GoodNafikiri kosa la Shetani siyo kumdanganya Eve/Hawa bali ni KUFICHUA SIRI ZA MUNGU KWA MWANADAMU. Jiulize kama kweli Adamu alikuwa na maisha ya milele kwanini Mungu apande mti wa Uzima? Apa inaonesha Adamu alipungukiwa vitu viwili ili awe kama Mungu, kwanza ni MAARIFA( Ujuzi wa mema na mabaya) pili ni MAISHA YA MILELE.
Aya mambo mawili ya utimilifu wa Adamu, Mungu aliyafanya fumbo ili Adamu hasiwe nayo ili awe tegemezi kwa bwana Mungu wake. Ili fumbo Mungu aliliweka kama tunda japo siyo tunda kama tunda! Na akamwambia Adamu hasiguse apo maana alijua Adam akifumbua ayo Mafumbo mawili basi hataweza tena kumdhibiti Adamu maana atakuwa na Utimilifu wote.
Kwahiyo shetani alichofanya ni kufichua siri ya Mungu kwa Adamu akiamini Adamu akitimilika basi atapata kiumbe mwingine wa kushirikiana naye kupambana na Utawala wa Mungu. Mungu kwa kutambua hila za Shetani akamfukuza Adamu kwenye ile Bustani ili hasile tunda la pili(kufungua code namba mbili) za kuishi milele.
Kwahiyo Shetani hajasema uongo ni ukweli japo ni ukweli ambao Mungu hakutaka ujulikane kwa Adamu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kwani uwepo wa kifo ndiyo unafanya wengine wazaliwe?Kifo kisingekuwepo hata haya maswali unayouliza pia yasingekuwepo,kwa kifupi Mungu ahitaji umsaidie kupanga ingekuwaje.Yeye anajua kila kitu,relax acha yeye atawale.Lakini ukiangalia vizuri kifo kililazimika kuwepo, jiulize je kisingekuwepo wengine wangezaliwaje? Na dunia hii sasa hivi tungekuaje?
mkuu naomba namba yako aisee wewe unaweza nisaidia issue zanguMkuu wewe ni mpotoshaji,kama wale jamaa tabia zao husoma maandiko hawayamalizii,umesema Mwanzo 3:22 mimi nakuomba uendelee usome mpaka Mwanzo 3:24
"Na basi akamfukuza huyo mtu, akaweka upande wa mashariki wa bustani ya Edeni+ makerubi+ na upanga unaowaka ambao ulikuwa unajizungusha-zungusha ili kuilinda njia ya kwenda kwenye ule mti wa uzima. "
Mungu alimwambia Adam hakika siku utakayokula tunda utakufa,kwa hiyo Neno litokalo kinywani mwa Bwana lazima litimie,hivyo angewaacha kwenye bustani wangekula tunda la uzima na kuishi milele.Na sababu aliyowafukuza ni ili wasiweze kula tunda la uzima wakaishi milele kitu ambacho kingefanya kile alichowaambia mwanzo kisitimie ndiyomaana aliweka malaika kuilinda njia ya kwenda kwenye mti wa uzima,Mungu huliangalia Neno lake apate kulitimiza.
Nakuuliza tena wewe ni Mkristo?Je ni msom,aji wa biblia mara kwa mara?Je umejazwa Roho Mtakatifu?
Swala la kufa lilikuja kama adhabu baada ya kula tunda,aliposema ukila tunda la mti wa kati hakika utakufa ni kama wew umwambie mwanao ukiweka sukari kwenye chai nitakuchapa,akaja mtu akamwambia chai inatakiwa iwekwe sukari,alipoweka sukari ukaja ukamchapa,kwahiyo hapo sio swala la ahadi yako ya kumchapa kutimia ila hiyo adhabu ya kumchapa ni haki?wewe mleta kwani adam na hawa wapo mpaka leo? siwalikufa? au tatizo ni kwakuwa ilichukua muda wao kufa ulitaka Mungu awambie mtakufa baada ya kipindi fulani mana sio kwamba Mungu aliwambia mtakufa hapo hapo aliwaambia tu mkila mtakufa na kweli mwisho wa siku walikufa
Mkuu njoo pm nitakusaidia,tuwasilaiane kwa private message.
Naona kuna haja ya somo la theolojia kuwa mandatory kwa wakristo wote hivi mpaka leo kuna watu wanaamini tunda lilioliwa ni Tunda as Tunda??
Jamani lugha iliyotumika hapa ni figurative yaani lugha ya picha ila haina maana ni mti kma hii miti yetu au tunda kama haya matunda yetu kama watu mnadai hii miti ya Eden ni miti ya kawaida naomba mnielezee hii sura
Ezekiel 31:9
9 Nalimfanya kuwa mzuri kwa wingi wa matawi yake; hata miti yote ya EDEN, iliyokuwa ndani ya bustani ya Mungu, ilimwonea wivu.
18 Umefanana na nani, hivi katika utukufu na ukuu, kati ya miti ya EDEN? Lakini utashushwa pamoja na miti ya EDEN, hata pande za chini za nchi; utalala kati ya hao wasiotahiriwa; pamoja na hao waliouawa kwa upanga.
SWALI
Je ni miti gani ya Eden imepelekwa kuzimu wakati kuzimu ni kwa ajili ya shetani na wafuasi wake??
Je miti inaweza kuoneana wivu kama wanadamu?
Je miti inaweza kuhukumiwa na Mungu kisa inaKIBURI yaani miti ina character za kibinadamu?
Biblia ni figurative otherwise mkisema mti ni mti wa kawaida basi mnisaidie hayo maswali angu hapo juu!!
Mkuu kwani uwepo wa kifo ndiyo unafanya wengine wazaliwe?Kifo kisingekuwepo hata haya maswali unayouliza pia yasingekuwepo,kwa kifupi Mungu ahitaji umsaidie kupanga ingekuwaje.Yeye anajua kila kitu,relax acha yeye atawale.
Mkuu take easy,aliposema na tuumbe mtu kwa mfano wetu alimanisha alikuwepo Mungu Baba,Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu.Hapa kuna watu huwa hawaelewi ukiwaambia Yesu alikuwepo wakati wa uumbaji,wao wanasema alianzia pale alipozaliwa na bikira Maria,hawajui maandiko yanelezea kule kuzaliwa na Bikira maria ni Neno kuuvaa mwili akaja kwetu tukauona utukufu,na Neno maana yake ni Yesu.Soma Yohana 1:1 "Hapo Mwanzo alikuwepo Neno,naye Neno alikuwepo kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu.....".Hapa wengi wameachwa ,usicheze na Jehova yeye anajua moyo wako unapokuwa unasoma biblia una nia ya kujifunza au unataka kuikosoa injili,lazima kuna mambo hutayajua au utayajua ndivyo sivyo.Mungu alisema tumuuumbe mtu kwa mfano wetu lakini cha kushangaza akatunyima ufahamu,yaani ni kama vile ali cheat,aliposema tumuumbe mtu kwa mfano WETU inamaana hakuwa peke ake,hata shetani alikuwepo na alishuhudia rafu tuliyochezewa,mpango wa mungu ilikua usitofautiane sana na mbuzi au nguruwe maana wote hamjui mema na mabaya,hii rafu shetani akaona sio poa kabisa,huu sio mpango wetu wa kumuumba kwa mfano wetu,kwahiyo kutoa siri ya mti wa kati ni kama ku insert program ambayo tulistahili ila tukanyimwa
Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu alisema tumuuumbe mtu kwa mfano wetu lakini cha kushangaza akatunyima ufahamu,yaani ni kama vile ali cheat,aliposema tumuumbe mtu kwa mfano WETU inamaana hakuwa peke ake,hata shetani alikuwepo na alishuhudia rafu tuliyochezewa,mpango wa mungu ilikua usitofautiane sana na mbuzi au nguruwe maana wote hamjui mema na mabaya,hii rafu shetani akaona sio poa kabisa,huu sio mpango wetu wa kumuumba kwa mfano wetu,kwahiyo kutoa siri ya mti wa kati ni kama ku insert program ambayo tulistahili ila tukanyimwa
Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna aliyepinga Biblia au mada yako ila point is haikumaanisha tunda au mti kama hii ya sasa yaani apple au embe ila ni lugha ya fumbo tu, maana nimeona kila anayechangia anaongelea miti na matunda ya kimwili ndio maana ikabidi niweke hiyo rai that's why nikasema kma walimaanisha ni miti kama miti yetu mbona Ezekiel 31 inaelezea miti ya Eden ina wivu? Miti ina kiburi?? Miti itahukumiwa kuzimu??Sasa kama biblia imeandika ni tunda unataka sisi tuseme sio tunda Bali walikula chips? Ulitaka tulifafanue vip hilo tunda? , Sasa kumbe hata biblia huiamini so which is which ?
Sent from my iPhone using JamiiForums
Hakuna aliyepinga Biblia au mada yako ila point is haikumaanisha tunda au mti kama hii ya sasa yaani apple au embe ila ni lugha ya fumbo tu, maana nimeona kila anayechangia anaongelea miti na matunda ya kimwili ndio maana ikabidi niweke hiyo rai that's why nikasema kma walimaanisha ni miti kama miti yetu mbona Ezekiel 31 inaelezea miti ya Eden ina wivu? Miti ina kiburi?? Miti itahukumiwa kuzimu??
Bible ni figurative
sasa hayo ni mawazo yako wewe sio mawazo ya MUNGU, na Mungu si mwanadamu hata aseme uwongo hivyo alichosema ndicho alichomaanisha hayo mengine umeyatunga wewe kwababu umetafuta shauri la kupingana na neno lakeSwala la kufa lilikuja kama adhabu baada ya kula tunda,aliposema ukila tunda la mti wa kati hakika utakufa ni kama wew umwambie mwanao ukiweka sukari kwenye chai nitakuchapa,akaja mtu akamwambia chai inatakiwa iwekwe sukari,alipoweka sukari ukaja ukamchapa,kwahiyo hapo sio swala la ahadi yako ya kumchapa kutimia ila hiyo adhabu ya kumchapa ni haki?
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ni kweli the bible is figurative but not all the time,shida ambayo pia nimeiona kwako nikuchukua kisehemu cha maandiko kama wale jamaa ambao hupotosha wakristo kwa kipande cha maandiko.Nikushauri hiyo Ezekiel 31:9,mimi nikushauri uisome kuanzia Ezekiel 31:1-9 hapo utaelewa,hii tabia ya kuchukua kisehemu wakati maelezo yalikuwa mengi ndiyo chanzo cha kutokuelewa na kupotosha.Nakubaliana na wewe lugha iliyotumika katika eneo hilo ni ya mfano(au ukitaka picha kama ulivyosema lakini biblia imesema mfano) ,kwa hiyo tunda la Edeni linabaki kuwa tunda wala si fumbo,ni kweli kwenye biblia kuna mafumbo ila hapo Edeni tunda ni tunda na si vinginevyo.Hakuna aliyepinga Biblia au mada yako ila point is haikumaanisha tunda au mti kama hii ya sasa yaani apple au embe ila ni lugha ya fumbo tu, maana nimeona kila anayechangia anaongelea miti na matunda ya kimwili ndio maana ikabidi niweke hiyo rai that's why nikasema kma walimaanisha ni miti kama miti yetu mbona Ezekiel 31 inaelezea miti ya Eden ina wivu? Miti ina kiburi?? Miti itahukumiwa kuzimu??
Bible ni figurative
Swala la kufa lilikuja kama adhabu baada ya kula tunda,aliposema ukila tunda la mti wa kati hakika utakufa ni kama wew umwambie mwanao ukiweka sukari kwenye chai nitakuchapa,akaja mtu akamwambia chai inatakiwa iwekwe sukari,alipoweka sukari ukaja ukamchapa,kwahiyo hapo sio swala la ahadi yako ya kumchapa kutimia ila hiyo adhabu ya kumchapa ni haki?
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu naelewa kabisa kwenye hii sura inaongelea Pharaoh kama Mti lakini hoja yangu ni kwamba miti ya Eden kwenye hii sura ya Ezekiel 31 umetumika figuratively ndio najengea hoja kwanini basi muamini Genesis inaongelea mti la kawaida what if ni fumbo kama Ezekiel??Mkuu ni kweli the bible is figurative but not all the time,shida ambayo pia nimeiona kwako nikuchukua kisehemu cha maandiko kama wale jamaa ambao hupotosha wakristo kwa kipande cha maandiko.Nikushauri hiyo Ezekiel 31:9,mimi nikushauri uisome kuanzia Ezekiel 31:1-9 hapo utaelewa,hii tabia ya kuchukua kisehemu wakati maelezo yalikuwa mengi ndiyo chanzo cha kutokuelewa na kupotosha.Nakubaliana na wewe lugha iliyotumika katika eneo hilo ni ya mfano(au ukitaka picha kama ulivyosema lakini biblia imesema mfano) ,kwa hiyo tunda la Edeni linabaki kuwa tunda wala si fumbo,ni kweli kwenye biblia kuna mafumbo ila hapo Edeni tunda ni tunda na si vinginevyo.
Tuangalie Ezekiel 31:1-9 nimechukua maandiko kutoka online bible sababu ya muda
31:1 Na ikazidi kutukia kwamba katika mwaka wa kumi na moja, katika mwezi wa tatu, siku ya kwanza ya mwezi huo, neno la Yehova likanijia, na kusema: 2 “Mwana wa binadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri na umati wake,+“ ‘Umefanana na nani katika ukuu wako? 3 Tazama! Mwashuru, mwerezi katika Lebanoni,+ wenye matawi ya kupendeza,+ wenye kifuniko chenye majani mengi kinachotoa kivuli, na wenye kimo kirefu,+ hivi kwamba kilele chake kilikuwa kati ya mawingu.+ 4 Ni maji yaliyoufanya uwe mkubwa;+ kilindi cha maji kiliufanya urefuke. Pamoja na vijito vyake kilikuwa kikienda kuzunguka pande zote mahali ulipopandwa; nacho kiliipeleka mifereji yake kwenye miti yote ya shambani. 5 Ndiyo sababu ulikuwa mrefu zaidi kwa kimo kuliko miti mingine yote ya shambani.+“ ‘Na matawi yake yalizidi kuongezeka, na matawi yake yaliendelea kuwa marefu zaidi kwa sababu ya maji mengi kwenye mifereji ya maji.+ 6 Viumbe vyote vinavyoruka vya mbinguni vilifanya viota+vyao kwenye matawi yake, na wanyama wote wa mwituni walizaa chini ya matawi yake,+ na mataifa yote yenye hesabu kubwa ya watu yalikuwa yakikaa katika kivuli chake. 7 Nao ukawa wenye kupendeza katika ukuu wake,+ katika urefu wa majani yake, kwa maana mizizi yake ilikuwa juu ya maji mengi. 8 Mierezi mingine haikulingana nao katika bustani ya Mungu.+ Nayo miberoshi, haikufanana nao kwa habari ya matawi yake. Na miaramoni yenyewe haikuwa kama huo katika matawi yake. Hakuna mti mwingine wowote katika bustani ya Mungu uliofanana nao katika uzuri wake.+ 9 Niliufanya kuwa mzuri katika wingi wa majani yake,+ na miti mingine yote ya Edeni iliyokuwa katika bustani ya Mungu wa kweli ikawa ikiuonea wivu.’+
Ukisoma kwa makini hapo mwanzoni Farao alikuwa anaulizwa umefanana na nani?Kufanana na kitu si kuwa kitu halisi ni lugha ya mfano,maandiko yakaendelea kwamba "Tazama ,Mwashuru(nchi ya Syria au Wasiria) imefanana na mti wa mwerezi ambao unapatikana katika nchi ya LEBANONI,kwa hiyo ulichochukua kwenye Ezekiel 31:9 kilitanguliwa na hayo uliyoyaacha amabyo yanaonyesha nchi ilifananishwa na mti,na ndiyo maana ikasemwa hata miti ya kwenye bustani ya Edeni iliuonea wivu huu mti wa mwerezi.Ni lugha ya mfano kuelezea jamabo lakini haijaondoa kwamba tunda la Edeni siyo Tunda na kwamba ni fumbo.
Ushauri wangu kwako mtu akikuletea andiko ikiwezekana nenda nyuma na mbele ya andiko hilo paragraph walau mbili au zaidi utaujua ukweli.Kwa hiyo lugha ya pale ni ya mfano,na miti mingine maana yake ni mataifa au watu wa mataifa fulani,kwa hiyo taifa linaweza kuhukumiwa na kwenda kuzimu(hapa namanisha wananchi wa taifa fulani) kwa hiyo wewe ukibaki kwenye je mti unaweza kuhukumiwa umejipotosha mwenyewe.Mwanzoni mwa Ezekiel 31 walianza na farao mtawala wa misri umefananishwa na nini?
Na kama ulikuiwa hujui syria ilikuwa nchi nzuri imara na yenye nguvu kabla ya vita,lakini kwa sasa sihitaji kukueleza juu ya Syria fuatilia mwenyewe.Biblia siyo kitabu cha hadithi za kufikirika,na wanaotumia akili zao kukikosoa kuna siku watakaa kimya.
Well said brother, Papa ni kiongozi wa kanisa la RC na sio kiongozi wa Ukristo, huyo papa angeulizwa pia hicho cheo kakitoa wapi ndani ya Biblia? Kwa ujumla kama ulivyo sema, Wakristu peke yake ndio wanao mkubali papa lakini Wakristo HAPANA, wanamuona kiongozi kama walivyo viongozi wengine tu. So papa sio mfano wa Ukristo popote duniani and by the way RC wameharibu misingi mingi sana ya Ukristo kwenye hi dunia.Hivi wewe faiza aliyekwambia Papa ndo mwakilishi wa ukristo Ni nani?mbona unapendaga kuwa Na kimbelembele kweny mambo hata usiyoyajua?so akisema papa ndo unadhani Ni Kweli ?sasa kwa taarifa yako papa anasikilizwa Na wakatoliki tu tena wakatoliki baadhi sio wote.Asilimia kubwa ya madhehebu ya kikristo yako against papa.Wewe kusema papa ndo anawakilisha ukristo Ni sawa Na Mimi MKRISTO Leo niseme sheikh wenu sheikh yahya ndo anaewakilisha uislamu huku Tanzania Na yale majini aliyokuwa anatumia basi Dini yenu waislamu wote inakubali kutumia majini.Upunguze kiherehre kwa vitu usivyovijua especially Dini za watu unaboaaa
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wewe ni mtu makini sana sitegemei ufanye hizi errors zitasusha credibility yako..... Syria na Assyria ni vitu viwili tofauti kwenye Biblia Syria ni nchi Aram na Assyria kwa sasa ni Uturuki na Iraq kaskazini ni eneo dogo sana la Syria ndio lipo Assyrian empire hivyo hakuna correlation yeyote kati ya Assyria empire na syria kuanzia jamii ya watu mpaka ardhi.Na kama ulikuiwa hujui syria ilikuwa nchi nzuri imara na yenye nguvu kabla ya vita,lakini kwa sasa sihitaji kukueleza juu ya Syria fuatilia mwenyewe.Biblia siyo kitabu cha hadithi za kufikirika,na wanaotumia akili zao kukikosoa kuna siku watakaa kimya.