Kati ya Mbagala na Gongo la Mboto wapi kuna watu wengi?

Kati ya Mbagala na Gongo la Mboto wapi kuna watu wengi?

Aisee kumbe wewe tunavyosema gomsi unapachukua pale pale gomsi mwisho stendi lakini wewe mbagara unaichukua hadi mbande huko na kina charambe nimekuuliza unaijua safari ya mbagara mwisho mpaka mbande umbali wake?

Ukiichukua mbagara kama jimbo na huku tutakuwekea ukonga kama jimbo maana ukisema GONGO LA MBOTO ni direct unaizungumzia ukonga.
Turahisishe : weka Mbagala unaiyoijua kiuhalisia mwanzo wa eneo mpaka mwisho kisha weka na kwa Goms mwanzo mpk mwisho kisha tushindanishe.
 
Mbagala ni jina la sehemu nzima

Gongo la mboto napo ni jina la sehemu nzima.

Sitaki kuamini kama ukifika kurasini, mtoni unasema upo mbagala sababu zipo njia ya kwenda mbagala

Maana ya hoja yako nikifika Tazara, kipawa ama banana niseme ni sawa na nipo gongo la mboto sababu ni njia moja.

Hoja ni mbagala kama mbagala na gongo la mboto kama gongo la mboto
Sasa mbona unawaweka wakina charambe na ndugu zake mbande ambao umbali wake sio chini ya Km 15 kutoka mbagara mwisho.
 
Hatangalii umbali tunaangalia je ipo ndani yake ? kutoka Dar na Morogoro town ni karibu zaidi kushinda hata kutoka pale Moro town kwenda wilaya nyingine ila hatuwezi kusema Moro ni Dar kwa kuzingatia ukaribu.

Elewa kwamba iyo Charambe na Mbande jina la zamani lililojulikana ilikuwa ni Mbagala Mbande ,Mbagala Charambe ila baada ya mji kukua jina la Mbagala likatoka sasa inaitwa Mbande tu lakini tukija 2008/9 mpk 2010 kote palijulikana kama Mbagala Maji matitu pekee ndio imeMaintain jina la Mbagala mpaka leo inaitwa Mbagala Majimatitu ila jina hilo linapotea mdogo mdogo .Hiyo case ni sawa na Buza jina la Buza limekuja sasa ila nyuma kidogo ilikuwa sehemu ya Yombo pamoja na Yombo Dovya Buza ilikuwa ikiitwa Yombo Buza ilikuwa nadra sana mtu kusema naenda Buza hata kiwalani nayo mpaka sasa ni Yombo Kiwalani.

Ila tukiwa kwa Goms Kitunda ,kivule hata Banana nk toka kitambo haina uhusiano na Goms kijina ,kiserikali hata raia wa kawaida hawachukulii kuwa wapo Gongo la mboto . Na ukija kiserikali maeneo yote niliyotaja kuwa yanauhusiano na Mbagala yapo Jimbo la Mbagala.

Na hitimisha kuwa Goms sio pa kufananisha na Mbagala na mnakimbilia polisi kujumlisha Goms na Airport na maeneo ya jirani .
Unawezaje kutenganisha Gomzi na Ukonga mbona havitengani?
Gomzi na Majohe?
Gomzi na Pugu?
Labda uwe hujaishi huko.......
Kwenye Mbagala unataka Mbagala na Mashoga zake, ila Gomzi unataka mtaa mmoja.
NJia rahisi ni kwenda kwa majimbo, jimbo la Ukonga vs Jimbo la Mbagala.
 
Turahisishe : weka Mbagala unaiyoijua kiuhalisia mwanzo wa eneo mpaka mwisho kisha weka na kwa Goms mwanzo mpk mwisho kisha tushindanishe.
Gomsi anzia banana,mombasa mpaka gomsi mwisho .....hapo pugu na wakina chanika watoe.

Ila hapa hoja ni ukanda wa mbagara na ukanda wa Gongo la mboto ambayo ndiyo ukonga hiyo ipi ina nyomi ........ila hata ukitaka pale center kama center ya mbagizo gomsi imejigawa kwa mombasa,banana na Gongo la mboto hayo maeneo yote ni vibe muda wote yenyewe wakati mbagara sehemu iliyochanganya ni mbagara mwisho tu.


