Katibu mkuu wa Wizara ya Afya lawamani (Blandina Nyoni) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu mkuu wa Wizara ya Afya lawamani (Blandina Nyoni)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, May 23, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,219
  Likes Received: 5,617
  Trophy Points: 280
  • Atuhumiwa kusababisha hasara serikalini
  KATIBU Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni ametengua uteuzi wa Mwambata wa Afya katika ubalozi wa Tanzania nchini India katika mazingira ya kutatanisha, MwanaHALISI limeelezwa.

  Tarehe 6 Agosti 2008, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Wilson Mukama alimteua Daktari Msaidizi Mwandamizi katika wizara hiyo, Edward Sawe, kuwa Mwambata wa Afya nchini India.

  Taarifa zinasema uteuzi wake ulitenguliwa miezi minane baadaye kwa madai kuwa Dk. Sawe hakuwa na “sifa za kushika nafasi hiyo.”

  Tayari uamuzi wa Nyoni umeisababishia serikali hasara ya dola 25,000 (sawa na Sh. 30 milioni) zilizolipwa kwa ajili ya pango la nyumba mjini New Delhi ambako Dk. Sawe angeishi na familia yake. Nyumba hiyo ilipangwa tangu tarehe 1 Oktoba mwaka jana.

  Gazeti hili limepata taarifa kuwa tarehe 6 Januari 2009, Nyoni alimuandikia barua Dk. Sawe kumtaka aripoti Ofisi ya Damu Salama (National Blood Transfusion Services) wakati akisubiri kukamilika kwa mipango ya safari.

  Lakini miezi mitatu baadaye Nyoni alimwandikia Dk. Sawe na kumweleza kuwa hakuwa na sifa ya kushika wadhifa huo.

  Barua ya Nyoni kwa Dk. Sawe inasema, “…Baada ya kupitia wasifu wako, imeonekana kwamba haukidhi matakwa ya kuwa Mwambata wa Ubalozi kuhusu masuala ya Afya nchini India...Kwa msingi huo, tutakupangia kazi nyingine hivyo uripoti kwa katibu mkuu kwa kupangiwa kazi nyingine.”

  Akizungumza na MwanaHALISI wiki iliyopita, Nyoni alikiri kutengua uteuzi wa Sawe, lakini alisema hatua hiyo haikulenga kubeba mtu, bali kwa sababu “Serikali inataka kupeleka mtu mwenye sifa.”

  “Uteuzi wake umetenguliwa kwa mujibu wa kanuni za utumishi. Mimi kama mwajiri ndiye ninayepanga kazi. Hivyo ndivyo nilivyofanya kwa Sawe. Kule India, hatupeleki karani. Tunapeleka daktari bingwa ili kutimiza lengo lililokusudia,” alisema kwa sauti ya ukali.

  Nyoni alisema daktari anayehitajika ni yule atakayeweza “kujadiliana na madaktari wa India ili kujua wagonjwa tunaowapeleka wanahitaji huduma gani na kuhakikisha wanahudumiwa kutokana na magonjwa yanayowasumbua.”

  Alikuwa akijibu hoja kwa nini Dk. Sawe ambaye amekuwa katika kitengo cha kusafirisha wagonjwa wa Tanzania kwenda nchi za nje asiweze kuwa na sifa za kuwa mwambata wakati kazi hiyo haihusishi ubingwa katika tiba.

  Alipong’ang’anizwa kutoa maelezo zaidi kuhusu mashaka yake kwa Dk. Sawe, na kwa nini Mukama aliona anafaa au yeye alitaka kuweka “mtu wake,” Nyoni alisema “Naomba uje ofisini kwangu tuzungumze.”

  “Ninakuheshimu sana kwa sababu ya msimamo wako. Siwezi kuzungumzia mambo ya ajira katika simu. Nakuomba uje ofisini kwangu tuzungumze,” alisema kwa upole.

  Alisema, “Kaka yangu hapa kuna majungu mengi sana. Watu wa hapa hawataki mtu wa kuwasimamia. Kuna majungu kila kona hapa. Watu wananisakama. Nakuomba usiingie huko.”

  Alipoambiwa kwamba tayari kuna madai kuwa ameteua “mtu wake,” mwanamke aliyetajwa kwa jina la Dk. Chale na ambaye hana sifa ya kushika nafasi hiyo kwa kuwa si mtumishi wa serikali, mara hii Nyoni aling’aka akisema:

  “Hapana. Njoo hapa, nitakuonyesha CV zake. Ni mtumishi wa serikali. Huyu unayemtaja yupo Muhimbili (Hospitali ya taifa). Anafanya kazi pale kama daktari bingwa,” alisema.

