Kati ya simu tatu zinazopigwa, mbili ni za mtu anayetaka apewe pesa

Kwanza panga mipango yako alafu jifunze kusema sina hata kama unacho ilimradi kiwe kwenye ratiba. Iwe ndugu au masela wote fyekelea mbali usiwe na huruma maana hata ww ukikosa hawawezi kukuhurumia. Usiache kutembeza maokoto kwa wazazi na wenye uhitaji. Utaziona baraka za Mungu
 
Mwanangu simu tatu tu unalalamika ?? Kuna maana gani ya kuwa na chochote kitu.

Kama unacho alafu mdau au.ndugu amekucheki fungua moyo.

Kama huna usiikalifishe nafsi.

Mpaka mtu amekucheki ina maana kashacheki kwenye contact yake kuwa ww ndio unaweza ukamsaidia, mana Kuna ndugu kibao hakuwacheki alishachungulia akaona hawa wengine ni miyeyusho tu.

Note

Unapotoa sana na ndio unapata zaidi Nisha prove hiki kitu, ila saidia wenye shida kweli sio wale wapiga vizinga mana Kuna watu anaweza kuomba Hela kwa watu WA Tano kama anadaiwa rejesho.

Kuna muda unaombwa Hela Hadi unajisikia kichefu chefu ila jikaze ndio ukubwa huo ,mkono mtupu haurambwi mpaka unaombwa ujue ww una nafuu KULIKO wengine.! Jipongeze
 
Kama kweli huna pesa mwambie ukweli kwamba huna pesa, ila kama unazo na una uwezo wa kumsaidia lakn bado ukakataa sio sawa, huwezi kusaidia kila mtu katika hii dunia lakn inapotokea nafasi ya kusaidia na umethibitisha kweli muombaji ana changamoto mi naona saidia tu.
personally mm nikisaidia alafu mtu akasema asante sana huwa napata feelings flani za furaha na hunitokea automatically.
Bottom line kama unaweza kusaidia fanya hvyo kama huna uwezo kuwa mkweli, what goes around comes around.
Watu wanajikuta wanaishi kwa bajeti sana siku hizi kiasi kwamba ubinafsi unawavaa wanasahau kuwa mwenye shida akikuomba na unachokidogo cha kutoa basi usianze visingizio. Toa itajulikana mbele. Leo umenipiga tafu 10,000 kesho utanikuta mazingira ya kukusaidia milioni.

Ila kwasababu watu wameamua kuwa watata wacha tuishi humo ila tusilaumiane baadae picha likigeuka.
 
Wewe nae ni mmoja wao? Maana na namna ya uhandishi huu kuna namna hapa..
Unamaanisha Mimi ni mmoja ya waombaji? Yaani ukiniuliza mara ya mwisho kuomba ni lini hata sikumbuki, inaweza kuwa hata miaka 10 iliyopita. Namshkuru Mungu napata riziki ya kutosha kuniwezeaha mimi na familia yangu, aibu ndogo ndogo za kuomba zimenipitia mbali sana
 
Back
Top Bottom