Kati ya Miili 1,294 iliyofukuliwa ni 52 pekee ilipata idhini ya Mahakama, mingine ilifukuliwa kinyume cha Sheria

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Katika uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dar es Salaam, unaonesha kuwa tangu mwaka 2015 hadi 2021, kulikuwa na matukio ya kufukua miili 1,294. Kati ya matukio hayo, yaliyoruhusiwa kufukuliwa kwa amri ya mahakama ni 52 pekee.

Aidha, Mahakama ya Tanzania imesema ni kosa kisheria kufukua mwili wa marehemu bila kupata amri ya mahakama. Imesema mhimili huo ndio wenye mamlaka ya kutamka kwamba mwili wa marehemu ufukuliwe kama utakuwa umezikwa au kutozikwa endapo mazingira ya kifo yatakuwa na utata au vifo chini ya uangalizi wa polisi au magereza.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Richard Kabate amesema hayo alipozungumza katika kipindi cha televisheni cha Sema na Mahakama. Kabate alisema Sheria ya Uchunguzi wa vifo vyenye mashaka kifungu cha 12, kinamtaka yeyote atoe taarifa kwa hakimu mchunguza maiti kuhusu kifo cha mashaka cha ndugu au mtu mwingine.

HABARI LEO
 
Kwa nini wanakimbilia kuizika miili ilhali wanajua vifo vina utata, na baadae kulazimika kufukua na kufanya uchunguzi? Hili jeshi ni balaa kwa WaTz!
 
Wazia tu mtu mliemzika miaka 2 juzi tena amaekufa kifo cha kawaida leo ameonekana tena yupo fresh tu kenn tusifukue kaburi?
 
Back
Top Bottom