Kati ya mama yako mzazi na Mungu unampenda nani?

Si vyema kufananisha chochote kile na Mungu sawa ndugu

Ndio maana nikakuambia ukiendelea kuwaza sana hayo mambo utakufuru

Mungu yu juu ya yote na yeye anajua ni namna gan ulimpenda mama yako na hiyo inatosha maana maandiko yalisema mpenda bwana Mungu wako kwa moyo wako wote kwa nguvu zako zote na kwaa akili zako zote na pia mpende jiran yako kama unavyo jipenda zaid nadhna haya maandish yanajieleza kikubwa Muombee mama kila siku ukiweza kama ishara ya upendo wako kwake. R I P mama
Wewe huwezi elewa kama mama unaye furahi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mm wazazi wangu wote nawapenda kwasababu katka malezi yang toka mdog mpaka sasa sijaona mama au baba akinitenga,
 
[
Binafsi ninampenda sana mama yangu mzazi japo ameshafariki few weeks ago .Ninampenda kwa sababu alikuwa ananipenda sana zaidi ya sana ,siwezi kufananisha upendo wa mama yangu mzazi na kitu chochote kile.
Una uhakika gani kuwa huyo ni mama yako mzazi? Kuna wengine hulea watoto waliotupwa wakawachukua wakawalea Kama wao.Kwa unavyosema unaupenda mama kuliko Mungu Nina wasi wasi
 
Dini ni nini? Ukijibu hilo, then tunaendelea
Dini ni utaratibu wa maisha anaoufuata katika kuendesha maisha yake. Dini ziko nyingi sana. Lakini utaratibu wa maisha anaouridhia Muumba ni mmoja tu,na hii ndo sababu akatuma wajumbe maalum duniani kuja kuufundisha,katika hili wanapatikana wenye kuuamini na kufuata,wenye kuchukua mafunzo nusunusu na wapingao asilimia zote. Kwa ufupi mwanaadamu amepewa khiyari ya kuchagua.****. ".....Tayari ameshahukumu Mola wako ya kwamba asiabudiwe yeyote isipokuwa yeye ( Muumba) na wazazi 2watendewe wema.......
 
Utaratibu upi mmoja tu wa maisha anaouridhia Muumba?
Dini ni utaratibu wa maisha anaoufuata katika kuendesha maisha yake. Dini ziko nyingi sana. Lakini utaratibu wa maisha anaouridhia Muumba ni mmoja tu,na hii ndo sababu akatuma wajumbe maalum duniani kuja kuufundisha,katika hili wanapatikana wenye kuuamini na kufuata,wenye kuchukua mafunzo nusunusu na wapingao asilimia zote. Kwa ufupi mwanaadamu amepewa khiyari ya kuchagua.****. ".....Tayari ameshahukumu Mola wako ya kwamba asiabudiwe yeyote isipokuwa yeye ( Muumba) na wazazi 2watendewe wema.......
 
Binafsi ninampenda sana mama yangu mzazi japo ameshafariki few weeks ago .Ninampenda kwa sababu alikuwa ananipenda sana zaidi ya sana ,siwezi kufananisha upendo wa mama yangu mzazi na kitu chochote kile.

Nipo gizani au ndotoni mpaka leo.

Pole kwa kufiwa na Mama.

Kichwa cha habari hakiendani na maudhui ya post yako.

Nikijibu swali la kichwa cha habari, nasema hivi; Mimi ninampenda Mungu kuliko kitu chochote, na inatakiwa iwe hivyo kwani Mungu ndiye kaumba kila kitu na ni yeye anayeshikilia uhai wetu na ndiye anayetupatia riziki nk, kwa maneno mengine haiwezekani kumlinganisha Mungu na kitu chichote kwani yeye utukufu wake ni mkubwa mno kuweza kufananishwa na vitu alivyoumba, bali hiyo siyo heshima na ni ushirikina kumlinganisha Mungu na chochote.

Kumbuka hata huyu Mama yako naye aliumbwa na Mungu.

Ni kweli Lazima mama au wazazi wapendwe lakini upendo wao huwezi kuulinganisha na upendo kwa Mungu ambaye pia ni lazima aabudiwe, je wewe unaweza kumuabudu mama yako???!!.
 
We jemaa huamini mungu, kwa sababu anaye muamini mungu anajua ni mungu ndiye aliye umba kila kitu.

Hivyo hawezi kumlinganisha na chochote/yeyote katika viumbe vyake.

Hivyo kusema hivyo sio kuonyesha kumthamini mama yako, bali ni kumdharau mungu.

Tafuta njia nyingine ya kuonyesha hisia zako lakini sio hii.
 
Binafsi ninampenda sana mama yangu mzazi japo ameshafariki few weeks ago .Ninampenda kwa sababu alikuwa ananipenda sana zaidi ya sana ,siwezi kufananisha upendo wa mama yangu mzazi na kitu chochote kile.

Nipo gizani au ndotoni mpaka leo.
Mungu ni nafasi ya kwanza. Mungu ndiye aliyekupa mama yako.

Mungu yupo milele. Upendo wa Mungu kwako ni wa kudumu.

Mama ameshaenda Mbinguni , umebaki na Mungu sasa, Mungu pekee yake ndiye atakaweza kuziba pengo la mzazi

Pole.

Rest in Paradise Mama wa Rafiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utapendaje vitu ambavyo ni vya kusadikia? Huna uhakika usiokuwa na mashaka kama vipo
Sasa kama huamini usivitukane, sasa unatukanaje vitu ambavyo havipo kama unaakili.

Na kwa upande mwingine kama wewe huamini, basi wenzio waamini.
 
Pole kwa kufiwa na Mama.

Kichwa cha habari hakiendani na maudhui ya post yako.

Nikijibu swali la kichwa cha habari, nasema hivi; Mimi ninampenda Mungu kuliko kitu chochote, na inatakiwa iwe hivyo kwani Mungu ndiye kaumba kila kitu na ni yeye anayeshikilia uhai wetu na ndiye anayetupatia riziki nk, kwa maneno mengine haiwezekani kumlinganisha Mungu na kitu chichote kwani yeye utukufu wake ni mkubwa mno kuweza kufananishwa na vitu alivyoumba, bali hiyo siyo heshima na ni ushirikina kumlinganisha Mungu na chochote.

Kumbuka hata huyu Mama yako naye aliumbwa na Mungu.

Ni kweli Lazima mama au wazazi wapendwe lakini upendo wao huwezi kuulinganisha na upendo kwa Mungu ambaye pia ni lazima aabudiwe, je wewe unaweza kumuabudu mama yako???!!.
Huyu jamaa itakuwa haamini mungu, sasa kama anampenda sana mama yake kuliko mungu, na mama yake kafa inamaana hamthamini tena mungu, sasa hii akili au matope.
 
Binafsi ninampenda sana mama yangu mzazi japo ameshafariki few weeks ago .Ninampenda kwa sababu alikuwa ananipenda sana zaidi ya sana ,siwezi kufananisha upendo wa mama yangu mzazi na kitu chochote kile.

Nipo gizani au ndotoni mpaka leo.
Nadhani una psychological problems kufuatia kifo cha mpendwa wako wiki chache zilizopita. Kwanini ufanye comparison ya mapenzi yako kwa Mungu Vs mama yako?
Mbona hapa baba yako hatajwi?
Pia nina wasi wasi na umri wako wa kuzaliwa maana inaelekea bado akili yako haijakomaa vilivyo kuweza ku handle stress.
Pole though!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom