Katavi: Kaya 17 zakabidhiwa msaada baada ya kuathirika na mafuriko

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini zimeendelea kuleta madhara makubwa ndani ya jamii ambapo mnano tarehe 02 mwezi huu kaya zaidi ya 17 katika Mtaa wa Msufini Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ziliathirika na mafuriko ambapo baadhi ya nyumba zilianguka na wengine kupoteza vyombo vyao.

Kamati ya maafa na majanga katika manispaa ya Mpanda ikiongozwa na mwakilishi wa mkuu wa wilays Geofrey Mwashitete ambaye ni katibu tawala wa manispaa hiyo imepeleka moyo wa mawingu kwa kaya hizo zilizoathirika ikiwa ni sehemu ya kutoa faraja na kuwashika mkono wahanga hao.

Kaimu Mkurugenzi Tulinalo Nswila amewataka wananchi wanaoishi maeneo hatarishi kuchukua tahafhari hasa katika msimu huu wa masika huku diwani wa kata ya uwanja wa ndege Kamande Mbogo akiiomba serikali kutengeneza miundombinu mizuri katika mtaa huo ili kuondokana na adhaa ambayo kila mwaka inajitokeza.

Daud Paul na Amina Hamis mbali na kuishukuru Serikali na Wananchi wote lakini wameiomba Serikali kutengeneza miundombinu katika mtaa huo wa Msufini huku Mwenyekiti wa Serikali katika Mtaa wa Msufini Peter Kasanda akiishukuru kamati ya maafa na majanga ya Manispaa ya Mpanda kwa kuwatia faraja ya kuwapatia bidhaa mbalimbali ili kujikimu katika kipindi hiki kigumu.
 
Back
Top Bottom