Katiba mpya na huru shakani

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,845
Ni rahisi mno kuona mrejesho uliotokea kwenye SERIKALI nyingi Afrika baada ya mahakama kuu Kenya kutengua uchaguzi uliompa ushindi Kenyatta....

Sikuona pongezi zozote toka serikali zilizoko madarakani.... Ni habari za mshtuko kwa wengi ambao walitegemea matokeo tofauti....

Furaha na shangwe nyingi zimetoka kwa wapinzani
Tanzania tuko kwenye mchakato unaosuasua wa katiba mpya..lakini kwa haya yaliyotokea Kenya na hali yetu ya kisiasa kwasasa....

Tuandike patapotea.... Hakuna katiba mpya tena halafu huru

Kenya wameweza kwakuwa kuna kifungu kwenye katiba kinachotoa uwezo wa matokeo ya urais kuhojiwa na kupingwa mahakamani.... Kifungu hiki kimepatikana.

Kwa gharama kubwa!
Wengi tunatamani katiba kama ya Kenya... Lakini bado tuna njia ndefu halafu ngumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu hiyo katiba unayoitaka waliosigina tunao ndani ya chama chetu tutapoteza ujasiri wa kuipagania kama linavyotukaba koo jinamizi la kutamka neno ufisadi!
 
mkuu hiyo katiba unayoitaka waliosigina tunao ndani ya chama chetu tutapoteza ujasiri wa kuipagania kama linavyotukaba koo jinamizi la kutamka neno ufisadi!
Kura ya wazi au Siri!?Hayo nikikumbuka na ile hali ya kupiga kura hata waliokua nje ya nchi na wengine wakiwa wagonjwa ili kulazimisha AKIDI KUTIMIA,kwa kweli mchakato ulivurugwa sana. Lengo mahsusi la maoni ASILIA yaliyokusanywa na Tume ya Mzee Warioba ikawa diverted totally,na lugha moja rahisi ni kuwa pesa za walipa kodi mabilioni yakapotea bure kabisa,tofauti na ilivyotarajiwa.
 
Mkuu kumbuka kudai kunaitaji kujitoa...ukitaka kuwa mmbaya Dai chako kwenye wimbo WA nilipe nisepe...kenya katiba waliyotumia hawakuipata kwa kuandika Tu mitandaoni damu ilimwagika..ccm sio wapumbavu waruhusu huu mchakato ambao utamnyang'anya mwenyekiti WA ccm uwezo WA kujichagulia apendacho unless tumekabana
 
Katiba mpya itakuwa ndo mwisho wao hao wanaojua kusoma na kuandika tu wenye maamuzi ya siku utegemea wameamkaje.Katiba mpya itakuwa ukombozi wa pili wa kwanza mkoloni mweupe wa pili mweusi ambae ni mbaya heri ya shetani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo m
Exactly...ndo mana hawawezi fanya ujinga huo maana kwao Ni kama upuuzi..kwani hawataki kuongoza tens???

Lakini kumbuka pia hapa Tanzania hatuna upinzani ambao kenya wanao, yaani wewe unajua fika katiba mpya ni mwiba kwa chama tawala alafu badala ya kuweka kipaumbele kudai eti unamuomba mtawala akupe katiba mpya, maisha yako yote utaisikia kwenye bomba tu.
 
Lakini kumbuka pia hapa Tanzania hatuna upinzani ambao kenya wanao, yaani wewe unajua fika katiba mpya ni mwiba kwa chama tawala alafu badala ya kutumia nguvu kudai eti unamuomba mtawala akupe katiba mpya, maisha yako yote utaisikia kwenye bomba tu.

Mkuu;
Samahani mimi ni miongoni mwa wale ambao huwa wanachelewa kuyaelewa mambo. Tuseme unapotuambia ya kuwa tutumie nguvu, ni kwamba ipo mahali fulani tuingie hapo kwa nguvu tukaichukue au unataka twende msituni na hapa sijui ni msitu gani tukaanzishe mau mau?? Jamani tuvumilieni sisi wavivu kuyaelewa mambo.
 
sio kuingia msituni na wala si kuanzisha vurugu hapana, kuweka kipaumbele kwenye agenda ya vyama vyetu na kuipigia kelele pia inasaidia, unaweza kutumia nguvu kwa maana ya kumwaga damu na usiipate. ila upinzani wa tanzania wenyewe hauna haja na katiba ndio maana hukuti wakiweka kipaumbele,
 
Mkuu

Mkuu Kuna vitukwa sasa Tanzania havikwepeki ikiwa hatutapata kwa kuomba basi tupate kwa kukwapua..haki juwa haiombwi inadaiwa na kudai kunatumia nguvu na muda...na hizo cost zake zinaweza kuwa hadi uhai WA mtu
 
sio kuingia msituni na wala si kuanzisha vurugu hapana, kuweka kipaumbele kwenye agenda ya vyama vyetu na kuipigia kelele pia inasaidia, unaweza kutumia nguvu kwa maana ya kumwaga damu na usiipate. ila upinzani wa tanzania wenyewe hauna haja na katiba ndio maana hukuti wakiweka kipaumbele,
Mkuu hapa tutabishana hadi kesho nimeuliza hili swali sehemu nyingi but sipati majibu hivi kilichoplekea katiba ya warioba kupatikana sio kipaumbele??je tumepata katiba?ccm sio wajinga na wapumbavu kuachia golden chance iliyopo kwenye katiba ya sasa unless mmetumia mabavu..coz wote tunajua tatizo lwtu ni katiba hadi wapenzi wa ccm wanatambua udhaifu uliopo kwenye katiba na viongozi waliopita walituingiza chakani kwa kutumia katiba iliyopo na ccm itatumia katiba iliyopo kuiba na itatumia katiba hiyohiyo kuzuia watu kwenda mahakamani kuoinga wizio huo na rais ataongea na jaji mkuu aliemteua asimuangushe...so instead of wasting our money and time for vipaumbele ambavyo havitekelezeki ni bora kuanzisha vuguvugu la katiba kimenomeno mana hats Kenya walipata kimenomeno
 
Patapatikana kizazi cha kuyabadili haya! Katika muda usiotegemewa na wengi. Hakuna la kudumu milele
Hope is the last thing we have.
 
sio kuingia msituni na wala si kuanzisha vurugu hapana, kuweka kipaumbele kwenye agenda ya vyama vyetu na kuipigia kelele pia inasaidia, unaweza kutumia nguvu kwa maana ya kumwaga damu na usiipate. ila upinzani wa tanzania wenyewe hauna haja na katiba ndio maana hukuti wakiweka kipaumbele,
kwani wenye shida na katiba mpya ni upinzani au sisi wananchi?katiba mpya ni faida kwetu wananchi au upinzani?sisi wananchi nadhani ndio tunatakiwa tuidai katiba mpya.
 
Back
Top Bottom