Katiba tuliyonayo haitoi tafsiri yoyote kuhusu uchochezi

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wanabodi,

Mengi yametokea katika kinyang'anyiro hiki cha kudai tume huru na katiba mpya na mengi yatazidi kutokea. Hatujapata uamuzi wowote ila ni vyema kama tungetupia jicho kwenye katiba tuliyonayo sasa hivi kupata tafsiri ya yanayoendelea.

Zimepita siku chache tangia mwenyekiti wa baraza la wazee la CHADEMA kukamatwa na IGP Sirro alieleza kwamba makosa yaliyomfanya Hashim Juma kushikiliwa na polisi ni:
1. Maneno ya uchochezi
2. Maneno ya kujenga chuki kati ya wananchi na serikali



- Kitu cha kujiuliza baada ya kupokea habari ni tafsiri ya maneno ya uchochezi na tafsiri ya maneno ya kujenga chuki kati ya wananchi na serikali. Kitu ambacho unaweza kugundua ni kwamba maneno ya namna hiyo lazima yanatolewa na watu wengi haswa ambao wanaweza wasiwe na umaarufu au wadhifa kama mwenyekiti wa baraza la wazee wa CHADEMA.

Inawezekana kabisa kuwa na idadi kubwa ya watu wasiotumia mitandao vizuri au wasiokuwa na kauli nzuri katika shughuli zao za kila siku kufanya makosa kama haya na kukwepa mkono wa sheria kwasababu hawana ushawishi au hawasikilizwi na watu wengi katika kipindi ambacho wanafanya uchochezi huu.

Sambamba na hayo ni vyema kama tunge mtazama mlengwa wa maneno ya uchochezi. Hii sio mara ya kwanza kwa mwana CHADEMA kukamatwa kwasababu ya maneno ya uchochezi lakini je, maneno ya uchochezi yana adhari ipi kwa wananchi?

Je, mwananchi wa kawaida ana akili timamu na anaweza kupuuza maneo kama hayo?. Je katiba yetu inasema nini kuhusu hayo?

-18(1): Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
Kwa bahati mbaya katiba yetu haitoi tafsiri yoyote kuhusu maneno ya uchochezi na mipaka ya haki ya kujieleza
 
Uchochezi ulikuwa unatumiwa na sheria za kikoloni kuwagandamiza wakosoaji wao kipindi kile cha vuguvugu la kudai uhuru.
 
Back
Top Bottom