Katibu mkuu wa CCM tunaomba utembelee Kata ya Matundasi iliyopo Wilaya ya Chunya, vijiji vyote Tangu uhuru havijawahi kupata maji safi na salama

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,829
21,460
Kwa masikitiko makubwa na hizi ni kubwa, ninaomba kumjulisha Katibu Mkuu wa CCM kuwa, Kata ya Matundasi iliyopo Wilaya ya Chunya, mkoa wa mbeya.

Haina maji safi na salama Tangu Tanzania upate uhuru hadi leo.
Kata ya Matundasi ina vitongoji vifuatavyo:-
Itumbi
Kisimani
Makatang'ombe
Matondo
Matundasi a
Matundasi b
Nanyuki
Nzingwa

Vitongoji vyote hivi vinaongozwa na CCM , Diwani wa CCM, Mbunge wa CCM .

Kumekuwa na kuibuka Kwa magonjwa na wananchi wengi hawana vyoo , wanajisaidia porini, hakuna maji safi na salama, hakuna Tarura( barabara ni mbovu) , hakuna shule za msingi na za sekondari za kutosha idadi ya wananchi walioko maeneo hayo, hakuna mitandao ya simu, hakuna vituo vya polisi, hakuna zahanati za kutodha idadi ya watu, ninsomba Katibu mkuu wa CCM atembelee kata hii akiwa na viongozi au mawaziri wafuatao:-

1. Waziri wa mambo ya ndani ya nchi.- Hakuna vituo vya polisi
2. Waziri wa Maji ( Juma Aweso) - Hajuna maji safi na salama
3. Waziri wa Afya- Hakuna vituo vya afya na wananchi wanajisaidua porini.
4. Waziri wa Elimu - Hakuna shule za msingi na sekondari wala chuo.
5. Waziri wa mawasiliano- Hakuna mawasiliano ya simu.
6. Waziri wa ujenzi - Hakuna Barabara za kudumu.
7. Waziri wa Madini - Aje aone wananchi wanavyo zalisha madini na hawapati huduma taja hapi juu.

Tutashukuru iwapo ujio wa kiongozi huyu itafanyika mapema kuinusuru kata ya matundasi na wananchi wake.
 
Back
Top Bottom