Vijana wanao ongoza kampeni ya "kataa ndoa" wanamatatizo ya kisaikolojia, wasaidiwe tusiwaache

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,646
9,226
Mwana saikolojia ABRAHAM MASLOW anasema kwamba, kupenda au kupendwa ni hitaji la msingi akimaanisha kuwa na mke, watoto na familia kiujumla ni hitaji la msingi la kila binadamu.

Ikitokea mtu akawa anaenda kinyume na hitaji hilo mfano kampeni ya kataa ndoa, huyo mtu anakua anaenda kinyume na jamii na matakwa ya kibinadamu kiujumla.

Kisaikolojia ni mgonjwa na kuna sababu za msingi za yeye kuwa hivyo mfano kutelekezwa utotoni na mzazi au wazazi wote, kufanyiwa vitendo vya kikatili utotoni na mama wa kambo, kuishi kwenye familia yenye migogoro, kubakwa au kulawitiwa utotoni n.k.

Moja kati ya hizo sababu ndizo zinaperekea mtoto hasa hasa wa kiume kupata hasira na chuki ambazo hujichimbia kwenye ufahamu usiokuwa wa hiari yaani huko ukubwani anajikuta tu anachukia mambo ya familia/mahusiano bila yeye kujua wala kuwa na sababu za msingi.

Akiona matukio ya migogoro ya ndoa huitumia kama kielelezo cha kuhalalisha imani yake kuwa ndoa ni kitu haramu na mara nyingi huishi kwa kutembea na wanawake wengi
 
Hata usitulaumu mkuu, kupata mwanamke wa kuoa ni ngumu kinoma, tokea nilipofikisha miaka 27 nilikua natafuta mwanamke wa kuoa mpaka sasa niko 35 sijaona, nimeamua kwenda kuongeza elimu tu, wanawake ni pasua kichwa, ukisema utafute hawa 20's ni pasua kichwa kinoma vinagongwa balaa, hawa 30's na wao wana ex kama 20 hivi, unaweza kumuoa kwa kumuonea huruma baada ya hapo week tu unageukwa, hata mkiachana tayari anakua na status ya kuolewa na kuachika kitu ambayo haiwipi stress tofauti na kutokuolewa kabisa.
 
Hii Abraham Maslow anatumika hadi kwenye ndoa, nashukuru sana kwa kunifungua akili

Ila kwa nini wasiooa hawajishughulishi na waliooa kama waliooa wanavyojishughulisha na wasiooa. Kuna siri gani hapo mkuu

Maana kwa bongo yetu si rahisi mtu akuhimize au kukushawishi uingie katika pepo unless inamfaidisha
 
Mm sitembei na wanawake wengi wala c malaya ,ilaa uwezi nishawishi nikaoa hata Kwa bunduki na mabomu haswaa Kwa Yale niliyoshuhudiaa mwanamke ambaye n mama yangu mzazii akimnyanyasaa baba yangu mpk kufa kwakeee,aiseee yulee Mzee aliburuzwa aiseee na yulé mama alafu bila hata chembe ya aibu wala hurumaa ,na nilishuhudia live yt bila chengaa alafu unishawishii ndoaaa mkuuu ,

Nasemaa kataaa ndoaa tupo sahihi kbs.
 
Hata usitulaumu mkuu, kupata mwanamke wa kuoa ni ngumu kinoma, tokea nilipofikisha miaka 27 nilikua natafuta mwanamke wa kuoa mpaka sasa niko 35 sijaona, nimeamua kwenda kuongeza elimu tu, wanawake ni pasua kichwa, ukisema utafute hawa 20's ni pasua kichwa kinoma vinagongwa balaa, hawa 30's na wao wana ex kama 20 hivi, unaweza kumuoa kwa kumuonea huruma baada ya hapo week tu unageukwa, hata mkiachana tayari anakua na status ya kuolewa na kuachika kitu ambayo haiwipi stress tofauti na kutokuolewa kabisa.
kuanzia hapo unapoishi kuna mwanaume ameoa ana mke na watoto, nyumba jirani kuna baba mke na watoto nyumba inayofuata hivo hivo mtaa, kata wilaya mkoa nchi nzima asilimia 90 kila nyumba kuna mke mme na watoto jitafakari
 
Mm sitembei na wanawake wengi wala c malaya ,ilaa uwezi nishawishi nikaoa hata Kwa bunduki na mabomu haswaa Kwa Yale niliyoshuhudiaa mwanamke ambaye n mama yangu mzazii akimnyanyasaa baba yangu mpk kufa kwakeee,aiseee yulee Mzee aliburuzwa aiseee na yulé mama alafu bila hata chembe ya aibu wala hurumaa ,na nilishuhudia live yt bila chengaa alafu unishawishii ndoaaa mkuuu ,

Nasemaa kataaa ndoaa tupo sahihi kbs.
mbona unachokieleza ndicho nimekielezea hapo juu! Soma kwa kutulia
 
Mm sitembei na wanawake wengi wala c malaya ,ilaa uwezi nishawishi nikaoa hata Kwa bunduki na mabomu haswaa Kwa Yale niliyoshuhudiaa mwanamke ambaye n mama yangu mzazii akimnyanyasaa baba yangu mpk kufa kwakeee,aiseee yulee Mzee aliburuzwa aiseee na yulé mama alafu bila hata chembe ya aibu wala hurumaa ,na nilishuhudia live yt bila chengaa alafu unishawishii ndoaaa mkuuu ,

Nasemaa kataaa ndoaa tupo sahihi kbs.
kaangalie movie ya kanumba inaitwa moses unatembea mule mule
 
Mwana saikolojia ABRAHAM MASLOW anasema kwamba, kupenda au kupendwa ni hitaji la msingi akimaanisha kuwa na mke, watoto na familia kiujumla ni hitaji la msingi la kila binadamu.

Ikitokea mtu akawa anaenda kinyume na hitaji hilo mfano kampeni ya kataa ndoa, huyo mtu anakua anaenda kinyume na jamii na matakwa ya kibinadamu kiujumla.

Kisaikolojia ni mgonjwa na kuna sababu za msingi za yeye kuwa hivyo mfano kutelekezwa utotoni na mzazi au wazazi wote, kufanyiwa vitendo vya kikatili utotoni na mama wa kambo, kuishi kwenye familia yenye migogoro, kubakwa au kulawitiwa utotoni n.k.

Moja kati ya hizo sababu ndizo zinaperekea mtoto hasa hasa wa kiume kupata hasira na chuki ambazo hujichimbia kwenye ufahamu usiokuwa wa hiari yaani huko ukubwani anajikuta tu anachukia mambo ya familia/mahusiano bila yeye kujua wala kuwa na sababu za msingi.

Akiona matukio ya migogoro ya ndoa huitumia kama kielelezo cha kuhalalisha imani yake kuwa ndoa ni kitu haramu na mara nyingi huishi kwa kutembea na wanawake wengi
Ni sahihi.
Kukataa NDOA ambayo ni mpango kamili wa Mungu kuongeza watu duniani ni kuhalalisha ushoga,uzinzi na usagaji.
Mungu atutetetee.
Wote wanaopingana na mpango wake wakutane na ghadhabu yake na wageuzwe upya.
 
moses sio kataa ndoa yeye alikuwa anawachukia wanawake wote, lakin kataa ndoa wapitiaji tu
moses alikuwa hataki kuoa wala kuishi na mwanamke yeyote ndani kwake ila alikuwa anawatafuna, hapa neno ndoa kuna kuoa ndani yake
 
Mm sitembei na wanawake wengi wala c malaya ,ilaa uwezi nishawishi nikaoa hata Kwa bunduki na mabomu haswaa Kwa Yale niliyoshuhudiaa mwanamke ambaye n mama yangu mzazii akimnyanyasaa baba yangu mpk kufa kwakeee,aiseee yulee Mzee aliburuzwa aiseee na yulé mama alafu bila hata chembe ya aibu wala hurumaa ,na nilishuhudia live yt bila chengaa alafu unishawishii ndoaaa mkuuu ,

Nasemaa kataaa ndoaa tupo sahihi kbs.
pole sana ndugu. Ushuhuda mbaya kabisa.
Unaamini watu wote wanafanana??
 
Back
Top Bottom