Kati ya mama yako mzazi na Mungu unampenda nani?

Tofauti ya upendo wa mzazi na Mungu ni hii, mzazi hata umkosee vipi hawezi kukuchoma moto atakusamehe mara zote tena hata bila kuomba msamaha. Mzazi hahitaji umsujudie wala kumuabudu anachohitaji ni heshima na kumthamini tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengine walitupwa na kutelekezwa na mama zao hivyo hawana sababu ya kupendezwa nao

Na Mungu alishuhudia wakiliwa na mbwa koko, mungu muhuni asiyejali
 
Binafsi ninampenda sana mama yangu mzazi japo ameshafariki few weeks ago .Ninampenda kwa sababu alikuwa ananipenda sana zaidi ya sana ,siwezi kufananisha upendo wa mama yangu mzazi na kitu chochote kile.

Nipo gizani au ndotoni mpaka leo.
Maswali ya Moko haya unayaleta huku...
 
Binafsi ninampenda sana mama yangu mzazi japo ameshafariki few weeks ago .Ninampenda kwa sababu alikuwa ananipenda sana zaidi ya sana ,siwezi kufananisha upendo wa mama yangu mzazi na kitu chochote kile.

Nipo gizani au ndotoni mpaka leo.
Mama ni Mungu,na Mungu ni Mama nadhani umeelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi ninampenda sana mama yangu mzazi japo ameshafariki few weeks ago .Ninampenda kwa sababu alikuwa ananipenda sana zaidi ya sana ,siwezi kufananisha upendo wa mama yangu mzazi na kitu chochote kile.

Nipo gizani au ndotoni mpaka leo.
Sisi kwenye Uislam hilo sio swali hata kidogo. Ni mambo ya ajabu kabisa. Kuran inatuelekeza kitu cha kwanza ni Mwenyezi Mungu na kisha uwafanyie ihsan wazazi wako wawili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani una psychological problems kufuatia kifo cha mpendwa wako wiki chache zilizopita. Kwanini ufanye comparison ya mapenzi yako kwa Mungu Vs mama yako?
Mbona hapa baba yako hatajwi?
Pia nina wasi wasi na umri wako wa kuzaliwa maana inaelekea bado akili yako haijakomaa vilivyo kuweza ku handle stress.
Pole though!

Sent using Jamii Forums mobile app
Umemnenea vema mkuu, we both love our moms lkn pia ni lazima tukumbuke kwamba wao pia ni binadamu na kila chenye pumzi hakina budi kumrejea alietoa pumzi hiyo siku ikifika, hivyo basi maisha lazima yaendelee regardless kile muondokewa anakipitia. Kijana akaze to moyo maana the world has never been a fair arena! RIP MAMA.
 
Tofauti ya upendo wa mzazi na Mungu ni hii, mzazi hata umkosee vipi hawezi kukuchoma moto atakusamehe mara zote tena hata bila kuomba msamaha. Mzazi hahitaji umsujudie wala kumuabudu anachohitaji ni heshima na kumthamini tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo hapo sasa, huyo Mungu wanasema anaupendo lakini ukimkosea anakuchoma moto.
 
Back
Top Bottom