Kwa
Mkuu
1.Magufuli hajawahi kuwa WAZIRI wa MADINI. Na katika mikataba hiyo hakuhusika.
Mikataba hii ilizungumzwa na kupitishwa katika level ya cabinet. Hivyo alihusika.
2.Akiwa waziri. Maoni yake YALIPUUZWA japokuwa alikuwa na a lot of reservations ya mikataba hiyo MIBOVU.
Kupuuzwa huko kulitokana na UTAWALA uliokuwepo.
Kanuni za collective responsibility zinasema hivi, ukipingana na kitu, ama mawazo yako yatakubalika ama yatapuuzwa.
Yakikubalika unaendelea na kazi na una ownership ya maamuzi.
Yakipuuzwa una uamuzi wa kufanya. Ama ukubaliane na kupuuzwa huko na uendelee na kazi, ama ujiuzulu na kupinga mambo kutoka nje.
Magufuli alikuwa na nafasi ya kujiuzulu uwaziri na kusema mabaya haya akiwa nje. Hakuthubutu kufanya hivyo.
Maana yake alikubaliana na maamuzi.
By the way SI kila kitu kinachozungumzwa katika baraza la Mawaziri huwa kinawekwa wazi. Ndo maana alipoona mambo mengine hayaendi sawa akafanya alivyofanya kama Waziri sababu ya UCHUNGU wa kuona Watanzania WANADHURUMIWA wazi wazi.
Angekuwa na uchungu angejioa uwaziri abaki mbunge backbencher aweze kuinanga serikali vizuri. Mikataba mikubwa kama hii katika ngazi ya cabinet mawaziri wanaiona, kusema kuna mambo hayako wazi ni kumtetea tu.
3. In case haya makampuni yatafute kesi ya arbitration ambayo nina UHAKIKA HAWAWEZI kutokana na sababu zilizo wazi na MADHARA ya kufuata njia kama hiyo.
Una uhakika hawawezi wakati watu washaanza kazi hiyo?
Maana the EVIDENCE against them is too overwhelming na inaweza ku work in FAVOUR of The United RPT. Subsequently costing them a lot.
Evidence gani against them? Unajua mikataba iliwaruhusu kuchukua mchanga na Magufuli kukataza kuchukua mchanga anavunja mikataba?
4. Mikataba na makampuni ALWAYS can be revisited and revised as needs arise.
Mfano Trump Ametumia EXECUTIVE powers/ yaani MAMLAKA ya KIRAIS KUVUNJA mikataba MIBOVU iliyowekwa na WATANGULIZI WAKE ili kuhakikisha Marekani HAWAIBIWI kiholela holela tu.
Na wananchi wamefurahia hatua hizo.
Mikataba inavunjwa. Evo Morales wa Bolivia kavunja mikataba mibovu. Alichofanya - ambacho ndicho kitu Trump anafanya sasa- ni kuitoa Bolivia katika international conventions ambazo Bolivia ni signatory kwanza, mikataba hii ndiyo inashurutisha nchi kufanya hivi na vile etc.Ukishajitoa katika hizo conventions, then unaweza kuvunja mikataba na makampuni.
Magufuli kavunja mikataba na makampuni kabla ya kujitoa katika conventions. Wawekezaji wanamcheka kwa ujinga wake.
Inawezekana kabisa wamechimba mchanga mpaka umekwisha, sasa unakwisha, Magufuli anavunja mkataba, deal lao linaendelea sasa watalipwa kwa sababu Magufuli kavunja mkataba hata kama mchanga umeisha.
Hata kwetu Kuna VIFUNGU vya sheria VINAVYOMPA RAIS EXECUTIVE powers KU REVISIT mikataba mingine MIBOVU kama hii.
Executive power ya rais haina nguvu kwa wawekezaji wenye mikataba ya kimataifa, atashitakiwa London na kushindwa kesi na kuambiwa alipe fidia. Waziri wa Magufuli alikwenda Mgodini na kumtisha James Sinclair KI Magufuli Magufuli kwamba atafunga mgodi, James Sinclair akamwambia "Go ahead, make my day, nitakupiga daflao la "Force Majeure" ushindwe kujua nini kimekupiga.
Waziri akanywea sikusikia kumfuatilia Sinclair