumpa lift dada wa jirani au niende kazini kwa gari ya staff?! Hii kauli ya kutamka kuwa gari ni yake ilinipa mawazo sana kwa kuwa mke wangu huyu mpendwa hajawahi kuwa mtu anayeonyesha ubinafsi, tumekuwa na ndoa nzuri yenye amani na upendo wa hali juu.
Ndipo nikauliza ana tatizo gani na huyu dada? bado alinijibu kuwa hataki tu.
Nikampigia simu dereva wa staff bus kuwa anipitie asubuhi, na kuwakuwa basi huwa halijai kwa kuwa staff tunaoishi huko ni wachache na huyu dada alikuwa nje muda basi lilipofika kunichukua naye pia akapanda kwenye staff bus.
Niliporudi home wife amenuna na hataki kuongea, nashindwa kuelewa tatizo lake kwa huyu dada ni nini hasa?
Kiukweli naishi maisha yenye kuheshimu ndoa na kumpenda mke wangu kwa kiwango cha juu kabisa.

Waungwana, kama hivi ndivyo wanawake wanavyoweza kuwa na maamuzi yasio na chembe ya aibu napata shida sana kumuelewa mke
Dada wa lift ni kutumia busara yake tu hapo. Jambo kama hilo si la kusubiri kuambiwa njia nzima na foleni hizi asubuhi na jioni kama mke na mume mnaongea nini? Kukaribisha vishawishi tu hapo. Mkeo yupo sahihi kabisa.
 
Teh sawa nyie mkichepuka chepukeni tu, ila isiwe kama na me nimekurahisishia njia ya wewe kuchepuka. Daddy hapo unaongea tu, ingekuwa ndo nyie na makofi mngetupa kwanza kabla ya maelezo. Wanawake ni watu wa hisia sana, so please ishini na sisi kwa akili
Teh teh..Na nyie muache kutoforce sasa kuchepuka...Mnamkaribisha shetani nyie wenyewe..Si hatuna Gubu kihivyo..Ukiona husband kakwambia hivyo ujue kuna vitu kashaviona ndo mana anachukua tahadhari teh
 
Mawazo aliyonayo huyo dada dhidi yako huenda yana ambatana na mawazo ya mkeo kwa waume wa marafiki zake. Siku zote adui mkubwa wa mwanamke ni mwanamke mwenzake.
 
mkeo anakujua we dhaifuu anything might happen na pia kuna namna anamjua huyo dada mana huwa wanaongea,,,..afu wivu ni ishara ya upendo we kama vip msikilize mkeo kama umeshindwa kumpa lift bila mke kujua
 
Back
Top Bottom