Kassim Majaliwa akwea pipa kuelekea Japan kumzika ABE

Nasema Uongo Ndugu Zangu

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
279
773
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo Jumamosi, Septemba 24, 2022 kwenda Tokyo, Japan ambako atamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mazishi ya ya kitaifa ya Waziri Mkuu mstaafu wa nchi hiyo, Shinzo Abe.

Taratibu za kutoa heshimaza mwisho zinatarajiwa kufanyika Jumanne, Septemba 27, mwaka huu kwenye ukumbi wa Nippon Budokan.

Waziri Mkuu huyo mstaafu aliuawa Julai 8, mwaka huu kwa kupigwa risasi akiwa kwenye mkutano wa kampeni za kisiasa katika jiji la Nara nchini humo.

Abe ambaye anatajwa kuwa Kiongozi aliyeshika wadhifa wa Waziri Mkuu wa Japan kwa muda mrefu katika historia ya Japan, aliingia madarakani kuanzia mwaka 2006 hadi 2007 na akarudi tena mwaka 2012 hadi 2020.

Imeelezwa kwamba akiwa Nchini Japan, Waziri Mkuu Majaliwa atakutana na Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida.
 
Marais wote duniani wana kikoba chao kasoro huyu putin wamemu amber kati

Mawaziri wakuu wote dunian wana kikoba chao

Kila siku wanacheza mchezo wa 50000

Wazee kuna ushirikiano na ushirikina
 
Back
Top Bottom