Katibu mkuu wa Wizara ya Afya lawamani (Blandina Nyoni)

Masanja,

..mama Nyoni nimekuwa nikimsikia sifa zake kwamba ni mchapa kazi.

..sasa kinachonishangaza ni kuja kufanya uamuzi kama huu --ikiwa madai ya Mbunge ni ya kweli.

..Tanzania sijui tuna matatizo gani hapa. yaani karibu kila mtu I have been looking up to amekuja kuni-disappoint.

NB:

..hili suala lilishazungumziwa mwanzoni.

..moderator, at your convinience, unaweza kuunganisha na thread ya zamani inayomhusu Blandina Nyoni.

Mkuu, ilianzishwa thread ya Mama Nyoni, lakini kwasababu alikuwa na wapambe humu yakaisha

The fact is that, Mama Nyoni is a good leader and a good follwoer of her strategies (or allies, need to say). However, if things go wrong, she really sink in so deep as she is one dimensional... kuna misala iko maliasili, kuanzia sabsaba money, mikataba na adverts, etc. etc. Being a key stakeholder at MOHSW kuna vimeo pia vipo humo

She is good as long as her strategies work but she isnt flexible hence high risk index

 
Waandishi bana, tangu yalipuke kule Mbagala sasa hivi neno ni "kulipua, kalipuliwa, kamlipua" Kaazi kweli kweli
 
Jamani iansikitisha sana kwa hii case....waiamue tu jamani na kama amestaafu inakuwaje anarudishwa serikalini????hii haikubaliki kabisa....
 
Namfahamu fika huyu mama nilikuwa nae Canada. Yeye alikuwa akifanya kazi katika ubalozi wa TZ pale Canada kama first officer.

Songea hoyeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Mi ninadhani hili jina Blandina Nyoni kama sikosei nalikumbuka liliwahi pia kutajwa katika maofisa wa serikali walioshiriki kikamirifu katika kufanikisha mikataba feki hasa ule wa Richmond! na ni miongoni mwa maofisa ambao kamati ya bunge ilishauri wawajibishe!
 
Namfahamu fika huyu mama nilikuwa nae Canada. Yeye alikuwa akifanya kazi katika ubalozi wa TZ pale Canada kama first officer.

Songea hoyeeeeeeeeeeeeeeeee

This is news!
Lets put the record straight jamani.
Alifanya kazi CIDA ( development cooperation arm of the Canadian High Commision Tanzania ) kama mhasibu na siyo First Officer Ubalozini Tanzania Canada.
 
..naona kina mama Shelukindo kaamua kumkomalia mama Nyoni PS wizara ya afya.

..kuna waliotetea utendaji wa mama Nyoni. binafsi sina habari zake zaidi ya kumsikia hapa jamii forums.

..kama kweli mama Nyoni ameteua Daktari aliyestaafu utumishi kwenda India, akamuacha aliyeko kwenye utumishi, basi atakuwa amefanya makosa.


Kwa kweli nchi haina mwenyewe kila mtu anasema lake anafanya lake ,kwani Blandina Nyoni ni mwana JF
 
Mi ninadhani hili jina Blandina Nyoni kama sikosei nalikumbuka liliwahi pia kutajwa katika maofisa wa serikali walioshiriki kikamirifu katika kufanikisha mikataba feki hasa ule wa Richmond! na ni miongoni mwa maofisa ambao kamati ya bunge ilishauri wawajibishe!

Alikuwa Board Chairman wa DAWASCO, alisababisha ulaji na uzembe wa utendaji wa DAWASCO mnaouona sasa.......alipokuwa katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, wakatunishiana misuli/walikuwa hawapatani na Waziri wake Shamsa Mwangunga kwani kila mtu anajiona anajua,na wakamwamisha wizara....cha ajabu nini?anaendeleza libeneke lake la u-much know
 
labda tungeanza kwa kumuuliza yeye huyo Beatrice ni wapi serikali imepitisha sheria ya uraia wa nchi mbili wakati wanae 4 wana passports mbili mbili
 
labda tungeanza kwa kumuuliza yeye huyo Beatrice ni wapi serikali imepitisha sheria ya uraia wa nchi mbili wakati wanae 4 wana passports mbili mbili


Kwi kwi kwi GT...sikuwezi.

B. Nyoni huyu ndiye aliyekuwa Hazina au Fedha na Mumewe yupo BoT. Au ni mwingine?
 
Wana JF; hii ngoma ilishatoka tangu mei na JF ikainyaka.

(Mwanahalisi toleo na. 137 Mei 20, 2009
Na Saed Kubenea
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni ametengua uteuzi wa Mwambata wa Afya katika ubalozi wa Tanzania nchini India katika mazingira ya kutatanisha, MwanaHALISI limeelezwa.
Tarehe 6 Agosti 2008, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Wilson Mukama alimteua Daktari Msaidizi Mwandamizi katika wizara hiyo, Edward Sawe, kuwa Mwambata wa Afya nchini India.
Taarifa zinasema uteuzi wake ulitenguliwa miezi minane baadaye kwa madai kuwa Dk. Sawe hakuwa na “sifa za kushika nafasi hiyo.”

Tayari uamuzi wa Nyoni umeisababishia serikali hasara ya dola 25,000 (sawa na Sh. 30 milioni) zilizolipwa kwa ajili ya pango la nyumba mjini New Delhi ambako Dk. Sawe angeishi na familia yake. Nyumba hiyo ilipangwa tangu tarehe 1 Oktoba mwaka jana. Gazeti hili limepata taarifa kuwa tarehe 6 Januari 2009, Nyoni alimuandikia barua Dk. Sawe kumtaka aripoti Ofisi ya Damu Salama (National Blood Transfusion Services) wakati akisubiri kukamilika kwa mipango ya safari.
Lakini miezi mitatu baadaye Nyoni alimwandikia Dk. Sawe na kumweleza kuwa hakuwa na sifa ya kushika wadhifa huo.
Barua ya Nyoni kwa Dk. Sawe inasema, “…Baada ya kupitia wasifu wako, imeonekana kwamba haukidhi matakwa ya kuwa Mwambata wa Ubalozi kuhusu masuala ya Afya nchini India...Kwa msingi huo, tutakupangia kazi nyingine hivyo uripoti kwa katibu mkuu kwa kupangiwa kazi nyingine.”
Akizungumza na MwanaHALISI wiki iliyopita, Nyoni alikiri kutengua uteuzi wa Sawe, lakini alisema hatua hiyo haikulenga kubeba mtu, bali kwa sababu “Serikali inataka kupeleka mtu mwenye sifa.”
“Uteuzi wake umetenguliwa kwa mujibu wa kanuni za utumishi. Mimi kama mwajiri ndiye ninayepanga kazi. Hivyo ndivyo nilivyofanya kwa Sawe. Kule India, hatupeleki karani. Tunapeleka daktari bingwa ili kutimiza lengo lililokusudia,” alisema kwa sauti ya ukali.
Nyoni alisema daktari anayehitajika ni yule atakayeweza “kujadiliana na madaktari wa India ili kujua wagonjwa tunaowapeleka wanahitaji huduma gani na kuhakikisha wanahudumiwa kutokana na magonjwa yanayowasumbua.”
Alikuwa akijibu hoja kwa nini Dk. Sawe ambaye amekuwa katika kitengo cha kusafirisha wagonjwa wa Tanzania kwenda nchi za nje asiweze kuwa na sifa za kuwa mwambata wakati kazi hiyo haihusishi ubingwa katika tiba.
Alipong’ang’anizwa kutoa maelezo zaidi kuhusu mashaka yake kwa Dk. Sawe, na kwa nini Mukama aliona anafaa au yeye alitaka kuweka “mtu wake,” Nyoni alisema “Naomba uje ofisini kwangu tuzungumze.”
“Ninakuheshimu sana kwa sababu ya msimamo wako. Siwezi kuzungumzia mambo ya ajira katika simu. Nakuomba uje ofisini kwangu tuzungumze,” alisema kwa upole.
Alisema, “Kaka yangu hapa kuna majungu mengi sana. Watu wa hapa hawataki mtu wa kuwasimamia. Kuna majungu kila kona hapa. Watu wananisakama. Nakuomba usiingie huko.”
Alipoambiwa kwamba tayari kuna madai kuwa ameteua “mtu wake,” mwanamke aliyetajwa kwa jina la Dk. Chale na ambaye hana sifa ya kushika nafasi hiyo kwa kuwa si mtumishi wa serikali, mara hii Nyoni aling’aka akisema:
“Hapana. Njoo hapa, nitakuonyesha CV zake. Ni mtumishi wa serikali. Huyu unayemtaja yupo Muhimbili (Hospitali ya taifa). Anafanya kazi pale kama daktari bingwa,” alisema.
MwanaHALISI ilimuuliza Mukama kutaka kujua iwapo aliteua mwambata asiyekuwa na sifa, naye alisema, “Muulizeni mhusika. Mimi sipo huko tena.”
Taarifa za ndani ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Hazina zinasema Sawe alishagharamiwa safari pamoja na familia yake kwenda India na kwamba alijulishwa usitishaji dakika za mwisho.
Sawe alijulishwa mabadiliko baada ya kusubiri ruhusa ya Nyoni kwa muda mrefu kinyume na matarajio yake kwa kuwa mipango mingine ilikuwa imekamilika ikiwemo mkewe kupata likizo kazini kwake.
Daktari mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe aliiambia MwanaHALISI kuwa kazi ya mwambata haihitaji daktari bingwa. “Hiyo itakuwa kupoteza mtaalamu anayehitajika zaidi nchini. Hapa anahitajika daktari wa kawaida anayemudu kutambua magonjwa mbalimbali,” amesema.
Uzoefu unaonyesha kwamba madaktari wanaofuatana na wagonjwa waliotoka nchini huwa hawatibu isipokuwa kutoa maelekezo tu ya historia ya mgonjwa na kuratibu tiba yake itakavyokuwa inafanyika.
Serikali imeamua kuteua daktari wa kushughulikia jukumu hilo nchini India kwa vile ndiko wagonjwa wengi wanakopelekwa baada ya tiba zao kushindikana kwenye hospitali za nchini.
Tanzania inapeleka wagonjwa wengi wa maradhi mbalimbali kila mwaka nchini India.
Uteuzi wa mwambata wa afya unafuatia ziara ya Makamu wa Rais, Mohammed Shein nchini India, Machi mwaka jana alipoagiza ubalozi uwe na ofisa wa kushuhgulia masuala ya afya (Medical Attache).
Barua ya ubalozi wa Tanzania mjini New Delhi, Kumb. THC/ND/PF.186 ya tarehe 23 Oktoba 2008 iliyosainiwa na Yahya A. Mhata kwa niaba ya balozi inatoa mchanganuo wa gharama za pango la nyumba ya mwambata.
Kwa mujibu wa barua hiyo, Rupia 80,000 ni pango kwa mwezi na kwa mwaka inakuwa Rupia 960,000, wakati gharama ya wakala wa nyumba ni Rupia 40,000. Jumla ni Rupia 1,000,000 (sawa na dola 25,000 wakati huo).
Barua ya balozi ilikuwa ikijibu barua ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Kumb. AB 226/580/01/114. MwanaHALISI inayo mawasiliano yote kuhusiana na suala hili
 
Tanzania kuna upungufu wa madaktari, hivyo kwa nini walikuwa wanampeleka daktari India kuwa co ordinator ubalozini wakati hiyo kazi hata medical assistant wanaweza? Mi nafikiri alifanya vema kubadili uamuzi wa mwanzo...
 
labda tungeanza kwa kumuuliza yeye huyo Beatrice ni wapi serikali imepitisha sheria ya uraia wa nchi mbili wakati wanae 4 wana passports mbili mbili

GT Nakumbuka tangu mjadala wa kwanza wa Blandina Nyoni wewe ulikuwa mtetezi wake. You are still a staunch ally of the woman.

Nyoni hawezi kuwa sahihi eti tu kwa sababu Beatrice ana makosa.

Please, please regain your JF reasoning!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom