Katika hili nashindwa kumuelewa mke wangu

Kawaida sana! Atazoea tu, kuwa na msimamo! Mwanaume lazima uwe na msimamo ukikubali kuyumbishwa utayumbishwa kwa mengi
 
Mwenzio keshamsoma hyo Dada ni mroho mroho sasa akitaka kukudokoa uwez chomoa. Anajiham ndoa yake iwe safe ukizingatia amejifungua na dudu yake IPO leave unaweza dokolewa wewe
 
Rahisi tu, wewe una gari ambayo mnaitumia kwenda kazini asbh na kurudi jioni kila siku, mnampa lift kaka wa nyumba ya jirani na kwako, bahati mbaya unaugua na unalazimika kubakia nyumbani, swali; ungemruhusu mkeo kwa roho nyeupe kabisa kuendelea kuondoka na kaka jirani kuelekea kazini na kurudi jioni kwa gari?. Kukosa wivu kwa mwandani wako ni tatizo pia(usizidi sana lkn), anakulinda na anapigania ndoa yenu huyo, mbona rahisi tu kumueleza jirani
 
Wadau,
Sina haja ya kuunganisha wanawake wote katika suala ninalopitia. Kwa ujumla ninaishi vizuri kabisa na mke wangu mpendwa ambaye tumeoana mwaka 2014. Tulibahatika kujenga na kuhamia nyumbani kwetu mwaka jana. Kwa bahati nzuri ambayo sasa imekuwa mbaya tulijenga urafiki na familia ya jirani na kwetu, mke wangu na dada wa nyumba ya jirani wakawa marafiki wakubwa.
Hali hii ilipelekea hata kuwa tunatoka wote asubuhi kwa gari ya mke wangu na kurudi pamoja pia muda wa jioni kwa kuwa wote tunafanya kazi katika maeneo jirani. Sasa mke wangu mpenzi amejifungua na sasa yupo ''maternity leave''. Jumatatu ikabidi nitoke mwenyewe na dada wa jirani ambaye huwa tunampa lift asubuhi na jioni. Sasa niliporudi usiku huo wa jumatatu wife akaniambia hataki nimpe lift tena dada wa jirani, nikauliza kwa nini? Akajibu hataki tu; niliwaza usiku ule na kuamua kuendelea kumpa lift huyu dada kwa kuwa wazo la kumpa lift lilikuwa la wife mwenyewe na kwangu ni ngumu sana kumpita huyu dada ambaye ameshazoea kuwa anapanda gari hii ukizingatia kuwa ni wife mwenyewe aliyemkaribisha. Nilipoamka jumanne nikamkuta huyu dada ananisubiri nje, nikampa lift kama kawaida na jioni pia nikarudi naye nyumbani pamoja.
Sasa mke wangu baada ya kuona hivyo, usiku wa jumanne akaniambia nikubali moja, kuendesha gari yake bila kumpa lift dada wa jirani au niende kazini kwa gari ya staff?! Hii kauli ya kutamka kuwa gari ni yake ilinipa mawazo sana kwa kuwa mke wangu huyu mpendwa hajawahi kuwa mtu anayeonyesha ubinafsi, tumekuwa na ndoa nzuri yenye amani na upendo wa hali juu.
Ndipo nikauliza ana tatizo gani na huyu dada? bado alinijibu kuwa hataki tu.
Nikampigia simu dereva wa staff bus kuwa anipitie asubuhi, na kuwakuwa basi huwa halijai kwa kuwa staff tunaoishi huko ni wachache na huyu dada alikuwa nje muda basi lilipofika kunichukua naye pia akapanda kwenye staff bus.
Niliporudi home wife amenuna na hataki kuongea, nashindwa kuelewa tatizo lake kwa huyu dada ni nini hasa?
Kiukweli naishi maisha yenye kuheshimu ndoa na kumpenda mke wangu kwa kiwango cha juu kabisa.

Waungwana, kama hivi ndivyo wanawake wanavyoweza kuwa na maamuzi yasio na chembe ya aibu napata shida sana kumuelewa mke wangu.

Epusha shari, panda basi. Au lah, kama unaona kupanda basi ni kero, basi mwambie mkeo amwambie huyo dada yeye mwenyewe kwamba hataki upande hilo gari.

Halafu madhara ya kuishi ''kiujamaa'' ndiyo haya sasa. Yaani lifti ambayo ilikuwa ni ''favour'' sasa imegeuka kuwa ''right'' na ndio mana hata kwenye basi la kazini kwenu kapanda. Sasa hapo watu wa ofisini kwenu wanakushangaa kupakiza abiria ambaye sio mfanyakazi. Na pengine hata mkeo alishachoshwa na tabia ya huyo dada kuwa na ninyi kwenye gari muda wote, maana kuna wakati mnahitaji uhuru, ila mnaukosa.
 
Hebu jaribu kuvaa viatu vyake huyo mkeo....iko hivi; kila siku umezoea kumpa lift kwenye gari yako jirani/ mshkaji wako (rafiki yako mwanaume) lakini umepata likizo au safari, gari yako kabaki nayo mkeo na jiranj/ rafiki/mshkaji wako bado anataka aendelee kupata lift kwa mkeo ikiwa wewe haupo, tena asubuhi na jioni, je! na wewe hutopata wasiwasi rafiki/mshkaji/jirani yako wa kiume kuwa na mkeo kila siku asubuhi na jioni?

Mkeo anawaogopa walimwengu na visa vyao na sio wewe!

Huu mfano wako umekaa vizuri sana.....
unampigia simu mkeo muda wa saa moja usiku anakwambia nipo na fulani hapa kwenye foleni Mwenge......
 
Jambo kama hili nalo linahitaji thread? kweli wanaume tumebaki wachache sana..yani matatzo ya ndoa zenu hamuwez kuyamudu unaacha kujenga taifa unawaza upuzi....kama hataki its well and good unamwambia mhusika pls gari ina tatizo sitaitumia kwa muda...then icho kiherehere cha kumpandisha dada wa jiran kwenye gari ya staf iwe mwisho leo......hutak utaivunja ndoa yako kwa mikono yako mwenyewe.....mxeeew tena uchukue partenity leave ujifunze kubadili pampas
 
Epusha shari, panda basi. Au lah, kama unaona kupanda basi ni kero, basi mwambie mkeo amwambie huyo dada yeye mwenyewe kwamba hataki upande hilo gari.

Halafu madhara ya kuishi ''kiujamaa'' ndiyo haya sasa. Yaani lifti ambayo ilikuwa ni ''favour'' sasa imegeuka kuwa ''right'' na ndio mana hata kwenye basi la kazini kwenu kapanda. Sasa hapo watu wa ofisini kwenu wanakushangaa kupakiza abiria ambaye sio mfanyakazi. Na pengine hata mkeo alishachoshwa na tabia ya huyo dada kuwa na ninyi kwenye gari muda wote, maana kuna wakati mnahitaji uhuru, ila mnaukosa.
Ujue wanaweza tu wakamwambia huyo mdada kuwa, kwa kuwa now mke amejifungua wanaona ni vyema gari libaki home, kwa ajili ya mtoto, mama na mizunguko yao mingine. Sasa kama dada naye ataendelea kupanda staff bus tena eeh
 
Embu mpunguze gubu na nyie..
Daddy wivu hatuna ila roho inauma teh. Utamruhusu ma mdogo awe anapewa lift na Kaizer daily? On a serious note, tunawaepusha kurubunika maana nyie hamkawii kuset appointment na shetani akawapitia
 
Huu mfano wako umekaa vizuri sana.....
unampigia simu mkeo muda wa saa moja usiku anakwambia nipo na fulani hapa kwenye foleni Mwenge......

Ajaribu yeye kufanyiwa hivyo then aje hapa na mrejesho! Mwanamke ambae ni mkeo akikuzuia kitu tena kwa utaratibu tu wa maneno bila kukuzushia ugomvi, kummheshimu ni mapenzi toSha kwake otherwise ungekutana na wale kina Asha ngedere angeanza kuku-accuse kwamba unatembea na jirani yenu tena na ugomvi juu!!
 
Mbona simple tu,Mwalike huyo dada wa jirani siku za wikiendi hapo nyumbani umwambie mkeo ana mazungumzo naye then akija mpambanishe amwambie mwenyewe.
 
acha anune piga kimya Fanya yako akichoka atajirud asipojirud pga kimya
 
Tafuta pesa zako boss, acha kutumia gari ya mkeo
 
Mi mazoea hayo ili iwejee,mi sitaki mwanamke yeyote awe na mazoea hayo,nae mpewa lifti hata hajiongezi kageuza gari la kwao ,mazoea gani hayo ya kua na mme wangu karibu vile ,namshangaa mke wako kumzoesha kumpa lifti mi hata lifti asingepata angeipata nikiwa ndani ya gari peke yangu
Wewe ndo Umeongea,
Jaman kina hebu tujifunze basi!

Iweje mazoea baadae yanageuka mateso yenu wenyewe! ?
 
