Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Naweza kuwa natoka ne ya mada lakini naomba kujuzwa au kuelimishwa.

From CHADEMA, NCCR na wataka mabadiliko wengine yote.

  • Nini hasa kilitakiwa au kinatakiwa kufanyika ?
  • Assume CDM ndio wangekuwa na nchi na tuko atia hali hii ya kaitba tata hasa process gani zingefanyika. zingefanyika kivipi? washiriki wakuu wa kuandika na kukusanya maoni ya katiba mpya wangepatikana vipi ? Nini hsa kinatakiwa kufanyika tofauti na JK ( CCM )wanavyopendekeza? Jiulize na mswali mengine mengi yanyoendana na hayo.....
NB.
Mimi ni mmoja wa wataka mabdiliko( Sio ya Kisiasa tu) lakini so far niko gizani. Ebu wana Jf nifumbueni macho zaidi ni wapi CCM na Jk wanapokosea na ni upi ambao ni mwelekeo sahihi kutokana na baadhi ya maswali niliyouliza pale juu.

acha uvivu tafuta ho2ba ya lissu soma... Kuna mapendekezo hop maswal yako yatajibiwa kwa kias kikubwa
 
MMM na FJM wamenena vyema sana. Najua Pasco wewe ni muungwana utakuja kama kawaida yako kuomba radhi. Naheshimu maoni yako sana. Kwenye hili nadhani homework yako haikujitosheleza! Nafurahi JF kuna really Great Thinkers. Wewe kuleta huu mjadala kunasaidia pia kwa walio wengi kuelewa vizuri nini kilichojiri na unatoa nafasi watu kuelewa zaidi na vizuri yanayoendelea kwani some of the things ziko technical na najua wengi wanaweza wasizielewe kwa haraka na undani. Hoja kama yako inasaidia kuweka mambo sawa then tunasonga mbele.
 
Pasco hajagundua Spika anaendeshaje bunge. Mambo ya kushika shilingi mara vifungi vya kuzuia hoja vyote vinaishia na kuhoji, mwisho ni wengi wape! Hatuna bunge!
Kwahiyo mkuu whats the solution on your opinion?
 
Hakuna namna ambayo CDM wangeweza kuzuia mjadala wa mswada. NONE. Ibara ya 86 haitoi automatic stay au halt ya mjadala. Inatoa nafasi tu kwa hoja kusikilizwa halafu Spika awaulize wabunge ili kuchukua uamuzi. Hiyo kanuni ishawahi kutumika kwenye mambo mengine huko nyuma..

Acha speculation!
Jibu swali, Je wali jaribu kufuata mkondo huo?
Nawashauri chadema, Pamoja na midahalo wanayofanya, waitishe mikutano ya hadhara na kuelezea umma kwa ufasaha ni nini kinaendelea.
Kama watanyimwa vibali, wakubali kugharamia vipindi maalum Kwenye media mbali mbali ili kufikisha ujumbe wao kabla ya kuanzisha maandamano.
Binafsi naona CHADEMA wamekosea kwa sababu labda sijapata maelezo ya upande wao.
 
hapana ni kwamba ana maoni tofauti na kuwa anaamini maoni yake ni sahihi. Ni jukumu letu kuonesha kuwa maoni yake si sahihi. Mtu kuwa na maoni tofauti haina maana ni mnafiki.
Unataka kuniambia kuwa hajui kabisa kuwa isingewezekana muswada huo kutokusomwa mara ya pili na hatimaye kupitishwa hata kama wangetumia hicho kifungu namba 86?
 
Point kubwa hapa ni kuwa CHADEMA walishindwa kuitumia kanuni ya 86 effectively kuzuia muswada, na hivyo kwa kuondoka kwao wakaruhusu muswada upite kirahisi. Nitafurahi na kushukuru sana iwapo atajitokeza mtu anielemishe hicho kifungu cha 86 kinasemaje, je ni sawa na filibuster kwenye senate ya marekani? Yaani kinalazimisha maoni ya minority nayo yasikilizwe?; na kama ni sawa na filibuster, je ni asilimia ngapi inayotakiwa ili kusimamisha mswada? na Je CHADEMA peke yake wanaweza kuifikia hiyo pasenti?

Nadhani kupiga kura inayohalalaisha upuuzi ni kubaya zaidi kuliku kutohusika kupiga kura hiyo; hata kama kura yako itakuwa inalipinga jambo hilo, bado rekodi zitaonyesha kuwa na wewe ulikuwa ni sehemu ya wale waliohalalisha upuuzi huo.
 
Kwahiyo mkuu whats the solution on your opinion?

@jmushi1, solution ni kupeleka hili jambo to the upper house - bunge la juu kabisa =wananchi. Pamoja na matatizo yake lakini katiba ya sasa inatamka wazi kabisa kuwa wananchi ndio wenye mamlaka ya mwisho. Hivyo wabunge CHADEMA wako sahihi kabisa kurudisha hili jambo kwa wananchi kwani ndio wenye mamlaka ya mwisho.

Kwa upande mwingine CHADEMA wanaweza kuongoza harakati za kupata katiba mpya sambamba na hii ya ccm. Hii ingetoa fursa pana kwa wananchi maana ccm wameshaonesha nia ya kuleta ujanjaujanja kwenye hii katiba mpya. Let ccm do their thing CHADEMA wajipange kivyao halafu wananchi wataamua ni katiba ipi wanaitaka. Simple.
 
CDM wengi humu ni mbumbu wa sheria na watu wakufuata mkumbo tu. Wao wanamchukulia mh. Lisu kama Mungu na hakosei hata kidogo.

Mfano uliotoa kuhusu ushauri wake kwa mh Mbowe na kilichomtokea ni kielelezo cha imani ya kibubusa kwa mwanasheria huru kijana.

Utakachokipata humu ni matusi tu badala ya admission of mistakes.
Mkuu Kikwebo Heshima sana
Umenifurahisha sana katika mchango wako hapo juu, umekuwa kama wabunge wa ccm waliotumia siku tano kumponda Tundu Lisu na CDM badala ya kutoa mchango wao juu ya mswada wenyewe au maoni ya kambi ya upinzani. wewe badala ya kutoa mchango wako juu ya bandiko al Pasco umetumia muda wako kupambana na wana CDm humu jamvini jambo ambalo si muhimu kwako na kwa umma wetu! we are doing the same mistakes like magamba hahahhahaha nchi ina safari ndefu sana

 
Pasco Mayala, sıjaelewa hasa nııpı hoja yako ulıyotundıka tuweze kuıjadılı! Je, unatafta majıbu ya swalı lako baada ya kutorıdhıshwa na TL? Au hujakubalıana na dhana nzıma ya walkout ya kambı rasmı ya upınzanı Bungenı?
Kwanza napenda nıkukosoe kwamba walıosusıa mjadala hawakuwa CDM peke yake.
Kwa alıchokujıbu TL nı summary tosha ya nını CDM wanadaı, alısema pamoja na yeye kuwepo ndanı ya kamatı ya Katıba na Sherıa alıshuhudıa jınsı utaratıbu mzıma kamatı ambavyo haıkusıkılızwa na serıkalı na hatımaye kulazmısha kuleta rasımu ya muswada ndanı ya Bunge.
Pamoja na hılo, chadema wameahıdı hawatakaa kımya balı wanayaleta mapendekezo yao ya Kambı rasmı ya upınzanı kwa Wananchı ılı wawaelımıshe jınsı ganı the whole process ya uandaajı huu wa rasmu ungeptıa pasıpo kumpa madaraka makubwa Raıs kama jınsı muswada ulıoptshwa ulıvyo.
Kıngıne mhımu cha kujıulıza!
Kwa udhaıfu mkubwa walıvyoonyesha Wabunge wa CCM katıka kujadılı muswada huu ınaonesha nı jınsı ganı wanavyowategemea CDM katıka kujenga hoja zenye mashıko kıfungu kwa kıfungu katıka kuulekebısha muswada. Lakını matokeo yake wamekuwa vınara wa kurusha vıjembe kama wantaarab na hatımaye kuufınyanga fınyanga muswada wenyewe wakımuachıa Kombanı kuroundup hoja yake pasıpo ugumu wowote wa kujıbu hoja za wachangıajı.
Mwısho, naomba ıeleweke tu kwamba CCM hawana uwakılıshı mzurı Bungenı, 99% ya wabunge wa CCM sıo crıtıcal Thınkers! Unategemea Mbunge kama JAH People, Prof Majımarefu, Olesendeka, Vıck Kamata n.k kujenga hoja zenye mashko paspo vıjana machachalı kama Mnyıka,Kafulıla,Mdee ndanı ya Bunge letu?
 
