Dar: Dibron Saidi ahukumiwa kunyongwa kwa kosa la kumuua Mkewe Herieth Justine kwa kisu, ni baada ya kumfumania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imemtia hatiani na kumhukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa, Dibron Saidi kwa kosa la kumuua aliyekuwa mkewe, Herieth Justine kwa kumchoma na kisu mara tatu.

Hukumu hiyo imesomwa leo na Hakimu mkazi mkuu, Evodia Kyaruzi aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo.

Akisoma hukumu hiyo, Kyaruzi amesema Mahakama imeona hoja zilizotolewa na mshitakiwa wakati akitoa utetezi wake hazikuwa na ukweli.

IMG-20230117-WA0027.jpg


Amesema kuwa mshitakiwa alidai kuwa alimchoma kisu, Herieth kutokana na hasira alizokuwa nazo kwa kujibiwa maneno ya karaha baada ya kumfumania akiwa anafanya mapenzi na mwanaume mwingine uchochoroni hivyo aliwezaje kuvumilia kumchoma alipokuta akifanya hiko kitendo na amchome kwa maneno aliyokuwa akitoa marehemu?

Amehoji kuwa wakati alipomfumania kulikuwa na purukushani ambayo alidai ilidumu kwa dakika kumi kabla ya mwanaume aliyemfumania kukimbia kwanini hakumchoma mida huo kama alikuwa na hasira.

Pia amesema Mshitakiwa alidai kuwa alimchoma kisu marehemu mara moja lakini ripoti ya uchunguzi wa kitabibu pamoja na maelezo ya shahidi namba tatu ambaye alimshuhudia mshitakiwa akiwa anamchoma kisu pamoja na shahidi namba nne ambaye alikabidhiwa mwili kwa ajili ya mazishi yanaonesha alimchoma kisu mara tatu.

Vilevile alisema kuwa mshitakiwa alidai kuwa marehemu aliteleza katika ganda la ndizi na kuangukia katika kisu ambacho alikuwa amekishika haikuwa kweli.

Hivyo amesema kwa hoja hizo pamoja na ushahidi uliotolewa na mashahidi sita upande wa mashitaka unajitosheleza kumtia hatiani kwa kosa la kumuua, Herieth kwa kukusudia.

Akizungumza Mahakamani hapo baada ya mshitakiwa kukutwa na hatia Wakili wa serikali, Tumaini Maingu ameiomba Mahakama kutoa adhabu kwa mujibu wa sheria na kanuni ya adhabu sura ya ishirini na ishirini na mbili.

Ameieleza Mahakama kuwa Maisha ya binadamu ni zawadi pekee inayotolewa mara moja na ikishapotea haiwezi kurudi tena ndio maana yanalindwa kwa sheria kali kama inavyoelezwa katika vitabu vya dini na Katiba ya nchi katika ibara ya 14 hivyo kitendo cha Dibron ni kukiuka sheria hizo.

Amedai marehemu kaacha watoto watatu na mama ambao walikuwa wakimtegemea na kusisitiza kuwa hukumu haina huruma kwa aiyekiwa na huruma.

Kwa upande wake wakili wa utetezi, Yohana Kibindu ameieleza Mahakama kuwa chanzo cha ugomvi ni wivu wa mapenzi na hauwezi kuwa na wivu kwa usiyempenda hivyo Dibron alikuwa na mapenzi ya dhati kwa marehemu hivyo hakudhamilia kumuua.

Amedai kisu alichotumia kumchoma marehemu hakwenda kukinunua dukani bali kilikuwa ni moja ya nyenzo zake na alikuwa nacho pindi anatoka kazini pia mteja wake ni mgonjwa na anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa henia Machi 2 mwaka huu.

Hivyo aliiomba mahaka kumpa mteja wake adhabu nafuu kwani kwa muda aliokaa jela amejigunza na kujutia yote aliyofanya.

Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa Machi 11 mwaka 2018 katika eneo la Vingunguti Majengo, Dibron Saidi alimuua anayedai mkewe, Herieth Justine kwa kumchoma kisu mara kadhaa kwa madai kuwa alimfumania na yeye mwenyewe kujaribu kujiua kwa kujichoma na kisu bila mafanikio
 
Hizi hukumu hewa, hukumu jina tu, eti kunyongwa hadi kufa,


hukumu ambazo hazijawahi hata kutekelezwa, ni wakati sahihi zifutwe tu, ni kuogopesha watu tu kunyongwa hadi kufa huku uhalisia uliopo hiyo ni adhabu ya kifungo cha maisha tu..

Maana waliohukumiwa kunyongwa adhabu hizo hazijawahi kutekelezwa hata mara moja kama wenzetu saudia. Gerezani wanaishi kama peponi! Hawafanyi Kazi yoyote ila hawaonani na binadamu yeyote....nadhani huo upweke wanaokuwa nao unawatosha.
 
Back
Top Bottom