JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
"TUNAMPONGEZA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KWA MAONO YAKE " Bi. Kate Kamba

Kamati ya siasa mkoa wa Dar es Salaam leo Januari 15,2022 imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Temeke kwa kukagua miradi mbalimbali iliyotekelezwa kupitia fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19.

Akiongoza ziara hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Bi. Kate Kamba alisema viongozi na wananchi wa Tanzania wanajivunia Rais Samia Suluhu Hassan kwa mambo makubwa aliyoyatenda kwa kipindi kifupi tangu aingie madarakani huku akiwapongeza viongozi wa Wilaya na halmashauri ya manispaa ya Temeke kwa kusimamia miradi iliyokamilika kwa wakati.

"Namshukuru sana Mama Samia Suluhu kwa kuona na kukamilisha haya kwa muda mfupi tu, ametusaidia kutoa elimu nzuri kwa watoto wetu".Alisema Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwegelo alimshukuru Mwenyekiti huyo kwa kuweza kufika na kukagua miradi ambayo wananchi wa Temeke watanufaika nayo.

"Temeke tumekua wanufaika wa mradi huu ambao utapunguza msongamano wa wanafunzi darasani, tunaomba Mama Kate utume salamu zetu kwa Mheshimiwa Rais tunamshukuru sana".Aliongeza Mhe.Jokate.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ndugu Elihuruma Mabelya alisema kuwa sasa kazi kubwa iliyo mbele yao kama Manispaa ni kuhakikisha inajenga matundu ya vyoo kuendana na idadi ya madarasa na ujenzi wa maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi.

"Kama Manispaa tulishakuwa na mpango wa kujenga madarasa 147 kabla ya haya madarasa ya Mama, tutatumia fedha zile kujenga na kuboresha vyoo, ofisi za walimu,maabara za sayansi na maabara za kompyuta, niwaahidi wananchi wa temeke kuwa hali ya elimu inaenda kubadilika".Alisisitiza Mabelya

Mkuu wa shule ya Sekondari Toangoma Mwalimu Christopher Lucas Mtabutu alionesha kufurahishwa kwake na ujenzi huo wa madarasa ambayo yatakuwa chachu katika ufaulu wa wanafunzi.

Ziara hii ni ukaguzi wa mwisho kuelekea kuanza kwa muhula wa masomo wa mwaka 2022 siku ya Jumatatu Januari 17 ambapo wanafunzi wa kidato cha kwanza wanatarajia kuanza rasmi masomo yao.

IMG-20220115-WA0164.jpg

IMG-20220115-WA0165.jpg

IMG-20220115-WA0163.jpg

IMG-20220115-WA0168.jpg

IMG-20220115-WA0166.jpg

IMG-20220115-WA0167.jpg
 
Vision kubwa zaidi inahitajika ili nchi ifikie kwenye maisha ya dunia ya sasa.
 
"TUNAMPONGEZA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KWA MAONO YAKE " Bi. Kate Kamba

Kamati ya siasa mkoa wa Dar es Salaam leo Januari 15,2022 imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Temeke kwa kukagua miradi mbalimbali iliyotekelezwa kupitia fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19.

Akiongoza ziara hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Bi. Kate Kamba alisema viongozi na wananchi wa Tanzania wanajivunia Rais Samia Suluhu Hassan kwa mambo makubwa aliyoyatenda kwa kipindi kifupi tangu aingie madarakani huku akiwapongeza viongozi wa Wilaya na halmashauri ya manispaa ya Temeke kwa kusimamia miradi iliyokamilika kwa wakati.

"Namshukuru sana Mama Samia Suluhu kwa kuona na kukamilisha haya kwa muda mfupi tu, ametusaidia kutoa elimu nzuri kwa watoto wetu".Alisema Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwegelo alimshukuru Mwenyekiti huyo kwa kuweza kufika na kukagua miradi ambayo wananchi wa Temeke watanufaika nayo.

"Temeke tumekua wanufaika wa mradi huu ambao utapunguza msongamano wa wanafunzi darasani, tunaomba Mama Kate utume salamu zetu kwa Mheshimiwa Rais tunamshukuru sana".Aliongeza Mhe.Jokate.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ndugu Elihuruma Mabelya alisema kuwa sasa kazi kubwa iliyo mbele yao kama Manispaa ni kuhakikisha inajenga matundu ya vyoo kuendana na idadi ya madarasa na ujenzi wa maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi.

"Kama Manispaa tulishakuwa na mpango wa kujenga madarasa 147 kabla ya haya madarasa ya Mama, tutatumia fedha zile kujenga na kuboresha vyoo, ofisi za walimu,maabara za sayansi na maabara za kompyuta, niwaahidi wananchi wa temeke kuwa hali ya elimu inaenda kubadilika".Alisisitiza Mabelya

Mkuu wa shule ya Sekondari Toangoma Mwalimu Christopher Lucas Mtabutu alionesha kufurahishwa kwake na ujenzi huo wa madarasa ambayo yatakuwa chachu katika ufaulu wa wanafunzi.

Ziara hii ni ukaguzi wa mwisho kuelekea kuanza kwa muhula wa masomo wa mwaka 2022 siku ya Jumatatu Januari 17 ambapo wanafunzi wa kidato cha kwanza wanatarajia kuanza rasmi masomo yao.

View attachment 2082640

View attachment 2082641

View attachment 2082642

View attachment 2082643

View attachment 2082645

View attachment 2082646
Kazi iendelee
 
Maono? Hebu acheni upuuzi, mama huyu anayo maono😂!?
Mwenye maono yake ameshaitwa na Muumba bana hata tumebaki kusutana TU😂😂😂!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom