Katiba mya inawezekana?

Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
497
236
Ndugu wadau hivi kwa hali inayoendelea bungeni uundwaji wa katiba mpya unawezekana kweli? Napata mashaka kwa sababu zifuatazo:
1. Katiba zote zilizopita ambazo zinamapungufu zilitungwa na chama kimoja CCM, Kwahiyo kutoka nje kwa wabunge wa upinzani kwa sababu ya kunyimwa haki ya kusikilizwa kunaipa nafasi tena CCM kupitisha mswada utakaopelekea katiba nyingine yenye mapungufu.

2. Baadhi ya wabunge wanajadili swala la katiba katika misingi ya ushabiki wa vyama hivi kweli maeneo msingi kama vipaombele vya taifa yatapata nafasi?

3. Kama maono ya wabunge, wanaharakati, wanasheria na wananchi kwa umla yanapuuzwa, hivi huo mswaada unaoendelea kujadiliwa ni kwa ajili ya nani?
 
CCM wanadhani watatawala milele. katiba inatakiwa itoke kwa wananchi maana ndiyo sheria mama ila utashangaa hata sisi tuliyo hapa mjini mchakato haujatufikia wa kijijini sijui kama wanajua kuna kitu kinaitwa katiba.Ukweli ni kwamba huu mchakato wa katiba unaendeshwa mbio kwa maslahi ya watawala.kwa pamoja tuseme noooooooo!
 
Back
Top Bottom