Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Hatukubali yaishe mpaka hoja za msingi tulizopendekeza zijibiwe,wakati utaamua kama CHADEMA walikosea au la

Kwanza kwa sababu za kihistoria na zingine muswada unaweza kuendelea na kuwa sheria,lakini hiyo haimaanishi kwamba ni halali
 
Naweza kuwa natoka ne ya mada lakini naomba kujuzwa au kuelimishwa.

From CHADEMA, NCCR na wataka mabadiliko wengine yote.

  • Nini hasa kilitakiwa au kinatakiwa kufanyika ?
  • Assume CDM ndio wangekuwa na nchi na tuko atia hali hii ya kaitba tata hasa process gani zingefanyika. zingefanyika kivipi? washiriki wakuu wa kuandika na kukusanya maoni ya katiba mpya wangepatikana vipi ? Nini hsa kinatakiwa kufanyika tofauti na JK ( CCM )wanavyopendekeza? Jiulize na mswali mengine mengi yanyoendana na hayo.....
NB.
Mimi ni mmoja wa wataka mabdiliko( Sio ya Kisiasa tu) lakini so far niko gizani. Ebu wana Jf nifumbueni macho zaidi ni wapi CCM na Jk wanapokosea na ni upi ambao ni mwelekeo sahihi kutokana na baadhi ya maswali niliyouliza pale juu.
 
mpotezeeni huyu pasco ni snitch tu,sanasana anataka umaarufu ili tumfahamu kwa kuwa ameuliza swali na ameonekana kwenye tv.


kama ndo huyu mbona kila siku anaonekana kwenye tbc na vipindi vyake ..hata juzi alikuwa mnazi mmoja kwenye wiki ya wizara ya sheria na katiba .....huyu anatumika tu
 
Pasco, Lissu kashakujibu kwamba yeye ile baada ya kusoma spika alitakiwa aulize wanaounga mkono ni wangapi na wasiounga mkono ni wangapi lakini hakuuliza.halafu kama unakumbuka siku ile ya mswaada kuna Mbunge alisimama kuomba muongozo akanyamazishwa kwa kauli kwamba spika akiwa amesimama hamna muongozo akaongezea mswaada wenyewe ndo umeletwa sasa mwongozo wa kitu gani?kaa chini.akasema "tunaendelea, mh.Kilango malecela endelea".ndipo wabunge wakaanza kutoka nje.unajifanya huna chama sio kweli. Mia
 
We ni Pasco Mayalla tu maana tulikuona ukiuliza hayo maswali.
Mumwi, niko kwenye mobile hivyo sijaweza kuona status yako humu hivyo na presume wewe ni mgeni. Kumfananisha memba wa jf na yoyote ni kosa linaloitwa name calling na adhabu yake ni ban. Humu kwenye jujwaa la siasa tuna discuss issues na ideas hatujadili watu!.
Majukwaa ya kujadili watu pia yapo unaweza kuuliza na utajibiwa.
 
Pasco umenena vyema.

Hawa jamaa wa magwanda hawana wakitakacho zaidi ya "shortcut".

Hata Kikwete afanye nini kwao ni kosa tu, tatizo lao ni Kikwete na si Serikali. Hilo lipo wazi kabisa, lakini ukweli ni kwamba Kikwete ndiye aliyefanya mema Tanzania hii zaidi ya Rais yeyote mwingine wa kabla yake na hilo halina utata wala ubishi. Wakae wafikiri.

acha ushabiki wa kipuuzi!
 
Pasco

unaniangusha kwa kweli. Yaani na wewe unakubali kupotosha?, Huwezi kuwashinda watu walioingia katika mjadala na pre determined preference. Chadema wangetumika ku-legitimise mchakato haramu kwa kuonesha kuwa walishiriki wakashindwa kwa hoja na si ubabe wa CCM. Waswahili husema 'SAFARI MGUU WA KWANZA' kwenye katiba nchi imeisha jikwaa na ni dhahiri CCM haiwezi kuwa na legitimcy ya kuendesha mchakato huu kwa ufanisi na kupata baraka za watanzania hata kama watachakachua kura za maoni kushinda. Mchakato mzima huu ni FLAWED AB INITIO. Kwa ujumla kinachofanyika sasa ni waste of time and resources kwani mchakato huu utarudiwa huko mbeleni.

kuhusu hiyo kanuni ya 86, hoja yako ingekuwa na mashiko kama muswada ungepitishwa na MAJORITY YA WABUNGE ILIYO BELOW YA IDADI YA WABUNGE WOTE WA CHADEMA, WHICH MEANS WANGEKUWAPO IDADI YAO INGE OFF SET NA KUPITA YA WALIOUNGA MKONO.
 
Mumwi, niko kwenye mobile hivyo sijaweza kuona status yako humu hivyo na presume wewe ni mgeni. Kumfananisha memba wa jf na yoyote ni kosa linaloitwa name calling na adhabu yake ni ban. Humu kwenye jujwaa la siasa tuna discuss issues na ideas hatujadili watu!.
Majukwaa ya kujadili watu pia yapo unaweza kuuliza na utajibiwa.

pasco

je ni keli au si kweli ulionekana na kusikika ukiuliza swali regardless of the Id you have used
 
CDM wengi humu ni mbumbu wa sheria na watu wakufuata mkumbo tu. Wao wanamchukulia mh. Lisu kama Mungu na hakosei hata kidogo.

Mfano uliotoa kuhusu ushauri wake kwa mh Mbowe na kilichomtokea ni kielelezo cha imani ya kibubusa kwa mwanasheria huru kijana.

Utakachokipata humu ni matusi tu badala ya admission of mistakes.

sasa kwa hayo maneno uliyoyasema unategemea watu wakushangilie!? Kumbe matusi huwa mnayatafuta wenyewe... Sasa nani anamchukulia Lissu ni mungu!? Lissu ni kichwa nadhani hata wewe unakubaliana na mimi! Halafu sio fresh kuwaita wenzako mbumbumbu...
 
Pasco, Lissu kashakujibu kwamba yeye ile baada ya kusoma spika alitakiwa aulize wanaounga mkono ni wangapi na wasiounga mkono ni wangapi lakini hakuuliza.halafu kama unakumbuka siku ile ya mswaada kuna Mbunge alisimama kuomba muongozo akanyamazishwa kwa kauli kwamba spika akiwa amesimama hamna muongozo akaongezea mswaada wenyewe ndo umeletwa sasa mwongozo wa kitu gani?kaa chini.akasema "tunaendelea, mh.Kilango malecela endelea".ndipo wabunge wakaanza kutoka nje.unajifanya huna chama sio kweli. Mia


mzee wa mia...john mnyika ndiye aliyesimama supika akapotezea na kumuita yle mama mpiga kelele.....huyu psco toka juzi kakomaa kweli na hiyo knuni ya 86 ..halafu eti lissu amepiga chenga kujibu...kumbe ni ugumu wa uelewa wake
 
Pascho Mayala,msukuma mwenzangu,ulitaka pingamzi gani zaidi ya lile waliotoa wana-Chadema bungeni?kwani unajua tatizo la mkingamo wa kimawazo juu ya mswaada wa kuunda katiba mpya unatokana na nini?naomba usiwe mnafiki jaribu tu kuwa mkweli,kwani Chadema hawataki katiba mpya?nani hataki katiba mpya?CUF au CCM au ni nani hasa hataki katiba mpya?je kwenye hoja za Chadema kuna mahali walisema hawataki katiba mpya?je nani alisema kuna haja ya katiba mpya kuanzia kwenye ilani za uchaguzi wa mwaka 2010?Labda tujiulize ni kitu gani Chadema hawataki na ambacho kwa wananchi wa sehemu walizohojiwa baada ya huo mswaada kusoma mara ya kwanza,ni kitu gani kilionekana kuzungumziwa na wananchi wengi?au ni ushabiki kama wa mpira?Pascho Mayala nikuulize je ni kweli maelekezo ya bunge yalifuatwa baada ya ule mswaada kuondolewa bungeni?je ni kweli hata baada ya tu kile kipengele cha kuutafasir mswaada kwa kiswahili ulirudishwa tena kwa ile tu mikoa ulikojadiliwa mara ya kwanza?na hata hivyo wanajuaje wale wananchi wa Ngundangali walisema nini juu ya katiba mpya ambayo itaenda kuundwa?Lakini tujiuulize ni maazimio mangapi yaliyoazimiwa na bunge yaliyopelekewa kurudishwa kwa mswaada huo yametekelezwa?na je unadhani hotuba ya kambi ya upinzani iliyowasilishwa na Mh. Tundu inamapungufu gani yanayoeleza kupinga mswaada huo tofauti na vile unavyotaka wewe juu ya kuupinga mswaada huo?kupinga ni kupinga tu hata kusoma hotuba ya Mh.Tundu na kisha kutoka nje ya ukumbi wa bunge nadhani ni zaidi ya kuupinga mswaada huo,kwani kwako wewe kupinga mswada huo ni kutokusoma tu hotuba ya Lisu?na je pale ambapo waziri na wachangiaji wengine kutoka vyama vya CCM na CCM B wanapoomba KUAMINIANA ni kuaminiana gani huko wakati kuna mambo mengi yenye masilah ya kitaifa wameshindwa kutuaminisha kwa kuyafunika japo ukweli uko wazi?na hata hivyo unajua kwa ufasaha kile kinachowafanya CCM na washirika wao kama wewe kukataa mapendekezo ya Chadema juu ya katiba mpya?Lakini ngoja nikuulize Pascho hivi ulitegemea upinzani usingetikea kwenye hili suala la kuunda katiba mpya wakati kigezo kikubwa cha kuhalalisha unndwaji wa hii katiba unatokana na ushawishi wa KUAMININA baina ya vyama?ambavyo ndio vinatuongoza katika hili?Na je ni vipi wenzetu wanaoshika dola kwa kushirikiana na upande wa pili wa dola kwa maana ya kule ZNZ wana vitendo vingi vikubwa vinavyotuonyesha wao si waaminifu?au wew Pascho huyajui hayo?nikupe mfano,sakata la Richmond,sakata la EPA,sakata la Kiwira,sakata la Meremeta,Rada,ndege ya Raisi,Dowans,Aridhi ya watanzania dhidi ya nguvu ya mwekezaji,IPTL,UDA,na mengine mengi hata wewe najua ni shahidi,nisisahau vipi kuhusu uhru wa kweli juu ya Tume ya uchaguzi?VIP kuhusu Raisi kushitakiwa pindi anapomaliza vipindi vya madaraka yake?au wewe unaamini na kujua ya kwamba Raisi anapokuwa madarakani hawezi kuukosea umma wa watanzani uliomchagua?na je kama anaweza kuwakosea ni kweli kwa katiba ya sasa anaweza kushitakiwa?jibu ni hapana!Ni vipi leo akubali kupitisha katiba ambayo inaweza kuwa na kipengele cha kumshitaki?huoni kwamba mswaada huu umeandaliwa kulinda masilahi ya chama tawala?kwani wewe Pascho umerudi lini nchini TZ maana yawezekana hujui jambo lolote linalotokea TZ.na kwa nyongeza hao CUF ambao leo walikuwa wanawakilishwa na Mh Mnyaa ambao tayari wameunda serikali ZNZ unategemea angepingana na kile Katibu wake mkuu alikiridhia?na je wewe unadhani Mnyaa anakipi cha kupoteza juu ya katiba ya Jamhuri?wakati tayari wana katiba inliyowafanya wakawa ni sehemu ya utwala wa nchi yao ya ZNZ.anyway mpaka hapo kwanza nijibu maana ninamasikitiko na hoja zako ulizotoa leo
 
Pasco umenena vyema.

Hawa jamaa wa magwanda hawana wakitakacho zaidi ya "shortcut".

Hata Kikwete afanye nini kwao ni kosa tu, tatizo lao ni Kikwete na si Serikali. Hilo lipo wazi kabisa, lakini ukweli ni kwamba Kikwete ndiye aliyefanya mema Tanzania hii zaidi ya Rais yeyote mwingine wa kabla yake na hilo halina utata wala ubishi. Wakae wafikiri.

And the vice versa is also true.
 
Pasco, hivi wangetoa hoja kwa kutumia kanuni ya 86 mjadala ungesimamishwa automatically au Spika angeuliza Bunge na Bunge kuamua? Unafikiri Wabunge wa CCM wangekubali kusimamisha mjadala baada ya kuulizwa na Spika?



Sidhani kama wame lose; ukiangalia zaidi utaona kuwa wao wamegain kwa sababu mstari umechorwa kati ya wale wanaoamini Rais na wana CCM wanaweza kufanya yote wayatakayo na wale ambao wanaamini the CCM government is in contempt of the people. Tofauti hii ya maoni ni ya muhimu. Rais na CCM wameweza kulazimisha sheria waitakayo wao kupita - kama walivyofanya kwenye sheria ya gharama za uchaguzi - lakini mwisho wa siku watajikuta ni wao pekee ndio wanaandika hiyo Katiba mpya na wale wanaowaamini au kuwafuata. Je kwa vile sheria imepitishwa ina maana mchakato utakuwa halali kwa kuangaliai first principle? Ukweli ni kuwa CCM hawakuhitaji hoja za CDM au za mtu mwingine yeyote juu ya mswada huu, walikuwa na mawazo yao na wameyatekeleza bila kuzuiwa kwani hakukuwa na mtu yeyote ambaye angeweza kuwazuia.




Siyo lazima. Watanzania ambao hawaamini katika uhalali wa mchakato huu kwa sababu umevunja the First Principle wanaweza kuupinga, kukataa kushiriki na kuwahamaisha wengine wasishiriki kwa hoja ambazo zitaonesha kuwa mchakto mzima umekosewa toka mwanzo na haukuwa nafasi ya kufanikiwa kwa sababu ulikuwa ni wa kulazisha kwa kutumia tyranny of thte majority. Wananchi hawawezi kulazimishwa kuitii tume ambayo hawaamini ni halali. Tume kupitishwa na kuundwa hakuipi uhalali (legitimacy) kwani uhalali wa sheria hauji kwa kupitishwa tu bali pia kwa uhalali wa hoja zake na mantiki yake. Mwanadamu hawezi kulazimishwa kutii kitu ambacho ni kinyume na dhamira yake, ukweli na mantiki yake au kile ambacho kinaonekana kwa makusudi kimetengezwa ili kumkandamiza.




Wanaoamini kuwa sheria hii ni halali na kuwa mchakato ni halali wanayo haki ya kujitokeza kwa furaha kwenda kutoa maoni yao. Wale ambao wanaamini mchakato huu umesurp power ya wananchi na kuwa umelazimishwa wanayo haki ya kukaaa kushiriki na kuhamasishana kutoshiriki hadi hoja zao zisikilizwe vinginevyo wanalo jukumu la kuhakikisha kuwa itakapokuja kura ya maoni wataenda na kuhamasishana kupigia kura ya "hapana" hiyo referendum na kuzuia Katiba Mpya itakayopitishwa na wana CCM.

Wanaweza kukataa kusikiliza maoni juu ya mchakato na wanaweza kabisa kulazimisha watu waje kwenye tume yao lakini watakapoletwa swali hilo kwa wananchi hawana namna ya kuwazuia wale wasioshiriki mjadala kupiga kura ya hapana. Unless waseme watakaopiga kura ya maoni ni WALE TU walioshiriki kwenye kutoa maoni! Kitu ambacho hakimo kwenye mswada huu hadi waufanyie mabadiliko.

Mzee MM
Nakubaliana na wewe kiasi kikubwa. Napenda kufanya makusanyiko(Summarize .. i hope niko sawa kwenye translation) at the end of the day tunachotaka ni katiba BORA mpya na sio BORA katiba, kama Pascal anaona kuna makosa yameshafanyika (kama kweli yapo) na kwa maelezo yake basi tuache uchafu uendelee kutokea kwa kweli napata shida kuelewa ajenda yake, maana naamini kila mtu mwenye nia njema na nchi hii anaelewa katiba tuliyonayo imetufikisha wapi.

Nilitegemea sana Pascal aeleze makosa ambayo tumefanya kisha namna ya kurekebisha ili lengo letu liwe hilo moja kupata katiba bora(sio bora katiba), lakini inavyoelekea bwana Pascal anataka kutuaminisha kuwa madhali kuna kosa moja(kwa kweli kwa upande wa CCM na washirika wake makosa ni mengi mno kuliko hilo moja ambalo Pascal anakazana kulielimisha) basi sasa tuwape watu wale wale wanaofanya mambo kwa mazoea(eti sababu babu alifanya nasi tufanye) tuendelee na tusubiri watu wale wale watuamulie mustakabali wa taifa baada ya 2015.

Kwangu mimi huu ni upotoshaji mkubwa unaotaka kuendeleza, kama utakumbuka nimetoa angalizo(comments) kwenye moja ya post yako ya kuendeleza kitu wenzetu wanita "DIVERSIONARY TACTIS" ili hoja za msingi zisijadiliwe tena, tuendelee na mjadala wa CDM na CCM, Wanaharakati na CCM, (wanazuoni, wasomi, makundi mbali mbali na CCM), e.t.c

Jamani KATIBA ni fundamental law, its the basis of your life. Wengi tunafikiri katiba ni sheria kama sheria zingine lakini kwa kweli katiba ni msingi wa maisha yetu, ndo una define sisi ni watu wa aina gani. Labda kwa kuongezea kwenye mjadala niliongalia jioni ya leo, kuna swali aliulizwa Tindu Lissu kuhusu ufahamu wa katiba leo jioni kama watanzania wanaifahamu katiba,,,, naomba nimpe mtazamo wangu binafsi kuwa watanzania wanaijua katiba yao vizuri sana kupitia maisha yao wanayoishi, wanavyokula, wanavyopata huduma za jamii (mf. afya, elimu e.t.c) huo ndio ufahamu wa katiba ambao unaweza kuwapelekea. Hakuna sehemu duniani unaweza kupata katiba ambayo hata 25% ya wananchi wake wanaifahamu ki elimu dunia (academically)... NOOOOO!!!!

TUWE SERIOUS NA HII MIJADALA.
 
Pasco,
Suala la katiba lilianza siku nyingi lakini likapata msukumo wa nguvu pale CDM walipolipeleka mahakama ya wananchi. Kosa ni pale walipokubali kuwa rais Kikwete bila ridhaa ya serikali au chama chake alipoamua kulisamimia na CDM wakatulia na kuamini hivyo. Technically hapa ndipo kosa la CDM lilipoanzia.

Kama bunge letu lingekuwa na 'fair play' yote uliyoeleza ndiyo yalipaswa kutokea na lawama dhidi ya CDM zingekuwa haki, kwa bahati mbaya bunge halifanyi kazi kwa kuzingatia sheria au kanuni hasa zinapokinzana na masilahi ya rais na spika ni mjumbe wa CC ya CCM. Anatumwa kutekeleza yale ya chama ni si ya wananchi.

Mswada uliporudishwa baada ya maoni kuleta mushkeli CDM waliuliza je umeondolewa au umefutwa? Nakumbuka PM Pinda alisema umerejeshwa kwenye kamati. Alipobanwa hakuwa na jibu clear na pengine wapinzani wakjua hoja imekufa. Hili nalo lilikuwa kosa kwasababu ilipaswa CDM wapate majibu yasiyo na njia panda.

Kutoka nje ya bunge baada ya kuwasilisha maoni ni jambo la kiungwana kwasababu leo tunajua kwanini walitoka nje, vinginevyo tungebaki kujiuliza wametimka tu je wanajua kwanini wametimka.Kutimka kwao ndiko kumeishtua jamii kuwa lipo jambo, jamii kama ya kwetu ambayo wengi hawana ufahamu mpaka kitakapotokea kishindo ambacho CDM wamekifanya.

Nadhani suala la katiba ni letu sote, CDM wanajaribu kutuwakilisha kwa kadri wanavyoweza wakiwa katika 'stress' ya hali ya juu sana.
Kwa vile katiba ni yetu sasa tujadili tunaiokoaje katiba yetu kwa kushirikiana na CDM ili isipokwe na wanyang'anyi!

Kama ilivyokuwa Nkrumah hall, Karmjee na Zanzibar sisi wenye katiba tusimame na kuwaambia hata kama wamepitisha sheria, sheria hiyo si ile tunayoitaka na tusme No! Tunauwezo wa kuwalazimisha watusikilize, tunasababu tunachokosa kwa sasa ni uthubutu.
Badala ya kuwalaumu CDM tufikirie tutajengaje uthubutu kwa raia wetu ambao wapo tayari
 
hapana ni kwamba ana maoni tofauti na kuwa anaamini maoni yake ni sahihi. Ni jukumu letu kuonesha kuwa maoni yake si sahihi. Mtu kuwa na maoni tofauti haina maana ni mnafiki.

Sisi tutaendelea kuonyesha maoni yake yako sahihi na yenu yanakusudio la kupotosha au kutafuta media attention!
 
Back
Top Bottom