Katiba sifuri ya CUF kuvunja Muungano na kuitambua Tanganyika

..Zenj ni ndogo mno. hawa siyo saizi yetu kabisa kuungana nao.

..sasa hiyo serikali ya muungano itahusisha mambo yepi, na itachangiwa namna gani?

..hivi mnategemea Gavana wa Tanganyika atakubali kupokea maelekezo ya Raisi wa Muungano aliyetokea Zanzibar?

..nitaendelea kusisitiza kwamba ni bora tu muungano uvunjwe na tushirikiane na wa-Zenj kupitia East African Community.
 
Kwa hiyo kufa kwa Tanganyika sio dhuluma, ila kufa kwa Zenj ni dhuluma? Na kuvunja Zenj nina maana mikoa mitano ya Zenj iwe assimilated kwenye Serikali moja. Kama utaita majimbo au miko kwangu mi naona ni semantics, sio muhimu!

Mkuu,

Nani aliiua Tanganyika? na ni kwa sababu gani? Hivi kweli Tanganyika imeuliwa au Imekufa?
 
Rwanda na Burundi hawajaomba kuungana. Wao wanataka kushirikiana katika shirikisho la Afrika mashariki. Tanganyika na Zanzibar ziliungana, lakini tulipokosea ni kutozungumzia mizani ya equality. Haiwezekani nchi yenye watu 2.5 millioni ikawa na mizani sawa na watu 41 millioni. Niliwahi kusema kwingineko kuwa California na Rhode Island hawana nguvu sawa katika mwungano wa United States of America. Ni hilo tu. Zanzibar inaweza kuwa na sovereignty yake lakini isilingane na ya Tanganyika.

Mkuu,

Hata Tanganyika na Zanzibar hazikuungana katika hali ambayo wengi humu wanamaanisha. Tanganyika na Zanzibar waliunganisha baadhi ya mambo tu. Na kile nchi ikaendelea na mambo yake ambayo hayakuwa ya muungano. Kwa mantiki hii unataka ifahamike kuwa Tanganyika ilikufa? au iliondoka?
Au nakosea wapi, mkuu
 
..watu wanafikiri kuongoza nchi na serikali ni sawasawa na kuongoza vikao vya UN au AU.

..linapokuja suala la utawala, au serikali,haiwezekani hata siku moja watu milioni 41 wawe sawasawa na watu milioni 2.5.

..Zenj ina historia yake na identity yake ambaye wananchi wake wameelekeza bayana kwamba ni lazima ilindwe. kwa msingi huo ni sawasawa kuwapa some kind of autonomy.

..wa-Tanganyika nao wako wengi, na nchi yao ni kubwa. sasa ni vizuri muungano ukatambua hilo, zaidi serikali ya muungano lazima iwe more accomodating kwa wa-Tanganyika.

..kwa maoni yangu, muungano wa serikali tatu, ambapo Tanganyika na Zanzibar ni equal partners ktk serikali ya muungano, ni impracticable.

..ama tuwe na serikali moja, au tuendelee na hizi serikali mbili, au kila upande uchukue chake tukashirikiane kupitia EAC.
 
Rwanda na Burundi hawajaomba kuungana. Wao wanataka kushirikiana katika shirikisho la Afrika mashariki. Tanganyika na Zanzibar ziliungana, lakini tulipokosea ni kutozungumzia mizani ya equality. Haiwezekani nchi yenye watu 2.5 millioni ikawa na mizani sawa na watu 41 millioni. Niliwahi kusema kwingineko kuwa California na Rhode Island hawana nguvu sawa katika mwungano wa United States of America. Ni hilo tu. Zanzibar inaweza kuwa na sovereignty yake lakini isilingane na ya Tanganyika.

Mkuu,

Zanzibar iliomba kuungana na Tanganyika?
Baada ya kupitia ushahidi wa kihistoria- Kweli tunaweza kusema kuwa Zanzibar waliomba kuungana na Tanganyika?
Au ni Mwalimu ndiye aliye-initiate muungano? na kwa sababu gani? Hata ukipitia uendelezaji/uimarishaji wa muungano,mlolongo wa matukio wakati wa kipindi chote hiki cha Muungano unafikia hitimisho kuwa Zanzibar waliomba Kujiunga na Tanganyika? na wanataka nchi moja na serikali moja?

Last edited by a moderator:
Nonda,

..mbona mlolongo wa matukio unaonyesha kwamba Karume & co., walimtegemea Mwalimu na Tanganyika kuliko kinyume chake?

..kwanza kabla ya Mapinduzi, Karumeb na Abdulrahman Babu walikuwa Tanganyika.

..pia tumesoma kuhusu ushiriki wa Tanganyika ktk kumchomoa John Okello kutoka ktk utawala wa Zanzibar.

..je, ni nani aliwaomba wa-Tanganyika wasaidie ktk kumteka nyara Okello na kumrudisha Uganda?

..kuna kikosi cha Polisi toka Tanganyika kilichokwenda Zanzibar kusaidia ulinzi baada ya Mapinduzi.

..kuna kila sababu za kuamini kwamba bila Tanganyika ku-side na SMZ basi Sultani Mwarabu angeweza kurudi Zanzibar.

..kwa mtizamo wangu, bila Muungano, Zanzibar ingeweza kuwa unstable and prone to coups d'etat like Comoro islands.
 
Mkuu, nilivyosikia mimi ni kwamba Karume aliutaka mwungano zaidi ya Nyerere. Aliogopa kupinduliwa .
 
Last edited by a moderator:
Mimi napendelea serikali moja, tupunguze gharama, tutatumia resources tutakazobana kwa kupungua kwa ukubwa na namba ya viongozi kwa maendeleo mengine

Ili kuondoa uwezekano wa rais kutoka bara kila siku kutokana na kura then uwekwe utaratibu kwenye katiba kila baada ya miaka rais atatoka upande moja wa muungano

Hivyo kila chama cha siasa kitasimamisha mgombea kutoka upande mwingine wa muungano
 
Nonda,

..mbona mlolongo wa matukio unaonyesha kwamba Karume & co., walimtegemea Mwalimu na Tanganyika kuliko kinyume chake?

..kwanza kabla ya Mapinduzi, Karumeb na Abdulrahman Babu walikuwa Tanganyika.

..pia tumesoma kuhusu ushiriki wa Tanganyika ktk kumchomoa John Okello kutoka ktk utawala wa Zanzibar.

..je, ni nani aliwaomba wa-Tanganyika wasaidie ktk kumteka nyara Okello na kumrudisha Uganda?

..kuna kikosi cha Polisi toka Tanganyika kilichokwenda Zanzibar kusaidia ulinzi baada ya Mapinduzi.

..kuna kila sababu za kuamini kwamba bila Tanganyika ku-side na SMZ basi Sultani Mwarabu angeweza kurudi Zanzibar.

..kwa mtizamo wangu, bila Muungano, Zanzibar ingeweza kuwa unstable and prone to coups d'etat like Comoro islands.
Mkuu,

Points ulizozitoa hapa nakubaliana nazo kwa kiwango kikubwa. Na umechambua vizuri matukio at the surface.

Kuna behind the scene motives and moves za hofu ya ukomunisti na role ya Nyerere kumtia hofu Karume kuwa atapinduliwa. (pitia some literatures all over the place)
Kama ulivyosema hapa, ushiriki wa Nyerere na Kambona kufanikisha mapinduzi.

Sasa mkuu, jambo ambalo mimi linanipa tabu kulielewa ni hili :-
Baada ya juhudi zote ambazo Karume na Serikali yake ya Kuitaka Zanzibar kama nchi, kuomba msaada huku na huko kufanikisha kumpindua « sultani » ili wajitawale katika nchi yao, wakubali kirahisi kuitowa Nchi yao kwa Nyerere na iwe mkoa au wilaya ?

Na ni kwa sababu gani hawakuiunganisha nchi yao moja kwa moja na kuwa nchi moja , serikali moja badala yake waliunganisha baadhi ya mambo tu, 11 kwa idadi katika the articles of Union ?
 
Nonda,

..hofu ya Ukomunisti doesnt make much sense to me.

..lakini si Nyerere alikuja kuwa Mjamaa/Mkomunisti na tukawa na uhusiano wa karibu sana na Wachina?

..tena Nyerere akawatimua West Germany waliokuwa wakitushinikiza tuache mahusiano na East Germany. tulifungua ubalozi na East Germany kwasababu wao walikuwa kati ya nchi za mwanzo kabisa kutambua serikali ya Mapinduzi.

..halafu si Karume aliyenukuliwa akisema "Ujamaa mwisho Chumbe...."?!!

..tuchukulie kwamba ni kweli Nyerere alimtisha Karume kwamba usalama wake uko mashakani.

..sasa kama suala hilo lilikuwa la uongo basi Karume angeweza kuweka mguu chini na kukataa vitisho hivyo.

..lakini tunaona pia kwamba Tanganyika ilipeleka kikosi cha Polisi kusaidia Zanzibar, kwa msingi huo inawezekana kabisa kwamba hali ilikuwa tete huko visiwani.

..pia hivi kwa akili za kawaida tunaweza kubisha kwamba kikosi kilichompindua Sultani mwarabu kilikuwa na uwezo wa kuhimili mashambulizi ya mamluki kama Bob Denard aliyepindua Comoro, au wale walikodishwa na Holden Roberto wa Angola?

Nonda said:
Baada ya juhudi zote ambazo Karume na Serikali yake ya Kuitaka Zanzibar kama nchi, kuomba msaada huku na huko kufanikisha kumpindua « sultani » ili wajitawale katika nchi yao, wakubali kirahisi kuitowa Nchi yao kwa Nyerere na iwe mkoa au wilaya ?

..hapa umenena!!

..wanasiasa wa Zenj wanapenda muungano pale unapowafaidisha kimadaraka na kiuchumi.

..kuna waandishi wanadai Mzee Jumbe alianza kupinga Muungano baada ya kuona Nyerere amemtupa mkono ktk harakati za kutafuta mrithi wa nafasi ya Raisi wa Muungano.

..Maalim Seif naye baada ya kupata madaraka sasa msimamo wake kupinga muungano umefifia.

NB:
..kuna kipindi CUF walikuwa wakiita CCM "Catholic Church Movement." Maalim alikuwa haishi kuitukuza himaya ya Sultani iliyoshamiri kwa biashara ya utumwa. yaani ilikuwa kana kwamba analilia zama zile za Wabara kukamatwa utumwa zirudi tena.
 
Kwa hiyo kufa kwa Tanganyika sio dhuluma, ila kufa kwa Zenj ni dhuluma? Na kuvunja Zenj nina maana mikoa mitano ya Zenj iwe assimilated kwenye Serikali moja. Kama utaita majimbo au miko kwangu mi naona ni semantics, sio muhimu!

Kama population ni just 2.5 then iwe mkoa tu. Kama mbunge mmoja anachaguliwa na watu 3000, ah, kwanza ni matumizi mabaya ya resorces. MKOA AU TUACHANE KWA AMANI NA WAPEMBA MTUPISHE WOTE.
 
Nonda,

..hofu ya Ukomunisti doesnt make much sense to me.

..lakini si Nyerere alikuja kuwa Mjamaa/Mkomunisti na tukawa na uhusiano wa karibu sana na Wachina?

..tena Nyerere akawatimua West Germany waliokuwa wakitushinikiza tuache mahusiano na East Germany. tulifungua ubalozi na East Germany kwasababu wao walikuwa kati ya nchi za mwanzo kabisa kutambua serikali ya Mapinduzi.

..halafu si Karume aliyenukuliwa akisema "Ujamaa mwisho Chumbe...."?!!

..tuchukulie kwamba ni kweli Nyerere alimtisha Karume kwamba usalama wake uko mashakani.

..sasa kama suala hilo lilikuwa la uongo basi Karume angeweza kuweka mguu chini na kukataa vitisho hivyo.

..lakini tunaona pia kwamba Tanganyika ilipeleka kikosi cha Polisi kusaidia Zanzibar, kwa msingi huo inawezekana kabisa kwamba hali ilikuwa tete huko visiwani.

..pia hivi kwa akili za kawaida tunaweza kubisha kwamba kikosi kilichompindua Sultani mwarabu kilikuwa na uwezo wa kuhimili mashambulizi ya mamluki kama Bob Denard aliyepindua Comoro, au wale walikodishwa na Holden Roberto wa Angola?

..hapa umenena!!

..wanasiasa wa Zenj wanapenda muungano pale unapowafaidisha kimadaraka na kiuchumi.

..kuna waandishi wanadai Mzee Jumbe alianza kupinga Muungano baada ya kuona Nyerere amemtupa mkono ktk harakati za kutafuta mrithi wa nafasi ya Raisi wa Muungano.

..Maalim Seif naye baada ya kupata madaraka sasa msimamo wake kupinga muungano umefifia.

NB:
..kuna kipindi CUF walikuwa wakiita CCM "Catholic Church Movement." Maalim alikuwa haishi kuitukuza himaya ya Sultani iliyoshamiri kwa biashara ya utumwa. yaani ilikuwa kana kwamba analilia zama zile za Wabara kukamatwa utumwa zirudi tena.

Mkuu,

Tafakari haya maneno ya Mkulu. Pia kwa nini katika miaka 24-26 ya utawala wake hakubadilishana na Rais wa Zanzibar kushika Urais wa Muungano na yeye kubaki rais wa Tanganyika.?... si kuna mambo ya Tanganyika pekee hadi leo??

Last edited by a moderator:
Hakuna Tanganyika! That is the puzzle of this Muungano!

Mkuu,
Unajua kuwa kuna kitu kinaitwa the articles of Union?
Uki-google utakumbana nayo.

weka kwenye search- The articles of Union between Tanganyika and Zanzibar

Kifungu hiki:-

(v) The existing laws of Tanganyika and of Zanzibar shall remain in force in their respective territories subject-

"in their respective torritories" .... Sasa hapo mkuu niambie hizo torritories ni zipi?

Jee Muungano uliiua Tanganyika au Muungano uliipoteza Tanganyika?

Kulitokea nini mpaka Tanganyika ikawa haisikiki tena?
Do your home-work, Mkuu.

[video]http://www.stampmasteralbum.com/ForeignCountryIdentifier/Stu/TanganyikaZanzibar.htm[/video]
 
Zanzibar hawatumii hili jina tunaloita Tanzania. Hivyo Tanganyika ilibadili jina na kuitwa Tanzania. Zanzibar ni nchu huru kama nyinginezo duniani. Walipoonekana kushindwa kustahimili mikiki ya kiuongozi, tukawameza kwa janja fulani, lakini hawakumezeka. Sasa wametulia, waachwe wawe na uhuru wao. Sisi wa Tanganyika wa zamani, Tukubaliane nchi yetu tuiite Tanzania.

How is that?
 
Back
Top Bottom