Daddy wivu hatuna ila roho inauma teh. Utamruhusu ma mdogo awe anapewa lift na Kaizer daily? On a serious note, tunawaepusha kurubunika maana nyie hamkawii kuset appointment na shetani akawapitia
Teh teh..Douta ilo ni gubu lisilo na maana..Na sometimes nyie ndo uwa mnaamsha hisia hata ambazo hazikwepo mwanzo..Unakuta mtu hata hana mawazo hayo lakini we ndo unaanza kumjengea....Btw kama mwanaume ni mchepukaji kusitisha kumpa lift huyo dada hakuta mzuia yy kuchepuka...Still bado ana uwanja mpana wa kufanya yake
 
Teh sawa nyie mkichepuka chepukeni tu, ila isiwe kama na me nimekurahisishia njia ya wewe kuchepuka. Daddy hapo unaongea tu, ingekuwa ndo nyie na makofi mngetupa kwanza kabla ya maelezo. Wanawake ni watu wa hisia sana, so please ishini na sisi kwa akili
 
We sikiliza moyo wako! Akili ya kuambiwa changanya na zako - kwani unaonaje hapo kwa jran? You go boy
 
Wadau,
Sina haja ya kuunganisha wanawake wote katika suala ninalopitia. Kwa ujumla ninaishi vizuri kabisa na mke wangu mpendwa ambaye tumeoana mwaka 2014. Tulibahatika kujenga na kuhamia nyumbani kwetu mwaka jana. Kwa bahati nzuri ambayo sasa imekuwa mbaya tulijenga urafiki na familia ya jirani na kwetu, mke wangu na dada wa nyumba ya jirani wakawa marafiki wakubwa.
Hali hii ilipelekea hata kuwa tunatoka wote asubuhi kwa gari ya mke wangu na kurudi pamoja pia muda wa jioni kwa kuwa wote tunafanya kazi katika maeneo jirani. Sasa mke wangu mpenzi amejifungua na sasa yupo ''maternity leave''. Jumatatu ikabidi nitoke mwenyewe na dada wa jirani ambaye huwa tunampa lift asubuhi na jioni. Sasa niliporudi usiku huo wa jumatatu wife akaniambia hataki nimpe lift tena dada wa jirani, nikauliza kwa nini? Akajibu hataki tu; niliwaza usiku ule na kuamua kuendelea kumpa lift huyu dada kwa kuwa wazo la kumpa lift lilikuwa la wife mwenyewe na kwangu ni ngumu sana kumpita huyu dada ambaye ameshazoea kuwa anapanda gari hii ukizingatia kuwa ni wife mwenyewe aliyemkaribisha. Nilipoamka jumanne nikamkuta huyu dada ananisubiri nje, nikampa lift kama kawaida na jioni pia nikarudi naye nyumbani pamoja.
Sasa mke wangu baada ya kuona hivyo, usiku wa jumanne akaniambia nikubali moja, kuendesha gari yake bila kumpa lift dada wa jirani au niende kazini kwa gari ya staff?! Hii kauli ya kutamka kuwa gari ni yake ilinipa mawazo sana kwa kuwa mke wangu huyu mpendwa hajawahi kuwa mtu anayeonyesha ubinafsi, tumekuwa na ndoa nzuri yenye amani na upendo wa hali juu.
Ndipo nikauliza ana tatizo gani na huyu dada? bado alinijibu kuwa hataki tu.
Nikampigia simu dereva wa staff bus kuwa anipitie asubuhi, na kuwakuwa basi huwa halijai kwa kuwa staff tunaoishi huko ni wachache na huyu dada alikuwa nje muda basi lilipofika kunichukua naye pia akapanda kwenye staff bus.
Niliporudi home wife amenuna na hataki kuongea, nashindwa kuelewa tatizo lake kwa huyu dada ni nini hasa?
Kiukweli naishi maisha yenye kuheshimu ndoa na kumpenda mke wangu kwa kiwango cha juu kabisa.

Waungwana, kama hivi ndivyo wanawake wanavyoweza kuwa na maamuzi yasio na chembe ya aibu napata shida sana kumuelewa mke wangu.
Boss pole,
Mkeo anaogopa utachepuka, wewe unajiamin sawa! Lakn shetani huwatafuta waliosimama na kujiamini sio walioanguka tayar! So acha kujiuliza uliza, Msikilize!

Utampitaje huyo jirani, fanya hiv,
Acha kutumia gari hiyo, tumia ya staff!
Akikuuliza kwa nini? mjibu kwa upendo tu, nimeshindwa kupata moyo wa ujasir kumpita huyu dada na siwezi kukukwaza, kama unaweza nisaidie kumwambia.

Mwachie hapo! Mengine ya kawaida!
Kuna wakati huwa naamini wanawake Mungu wetu alikufa, tunakuwaga na maamuzi baadae yanatugharimu.

Ushoga kautaka mwenyewe huku hajiamin!
Mweeeeeh! mtusamehe bure lakn, chukulianeni na sisi tu! Mtafanyaje sasa! ! !
 
Back
Top Bottom