Katiba sasa ibadilishwe Zanzibar kuondosha ukomo wa muda wa Urais

Torero

Senior Member
Dec 22, 2017
122
138
Ndugu, wakati umefika Sasa wa Kubadilisha katiba ya Zanzibar Kuondosha ukomo wa Urais kwa upande wa Zanzibar. Nashauri Rais aliyopo Sasa aendelee kuingoza Zanzibar hata kipindi chake Cha miaka kumi ikiisha Kwa uwezo wa Mungu. Sote tunashuhudia siku chake tu amefanya Mambo makubwa sana. Na hii naelewa ya kuwa yeye mwenyewe wala HAJAWAZA jambo hili lakini atake asitake alazimishwe

lngawa ni mapema mnoo kulisemea jambo hili kwa Sasa lakini lakini lazima tuseme Sasa Zanzibar imepata kile ilichokuwa inatafuta kwa muda wa miongo kadhaa nacho ni Uongozi makini na wa busara wa ndugu Hussein Ali Mwinyi. Kwa hakika anafanya kazi nzuri sana siyo tu kuwaunganisha Wazanzibar waliofarikiana kwa muda mrefu Bali pia Spidi ya Maendeleo na mafanikio ni ya kupigiwa mfano. Anapiga vita ufisadi sana.

Wazanzibar wote saivi wametulia kwa Uongozi wake uliotukuka mfano mzuri ndani ya siku 100 tu amesha saini Mkataba na kampuni ya Kiarabu kwa ajili ya Mradi mkubwa wa Bandari ya Mangapwani Zanzibar kama ule mradi wa Bagamoyo mfano wake.

Uchimbaji wa Mafuta na gesi asilia unatarajiwa kuanza wakati wowote chini ya Uongozi wa Dr. Mwinyi na hakika tukibadilisha katiba tukampa miaka mingi ya kuongoza visiwa basi Zanzibar itapaa sana kiuchumi na kimaendeleo Afrika.

Namalizie kwa kusema Dr. Hussein Mwinyi mwenyewe hataki jambo hili lakini atake asitake alazimishwe. BARAZA LA WAWAKILISHI Badilisheni katiba haraka sana.
 
Bila kusahau hata raisi wetu ni wao Zanzibar hii ndo nafasi yao nashauri samia ajenge ikulu kubwa zanzibar kwaajili ya kupumzika
 
Back
Top Bottom