Yajue Mamlaka (Jurisdiction) ya Mahakama ya Mwanzo (Primary Court)

Apr 26, 2022
64
97
Hello, naitwa Zakaria (lawyer by profession).🎓

Leo napenda tujifunze kuhusu MAMLAKA YA MAHAKAMA ya Mwanzo (Primary Court).

Kwa ufupi, Mahakama ya mwanzo ni Mahakama ya chini kabisa katika mfumo wa Mahakama nchini Tanzania. Mahakama hii imeanzishwa kwa mujibu wa section 3 ya sheria ya Mahakama za Mahakimu (The Magistrates’ Courts Act, [CAP 11 R.E. 2019] hereinafter referred to in short as MCA).

Mahakama ya mwanzo inapatikana (karibia) kila Wilaya nchini Tanzania, 🇹🇿 na ina mamlaka ya kusikiliza kesi ndani ya wilaya husika tu ambapo imejengwa au kuanzishwa.

Kabla sijaendelea, tufahamu kwanza nini maana ya Mamlaka/Jurisdiction kisheria?

Kwa ufupi, Mamlaka ya Mahakama (Jurisdiction) ni mipaka au nguvu ya Mahakama kusikiliza na kuamua kesi. Sio kila Mahakama unayoiona inaweza kusikiliza kesi yoyote ile.

And, Jurisdiction is purely statutory/it is a creature of statutes. Mamlaka ya Mahakama yanapatikana kwenye sheria. đź“š Watu kwenye kesi hawawezi kujipangia tu wenyewe na kuipa Mahakama Mamlaka ambayo haina. Hivyo kuna aina nyingi za Mamlaka kama zinavyoainishwa na sheria mbalimbali.

Sasa tuendelee na Mamlaka ya Mahakama ya Mwanzo.

Zifuatazo ni aina za mamlaka (JURISDICTION) mbalimbali za Mahakama popote duniani, 🌎 lakini ambazo Mahakama ya Mwanzo pia inazo nchini Tanzania. Hapa nataja aina ya mamlaka na kuelezea relevance yake ikoje kwa upande wa Mahakama ya Mwanzo (if any/ikiwa ipo, maana Mahakama inaweza isiwe na aina zote za Mamlaka tajwa hapo chini):

1: TERRITORIAL JURISDICTION (MAMLAKA YA KIENEO/KIJIOGRAFIA):

Haya ni Mamlaka ya Mahakama kusikiliza na kuamua masuala ambayo yanatokea ndani ya mipaka/eneo ambapo mahakama hiyo imeanzishwa. Mfano, Mahakama ya Mwanzo nchini Tanzania, ina mamlaka ya kusikiliza na kuamua kesi zinazotokana na matukio yaliyotokea ndani ya wilaya ambapo hiyo Mahakama ipo. Section 3(1) of the MCA.

2: SUBJECT MATTER JURISDICTION (MAMLAKA KULINGANA NA AINA YA MGOGORO):
This means Jurisdiction by categorization of offenses. Ni mamlaka ya Mahakama kutegemeana na aina ya kesi au makosa.

Kila suala au mgogoro una Mahakama yake. Mfano Mahakama ya Mwanzo ina Mamlaka ya awali kusikiliza baadhi ya makosa ya jinai ambayo imeruhusiwa kisheria. Pia ina Mamlaka ya kusikiliza kesi ya madai, ndoa/talaka na mirathi pale ambapo SHERIA INAYOTUMIKA NI YA KIMILA AU KIISLAM.

3: ORIGINAL JURISDICTION (MAMLAKA YA AWALI):
Haya ni Mamlaka ya Mahakama (yoyote) kusikiliza kesi/shauri kwa mara ya kwanza. Mfano, Mahakama ya mwanzo ina Mamlaka ya awali kusikiliza kwa mara ya kwanza mashauri yote ya madai pale ambapo sheria inayotumika ni ya Kiislam au kimila. Pia ina Mamlaka ya kusikiliza kwa mara ya kwanza baadhi ya makosa ya jinai ambayo imeruhusiwa kisheria.

Vile vile, Mahakama ya Mwanzo ina (UNLIMITED) ORIGINAL JURISDICTION kwenye kesi za mirathi kama sheria inayohusika ni ya Mila au dini ya Kiislamu (where the law applicable is customary law or Islamic law) haijalishi aina ya mirathi (hata iwe ardhi) na haijalishi kiasi cha fedha au thamani (pecuniary/value) ya mirathi hiyo.

Kiufupi, Mamlaka ya Mahakama ya Mwanzo kwenye mirathi hayana kikomo/mipaka. Kinachoangaliwa ni ikiwa marehemu wakati wa uhai wake aliishi kwa kufuata taratibu za kimila au taratibu za dini ya Kiislamu, na ikiwa Marehemu alikuwa ana makazi ndani ya mipaka ilipo Mahakama ya Mwanzo. Soma section 19(1) (c) of the MCA & paragraph 1(1) of the Fifth Schedule to the MCA.

4: CONCURRENT JURISDICTION (MAMLAKA YA MLINGANO):

Haya ni mamlaka ya aina moja au yanayofanana kwa Mahakama zaidi ya moja. Mfano Mahakama ya Wilaya na Mahakama ya Hakimu Mkazi zote zina Mamlaka sawa, isipokuwa Mahakama ya Wilaya inasikiliza kesi katika wilaya husika tu, lakini Mahakama ya Hakimu Mkazi inaweza kusikiliza kesi inayotokea katika wilaya yoyote kwenye mkoa mzima (hata hivyo hiyo haimaanishi tuna Mahakama ya Mkoa - hatuna Mahakama ya Mkoa).

Vivyo hivyo, Mahakama ya Mwanzo ina Mamlaka sawa na Mahakama Zingine katika baadhi ya kesi/mashauri. Mfano kwenye mashauri ya ndoa, Mahakama ya Mwanzo ina mamlaka sawa na Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama Kuu.

Kwa hiyo kesi ya ndoa inaweza kufunguliwa Mahakama yoyote kati ya hizo, maana zina Mamlaka sawa (concurrent jurisdiction). Soma section 76 of the Law of Marriage Act, CAP. 29 R.E 2019.

5: REVISIONAL JURISDICTION (MAMLAKA YA MAPITIO):

Ni Mamlaka ya Mahakama (ya juu) kupitia au kukagua mwenendo, hukumu, adhabu na amri za Mahakama ya chini ili kujiridhisha usahihi na uhalali wake kisheria.

Mahakama ya Mwanzo ina mamlaka ya kuitisha kumbukumbu (records) za mwenendo wa shauri/kesi kutoka baraza la kata na kukagua ili kujiridhisha iwapo uamuzi wa baraza haukiuki Sheria au misingi ya haki.

6: APPELLATE JURISDICTION (MAMLAKA YA RUFAA):

Haya ni Mamlaka ya Mahakama kupokea na kusikiliza rufaa ya mlalamikaji au mshitakiwa ambaye hajaridhika na maamuzi au amri ya Mahakama ya chini.

Ingawa wengi wanasema Mahakama ya Mwanzo haina mamlaka ya kusikiliza na kuamua rufaa (sio Appellate Court - which hears an appeal from another court), kwa sababu ni Mahakama ya chini kabisa katika mfumo wa Mahakama ambayo mara nyingi inasikiliza kesi kwa mara ya kwanza (ni trial court - a court which hears a case for the first time), hata hivyo, Mahakama ya Mwanzo inapokea na kusikiliza rufaa kutoka Mabaraza ya Kata isipokuwa maamuzi yanayohusu migogoro ya ardhi.

7: PECUNIARY JURISDICTION (MAMLAKA YA KIFEDHA):

Haya ni mamlaka ya Mahakama kusikiliza na kuamua kesi kwa kuzingatia kiwango au kiasi cha fedha au thamani ya kitu. Kuna mipaka ya kiasi cha fedha kwa kila Mahakama.

Kwa upande wa Mahakama ya Mwanzo, pecuniary jurisdiction ni milioni thelathini hadi milioni hamsini (thirty to fifty millions Tanzania shillings). Refer Section 18(1)(a)(ii) & (iii) ya MCA inasema, Primary Court shall have jurisdiction in all proceedings of a civil nature:-

{ii} “for the recovery of civil debts due to the Republic, any district, city, municipal or town council or township and for contracts, if the value of the subject matter of the suit does not exceed 50,000,000/= (fifty million shillings)”

Kwa kiswahili Mahakama ya Mwanzo ina Mamlaka ya Kusikiliza mashauri yote ya madai ya fedha tasilimu ambayo mdai ni Mamlaka za serikali za Mitaa (Jiji, Manispaa, Halmashauri za Wilaya, Halmashauri za Miji), na mikataba yasiyozidi shilingi 50,000,000/= (Milioni Hamsini).

