Katavi: Viongozi wa Elimu watakiwa kupandisha kiwango cha uandikishaji wa Wanafunzi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Viongozi na Wadau wa Elimu Mkoa wa Katavi wametakiwa kuhakikisha kila mtoto mwenye sifa za kuanza darasa la kwanza anaandikishwa haraka ili aweze kuanza masomo Januari 2024.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf wakati akimwakilishi Mkuu wa Mkoa wa Katavi wakati wa kikao cha Viongozi wa Elimu wa Mkoa wa Katavi ambacho kilikuwa na lengo la kupanga mikakati ya kuinua na kuboresha taaluma kwa wanafunzi wa Elimu ya Msingi na Sekondari.

Afisa Elimu Mkoa wa Katavi, Upendo Rweyemamu amesema Mkoa wa Katavi utahakikisha mikakati yote ikiwemo ya kupandisha kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi unaongezeka sanjari na kuongeza kiwango cha Wanafunzi kufaulu vizuri hasa daraja la pili na la kwanza huku katibu tawala mkoani humo Hassan Rugwa akisisitiza serikali kuendelea kuwaheshimu walimu kwa kutatua changamoto zao.


Charles Mwanakatwe na Diana Magazwa ni baadhi ya walimu Mkoani Katavi wamesema kikao maelekezo yote yaliyotolewa yamewapa msukumo zaidi katika uwajibikaji huku eakiomba wazazi kutoa ushirikiano kwa Walimu.
 
Back
Top Bottom