LA7
JF-Expert Member
- Aug 26, 2019
- 457
- 1,721
Binafsi natamani siku moja mama yangu akae kwa amani lakini ndo hivo nawaza bado sina pa kumlaza pia yule ni mumewe na hatujui walikutana vipi.
Nawapenda sana wazazi wangu wote wawili ila kinachoniumiza haupiti mwezi bila baba kumkosesha mama amani.
Kwa vitu ambavo baba ndo huanzisha ugomvi, mm nipo mbali na nyumbani ila kuna ugomvi umetokea huko.
Mama yangu anauzaga vitumbua sasa alikuwa amesafiri kama siku tatu hivi baada ya kurudi akakuta baba ameuza yale mahindi kwenye gunia moja ametoa debe mbili mahindi ambayo ni yametokana na vitumbua.
Sasa alipoulizwa akawa mkali eti amenunua mbolea, ni kweli amenunua mbolea ila hiyo haikuwa shida sana, shida inakuwa hapa hiyo mbolea aliyonunua huwa anapeleka kwa wanawake wengine, yaani baba ana ndoa za wake 3
Na hakunaga usawa hawezi toa huko kwa wake wadogo alete kwa mama yangu zaidi ni kutoa kwa mama na kupeleka kwa wake wale wadogo.
Kuna kipindi sisi tunaweza lala njaa ila kule kwingine wakala lakini kule kukiwa hakuna unga anakuja ndani anachota na kupeleka kwa wake wadogo na mama akiongea tu anaanza kumpiga japo ss hivi amebakia kwenye mdomo tu, ila mama yangu ndo namuonea huruma
Hanaga roho mbaya yakipikwa mkande jungu kubwa mchana mpaka jioni huyakuti ila kwa wake wengine mpaka kesho yapo ikibidi na kichacha kabisa, nafikiri mmenielewa,
Ila shida yangu namsaidiaje huyu mama yangu