Kasi ya Magufuli imewapotezea dira ya UKAWA

Kasi ya Magufuli imewapotezea dira ya UKAWA

Umesema vema. Magufuli alishasema ccm kumejaa wanafiki. Alimwambia jk m/kiti wao kwenye mkutano wa hadhara pale Lumumba.
Daaaa mkwere amepatikana mwaka huu,ndio maana wenzake kina museveni wanabadilisha katiba
 
Niwakumbushe Maneno aliyosema Bwana Yesu Kristo yalijaa mafunzo kwa wale wote wanajijua kama Matawi hawaguswi alisema"IKIWA MTI MBICHI UNAFANYIWA HIVI JE MTI MKAVU" Tutafakari wote wenye Dhamana.Hiki ni Zama nyingine na Kitabu kingine Maneno ya Mzee Mwinyi
 
Mkuu sija kuelewa sana lakini katika kidogo nilicho kuelewa nikuhusu mfano wa kiongozi wa upinzan alie wahi kuingia madarakani...kumbuka mimi nime sema viongozi wa ki Afrika sio hapa bongo tu! Bali bara zima mfano Kenya.

Nahata hapa kwetu wabunge wa upinzani wali paswa kuonyesha njia...lakini nao hola!
Nilikuelewa ila nilitaka kukumbusha kuwa kwasababu tunaongelea hapa kwetu, ujue haijatokea upinzani ukachukiua nchi. Upande wa Kenya umeona jinsi wamekuwa wanabadilishana ukianza na Kibaki. Zambia wameonsha njia na uzuri mzee Kaunda yupo hai na anaona jinsi nchi ile inavyosonga mbele kwa kasi. Malawi na Rwanda je umeenda umeona wanavyokimbia wenzetu?
Nchi kubwa unaziona kama Marekani upinzani unaweza fanya maandamano na kukwamisha maamuzi kwenye seneti kitu ambacho hapa kinashindikana sababu ya idadi. Lakini je kashfa zote zilizoibuliwa na kuwafanya mawaziri wajivue nyadhifa zao nani alitingisha kibiriti? Be fair usiwe mtu asiyeona upande ule usiopenda kutazama. Jilazimishe utumie hata kope.
 
Subiri tumalize movie ya watumishi hewa, ndo ulete siasa zako hapa. Nchi kwa sasa imejawa na simanzi kuhusu hili la watumishi hewa. Hatutaki kusikia habari za UKAWA, Bulembo au nani. Na anayefikiria kuwa JPMJ anatekeleza ilani ya chama chake, huyo kachelewa sana. Pia naamini kuwa haya majipu na huu uozo unatumbuliwa kila siku sio UKAWA.

Lakini nimefurahi mwandishi mmoja wa gazeti la kiingereza alitafsiri neno WATUMISHI HEWA kama GHOST WORKERS yaani kawaita mizimu. Wachafu ndani ya chama walikifanya chama chote kionekane hakifai, tunajua kuwa Mheshimiwa yeye anarusha mawe gizani tu ambako tunajua wamekaa wahalifu na sio UKAWA au CCM
 
Tupe mfano tangu tupate uhuru nani alishinda uchaguzi akiwa upinzani akaingia madarakani hapa Bongo? Pili wewe unajua wazi kuwa Siasa tumeambiwa uchaguzi umeisha hivyo hapa kazi tu au unawatakia wenzio kunyea debe bila sababu. Mara tumeona wanamfananisha Alcohol na Hitler kitu ambacho sikubaliani sababu hakuna ambaye ameishaanza kuwekwa Lupango kwa sababu za kisiasa au asili yake kama alivyofanya Hitler kukusanya wayahudi na watu wenye ulemavu. Oho nimesahau isijeikawa MA Ko ndakta alikuwa anaanzia hapo kuzuia ombaomba wasisaidiwe.

ulowataja ni wabunge uwanja wao ni kwenye mjengo labda ututajie wenyeviti wa vitongoji hadi taifa ndo wana ubavu wa kusema siasa.
naomba kutofautina na wewe kuwa
"ulowataja ni wabunge uwanja wao ni kwenye mjengo"
Ni kweli kabisa kwa mujibu wa katiba ibara ya 63 na 64 mbunge anakazi kubwa mbili,
1:Kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri serikali na vyombo vyake vyote katika kutekeleza majukumu yake.
2:Mamlaka ya kubuni na kutunga sheria zitakazolisaidia taifa hili.
kwa sababu yote yanafanyika bungeni. kipindi hiki bunge halipo, wanapaswa kuwa wanainteract na raia wao, wanahamasiha maendeleo na ubunifu majimboni mwao, kwa mfano wa Deo Filknjmb kufuatilia matumizi ya pesa za serikali kama zinnatumika ipasavyo majimboni mwao. Ili wanapokuja BUNGENI wawe na msingi wa wanayoyapigia kelele. Ndio maana mbunge alipokuwa analaumu kuhusu kivuko cha MV DSM alipoulizwa umewahi kupanda/kukagua akasema nimesikia tu kwa wananchi wangu. Hii sehemu ya pili ni muhimu sana kwa ubora wao bungeni.
 
naomba kutofautina na wewe kuwa
"ulowataja ni wabunge uwanja wao ni kwenye mjengo"
Ni kweli kabisa kwa mujibu wa katiba ibara ya 63 na 64 mbunge anakazi kubwa mbili,
1:Kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri serikali na vyombo vyake vyote katika kutekeleza majukumu yake.
2:Mamlaka ya kubuni na kutunga sheria zitakazolisaidia taifa hili.
kwa sababu yote yanafanyika bungeni. kipindi hiki bunge halipo, wanapaswa kuwa wanainteract na raia wao, wanahamasiha maendeleo na ubunifu majimboni mwao, kwa mfano wa Deo Filknjmb kufuatilia matumizi ya pesa za serikali kama zinnatumika ipasavyo majimboni mwao. Ili wanapokuja BUNGENI wawe na msingi wa wanayoyapigia kelele. Ndio maana mbunge alipokuwa analaumu kuhusu kivuko cha MV DSM alipoulizwa umewahi kupanda/kukagua akasema nimesikia tu kwa wananchi wangu. Hii sehemu ya pili ni muhimu sana kwa ubora wao bungeni.
Unakumbuka Lwakatare mwezi NOv au Dec alienda kutoa misaada na kutembelea vituo vya afya, vingi vilikataa misaada eti sababu ni mpinzani? Mbona sisi tulipokea misaada ya Bush alipoingia madarakani Obama akaendeleza yale yale na bado tukapokea? Mtu wa nje ruksa kutoa misaada lakini mpinzani hatupokei? Hivi ndo vinakatisha tamaa upinzani kukosa ushirikiano toka viongozi wa juu serikalini ingawa siyo sehemu zote. Rais mwenyewe ni mfano alivyowatolea uvivu madiwani wa CCM Dar.
 
Unakumbuka Lwakatare mwezi NOv au Dec alienda kutoa misaada na kutembelea vituo vya afya, vingi vilikataa misaada eti sababu ni mpinzani? Mbona sisi tulipokea misaada ya Bush alipoingia madarakani Obama akaendeleza yale yale na bado tukapokea? Mtu wa nje ruksa kutoa misaada lakini mpinzani hatupokei? Hivi ndo vinakatisha tamaa upinzani kukosa ushirikiano toka viongozi wa juu serikalini ingawa siyo sehemu zote. Rais mwenyewe ni mfano alivyowatolea uvivu madiwani wa CCM Dar.
Hayo ndio majukumu makubwa ya mbunge. Kuhakikisha kodi na pato la taifa linatumika kuendeleza na kuwanufaisha wananchi wake na watanzania wote kwa ujumla. Sio yeye kuwagawia pesa au kujenga barabara, au kuanzisha miradi yake binafsi, afanye hiyo kama option tu lakini sio lazima. Suala la kutoa msaada kila mtanzania anahaki ya kumsaidia mtanzania mwenye hali duni kihalali. Hapo ndio unamkuta nasali anatoa ambulance kama msaada lakini sio kazi yake, yeye alitakiwa kuifanya serikali ipeleke ambulance kwa wananchi. Tatizo hata wananchi hatujui kazi za tuliyemtuma
 
KASI YA MAGUFULI IMEWAPOTEZEA DIRA YA UKAWA.

