Kati ya Mbagala na Gongo la Mboto wapi kuna watu wengi?

Gongo la Mboto kwa Mbagala ni sawa na Chamazi hadi Mbande.

Mbagala ni Jimbo wakati Gongo la Mboto ni Kata.

Baada ya kumegwa kutoka Kigamboni na kuanzishwa Jimbo la Mbagala, Jimbo la Mbagala lilikuwa kwenye plan ya kumegwa kuanzisha Jimbo lingine.

Sasa hivi Mbagala huenda ikawa inafukuzia kwenda kuwa Wilaya.

Miaka mitano iliyopita Mbagala ilikuwa na wakaazi milioni moja na ushee.
Pia fahamu kuwa jimbo ni eneo la uchaguzi siyo utawala. Hivyo kata inaweza kuwa na jimbo zaidi ya moja. Kata ni sehemu ya utawala baada ya shaia/kitongoji, mtaa/kijiji. Hivyo jimbo na kata ni vitu viwili tofauti.
 
Pia fahamu kuwa jimbo ni eneo la uchaguzi siyo utawala. Hivyo kata inaweza kuwa na jimbo zaidi ya moja. Kata ni sehemu ya utawala baada ya shaia/kitongoji, mtaa/kijiji. Hivyo jimbo na kata ni vitu viwili tofauti.
Kwa hiyo kata siyo eneo la uchaguzi?
Nitajie kata yenye wabunge zaidi ya mmoja au majimbo zaidi ya moja, halafu nitajie jimbo lenye kata zaidi zaidi moja.
 
Endeleeni kujidanganya kama bakhresa unaandika baresa huwezi kuielelewa mbagara

Ushawahi kufika chamazi ???

Usiwe na akili za kubebwa bebwa na maneno ya watu
Mkuu hayo makosa ya kiuandishi ni Yako au Simu inazingua?
 
Kwanza unaizungumzia Mbagala ipi?! Mbagala ya kwenye vitabu vya Serikali au Mbagala ya Asili ambayo kutokana na ukubwa wake ikalazimika kuvunjwa vunjwa?! Mbagala ya asili inahusisha Mbagala yenyewe, Kiburugwa, Charambe, Kilungule, na Kibonde Maji. Hapo population ni zaidi ya 200K. Ukisema uiingize na Chamazi hesabu unanusa 500K! Hiyo, ndo MBAGALA.

Kuna mtu kaitaja Tandika na Buza. Hizo hazihusiani kabisa na Mbagala, labda angeitaka Maji Matitu, kwa sababu na yenyewe ni Mbagala!

Kwa upande mwingine, unakosea sana kutumia kigezo cha watu kujazana kwenye daladala. Hebu kwanza tafakari: Je, unaamini Gongo la Mboto ina Machinga wengi kuliko Mbagala?! Je, unaamini Gongo la Mboto kuna sehemu yenye pilikapilka nyingi za kibiashara kama ilivyo pale Rangi Tatu?! Je, ni maeneo mangapi Gongo la Mboto yapo busy sawa na pale Zakhem?!

Maeneo yote ya Mbagala niliyokutajia yana Machinga wengi sana. Na kutokana na kukua kwa Mbagala, Machinga wengi hawana sababu ya kupanda magari kwenda mjini kufanya biashara kwa sababu biashara zao zinaishia kule kule Mbagala! Ukiacha Rangi3 as a business center, mbele kidogo unaikuta Zakheim, napo kuna wafanyabiashara kibao ambao hawalazimiki kupanda gali kufika hapo. Ukitoa wa Rangi3 na Zakhem kuna kundi lingine kubwa sana linalofanyia biashara zao Tandika. Nadhani unafahamu ukubwa wa Tandika as business center. Hawa wa Tandika nao hata wakipanda daladala, hawapandi BRT wala zinazoenda mjini. Ukitoa kundi la Wachuuzi wanaoenda Tandika, kundi lingine kubwa linaenda Buguruni, Machinga Complex, na Mchikichini. Hawa nao wanapanda daladala lakini sio ziendazo mjini wala BRT.

Ukiondoa kundi hilo, unakutana na kundi lingine kubwa sana sana. Hawa hawapandi daladala ya aina yoyote kwa sababu biashara zao ni za kutembeza. Naandika sentensi hii takribani saa moja kasoro jioni. Ukifika pande za kuanzia Mtongani kuelekea Mbagala mida kama hii, utakutana na kundi kubwa sana la watu wanaotembea kuelekea Mbagala na wengi miongoni mwao ni Wachuuzi ambao ukitaka kupima uwingi wao kwa kuangalia wanapopanda daladala lazima uibuke na wrong data! Wachuuzi pekee watakaopanda sana BRT na Daladala za K/koo ni wale wanaofanyia biashara zao K/koo na wenyewe ni wengi sana!!
Mbagala ni bus stop center. Inaonekana baba lao sabab watu wote wanapenda kawe,makumbusho, mbezi au mawasiliano na Tabata kutoka toangoma,kisemvule na mbande wanakutania hapo.

Hii ndo inaifanya mbagala kuwa bigger than DSM, lakin pia centercity hii hata tegeta inayo. All in all hakuna eneo lenye accumulation kubwa ya watu dsm kama mbagala. Lakin pia ni wrong assumption kuona mbagala ni totally slums area.
 
mbagala ni habari ingine bro... ndio maana wanataka wilaya yao...

Kwa idadi ya watu mbagala iache tu kama ilivyo.

we ukipata muda kapite pite ujionee shazi.
 
Back
Top Bottom