{ii} “for the recovery of any civil debt arising out of contract, if the value of the subject matter of the suit does not exceed 30,000,000/= (thirty million shillings)”.

Ina Mamlaka ya Kusikiliza mashauri mengine ya madai ya madeni ya fedha au mikataba kwa kiwango kisichozidi shilingi 30,000,000/= (milioni thelathini).

Kwa lugha rahisi, ukomo wa mamlaka ya Mahakama ya Mwanzo katika kesi za madai ni shilingi milioni 30 kwa mali inayohamishika na shilingi milioni 50 kwa mali isiyohamishika.

Pecuniary Jurisdiction of the Primary Courts is Tshs. 50,000,000/= for Immovable properties and Tshs. 30,000,000/= for movable properties. Section 18(1) of the MCA.

NB: Mamlaka ya Mahakama ya Mwanzo hayatakuwa na mipaka ya kiasi cha fedha kwenye kesi ya madai, IKIWA SHERIA INAYOTUMIKA NI YA KIMILA AU KIISLAM, kwa sababu kesi za madai kuhusu masuala yanayotumia sheria za kimila na sheria za Kiislamu ni lazima yaanzie Mahakama ya Mwanzo bila kujali kiasi cha fedha.

8: EXTENDED JURISDICTION (MAMLAKA YA ZIADA):

Haya ni Mamlaka ya nyongeza/ziada ambayo Hakimu huwa anapewa ili kusikiliza mashauri ambayo kwa kawaida yanasikilizwa na Mahakama Kuu tu. Na maamuzi ya Hakimu huyo yatachukuliwa kuwa ni maamuzi ya Mahakama Kuu.

Zipo aina nyingi za mamlaka (jurisdiction) kama vile;-
-Exclusive Jurisdiction* (Mamlaka ya kipekee)
-Mamlaka ya marejeo (review)
-Supervisory Jurisdiction
-Inherent Jurisdiction etc.

Kwa ufupi Mamlaka ya Mahakama ya mwanzo tunaweza kuyagawa mara mbili:-

1: MAMLAKA ya Mahakama ya Mwanzo kwenye kesi za madai (civil cases) na

2: MAMLAKA ya Mahakama ya Mwanzo kwenye kesi za jinai (criminal cases).

1: Tuanze na MAMLAKA ya Mahakama ya Mwanzo kwenye kesi za madai (civil cases):

Kwa ujumla, Mamlaka ya Mahakama ya Mwanzo kwenye kesi za madai yamefafanuliwa kwenye sections 18(1),19(1)(b) na 19(1)(c) ya MCA na kwenye jedwali la nne na la tano/the Fourth and Fifth Schedules to the MCA.

Ambapo Mahakama ya Mwanzo imepewa Mamlaka ya kusikiliza na kuamua kesi zote za madai pale ambapo sheria inayotumika ni ya kimila au Kiislam.

Hivyo, kesi za madai kuhusu masuala yanayotumia sheria za kimila na sheria za kiislamu ni lazima yaanzie katika Mahakama ya Mwanzo. (Civil cases on matters which apply customary law and Islamic law must be initiated at the level of the Primary Court).

2: MAMLAKA YA MAHAKAMA YA MWANZO KWENYE KESI ZA JINAI:

Sheria imetaja makosa ya jinai ambayo yanaweza kusikilizwa na Mahakama ya mwanzo na adhabu zinazoweza kutolewa na Mahakama ya Mwanzo. Soma jedwali la kwanza na la tatu la Sheria za Mahakama za Mahakimu (the First and third Schedules to the MCA).

NB: Sio kila kosa la jinai linaweza kusikilizwa na Mahakama ya Mwanzo, mfano Mahakama ya mwanzo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya ubakaji, unyang’anyi wa kutumia nguvu, mauaji, uhujumu uchumi, rushwa, kugushi, uhaini na mengineyo ambayo haijapewa mamlaka na sheria kusikiliza.

Mwisho, usiporidhika na hukumu au amri ya Mahakama ya Mwanzo unaweza kuomba rufaa Mahakama ya Wilaya.

(Maelezo haya ni kwa mujibu wa sheria zilizokuwa zinatumika mpaka siku ya kupost humu andiko hili, hivyo unaposoma leo maelezo haya soma na marekebisho ya sheria yaliyopo sasa hivi).

Kama una maoni au swali karibu.

Imeandaliwa na kuletwa kwako na mimi Zakaria (0754575246 - WhatsApp).
 
Back
Top Bottom