Tangu rais Magufuli aanze kututumikia kama rais amefanya mambo mengi na karibu mambo yote hayo yamekuwa yakipingwa na UKAWA.

Rais alianza kufukuza fukuza na kuteua watendaji wapya wa serikali. Walimbeza kwa kumsema hao watumishi aliwakuta na ndio maana imemwiia rahisi kuwafuta kazi. Mbowe alisema huku akiwaonea huruma watumishi wanao fukuzwa kazi, lakini ni Mbowe huyuhuyu aliyekuwa analalamika kuwa watumishi wa umma wanavurunda na hawachukuliwi hatua, na kama wakichukuliwa hatua basi kubadilishwa kituo cha kazi, sasa wanafukuzwa, analalamika kwanini wanafukuzwa.

Sasa hivi kamfuta kazi mkuu wa mkoa wa Shinyanga baada ya kumteua yeye mwenyewe mwezi uliopita. Huyu kamteua mwenyewe na sababu za kumfuta ziko wazi na jambo zuri alisema mapema kuwa suala la watumishi hewa litawafukuzisha kazi.

Ajabu sasa Julius Sunday Mtatiro anamtetea Mama Malecela kwa kusema kazi yake si ya kiutendaji na ya kwamba alitakiwa kutumia taarifa za kiintelejensia alizopewa rais na timu yake.

Kwa vyovyote vile baada ya kugudulika hao watumishi hewa 45, Mama Malecela alipewa taarifa, na kwa mujibu wa maneno yake mwenyewe rais, Anna Malecela hakuchukua hatua yoyote baada kujua kuna watumishi hewa tafauti na taarifa yake alokuwa nayo.

Kitendo hichi cha mkuu wa mkoa kusubiria hatua za rais badala ya yeye mwenyewe kuwachukulia hatua watu walio mdanganya ndio sababu za kutimuliwa kwake kazi.

Tangu Mbowe ale pesa za Lowassa, na tangu Lowassa ajiunge na CHADEMA, ni kama vile UKAWA yote sasa hivi imeacha lengo lake la kupambana na ufisadi sasa inatetea ufisadi na ubadhilifu.

Walipokuwa wanamsafisha Lowassa kwa ufisadi wake tulidhani wataishia hapo tu kwasababu ndio mgombea wao na ya kwamba hawakuwa namna, lakini kuendelea kwao kutetea ufisadi au kunyamazia ufisadi ndio kunatutisha, zaidi, ni kama vile yule muonja nyama ya mtu, anashindwa kuacha hata kama kwa kuendelea kwake kula nyama hiyo kutamlazimu kula na watoto wake pia.

Hivi karibuni wahusika na dili la STANBINK walipopelekwa mahakamani, vijana wote wa UKAWA hawakushangilia na kusema lolote, sababu wanajua katika hilo dili mzee wa madili kwa namna moja au nyingine naye yumo, sababu swahiba zake wakubwa na watafutaji wake wa fedha za kampeni ndio wahusika wakuu.

Akili yao ni kuwa upinzani ni kupinga, upinzani si kupinga tu, bali upinzani ni kuja na hoja zitakazo tibu matatizo yetu au kuboresha hali zetu. Hoja ya Mtatiro ni ya kupinga kijahili na si ya kututoa hapa na kutupeleka mbele zaidi.

Watanzania tunahitaji kwenda mbele, na kwa kauli rais yeyote atakaye jaribu kutukwamisha atashindwa na kulegea, Mtatiro kaka yangu jua fika umeshindwa na kulegea.

MGENI KARIBU, JUISI YA PILIPILI.

MWENYEJI:
Karibu mzee Chali, ukaribie nyumbani,
Uketi upige wali, upoze chango tumboni,
Kisha tujalie hali, za wenzetu Kinondoni.
Karibu wetu mgeni, juisi ya pilipili.

MGENI:
Loo! msinite Chali, jina langu Abuduni,
Nina njaa kwelikweli, ninawapa shukurani,
Hali zao afadhali, watia gia angani.
Ni mwenyeji si mgeni, asante kwa pilipili.

MWENYEJI:
Somo la uliberali, tulo nao Buguruni?
Sema wamelikubali, bila kinyongo rohoni,
Ama hawajakubali, wamelitupa jaani?
Karibu wetu mgeni, juisi ya pilipili.

MGENI:
Naona wamekubali, watazame visogoni,
Wakiliwa kwa ugali, wachomachoma kooni,
Ni michicha kwelikweli, yenye miba vikonyoni,
Ni mwenyeji si mgeni, asante kwa pilipili.

MWENYEJI:
Ya kwao ulo kubali, yatupie barazani,
Tupate kuyajadili, na kuyapima mzani,
Tuyabebe yalo kweli, tuyatumie kundini,
Karibu wetu mgeni, juisi ya pilipili.

MGENI:
Sina nilo yakubali, hamuwezi kuamini,
Tumewazidi akili, maono na umakini,
Nyumbu wamelala chali, wamevimbiwa majani,
Ni mwenyeji si mgeni, asante kwa pilipili.


MWENYEJI:
Kibopa wetu Munduli, naye ana hali gani?
Bado apiga msuli, wa kuwa bosi nchini?
Lile wazo kabadili, kuchunga ng'ombe porini?
Karibu wetu mgeni, juisi ya pilipili.

MGENI:
Tetesi kila mahali, aenda Ujerumani,
Ila hayana ukweli, yu mzima si utani,
Tatizo ni utapeli, uchungaji siuoni.
Ni mwenyeji si mgeni, asante kwa pilipili.

MWENYEJI:
Hatutaki kadi mbili, ichome ya unyumbuni,
Kichwa na kiwiliwili, vyote virejee ndani,
Mazito yatukabili, hasa kule visiwani.
Karibu wetu mgeni, juisi ya pilipili.

MGENI:
Nimesharudi madhali, nina moja mkononi,
Ninaapa kwa Jalali, nisemayo ya moyoni,
Mengine tutajadili, kwa idhini ya Manani.
Ni mwenyeji si mgeni, asante kwa pilipili.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
0622845394 Morogoro.


Njano5
0622845394
Ukisema UKAWA wamepotea utasema ACT Wasaliti wamefanyaje??
 
Ujinga huu muulize WASIRA atakupa majibu yake!
Wasira sina uwezo wa kukutana naye.
Labda wewe ambaye nna uwezo wa kuongea nawe, niambie ujinga huu majibu yake ni nini?
Ndio yaleyaleeeee, kujibu hoja kwa hoja... Na sio matusi na mipasho...
Nieleweshe ili nielewe. Kama hauna cha kusema kaa kimya kaka....
Badilika mkuu
 
Umeandika gazeti zima kwa mihemuko na imekufanya upoteze hata point uliyokusudia kuwakilisha nakushauri upitie tena andiko lako na kufanyia editing
Hadi kujuwa kuwa nimekosea najuwa utakuwa umeelewa na ujumbe niliotarajia ukufikie ndio huohuo uliokufikia....
Au we ulifikiri nna maana nyingine? Inatosha kaka.... Mengine utaamua wewe na uelewa wako.....
 
Hahaahaha UKAWA? ACT je? Kwa mwenye akili ataelewa kuwa anachokifanya Magufuli kinawaumiza wana CCM na nyie ACT Zaidi kuliko UKAWA, nambie ni UKAWA wangapi wamepoteza ajira au wamekamatwa au at least kutuhumiwa kwa rushwa hadi muda huu?? Au umesahau kuwa Kiongozi wako Mkuu wa ACT anatajwa tajwa kwenye scandal ya NSSF na kwingine???
mtafukuzwa wakati nyie si watumishi wa serikali mbn hujielewi
 
Wasira sina uwezo wa kukutana naye.
Labda wewe ambaye nna uwezo wa kuongea nawe, niambie ujinga huu majibu yake ni nini?
Ndio yaleyaleeeee, kujibu hoja kwa hoja... Na sio matusi na mipasho...
Nieleweshe ili nielewe. Kama hauna cha kusema kaa kimya kaka....
Badilika mkuu
Kama ungetaka kuelewa usingeongea namna ile MTU anaejua....wee endelea kuota ndoto
 
Back
Top Bottom