Kati ya Mbagala na Gongo la Mboto wapi kuna watu wengi?

Mnyunguli

JF-Expert Member
Dec 21, 2020
1,570
3,907
Wakuu mambo vipi?

Nawasogezea mada hapo ni hivi kati ya Gongo la mboto (Goms) na Mbagala(Mbajara in mateja voice) je ni sehemu gani ina watu(nyomi) wengi kuliko mwenzie ukija na hoja yako weka na sababu.

Binafsi na naanza na Mosi kusema Gongo la mboto ina watu wengi kuliko Mbagala kwa sababu Gongo la mboto kuna treni la mwakyembe ambalo lililetwa naamin linabeba sio chini ya watu buku au zaidi kwa tripu moja na kwa siku linapiga tripu 3 asubuhi na tripu 3 jioni ila pamoja na hivyo bado daladala za kkoo na posta zinazoenda Gongo la mboto zanapiga kazi kama kawaida wakati mbagara majuzi Mwendokasi wamefanya majaribio madaladala wameeanza kulia kulia abiria hakuna.

Mbili Mbagala wengi sio wakazi wa pale wengi wanatoka mikoa ya kusini kuja kufanya biashara na kutawanyika makwao wakati Gomsi ni makazi ya watu na Gari za Mbagala kwenda gomsi jioni hazikamatiki.

Yote kwa yote kwenye madaladala kuna vituko na vimbwangwa sana.

Nawasilisha.
 
Gongo la Mboto kwa Mbagala ni sawa na Chamazi hadi Mbande.

Mbagala ni Jimbo wakati Gongo la Mboto ni Kata.

Baada ya kumegwa kutoka Kigamboni na kuanzishwa Jimbo la Mbagala, Jimbo la Mbagala lilikuwa kwenye plan ya kumegwa kuanzisha Jimbo lingine.

Sasa hivi Mbagala huenda ikawa inafukuzia kwenda kuwa Wilaya.

Miaka mitano iliyopita Mbagala ilikuwa na wakaazi milioni moja na ushee.
 
wengi wanaopanda hiyo treni (ikiwemo mimi) wanakaa homboza, chanika, pugu, kisarawe,
yes na mishe anafanyia Mjini
Watu wanaichukulia poa gomsi kwa kulinganisha na mbagara ila mbagar hampati hata kidogo kwa nyomi gongo la mboto basi tu sijui mbagar kamzdi vipi umaaarifu gongo la mboto....

Au yale mambomu ya mbagara ya 2008 lakini hata gomsi yalilipuka pia 2012.
 
Hamna zimejaa kaya masikini
Tajiri hawezi ishi mbagala
Labda awekeze kama kina moo na baresa manake maskin ndo wamejaa huko,wa bidhaa za bei rahisi,za jero na buku buku zinazotoka daily
Endeleeni kujidanganya kama bakhresa unaandika baresa huwezi kuielelewa mbagara

Ushawahi kufika chamazi ???

Usiwe na akili za kubebwa bebwa na maneno ya watu
 
Mbagara ukiichukulia yenyewe kama yenyewe haina watu wengi ila chukulia kipande cha TANDIKA ule ukanda wote Mpaka BUZA alafu urudi sasa huko chamazi mpaka Mbande. Ndio utasema kuna watu nyomi.

Ila kwa Gomz anzia Banana , na kule Kwa WAKURYA uje Hapo mjini kati MOMBASA upandishe mpk Ulongoni B uje PUGU plus Chanika.. GOMZ ina watu.
 
Mbagara ukiichukulia yenyewe kama yenyewe haina watu wengi ila chukulia kipande cha TANDIKA ule ukanda wote Mpaka BUZA alafu urudi sasa huko chamazi mpaka Mbande. Ndio utasema kuna watu nyomi.

Ila kwa Gomz anzia Banana , na kule Kwa WAKURYA uje Hapo mjini kati MOMBASA upandishe mpk Ulongoni B uje PUGU plus Chanika.. GOMZ ina watu.
Kwnza huko tandika na buza umewapendelea sana maana hazipo mbagara hizo....

Gomsi ina nyomi sana sema kulijua hili inabidi utulie sana na ufike maeneo yote.
 
Back
Top Bottom