Kati ya mama yako mzazi na Mungu unampenda nani?

Naja naja

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
747
1,452
Binafsi ninampenda sana mama yangu mzazi japo ameshafariki few weeks ago. Ninampenda kwa sababu alikuwa ananipenda sana zaidi ya sana, siwezi kufananisha upendo wa mama yangu mzazi na kitu chochote kile.

Nipo gizani au ndotoni mpaka leo.
 
Naja naja, pole sana kwa kuondokewa na Mama mpenzi.

Siku za mwisho watu watakuwa ni wenye kupenda fedha na upendo wa wengi utapoa
Sio kwangu mimi, pesa kwangu si kitu bali uwepo wa mama yangu.
Kinachoniuma mama yangu kuondoka bila kuonja mafanikio yangu.
 
Binafsi ninampenda sana mama yangu mzazi japo ameshafariki few weeks ago .Ninampenda kwa sababu alikuwa ananipenda sana zaidi ya sana ,siwezi kufananisha upendo wa mama yangu mzazi na kitu chochote kile.

Nipo gizani au ndotoni mpaka leo.
Kwetu iringa huwa tunasema luhara lubaya;Mungu ni juu sana hafananishwi na chochote katika dunia yetu hii,maana hata huo upendo ni yeye pekee hutoa kwa wanadamu.
 
Tena, kwa mara ya pili ngoja nikupe Pole.

Pole ya kwanza kwenye lile bandiko la TANZIA.

Pole ya pili kwa mara nyingine tena nakupa hapa.

Pole sana Kiongozi
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom