Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Namalizia kwa kusisitiza, kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa!. Chadema kwenye uundwaji tume mmefanya kosa!. Sheria imetungwa na sasa sio kosa tena, kosa ni kurudia kosa kama hamtoa maoni yenu kwenye tume!. Two wrongs don't make right, better late than never!.

2015 sio mbali kihivyo!.

Wasalaam
Paskali
Chadema susa susa, walifanya kosa kususia mchakato wa uundwaji wa tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya.

Wakati wa kupiga kura kupitisha katiba mpya, Chadema walisusa tena!.

Sasa wamesusa tena eti wanataka ni mpaka katiba mpya!. Kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa. Chadema inafanya makosa makubwa kususa, huku ni kurudia kosa!.

Kila la kheri kwenye kususa.
P
 
Ccm wanachakachua maoni ya Wananchi halafu wewe unashabikia.. Ujinga gani huu?
 
Wanabodi,

Kitendo cha Mhe. Lissu kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani, yamemaanisha wameijibu hoja ya serikali hivyo kutoa go ahead majadiliano yaendelee. Uwasilishwaji wa hotuba hiyo ndio passport ya mjadala kuendelea, kama kambi ya upinzani wasingewasilisha maoni yao, muswada ungesitishwa kwanza na wao kusikilizwa. Hivyo iwasilishwaji wa hotuba ile ni kosa la pili, Chadema lazima wakiri kosa, waombe radhi na kusonga mbele!.

Kitendo cha kususia mjadala kwa siku ya kwanza na kutoka nje, was the right move kuonyesha protest dhidi ya unyanyasaji wa Mhe. Spika, lakini kuisusa hoja jumla, was a mistake hivyo sheria imetungwa bila imput yao, hivyo hili ni kosa la tatu, Chadema wakiri kosa, waombe radhi na kusonga mbele!.

Nimebahatika kuhudhuria mdahalo wa Star TV kuhusu Tanzania tuitakayo ambapo Mhe. Tindu Lissu ilikuwa ni mdahiliwa, na nilipata fursa ya kuuliza swali kuhusu kanuni ya 86 lililokuwa na vipengele a, b na c
(a) Kanini hawakitumia kanuni ya 86 kuuzuia muswada usisomwe?.
(b) Kwanini waliwasilisha hotuba ya maoni ya kambi ya upinzani yaliyotoa passport mjadala uendelee badala ya kuwasilisha pingamizi ambayo ingeusimamisha mjadala?.
(c) Chadema wamesusa sheria imepitishwa, jee wamefaidika na nini na kususa kwao?.

Mhe. Lissu amepiga chenga kutoa majibu ya kina kwa kujibu
(a). Amenisomea hitimisho la hotuba yake. Kanuni ya 86 ilimtaka Mhe. Lissu awasilishe pingamizi na sio hotuba!.
(b) Amepiga chenga kueleza ni kwanini amewasilisha hotuba badala ya pingamizi!.
(c) Wananchi wanaelewa ni nani mtetezi wao wa ukweli.

Kwa vile sheria imepitishwa na itasainiwa na rais kwa mbwembwe, lazima Chadema na wapenzi wao na mashabiki wao waukubali ukweli mchungu kuwa they lost the battle hivyo watake wasitake, lazima wakubali matokeo. Hawawezi kuendelea kususa, lazima wajisibmit kwenye tume ya kuratibu maoni na kutoa maoni yao hata kama tume hiyo itaundwa bila imput yao na bila ridhaa yao!.

Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo (Tume ya kukusanya maoni) na yajayo (Katiba Mpya).

Namalizia kwa kusisitiza, kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa!. Chadema kwenye uundwaji tume mmefanya kosa!. Sheria imetungwa na sasa sio kosa tena, kosa ni kurudia kosa kama hamtoa maoni yenu kwenye tume!. Two wrongs don't make right, better late than never!.

2015 sio mbali kihivyo!.

Wasalaam
Paskali
Ni kweli kasoma/mmesoma wote Ilboru lakini mlosoma Ilboru mlipaswa kuwa kitu kimoja na kumfanyia Lobbying mwanafunzi mwenzenu Tundu Lissu wa Alumni hiyo badala ya kumnanga kila siku il kusifia sifia kwamba Ilboru na ujinga mwingine.

What a nonsense!

Acha hizo Paschal.
Mkuu Richi, Richard , kwanza asante kwa hoja hii very objective, kutushauri kumfanyia Lobbying mwanafunzi mwenzenu Tundu Lissu, kwa vile wanasiasa waliosama Ilboru ni wengi, akiwemo Lazaro Mwigulu Nchemba, Nyalandu, Jeremia Maganja, Prof. Sifuni Mchome, na wengine wengi tuu, sasa tumlobie nani tumuache nani?,

Ila mimi kwa upande wangu, kwa Lissu, nimejitahidi sana kama kwenye uzi huu

Eid Mubaraka.

P.
 
Back
Top Bottom