Point kubwa hapa ni kuwa CHADEMA walishindwa kuitumia kanuni ya 86 effectively kuzuia muswada, na hivyo kwa kuondoka kwao wakaruhusu muswada upite kirahisi. Nitafurahi na kushukuru sana iwapo atajitokeza mtu anielemishe hicho kifungu cha 86 kinasemaje, je ni sawa na filibuster kwenye senate ya marekani? Yaani kinalazimisha maoni ya minority nayo yasikilizwe?; na kama ni sawa na filibuster, je ni asilimia ngapi inayotakiwa ili kusimamisha mswada? na Je CHADEMA peke yake wanaweza kuifikia hiyo pasenti?

Nadhani kupiga kura inayohalalaisha upuuzi ni kubaya zaidi kuliku kutohusika kupiga kura hiyo; hata kama kura yako itakuwa inalipinga jambo hilo, bado rekodi zitaonyesha kuwa na wewe ulikuwa ni sehemu ya wale waliohalalisha upuuzi huo.

@Kichuguu, Myinka alisimama kuomba mwongozo ili muswada urudi kwa wananchi kabla ya wabunge kujadili lakini Spika Makinda hakutaka hata kumsikiliza. Na kwa namna ambavyo Spika huyu na waliomuoweka kwenye hicho kiti walivyovuruga kanuni za bunge hicho kifungu ni kiini macho, hakina kazi kabisa kama CCM wameshapewa order na 'chief whip'.

Kumbuka hapa ccm na CUF walishaambiwa (well before the debate) kwamba muswada utasomwa kwa mara ya pili na lazima wote wauunge mkono.Hii ndio kazi ya Chief whip -Lukuvi akisaidiwa na Waziri Mkuu. Na sababu ya kufanya hivyo ni kuhahakikisha kuwa hata pale CHADEMA watakapoamua kutumia hicho kifungu cha 86 basi kupitia Spika (kuhoji wabunge) wote wakatae!

Jambo jengine ni kwamba Spika anakuwa na nakala ya hotuba ya kabla, hivyo alikuwa na hotuba ya Lissu atakuwa ameiona kabla hajasoma. Huu ndio utaratibu. Na hapa Spika Makinda kwa kuwa anaegemea zaidi chama chake CCM akaamua kupanga wasemaji wenye uwezo mkubwa kwa kupiga kelele (not neccessarily kujibu hoja) Mama Makinda na wale wa Zanzibar. Wasemaji wote siku walipangwa kwa makusudi. Kwa mara ya kwanza watanzania tumeshudia Spika wa bunge akiongoza kikao cha kumtukana mbunge mmoja badala ya kujadili hoja! Hili litabakia kuwa doa katika historia ya bunge letu kwamba kuna kipindi Spika aliruhusu wabunge kutumia muda wa kujadili hoja za wananchi badala yake watukanane!. Very unfortunate.!
 
@Pasco,kwanini hiyo sehemu ya hotuba yake aliyoitumia kuijibu usingetuwekea hapa tuamuwe wenyewe?

Wewe ume summersize na inaonekana wengine wameridhika na jibu ulilopewa.

Je unapindisha habari kwa maslahi yako binafasi?
Mkuu J. Mushi, tatizo members wengi humu sio tuu ni washabiki au wapenzi wa Chadema, bali ni ma fanatics wa Chadema wanawaona viongozi wa Chadema kama miungu watu hivyo wanajikuta wanawaabudu. Wanaamini viongozi wao hawawezi kufanya makosa!.

Amini nawaambieni hili la Chadema kushindwa kutumia kifingu cha 86 kuusimamisha muswada ule was a mistake.

Lissu ni mwanasheria makini, hilo halina ubishi, mimi si mwanasheria kwa sababu I don't practise ila nimetoa tongotongo za sheria za sheria kwa miaka minne full time pale UDSM, Mhe. Lissu hakupaswa kusoma hotuba, alipaswa kutoa pingamizi!. Baada ya pingamizi ndipo hotuba ya kambi ya upinzani ingefiatia.

Bila hotuba ya kambi ya upinzani, muswada wowote wa serikali hauwezi kusonga mbele!.

Nimemuuliza Mhe. Lissu, kwanini alisoma hotuba on the first place wakati alipaswa kuwasilisha pingamizi!.

Mhe. Lissu akanijibu kwa kusoma para ya pingamizi kwenye hotuba yake!. Jee kanuni hiyo ya 86 ndivyo ilivyoelekeza?!. Lissu alikosea pingamizi ni pingamizi tena amewekewa mpaka maneno ya kutamka na hivyo kusitisha process nzima!.

Mhe. Lissu aliposoma hotuba ya kambi ya upinzani, alimaanisha ameikubali hoja ya mtoa hoja, hivyo ku complete the process!.

Mimi ni miongoni mwa wakosoaji wakuu wa Spika Mhe. Mama Makinda tangu day 1. Niliripoti humu jinsi nilivyokutana na RA na kwa kinywa chake mwenyewe RA akanitambia na kusikia kwa masikio yangu mawili kuwa ni yeye RA aliyemuweka Spika SS tena kwa kulipia kura za Wanzanzibari baada ya wabara kumsuport Msekwa!.

RA akanihakikishia ni yeye aliyetoa SS na ni yeye aliyemuingiza Mama Makinda!. Kwenye Press Conference ya Kwanza ya Mama Makinda niliireport live humu na nilimuuliza kuhusu kuwekwa na RA, akajikanyaga kanyaga.

Nimewahi kuanzisha thread kadhaa juu ya madhaifu ya Mama Makinda lakini kwenye hili la kuzuia hoja yoyote baada ya kuwasilishwa hotuba ya kambi ya upinzani she was right!. Hivyo ndivyo kanuni inavyosema!.

Kwenye hili, naamini 100% kwa 100% Mhe. Lissu alichemsha!. Na kwa maoni yangu, JJ.Mnyika ni miongoni mwa hazina kubwa za Chadema, kama angeipitia hotuba ya Mhe. Lissu, isingekuwa vile ilivyo, tena nawaomba sana msiniprovoke nikaichambua hotuba ile, tutaishia kuvuana nguo hapa na kuachana uch..!

Lissu ni school mate wangu tangu Ilboru na ni kichwa cha ukweli, lakini kwenye hili amechemsha big time!.

Naombeni niwape angalizo all ma hopefulls kwamba there is something to be done!.

Please hear me loud and clear, baada ya rais kuusaini muswada huo kuwa sheria, there is nothing Chadema can do!. The only option ni kukubali matokeo, kama walivyojifanya hawamtambui rais Kikwete, japo ni kilaza wa tangu UDSM na GPA yake ya 2.0!, ( Facult wana uwezo wa kuongeza 2 points of grace ili ku salvage last year disco) yeye ndie rais. period.

Muswada ukishakuwa sheria inakuwa ni msumeno inakata nyuma na mbele kama upanga wa makali kuwili!. Chadema, Kibamba wala wanaharakati hakuna lolote wanaloweza kufanya!.

Msifikiri Watanzania ni kama Wamisri, Walibya au Wasyria, Watanzania ni kama kondoo!. Wanaomkumbuka mwanaharakati wa UDSM enzi zile, Bi Sikitiko Kapile alisema Watanzania tuna nidhamu ya ukondoo na hivyo ndivyo tulivyo. Kama Chadema ina bank on peoples powers!, wait for surprises, they are wrong again and again and again!.
 
@Kichuguu, Myinka alisimama kuomba mwongozo wa kuomba ili muswada urudi kwa wananchi kabla ya wabunge kujadili lakini Spika Makinda hakutaka hata kumsikiliza. Na kwa namna ambavyo Spika huyu na waliomuoweka kwenye hicho kiti walivyovuruga kanuni za bunge hicho kifungu ni kiini macho, hakina kazi kabisa kama CCM wameshapewa order na 'chief whip'.

Kumbuka hapa ccm na CUF walishaambiwa (well before the debate) kwamba muswada utasomwa kwa mara ya pili na lazima wote wauunge mkono. Na sababu ya kufanya hivyo ni kuhahakikisha kuwa hata pale CHADEMA watakapoamua kutumia hicho kifungu cha 86 basi kupitia Spika (kuhoji wabunge) wote wakatae!

Jambo jengine ni kwamba Spika anakuwa na nakala ya hotuba ya kabla, hivyo alikuwa na hotuba ya Lissu atakuwa ameiona kabla hajasoma. Huu ndio utaratibu. Na hapa Spika Makinda kwa kuwa anaegemea zaidi chama chake CCM akaamua kupanga wasemaji wenye uwezo mkubwa kwa kupiga kelele (not neccessarily kujibu hoja) Mama Makinda na wale wa Zanzibar. Wasemaji wote siku walipangwa kwa makusudi. Kwa mara ya kwanza watanzania tumeshudia Spika wa bunge akiongoza kikao cha kumtukana mbunge badala ya kujadili hoja! Hili litabakia kuwa doa katika historia ya bunge letu kwamba kuna kipindi Spika kuruhusu wabunge kutumia muda wa kujadili hoja za wananchi badala yake watukanane!. Very unfortunate.!

Nilipo underline acha kupotosha watu

Wabunge wa chadema ni member kamati ya sherai walishiriki, walikuwepo na walifahamu kila kitu prior na bunge kuanza..

Besides, Waziri kivuli alikuwa anajua kila kitu kama utasomwa mara pili prior to bunge session..
 
Kwa maana hiyo basi Pasco ni mnafiki.

...mkuu hilo ndo neno linalo mwelezea vizuri huyo Pasco kuwa ni nani au ni mtu wa aina gani...ukimwona mtu anasema ya kwamba "mimi siko ktk upande wowote",ktk mambo ya msingi basi elewa moja kwa moja kuwa huyo mtu ni MNAFKI MKUBWA...
 
Pasco,
Suala la katiba lilianza siku nyingi lakini likapata msukumo wa nguvu pale CDM walipolipeleka mahakama ya wananchi. Kosa ni pale walipokubali kuwa rais Kikwete bila ridhaa ya serikali au chama chake alipoamua kulisamimia na CDM wakatulia na kuamini hivyo. Technically hapa ndipo kosa la CDM lilipoanzia.

Absolutely! Sikuelewa toka mwanzo kwanini waliamini kuwa Rais ambaye hakuwa na ajenda ya Katiba Mpya muda wote wa kampeni (na miaka ishirini kabla yake) hatimaye ameona mwanga na sasa angeweza kuwa msimamizi mzuri wa mchakato wa kuelekea Katiba mpya.
 
Pasco nakuona upo hapo chini mbona hujibu hoja, umeelewa au la, nini mawazo yako baada ya michango kadhaa hapa?
Wa Ndima, niko harusi ya Jerry Muro mahali, nikimaliza, naahidi kila hoja zitajibiwe. Jerry ni kijana wangu, mimi ndio nilikuwa role model wake, alijikwaa mahali akaanguka, atasisima, kuangalia alipojikwaa na kusonga mbele!.

Tuko pamoja sana!.

Pasco
 
Please hear me loud and clear, baada ya rais kuusaini muswada huo kuwa sheria, there is nothing Chadema can do!. The only option ni kukubali matokeo, kama walivyojifanya hawamtambui rais Kikwete, japo ni kilaza wa tangu UDSM na GPA yake ya 2.0!, ( Facult wana uwezo wa kuongeza 2 points of grace ili ku salvage last year disco) yeye ndie rais. period.

Muswada ukishakuwa sheria inakuwa ni msumeno inakata nyuma na mbele kama upanga wa makali kuwili!. Chadema, Kibamba wala wanaharakati hakuna lolote wanaloweza kufanya!.

Msifikiri Watanzania ni kama Wamisri, Walibya au Wasyria, Watanzania ni kama kondoo!. Wanaomkumbuka mwanaharakati wa UDSM enzi zile, Bi Sikitiko Kapile alisema Watanzania tuna nidhamu ya ukondoo na hivyo ndivyo tulivyo. Kama Chadema ina bank on peoples powers!, wait for surprises, they are wrong again and again and again!.


Kwanini unafikiria hili ni suala la Chadema vs the government? Hili ni zaidi ya CDM na serikali.
 
Nilipo underline acha kupotosha watu
Wabunge wa chadema ni member kamati ya sherai walishiriki, walikuwepo na walifahamu kila kitu prior na bunge kuanza..
Besides, Waziri kivuli alikuwa anajua kila kitu kama utasomwa mara pili prior to bunge session..

@Topical, hapo kwenye red. hapana. Nadhani unachanga kamati za kudumu za bunge na party caucuses. Kamati za kudumu za bunge zinakuwa na wabunge wa vyama mbalimbali na kamati zinaongozwa na mwenyekiti (sio chief whip). Cauceses ina-apply kwa chama kimoja kimoja. Na kwa chama chochote (unless kina ugomvi wa kuua mtu) kabla ya kwenda kwenye mjadala wowote lazima wawe na vikao vya ndani ili kuweka msimamo. Hapo ndio tunakuwa na chief whip (mshika kifimbo). Kwa ccm ni Lukuvi na CHADEMA ni Lissu. Hao wengine sijui nani.
 
Back
Top Bottom