  MwanaHALISI ilimuuliza Mukama kutaka kujua iwapo aliteua mwambata asiyekuwa na sifa, naye alisema, “Muulizeni mhusika. Mimi sipo huko tena.”

  Taarifa za ndani ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Hazina zinasema Sawe alishagharamiwa safari pamoja na familia yake kwenda India na kwamba alijulishwa usitishaji dakika za mwisho.

  Sawe alijulishwa mabadiliko baada ya kusubiri ruhusa ya Nyoni kwa muda mrefu kinyume na matarajio yake kwa kuwa mipango mingine ilikuwa imekamilika ikiwemo mkewe kupata likizo kazini kwake.

  Daktari mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe aliiambia MwanaHALISI kuwa kazi ya mwambata haihitaji daktari bingwa. “Hiyo itakuwa kupoteza mtaalamu anayehitajika zaidi nchini. Hapa anahitajika daktari wa kawaida anayemudu kutambua magonjwa mbalimbali,” amesema.

  Uzoefu unaonyesha kwamba madaktari wanaofuatana na wagonjwa waliotoka nchini huwa hawatibu isipokuwa kutoa maelekezo tu ya historia ya mgonjwa na kuratibu tiba yake itakavyokuwa inafanyika.

  Serikali imeamua kuteua daktari wa kushughulikia jukumu hilo nchini India kwa vile ndiko wagonjwa wengi wanakopelekwa baada ya tiba zao kushindikana kwenye hospitali za nchini.

  Tanzania inapeleka wagonjwa wengi wa maradhi mbalimbali kila mwaka nchini India.

  Uteuzi wa mwambata wa afya unafuatia ziara ya Makamu wa Rais, Mohammed Shein nchini India, Machi mwaka jana alipoagiza ubalozi uwe na ofisa wa kushuhgulia masuala ya afya (Medical Attache).

  Barua ya ubalozi wa Tanzania mjini New Delhi, Kumb. THC/ND/PF.186 ya tarehe 23 Oktoba 2008 iliyosainiwa na Yahya A. Mhata kwa niaba ya balozi inatoa mchanganuo wa gharama za pango la nyumba ya mwambata.

  Kwa mujibu wa barua hiyo, Rupia 80,000 ni pango kwa mwezi na kwa mwaka inakuwa Rupia 960,000, wakati gharama ya wakala wa nyumba ni Rupia 40,000. Jumla ni Rupia 1,000,000 (sawa na dola 25,000 wakati huo).

  Barua ya balozi ilikuwa ikijibu barua ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Kumb. AB 226/580/01/114.

  MwanaHALISI inayo mawasiliano yote kuhusiana na suala hili.
   
 2. K

  Kamongo JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2009
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Namuunga mkono mama Nyoni 100% huyo W Mkama hapo wizara ya Afya tumemchoka ukabila kaweka mbele kwani anafanya mpango akishirikiana na kigogo mmoja wa Ikulu kuhakikisha mkurugenzi wa NIMR anakuwa mtu wa kutoka kwao BK..........a
   
 3. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wilson Mukama sio mtu wa Bukoba bali Musoma.
   
 4. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Mama Nyoni, ni kiongozi makini sana ni wachache sana bongo wa calliber yake, nilisema toka alipohamishiwa huku kuwa yeye na Sister Mapunjo ni balaa!

  Respect.

  FMEs!
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,219
  Likes Received: 5,617
  Trophy Points: 280
  Na masha??
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  May 23, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Masha si bado waziri au?

  FMEs!
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  May 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,219
  Likes Received: 5,617
  Trophy Points: 280
  Yeah br
  hav a nyc weekend sijakuona siku nyingi kidogo
   
 8. Sukununu

  Sukununu Member

  #8
  May 23, 2009
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 22
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  MwanaHALISI angesaidia sana wasomaji wake kama angetoa "Job Description" ya Medical Attache kwa sababu watu waliotajwa katika habari hii ni madaktari, japo kwa viwango tofauti.

  Huyu Dr. Chale ninahisi atakuwa ni Dr. Stella Chale ambaye ni daktari bingwa pale Muhimbili upande wa Internal Medicine. Ni daktari bingwa wa miaka mingi tu. Kama sikosei alimaliza digrii ya kwanza ya Medicine mwaka 1983 na specialization kwenye internal medicine mwaka around 1989/1990. Ni daktari mzuri tu na mchapakazi mzuri.

  Dr. Edward Sawe atakuwa ni Assistant Medical Officer (AMO), naye ni wa miaka mingi kidogo. (He was my classmate in Secondary School, 1972-1975). Japokuwa hatujaonana miaka mingi, ninaamini atakuwa bado ni mtu wa integrity na principles kama nilivyomfahamu.

  AMOs wana uwezo na ujuzi wa kufanya kazi nyingi tu karibu sawa na graduate wa medicine.

  Mama Blandina Nyoni naye anaeleweka kuwa mtu mwenye track record nzuri ya utumishi serikalini. Hivyo MwanaHALISI angefanya homework kidogo ya kutafuta requirements za Medical Attache, ili kutusaidia kuelewa kinachodaiwa kwenye habari hii. Nina wasiwasi kuwa huenda watu wanalinganisha majina: Nyoni & Chale (Songea), Sawe (Moshi) hivyo Sawe out!

  Labda kumpa benefit of doubt mwandishi wa habari hii: Wagonjwa wanaopelekwa India wana matatizo ya aina mbali, mengine yapo kwenye nyanja tofauti na specialization ya Dr. Chale ya Internal Medicine. Kwa hiyo "rationale" ya kuwa na daktari bingwa kuwa mwambata inakuwa ngumu kueleweka.
   
 9. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2009
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii habari imekaa kimajungu sana. Mwanahalisi hawajatuambia sifa za huyo Sawe, kulinganisha na sifa zinazotakiwa kwa mtu kushika nafasi hiyo.

  Maelezo ya mama Nyoni yanajieleza, mtu hakuwa na sifa. Sasa kung'ang'ania kuwa midhali pango limeshalipwa basi ndio lizuie kiongozi kurekebisha makosa!... Hivi tunataka viongozi wetu wasiwe na ujasiri wa kuchukua hatua kwa kuogopa kuandikwa magazetini?

  Mwanahalisi can do better than that. So far mama Nyoni is right.
   
 10. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #10
  May 23, 2009
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280

  Samahani kidogo maana kuna watu wanavuna sifa bila sababu. Huyu ni Nyoni aliyetoka Maliasili na Utalii??

  If yes! ni mmoja wa mafisadi wanaoibuka kwa nguvu. Maliasili aliwapa shida kubwa ya kila wakati kutaka amegewe pesa za wafadhili. kidogo alipata ugumu na okoka yao ilikuwa uhamisho maana alisha waahidi kipigo.

  Kumbukeni Maliasili ni wizara ambayo imeweka sura mbaya kwa matumizi ya pesa za wafadhili.
   
 11. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Ndiyo huyo huyo mama Blandina Nyoni aliyekuwa Maliasili na Utalii.
   
 12. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0


  Haya ni majungu! Mama Nyoni alifanya kazi nzuri ya kuwadhibiti wabadhilifu wa Wizara hiyo na bila shaka kaletwa Wizara ya Afya ajaribu kusafisha uozo uliopo Wizarani hapo.

  Nakubaliana na aliyesema kwamba Kubenea hakufanya homework yake ipasavyo kabla ya kuandika kumtetea Sawe. Huyu Dr. Sawe kama ilivyoelezwa ni AMO ambaye kwa miaka kadhaa amekuwa Wizarani. Lini ameweza kupata uzoefu wa kazi yake ya udaktari hata kuweza kuhudumia wagonjwa wenye maradhi ya kila aina yaliyoshindikana kutibiwa nchini? Wizarani kuna wagonjwa gani wa kuwaangalia na kutibu ukilinganisha na uzoefu wa Dr. Chale specialist wa Internal Medicine ambaye shughuli zake za kila siku Muhimbili ni kuona na kuhudumia wenye magonjwa mbalimbali?

  Binafsi, naomba Mama Nyoni apangue kikosi kizima cha watendaji katika kitengo cha kupeleka wagonjwa nje kwa sababu watumishi wa kitengo hicho hawafai kuhudumia wagonjwa. Kubenea ana bahati kwamba tatizo lake lilichukuliwa ‘kisiasa’ akapokelewa kama ‘mfalme’ na kupelekwa haraka haraka kwenda kutibiwa nje. Nashangaa kwa nini hakuweza kufanya homework yake vizuri na kujua sababu hasa za msingi ziliyofanya jina la Sawe lifutwe.

  Maafisa wa kitengo hicho wanatoa sura mbaya ya Wizara ya Afya kutokana na utendaji kazi wao mbovu usiozingatia maadili ya kazi ya uuguzi ama udaktari. Baadhi yao, wanapowasindikiza wagonjwa kwenda kutibiwa India huenda kama watalii tu kwa sababu hakuna kazi yoyote ya maana wanayofanya wakifika huko zaidi ya kunywa pombe na kwenda shopping. Kazi zote hufanywa na Afisa Ubalozi tena katika mazingira magumu kwa sababu anapaswa kwenda kupokea wagonjwa Airport, kuwafikisha hospitalini na kuhakikisha kwamba wanapokelewa na inabidi ajue kila wodi aliyolazwa mgonjwa na daktari anayemuhudumia. Wakati mwingine kwenye hospitali moja wanakuwepo wagonjwa zaidi ya 40 kutoka Tanzania. Kwa hiyo kila siku Afisa huyo hupita kuzungumza na madaktari na kujua maendeleo ya kila mgonjwa na kuweka kumbukumbu. Kazi hii ingeliweza kabisa kufanywa na muuguzi/daktari msindikizaji lakini sijui kama wanaifanya kikamilifu.

  Yupo jamaa yangu aliyetoka kutibiwa India hivi karibuni anaeleza kwamba walisindikizwa na muuguzi ambaye hata kujieleza kwa Kiingereza hajui kwa hiyo alikuwa akiwapiga chenga wagonjwa ili mapungufu yake yasidhihirike. Kwa hali hiyo ilibidi wagonjwa wengine wafanye kazi ya ukalimani kuwasaidia wagonjwa wenzao ambao hawajui kiingereza kueleza ugonjwa kwa madaktari!

  Mama Nyoni akiwafuta watumishi wa aina hii baadhi yetu tutasema anawaonea ama hafai!!!

  Tunaomba aliyeandika article hii afanye utafiti wa kutosha na atuletee taarifa sahihi za matatizo ya Dr. Sawe dhidi ya uzoefu na utaalamu wa Dr. Chale.
   
 13. O

  Ogah JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  1................kutokana na maelezo hapo juu yaonekana hata Dr Sawe anaweza kufanya hiyo kazi..............unless mtuwekee vigezo vinavyohitajika kwa kazi hiyo amabvyo vita-prove otherwise

  2. Najiuliza kwa nini pesa ipotee kama sehemu ya kuishi ilikodiwa na endapo muda wake haujesha

  3...........Kama wagonjwa wanapelekwa kuonana na Madaktari Bingwa huko India na NDIO HASWA KISA CHA WAGONJWA KUPELEKWA huko kwanini tena tuchukue mabingwa wetu walioshindwa kuwa-attend hao wagonjwa na kuwapeleka India.........kufanya nini........na kama kazi inaweza kufanywa na Muuguzi ambaye ni experienced...why sending mabingwa wetu?..........

  Anyway tupeni requirements za hiyo kazi ili tujue
   
 14. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Atuhumiwa kusababisha hasara serikalini

  "Anatuhumiwa" na nani?

  Wewe Kubenea ndie ulimfanya interview hukuridhika na majibu yake.
  Ulitakiwa utafute mtu/watu wengine huru ndio wao "third party" wamtuhumu Nyoni halafu wewe Kubenea uripoti Nyoni anatuhumiwa, na utaje wanaomtuhumu. Vinginevyo ni makala, opinion.

  Nyumba hiyo ilipangwa tangu tarehe 1 Oktoba mwaka jana...... tarehe 6 Januari 2009, Nyoni alimuandikia barua Dk. Sawe kumtaka aripoti Ofisi ya... wakati akisubiri kukamilika kwa mipango ya safari.

  Aliyesababisha hasara ni yule aliyeisaini mkataba wa nyumba toka October mwaka jana wakati uteuzi ulikuwa hata haujakamilika haujakamilika by January? Huyo ndie kasabisha hasara.
  Nyoni alikuwepo wizarani wakati mnakodi nyumba India wakati hata mfanyakazi hajafika India!

  Taarifa za ndani ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Hazina zinasema Sawe alishagharamiwa safari pamoja na familia yake kwenda India na kwamba alijulishwa usitishaji dakika za mwisho.

  Waligharimia vipi safari wakati mtu hakusafiri, manake umesema wali cancel dakika ya mwisho. Nani alilipa malipo hewa hayo, Nyoni au wengine?

  Tarehe 6 Agosti 2008, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Wilson Mukama alimteua Daktari Edward Sawe, kuwa Mwambata wa Afya nchini India...Sawe alijulishwa mabadiliko baada ya kusubiri ruhusa ya Nyoni kwa muda mrefu ...

  Kama alishateuliwa na Katibu Mkuu wa zamani, kwa nini alihitaji kusubiri ruhusa ya Katibu mpya?

  Daktari mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe aliiambia MwanaHALISI kuwa kazi ya mwambata haihitaji daktari bingwa. “Hiyo itakuwa kupoteza mtaalamu anayehitajika zaidi nchini. Hapa anahitajika daktari wa kawaida anayemudu kutambua magonjwa mbalimbali,” amesema.

  Hii inawezekana umetunga mwenyewe, mtaje huyo mtu ili tujue "anatuhumiwa" na nani. Mtaje.


  Kwa mujibu wa barua hiyo, Rupia 80,000 ni pango kwa mwezi na kwa mwaka inakuwa Rupia 960,000, wakati gharama ya wakala wa nyumba ni Rupia 40,000. Jumla ni Rupia 1,000,000 (sawa na dola 25,000 wakati huo).

  Mwenye makosa ni huyo aliyelipia pango la mwaka mzima, tena hata mpangaji hajafika. Huyo ndie aliyesababisha hasara.


  Alipong’ang’anizwa kutoa maelezo zaidi... Nyoni alisema “Naomba uje ofisini kwangu tuzungumze....Siwezi kuzungumzia mambo ya ajira katika simu. Nakuomba uje ofisini kwangu tuzungumze...Hapana. Njoo hapa, nitakuonyesha CV zake. Ni mtumishi wa serikali. Huyu unayemtaja yupo Muhimbili (Hospitali ya taifa). Anafanya kazi pale kama daktari bingwa,” alisema.”

  Sasa kwa nini hukwenda ofisini kwa Nyoni kupata maelezo ya huyo Nyoni ili utuletee complete story ?

  Kubenea ana potential ya kuwa bonge la dirt-dredging journalist, maana jamaa ni fearless hakuna mfano lakini anahitaji bonge la editor wa kumpiga brashi. Lakini hapo MwanaHALISI yeye ndio editor.
   
 15. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  AMO hawezi kuwa karibu sawa na MD labda yesu arudi. Usitake kumtetea kisa mlikuwa naye shule ya msingi.

  Mtu anayepanga kazi na anayezijua requirements and job description za medical attache keshakuambia huyo "dr" Sawe hana sifa stahiki wewe wataka uletewe criteria ufanye maamuzi? Uko serious au wacheza "rede"?

  Pamoja na mambo mengine huyo ndiye atakuwa "facebook" ya madaktari wa Tanzania - sasa ukimpeleka AMO hata katika discussion na madaktari kule atamudu vipi - shule atakuwa anayo ndogo sana.
   
 16. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani muacheni Mama Nyoni afanye vitu vyake
   
 17. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Haya ni majungu! Mama Nyoni alifanya kazi nzuri ya kuwadhibiti wabadhilifu wa Wizara hiyo na bila shaka kaletwa Wizara ya Afya ajaribu kusafisha uozo uliopo Wizarani hapo.

  Ni kazi gani nzuri aliyoifanya huyu mama Wizara ya Maliasili na Utalii? Nikiwa kama mdau wa karibu wa Wizara hii, naomba ueleze angalau fanikio moja la huyu mama alipokuwa Maliasili. Na kama alifanikiwa ni kwanini aliondolewa wakati Wizara bado ina matatizo kibao? Ninafikiri Nyoni ni miongoni mwa makatibu wakuu waliokaa muda mfupi sana Maliasili. Kweli alifanikiwa huyu?
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  May 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Dr. Chale ninamfahamu binafsi kwa muda mrefu sana; sina shaka na ujuzi au utaalamu wake. Hofu yangu ni kuwa asije akajikuta amekuwa bangusilo wawenye nguvu. Lakini napenda mwajiri awe na uwezo wa kumpanga mtu au kumtimua mtu kama anavyoona anafaa.. haya mambo ya kufikiri ajira ya umma ni kama haki ya mtu yamepitwa na wakati. Kama mkataba unaweka room ya kuondolewa "for any reason or no reason" basi ndiyo hivyo tena.

  Ila upande mwingine, naamini Dr. Chale kumpeleka India ni kuondoa utaalamu na uzoefu mkubwa nyumbani. Kama wanataka kumpangia kazi basi wampe kazi ya kusimamia programu ya wagonjwa wote wanaopelekwa nje (siyo India tu) na waende kwa idhini yake. Hapo ndipo wataweza kumtumia vizuri kuliko kumpeleka India ambako kuna madaktari wengi tu!
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ile ni medical tourism, anayehitajika ni zaidi ya Daktari bingwa... there coordination, logistcis and other skills associated with utalii-tiba. You can send the best specialist na akashindwa

  Na experience inaonyesha most of madaktari bingwa si wazuri kwenye PR na logistics...
   
 20. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Perception yako usiifanye kama experience. Unawajua wangapi out of wangapi? Toa mfano.
   
Loading...