Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
KASI YA MAGUFULI IMEWAPOTEZEA DIRA YA UKAWA.
Tangu rais Magufuli aanze kututumikia kama rais amefanya mambo mengi na karibu mambo yote hayo yamekuwa yakipingwa na UKAWA.
Rais alianza kufukuza fukuza na kuteua watendaji wapya wa serikali. Walimbeza kwa kumsema hao watumishi aliwakuta na ndio maana imemwiia rahisi kuwafuta kazi. Mbowe alisema huku akiwaonea huruma watumishi wanao fukuzwa kazi, lakini ni Mbowe huyuhuyu aliyekuwa analalamika kuwa watumishi wa umma wanavurunda na hawachukuliwi hatua, na kama wakichukuliwa hatua basi kubadilishwa kituo cha kazi, sasa wanafukuzwa, analalamika kwanini wanafukuzwa.
Sasa hivi kamfuta kazi mkuu wa mkoa wa Shinyanga baada ya kumteua yeye mwenyewe mwezi uliopita. Huyu kamteua mwenyewe na sababu za kumfuta ziko wazi na jambo zuri alisema mapema kuwa suala la watumishi hewa litawafukuzisha kazi.
Ajabu sasa Julius Sunday Mtatiro anamtetea Mama Malecela kwa kusema kazi yake si ya kiutendaji na ya kwamba alitakiwa kutumia taarifa za kiintelejensia alizopewa rais na timu yake.
Kwa vyovyote vile baada ya kugudulika hao watumishi hewa 45, Mama Malecela alipewa taarifa, na kwa mujibu wa maneno yake mwenyewe rais, Anna Malecela hakuchukua hatua yoyote baada kujua kuna watumishi hewa tafauti na taarifa yake alokuwa nayo.
Kitendo hichi cha mkuu wa mkoa kusubiria hatua za rais badala ya yeye mwenyewe kuwachukulia hatua watu walio mdanganya ndio sababu za kutimuliwa kwake kazi.
Tangu Mbowe ale pesa za Lowassa, na tangu Lowassa ajiunge na CHADEMA, ni kama vile UKAWA yote sasa hivi imeacha lengo lake la kupambana na ufisadi sasa inatetea ufisadi na ubadhilifu.
Walipokuwa wanamsafisha Lowassa kwa ufisadi wake tulidhani wataishia hapo tu kwasababu ndio mgombea wao na ya kwamba hawakuwa namna, lakini kuendelea kwao kutetea ufisadi au kunyamazia ufisadi ndio kunatutisha, zaidi, ni kama vile yule muonja nyama ya mtu, anashindwa kuacha hata kama kwa kuendelea kwake kula nyama hiyo kutamlazimu kula na watoto wake pia.
Hivi karibuni wahusika na dili la STANBINK walipopelekwa mahakamani, vijana wote wa UKAWA hawakushangilia na kusema lolote, sababu wanajua katika hilo dili mzee wa madili kwa namna moja au nyingine naye yumo, sababu swahiba zake wakubwa na watafutaji wake wa fedha za kampeni ndio wahusika wakuu.
Akili yao ni kuwa upinzani ni kupinga, upinzani si kupinga tu, bali upinzani ni kuja na hoja zitakazo tibu matatizo yetu au kuboresha hali zetu. Hoja ya Mtatiro ni ya kupinga kijahili na si ya kututoa hapa na kutupeleka mbele zaidi.
Watanzania tunahitaji kwenda mbele, na kwa kauli rais yeyote atakaye jaribu kutukwamisha atashindwa na kulegea, Mtatiro kaka yangu jua fika umeshindwa na kulegea.
MGENI KARIBU, JUISI YA PILIPILI.
MWENYEJI:
Karibu mzee Chali, ukaribie nyumbani,
Uketi upige wali, upoze chango tumboni,
Kisha tujalie hali, za wenzetu Kinondoni.
Karibu wetu mgeni, juisi ya pilipili.
MGENI:
Loo! msinite Chali, jina langu Abuduni,
Nina njaa kwelikweli, ninawapa shukurani,
Hali zao afadhali, watia gia angani.
Ni mwenyeji si mgeni, asante kwa pilipili.
MWENYEJI:
Somo la uliberali, tulo nao Buguruni?
Sema wamelikubali, bila kinyongo rohoni,
Ama hawajakubali, wamelitupa jaani?
Karibu wetu mgeni, juisi ya pilipili.
MGENI:
Naona wamekubali, watazame visogoni,
Wakiliwa kwa ugali, wachomachoma kooni,
Ni michicha kwelikweli, yenye miba vikonyoni,

Ya kwao ulo kubali, yatupie barazani,
Tupate kuyajadili, na kuyapima mzani,
Tuyabebe yalo kweli, tuyatumie kundini,
Karibu wetu mgeni, juisi ya pilipili.
MGENI:
Sina nilo yakubali, hamuwezi kuamini,
Tumewazidi akili, maono na umakini,
Nyumbu wamelala chali, wamevimbiwa majani,

Kibopa wetu Munduli, naye ana hali gani?
Bado apiga msuli, wa kuwa bosi nchini?
Lile wazo kabadili, kuchunga ng'ombe porini?
Karibu wetu mgeni, juisi ya pilipili.
MGENI:
Tetesi kila mahali, aenda Ujerumani,
Ila hayana ukweli, yu mzima si utani,
Tatizo ni utapeli, uchungaji siuoni.

Hatutaki kadi mbili, ichome ya unyumbuni,
Kichwa na kiwiliwili, vyote virejee ndani,
Mazito yatukabili, hasa kule visiwani.
Karibu wetu mgeni, juisi ya pilipili.
MGENI:
Nimesharudi madhali, nina moja mkononi,
Ninaapa kwa Jalali, nisemayo ya moyoni,
Mengine tutajadili, kwa idhini ya Manani.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
0622845394 Morogoro.
Njano5
0622845394