Nakupa kazi rahisi mtafute konda yeyote wa daladala muulize mbagara na Gongo la mboto wapi kuna nyomi utapata majibu
 
Unawezaje kutenganisha Gomzi na Ukonga mbona havitengani?
Gomzi na Majohe?
Gomzi na Pugu?
Labda uwe hujaishi huko.......
Kwenye Mbagala unataka Mbagala na Mashoga zake, ila Gomzi unataka mtaa mmoja.
NJia rahisi ni kwenda kwa majimbo, jimbo la Ukonga vs Jimbo la Mbagala.
Bora unisaidie anasema banana sio Gongo la mboto.

Hapa kwa majimbo ndio wamekaa asubuhi kweupe.
 
Bora unisaidie anasema banana sio Gongo la mboto.

Hapa kwa majimbo ndio wamekaa asubuhi kweupe.
Mojohe pia ni gomzi, mtu yoyote wa Majohe anajitambulisha Kama wa Gomzi, kwani Mahitaji yote ya msingi wanayatoa gomz.
Screenshot_20230919-104305_Drive.jpg
 
GOMSI ina watu wengiii!!! ukichukulia wanaotumia hii nyerere road kutoka posta mpka chanika ina michepuo ambayo ina wakazi wengi.

kuna njia panda segerea watu wa kinyerez, kuna banana watu wa kitunda, kuna mazizinii, majohe , pugu , kisarawe , chanika. watu mbagala mbande wegine hupitia nyerere road., watu wa mbezi mwisho wengne nyerere road katika main road ambazo rahisi kupitika dar es salaam ni nyerere road

ila watu wa gongo la mboto kidogo wanaustaarab flaniii, ila mbagala hapana kwa kweli.
 
Hajielewi huyo nimemuuliza anaishi wapi ambako hakuna maskini anaruka ruka ....watu wengi wanaijua mbagara kwa kuhadisiwa na clip za mtandaoni watu wakigombea magari so wanapaona sehemu duni sana....wakati kuna madoni kibao tu.
Huyo mjinga nishamblock
Aliniletea shobo nikamblock
Ana hasira anasapot ujinga
Mwenyewe anaishi charambe,kula yake ni my.ombe Nile🤣🤣
 
Wakuu mambo vipi?

Nawasogezea mada hapo ni hivi kati ya Gongo la mboto (Goms) na Mbagala(Mbajara in mateja voice) je ni sehemu gani ina watu(nyomi) wengi kuliko mwenzie ukija na hoja yako weka na sababu.

Binafsi na naanza na Mosi kusema Gongo la mboto ina watu wengi kuliko Mbagala kwa sababu Gongo la mboto kuna treni la mwakyembe ambalo lililetwa naamin linabeba sio chini ya watu buku au zaidi kwa tripu moja na kwa siku linapiga tripu 3 asubuhi na tripu 3 jioni ila pamoja na hivyo bado daladala za kkoo na posta zinazoenda Gongo la mboto zanapiga kazi kama kawaida wakati mbagara majuzi Mwendokasi wamefanya majaribio madaladala wameeanza kulia kulia abiria hakuna.

Mbili Mbagala wengi sio wakazi wa pale wengi wanatoka mikoa ya kusini kuja kufanya biashara na kutawanyika makwao wakati Gomsi ni makazi ya watu na Gari za Mbagala kwenda gomsi jioni hazikamatiki.

Yote kwa yote kwenye madaladala kuna vituko na vimbwangwa sana.

Nawasilisha.
Mkuu Mbagala ni noma na nusu!kuanzia pale misheni, Mbagala kuu kule kwa mabosi, mgeni nani, kizuiani,kiburugwa,charambe, zakiem na baba lao rangi 3 pale ni kariakoo ndogo kunanyomi sio poa kabisa.
 
mwambie huyo popote ulipo dsm hii gari ya gongo la mboto kuipata ni vita.

watu wanaonunua magari ya abiria daladal wanajua route ipi ina demand kubwa sana.ndio sababu uwekezaji wa gari za gharama zaidi uko gomz,sababu uhakika wa kurudisha pesa upo.

tata ni nyingi sana gomzi.
Umesema ukweli kabisa, magari mengi ya Mbagala yamechoka balaa.

Gongo La Mboto inabeba Abiria wengi sana kuanzia;

Banana,

Kitunda,

Segerea,

Pugu.

Kivule,

Majohe,

Ukonga,

Mongo La Ndege,

Mombasa,

Madafu,

Ulongoni,

Kwa Diwani,

Mkoremba,

Bomba mbili.

Chanika,

Zingiziwa.

Mvuti.

Homboza-Kisarawe.

Si daladala, treni, usafiri binafsi ni wa kugombania tu.

Mbagala pana Watu wa mishen town kama Machinga sababu ya uwepo wa biashara lakini wengi wao hutokea mbali mbali Dar..

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom