JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,177
- 7,472
Amesema Hayati Magufuli hakupenda mzaha katika kazi zake na alikuwa mkali, akikemea maovu, wizi, rushwa, na ubadhirifu wa mali za umma.
Majaliwa ameyasema hayo leo Machi 17, 2026, wakati wa kumbukizi ya miaka mitano ya kifo cha Dkt. Magufuli iliyofanyika Chato, mkoani Geita.
Aidha, Majaliwa amesema Watanzania wataendelea kumkumbuka Hayati Magufuli kwa busara na hekima zake katika kuongoza taifa na kusimamia rasilimali za nchi.
“Tunajiona kabisa tumempoteza, hatunae, nataka niwaambie kwamba yupo kwenye mioyo yetu, tuendelee kumuenzi,” amesema Waziri Mkuu Mstaafu Majaliwa.
Video: VIBES FM