Katibu mkuu wa Wizara ya Afya lawamani (Blandina Nyoni)

mmoja na ya Ireland, mwingine UK wawili USA bila kusahau kuwa wote hao wanazo za Tanzania pia

huyo ndio mbunge wetu ambaye yuko mstari wa mbele kutuambia madhambi ya wenzie

GT wewe una uraia wa nchi ngapi?

Isije ikawa unamlaumu huyu mama kwa kuwalaumu wenzake wakati yeye mambo yake hayako barabara, wakati wewe mwenyewe ...

Kama principle unayotaka kutumia hapa ni kuwa "kama wewe una issues huwezi kuwasema wenzako" basi wewe kumsema huyu mama kunamaanisha wewe huna issue?
 
Mkuu BoraMaisha.

Umeeleza mengi ya muhimu lakini bottom line ni kuwa inabidi tufunguwe wadi ya wagonjwa wetu India! Huyo Daktari mmoja ataweza kuwahudumia hao wagonjwa wote uliowatolea mifano? Pili, huyo Daktari atakaa New Delhi wakati wagonjwa wanapelekwa miji tofauti nchini humo. Hizo per diem za huyo Daktari akiwa anafuatilia masuala ya mgonjwa Chennai si zitatosha kujenga kadispensari Matombo?

Maamuzi haya ni mfano hai wa tunavyopenda majibu mepesi kwa maswali magumu. Badala ya kuborosha huduma za tiba nchini tunamtengenezea mtu ulaji nchini India!

Amandla.........

Naam, inabidi ijengwe dispensari ya Watanzania kwenye hizi hospitali huko India maana namba ya wagonjwa wanaokwenda huko kutafuta tiba inaongezeka kila siku. Wengine wenye vijisenti vyao wamefanya ni fasheni ya kwenda kwa check-up kila wakijisikia kufanya hivyo.

Nakubaliana nawe kabisa kwamba daktari atakuwa based New Delhi na kamwe hataweza kuhudumia wagonjwa walioko Chennai, Bombay na kwingineko. Suala hili la idadi ya wagonjwa wanaokwenda India kuzidi kuongezeka linahitaji mkakati unaostahili. Tunashukuru kwamba hivi sasa Muhimbili wameanza kushughulikia baadhi ya cases ambazo huko nyuma ilibidi zipelekwe India, hiyo ni hatua nzuri.

Kuna taarifa kwamba tangu Wahindi walipoona influx ya Watanzania wanaokwenda kutibiwa kwenye hospitali mbalimbali nchini India, kwa nia njema kabisa wakuu wa hospitali za Apollo wakashauri uwepo ubia kati ya Serikali yetu na wao ili watujengee hospitali ya aina ya Apollo nchini. Suala hilo limeketi kwenye meza za Wizara ya Afya kwa miaka. Nasikia ni hivi majuzi tu huyu Nyoni anayeshutumiwa ndiye ameweza kulishughulikia suala hilo na uamuzi umeishatolewa kwamba Apollo watajenga hospitali kubwaaaa kwenye viwanja vya Chuo kikuu Mlimani.

Bado sioni umuhimu wa suala la daktari gani aende ama asiende ama kwanini yule hakwenda likatafutiwe ufumbuzi bungeni!
 
Masanja,

..mama Nyoni nimekuwa nikimsikia sifa zake kwamba ni mchapa kazi.

..sasa kinachonishangaza ni kuja kufanya uamuzi kama huu --ikiwa madai ya Mbunge ni ya kweli.

..Tanzania sijui tuna matatizo gani hapa. yaani karibu kila mtu I have been looking up to amekuja kuni-disappoint.

NB:

..hili suala lilishazungumziwa mwanzoni.

..moderator, at your convinience, unaweza kuunganisha na thread ya zamani inayomhusu Blandina Nyoni.

Blandina Nyoni ni kimbelembele na mpenda sifa yaani anafanana na MEMBE kwa kujipendekeza na kutaka sifa huku uwezo wake zero.

tizama wizara ya Maliasili bajeti yake ilipopita kwa Taabu kwani wizara hiyo ilikuwa ikongozwa na huyu kimbelembele asiyejua kitu BLANDINA NYONI.
 
- mkuu pm, tupo pamoja sana hapo, ni majungu matupu hakuna substance wala facts!, muacheni mama afanye kazi ya taifa.

fmes!

huyu blandina hana kitu tizama bajeti ya wizara aliyokuwa akiiongoza ya maliasili ilivyovurunda.pitia ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali juu ya utumbo na madudu ya huyu mama kwenye matangazo ya wizara nje ya tanzania.
Ni kimbelembele kama membe utafikiri wamezaliwa baba mmoja na mama mmoja.
 
jamani nimepata nyeti za huyu mama tangu Jumapili na nimezipitia post zote humu naomba ni widhdraw my initial support kwake

That said, naona itakuwa si vibaya tukaanza na yale mabilioni yaliyotumika kwenye sherehe za mwanae aliyeoa mzungu

Then tu move on kwenye madudu yake mengine

duh!
 
MwanaHALISI angesaidia sana wasomaji wake kama angetoa "Job Description" ya Medical Attache kwa sababu watu waliotajwa katika habari hii ni madaktari, japo kwa viwango tofauti.

Huyu Dr. Chale ninahisi atakuwa ni Dr. Stella Chale ambaye ni daktari bingwa pale Muhimbili upande wa Internal Medicine. Ni daktari bingwa wa miaka mingi tu. Kama sikosei alimaliza digrii ya kwanza ya Medicine mwaka 1983 na specialization kwenye internal medicine mwaka around 1989/1990. Ni daktari mzuri tu na mchapakazi mzuri.

Dr. Edward Sawe atakuwa ni Assistant Medical Officer (AMO), naye ni wa miaka mingi kidogo. (He was my classmate in Secondary School, 1972-1975). Japokuwa hatujaonana miaka mingi, ninaamini atakuwa bado ni mtu wa integrity na principles kama nilivyomfahamu.

AMOs wana uwezo na ujuzi wa kufanya kazi nyingi tu karibu sawa na graduate wa medicine.

Mama Blandina Nyoni naye anaeleweka kuwa mtu mwenye track record nzuri ya utumishi serikalini. Hivyo MwanaHALISI angefanya homework kidogo ya kutafuta requirements za Medical Attache, ili kutusaidia kuelewa kinachodaiwa kwenye habari hii. Nina wasiwasi kuwa huenda watu wanalinganisha majina: Nyoni & Chale (Songea), Sawe (Moshi) hivyo Sawe out!

Labda kumpa benefit of doubt mwandishi wa habari hii: Wagonjwa wanaopelekwa India wana matatizo ya aina mbali, mengine yapo kwenye nyanja tofauti na specialization ya Dr. Chale ya Internal Medicine. Kwa hiyo "rationale" ya kuwa na daktari bingwa kuwa mwambata inakuwa ngumu kueleweka.

Duh. watu wameunganisha dots: Nyoni & Chale (Songea), Sawe (Jokakuu Moshi), hivyo Sawe out !!!!!!!!!!!!!!.

Ndio maana wengine tutabeba mabox huku.
 
Mkuu BoraMaisha.

Umeeleza mengi ya muhimu lakini bottom line ni kuwa inabidi tufunguwe wadi ya wagonjwa wetu India! Huyo Daktari mmoja ataweza kuwahudumia hao wagonjwa wote uliowatolea mifano? Pili, huyo Daktari atakaa New Delhi wakati wagonjwa wanapelekwa miji tofauti nchini humo. Hizo per diem za huyo Daktari akiwa anafuatilia masuala ya mgonjwa Chennai si zitatosha kujenga kadispensari Matombo?

Maamuzi haya ni mfano hai wa tunavyopenda majibu mepesi kwa maswali magumu. Badala ya kuborosha huduma za tiba nchini tunamtengenezea mtu ulaji nchini India!

Amandla.........

Wewe Fundi:

Acha kutajataja Matombo hapa.
 
Sasa weye njomba mbona unaonyesha uziro wako ! W Mkama ni mtu wa BK....?
Ni wazi una majungu tuu maana hata hujui ulisemalo.....
 
namjua sana huyu mama tangu nina miaka mitano na alikuwa jirani yangu kwa miaka mingi sana...ni chapa kazi sana lakini seems labda watu wakishaingia kwenye authority wanakuwa corrupted,anyway sijui nini kinaendelea sasa kwenye life yake maana niko huku west coast for many yrs nikila raha na sluts wa hollywood!
 
Vipi sluts wa huko nao wako maliasili na wachapa kazi wazuri kama huyo katibu mkuu??? au hiyo story ya west coast imeingiaje kwa mama Nyoni?
 
jamani nimepata nyeti za huyu mama tangu Jumapili na nimezipitia post zote humu naomba ni widhdraw my initial support kwake

That said, naona itakuwa si vibaya tukaanza na yale mabilioni yaliyotumika kwenye sherehe za mwanae aliyeoa mzungu

Then tu move on kwenye madudu yake mengine

duh!

GT.

Tafadhali share hizo nyeti na jamvi hili tukufu
 
Blandina Nyoni ni kimbelembele na mpenda sifa yaani anafanana na MEMBE kwa kujipendekeza na kutaka sifa huku uwezo wake zero.

tizama wizara ya Maliasili bajeti yake ilipopita kwa Taabu kwani wizara hiyo ilikuwa ikongozwa na huyu kimbelembele asiyejua kitu BLANDINA NYONI.

Blandina Nyoni ni mmoja katika wachapakazi mahili katika civil service ya Tanzania. She is a professional and a lady of intergrity; sehemu zote alizofanya kazi ameondoa uozo alioukuta; angalia tu alipokuwa Paymaster General, mishahara ilikuwa inalipwa on time na ghost workers wote wakatoweka kwenye payroll ya serikali!! Acheni majungu mpeni mama huyu sifa anazostahili. Mama Nyoni chapa kazi usiwasikilize hawa wachumia tumboni hawana maana kwa Taifa letu.
 
Maelezo zaidi kuhusu huu mjadala bungeni:

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo sina hofu ya kusema. Halafu cha kusikitisha anaenda kuteua mtu ambaye alishakua mtumishi ameacha, ameenda kwenye NGO, anaenda kumchukua kwa sababu tu sijui ni wifi au ana unasaba naye anamrudisha na kutoa force kwamba lazima kule Muhimbili wamkubali kama mtumishi na jana nimepewa taarifa aliitisha Kamati wakaandaa sifa upya ili ionekane huyu aliyekua amechaguliwa ambaye amekaa kwenye dawati la kupeleka watu nje hafai. Sawa basi huyu Dr. Sawe hafai. (Makofi)

Page28
Sawa Dr. Sawe hafai, kwanini watumishi wote usiwape uende ukamtoe wifi yako au Ndugu yako huko aliko kwenye NGO umpeleke? Mheshimiwa Waziri Mkuu no control no utekelezaji no maamuzi. That’s why tunafikia hapo tunapofikia. Kwa kweli inasikitisha na mimi ninasema kwa uchungu sana. Je, huu ni utawala bora? Kwa kweli vitu vingine vinauma.
Source: http://www.parliament.go.tz/POLIS/PAMS/Doc/HS-16-11-2009.pdf
Kuanzia ukuraza wa 27.
 
Duh..... Kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni!!!!!!!!!

Nimekuja kuta information za huyu mama na Utouh, i think this mama is better by far, ukiondoa hoja za mambo binafsi ambapo kafeli mia kwa mia

I am praying for the truth to prevail
 
Blandina Nyoni ni mmoja katika wachapakazi mahili katika civil service ya Tanzania. She is a professional and a lady of intergrity; sehemu zote alizofanya kazi ameondoa uozo alioukuta; angalia tu alipokuwa Paymaster General, mishahara ilikuwa inalipwa on time na ghost workers wote wakatoweka kwenye payroll ya serikali!! Acheni majungu mpeni mama huyu sifa anazostahili. Mama Nyoni chapa kazi usiwasikilize hawa wachumia tumboni hawana maana kwa Taifa letu.

- Tupo pamoja sana hapo mkuu.

Respect.

FMEs!
 
- Tupo pamoja sana hapo mkuu.

Respect.

FMEs!

Tatizo ni moja tu mazee....... ushabiki, i have done my homework and changed my mind, but all i get from people like you is ushabiki with limited substancial support to prove something

Anyway, i come from Kigwe!!!!!!!
 
mama nyon yupo juu pls respect

Mhhh!
Just because!

Hii ni tabia ya kutotaka kusikia ubaya wa mtu fulani. Au ni sababu kama za EL kwamba hatukukutana barabarani? :))

Hivi karibuni Wizara ya afya imejikuta ikilazimika kununua suti, toka nje ya nchi kwa amri ya Nyoni huyo huyo eti zikiwa ni uniform za watumishi ktk maonesho ya nane nane. Muagizaji yaaminika ni mtoto wake, akijificha nyuma ya kampuni nyingine.

Bado ni kuchapa kazi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom