Kashfa ya Richmond: The FACTS

Ni kupoteza muda wa wananchi, na hata mapesa zaidi ya wananchi walipa kodi, maana so far hatujaambiwa huu uchunguzi umeigharimu TAKURU, au serikali shillingi ngapi? Na zimetolewa na nani, katika kujaribu kuwasafisha wasiosafishika?

Katika taarifa yake, Mkurugenzi Hosea, anasema hakuna kiongozi wa serikali anayehusika na katika umiliki wa kampuni hiyo, huku akiwataja wamiliki wa kampuni hiyo kuwa ni Mohamed Gire na Mohamed Haque, wote wanatakiwa kuwa ni raia wa US, ingawa ukweli sasa unajulikana kuwa ni Wasomali, lakini hakuna uhakika kama ni raia wa US, au ni Wasomali wenye asili ya US, hivi kweli ni kiongozi gani mwenye akili timamu hapa Tanzania au Afrika kwa ujumla, leo mwaka 2006-2007, anayeweza kwenda kuwachukua Wasomali na kuwapa mradi mkubwa wa taifa lao kama huu wa Richmond? Hebu TAKURU, au kamati hiyo ya umeme watuonyeshe kwa ushahidi hawa Wasomali wako kwenye catalog gani duniani au huko US, katika mambo ya energy? Kigezo gani kilitumika kuiteua kampuni hiii ambayo haijadumu hata miaka kumi (10), kwenye hiii field ya energy, na kuziacha kampuni kubwa ambazo zimedumu kwa zaidi hata ya miaka 100 katika fani ya energy?

Leo tunayo orordha ya watoto wa wakubwa wa serikali yetu waliosomeshwa katika mpango huu wa Richmond, na wengine bado wako huko US wakifadhiliwa na huuu m-deal wa Richmond, na tunaweza kutaja kwa majina ikibidi sio siri, sasa mbona TAKURU, hawakusema hayo?

Naseeem Gire, ni Mtanzania according to Hosea, Okay! ana umaarufu gani katika fani ya Umeme, hapa au Marekani? Kwa nini TAKURU, haisemi kuwa ni kwanini aende kufungulia kampuni yake USA katika kipindi cha miezi sita na kupewa zabuni nono kama hii ya Richmond, tena nchini Tanzania? Na kwa nini Richmond, ilianzishwa only miaka miwili tu (2 Years), ninarudia only TWO YEARS, kabla ya uchaguzi wa Rais wa Tanzania, na hatimaye kupewa zabuni hii?


.........Tutaendelea..............!
 
Kha!


Leo tunayo orordha ya watoto wa wakubwa wa serikali yetu waliosomeshwa katika mpango huu wa Richmond, na wengine bado wako huko US wakifadhiliwa na huuu m-deal wa Richmond, na tunaweza kutaja kwa majina ikibidi sio siri, sasa mbona TAKURU, hawakusema hayo?


Am shocked! And almost bursting...

Naseeem Gire, ni Mtanzania according to Hosea, Okay! ana umaarufu gani katika fani ya Umeme, hapa au Marekani? Kwa nini TAKURU, haisemi kuwa ni kwanini aende kufungulia kampuni yake USA katika kipindi cha miezi sita na kupewa zabuni nono kama hii ya Richmond, tena nchini Tanzania? Na kwa nini Richmond, ilianzishwa only miaka miwili tu (2 Years), ninarudia only TWO YEARS, kabla ya uchaguzi wa Rais wa Tanzania, na hatimaye kupewa zabuni hii?


Gire ni geresha ES! Labda kwakuwa humjui kwa karibu... Huyu nafahamiana nae kwa karibu SANA na biashara yake kuwa ni Internet Cafes! Hainishangazi yeye kufahamiana na watu wa deal hili kwani kwa taarifa nilizopata ni kuwa hili deal alianza kuhangaikia zamani na almost alikuwa alikose lakini baadae alipoelewana na wakubwa na kuelewana terms basi mambo yakajipa na harakaharaka akaanza kuzisahau cafes zake za KIPATA (along Uhuru Rd), Mosque (City Centre near Jambo Inn), Richmond cafe near Riki Hill Hotel na nyingine ipo maeneo ya Kariakoo Mchikichini akafungua kijiofisi maeneo ya Posta kwa ajili ya deal lenyewe.

Maybe...
 
........Inaendelea.......!


Badala ya Takuru kututajia majina ya watu wasiojulikana hata huko ndani ya Marekani, taifa letu tulipaswa kupewa "Authoritative Sources au Procedures" ambazo ni kwa kufuata utaratibu wetu na wa kimataifa, kisheria. Pia Takuru na serikali, walitakiwa kututajia mabingwa wa kweli katika fani hiyo ya umeme duniani, kwa mfano leo ukiwataja Hewitt Parcard, kila mtu anaelewa kuwa unaongelea mabingwa wa dunia wa kompyuta, na ukiwataja Google inaeleweka na dunia nzima kuwa unaongelea mabingwa wa mawasiliano ya Mtandao duninani, kila bina-adamu atakuelewa, sasa kulikoni Ofisi ya Waziri mkuu na Richmond?


Takuru, inasema kuwa Richmond haikuwa na rushwa wala kasoro, sasa hizi barua tulizozisoma kwenye media zikitoka Ofisi ya Waziri Mkuu, kwenda kwa aliyekuwa Waziri wa Nishati, DR. Msabaha, zilikuwa ni za nini na mantiki gani? Na kwa nini serikali ikatae kata kata kuliruhusu bunge la wananchi, ambalo kisheria ndilo hasa linalohusika na ishu kama hizi kuichunguza hii deal la Richmond? Mbona bongo tuna miradi mingi sana inayofanana na Richmond, lakini haina kelele wala harufu za rushwa, WHy Richmond? Mbona Takuru, haisemi kifungu cha sheria kinachoipa Ofisi ya Waziri Mkuu, kuingilia suala hili la umeme na kuwaacha wataalamu na wanaoruhusiwa na sheria zetu? Badala yake Waziri Mkuu, akaruhusiwa kuingilia hiii deal?

.........Itaendelea............!
 
Mzee ES,

Nimevuta kigoda changu kuanza kukusikiliza kwa makini kwa vile najua huenda itakuchukua kama siku tatu hivi kumaliza hotuba yako.


Swala hili la Richmond sasa tunaanza kupata picha kamili baada ya ile blabla ya TAKURU. Kinachokera zaidi ni kuwa pesa yetu wamepewa wasomali, ili kusomesha watoto wa wakubwa USA, ambao watakuja kutuongoza huko mbeleni tena kwa mbwembwe.
 
Mzee Kichuguuu,

Heshima mbele mkuu, hiyo summary ndio mwanzo na mwisho wa yote kwa ufupi, ingawa bado tutaongeza lakini ubarikiwe mkuu!
 
Leo tunayo orordha ya watoto wa wakubwa wa serikali yetu waliosomeshwa katika mpango huu wa Richmond, na wengine bado wako huko US wakifadhiliwa na huuu m-deal wa Richmond, na tunaweza kutaja kwa majina ikibidi sio siri, sasa mbona TAKURU, hawakusema hayo?
.........Tutaendelea..............!

Mzee ES.
Please, wataje hawa!! Kweli tutaweza kumkoma nyani giledi hivi hivi tu? Nakumbuka enzi zile za BCS mtoto wa Mwandosya (Sekela?) alitajwa kuwa alilipiwa gharama za hoteli SA na Celtel, kama sijakosea, wakati Mwandosya akiwa waziri wa Mawasiliano.
 
Mh. ES,
Haya yote uliyosema ni kweli kabisa tatizo ni kuwa sehemu kubwa ya ''the so called wabunge ni KOKO'' Wakitupiwa tonge(mashangingi na posho) au kukemewa HUFYATA MIKIA na wanamwacha mwizi(serikali na washiriki wake) ajichukulie jinsi anavyotaka. Hawa si watu tunaowahitaji kuisimamia serikali kwa ni sawa na mbwa koko. Tunahitaji watu wanye uwezo wa kwenda mguu kwa mguu na hawa majambazi.
 
......Inaendelea.......!


Takuru na Hosea, kwanini ofisi ya Waziri Mkuu, ambaye suala la Umeme haliko chini yake auingilie kati na kuamua mbinu za kuwapa tenda Richmond? Kwa maneno yake Hosea, anasema kwamba kulikuwa na mapungufu yaliyosababishwa na dharura ya umeme na kusababisha kutofanyika uchunguzi makini wa kutambua uwezo wa kiutendaji wa Richmond, NONESENSE, alichopaswa kusema Hosea ni kwamba, viongozi wote waliohusika na mchakato mzima wa kuileta Richmond, hawakuwa na uwezo kiutaalamu, au uwezo wao uliwekwa pembeni na rushwa, na matokeo yake ni viongozi hao wetu wa taifa kutusababishia hasara ya mabilioni ya shillingi zetu za walipa kodi bila ya sababu, au kwa sababu zao za kibinafsi, kwa hiyo hawafai kuendelea na uongozi wa taifa, au wananchi kwa ujumla, manake kwa maneno pia ya Hosea, kosa kubwa lililofanyika lilikuwa ni kwa viongozi hao kutofanya uchunguzi wa kina kuhusu Competence ya Richmond, swali ni je ni kwa nini wakati sheria za nchi yetu zinawataka wafanye hivyo?

Kwa hiyo kwa maneno mengine, hao viongozi kama hawezi kupelekwa kwenye sheria, basi waatakiwe na Takuru yenyewe wajiuzulu kwa manufaa ya taifa, kitu ambacho enzi za Mwalimu kilikuwa ni cha kawaida kwa kiongozi wa serikali kuondoka kwa manufaa ya taifa, Mwinyi akiwa waziri wa Mambo ya Ndani, wa awamu ya kwanza ilibidi ajiuzulu baada ya mauaji ya wachawi Shinyanga, je ni Mwinyi waziri ndiye aliyewaua wananchi wanaoshukiwa kuwa wachawi?, hapana, ilikuwa ni wizara yake tu ndiyo iliyohusika, sasa hapa Hosea anasema kwamba viongozi waliotuletea Richmond walichaguliwa na waziri Mkuu mwenyewe, sasa hebu tuangalie the otherside of the coin, kama Mzee Fikiraduni, je Richmond wangefanya kazi yao inavyotakiwa bila ya matatizo credit angepewa nani? Si huyo waziri mkuu aliyejiiingiza bila hata kuruhusiwa na sheria, sasa baada ya ku-fail kwa nini asiwe responsible? Angalau hata kutuomba radhi wananchi, kwamba deal imekwenda vibaya?

Takuru, haipaswi kuaminiwa tena na wananchi pamoja na sheria mpya kupitishwa ya kuzuia rushwa, maana mpaka leo toka ianzishwe hakuna positive record ya kuonyesha kuwa as a nation we are better off baada ya kuwa na Takuru, as opposed na tulipokuwa hatunayo! Takuru imekuwa good kwa kuwakamata dagaaa tu, lakini sio samaki wakubwa? Je ina maana Tanzania haina wala rushwa wa high places ambao wanajulikana hata mitaani na wananchi kuwa ni wala rushwa? Sasa Hosea nani atawakamata ikiwa na nyinyi Takuru mmegeuka kuwa ni tool yao ya kufichia madhambi kwa maneno mengi ambayo ni hewa tupu, iweje uchunguzi mzima ambao ulianzwa baada ya wananchi kulalamika na kumpelekea hata rais kuwatengua uwaziri waliohusika, na hata wengine kuwakaripia kama watoto wadogo sasa leo Takuru inawezaje kusema kuwa kuna makosa yalifanyika lakini haya-amount to illegal activities ya viongozi waliohusika kuwa criminalized, kama sio usanii ni nini?

Kwako Ndugu Hosea, na wabunge wetu, honestly kazi yako ya kila siku ni nini hasa inayokufanya upate mshahara kama sisi wengine wanachi wa kawaida? Je serikali yetu haina haina au inao utaratibu wa kufuatilia kwa record kuona kama hiki kitengo kina-function au kiondolewe kwa kutokuwa nafaid yoyote kwa taifa letu?



........Itaendelea............!
 
Mzee Es,
Mzee wangu kwa nini usipewe Ubunge?..ama chukua sheria mzee wangu maanake hoja zako nzito sanaaa, hazibebeki!..
 
Mzee Bob,

Heshima mbele mkuu, mambo hapa hapa hadharani kwakweli hawa wabunge wetu sielewi cha kusema, na viongozi wetu ndio kabisaa maana sasa ni wizi wa mchana mchana, I mean ile tabia yao ya zamani ya kuiba usiku waliacha sasa ni mchana kweupe tunawaona!
 
Opposition MPs refuse to let go of Richmond saga

THISDAY REPORTER
Dodoma

THE controversial Richmond power deal saga erupted once more in the National Assembly yesterday when a prominent opposition legislator, Dr Wilbroad Slaa (CHADEMA � Karatu), called for the findings of an official investigation into the deal to be disclosed in the House.

Dr Slaa pinned the Minister of State in the President’s Office (Good Governance), Philip Marmo, noting that constitutionally parliament has all powers to demand that reports of such investigations mounted by the Prevention of Corruption Bureau (PCB) should be made public.

He was reacting to Marmo’s earlier statement in parliament in which he rejected calls for the said PCB report to be submitted in the House on grounds that the bureau had been dealing with a �criminal matter� that should not be discussed in parliament.

In a formal announcement after completing the probe into the emergency power generation contract between the government and US-based Richmond Development Company, PCB said it had found the deal to be ’’clean of corruption.’’

Speaking at a news conference, PCB Director General Edward Hosea asserted that the process of awarding the tender to Richmond had been ’’fairly transparent and done in a competitive manner.’’

At the same time, however, Hosea also acknowledged ’’some shortfalls’’ in the $30m (38bn/-) deal, which he did not specify.

Bringing up the subject again in parliament yesterday, Dr Slaa said legislators should be allowed to scrutinize PCB’s report on the Richmond affair and gain more information on the stated ’’shortfalls’’ in the deal.

He also demanded an official explanation regarding steps taken against government officials found to have been responsible for any shortcomings in the deal.

’’When responding to my written contribution, the minister (Marmo) described the PCB inquiry on the Richmond deal as a criminal investigation that cannot be brought for parliamentary debate. However, there is an administrative element to it, and it is likely that there was laxity in the process, in which case parliament does have the right to know,’’ Dr Slaa said.

He argued that since PCB itself had seen fit to give a news conference on the contents of the report, there was no call to keep it away from parliament.

In an apparent rejoinder to the legislator’s comments, Marmo reiterated that the PCB report was only for purposes of criminal prosecution or otherwise.

’’If Dr Slaa believes there was laxity in the process regarding the Richmond deal, he may use his own ways of presenting it to parliament, but without using the PCB report,’’ the minister insisted.

The opposition CHADEMA party has already issued a strong-worded criticism of what it described as PCB�s ’’poor handling’’ of the Richmond power deal investigation, questioning why a task force appointed by Prime Minister Edward Lowassa had picked Richmond as the eventual winner of the power generation contract despite the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO)’s stated rejection of the US-based company. ??CHADEMA said PCB’s decision to rule out corruption in the whole deal not only discredited the anti-corruption watchdog, but also frustrated the national campaign against graft. ??The opposition party called on PCB to make a copy of the full investigative report over the Richmond deal available for public perusal. ?
 
Na ya City Water Pia wa uilizie , na hasara tulizopata watuambie na nani atabeba huo mzigo, kama ni waliofanya huo uamuzi au wananchi
 
Kelele za mpangaji hazimsumbui mwenye nyumba. Wanatufanyia usanii tu. Mbona kwenye posho za wabunge hawasemi kitu?? Au kwa vile na wao wanafaidi?
 
Wanajaribu kutafuta fedha za kuendeshea vyama vyao ( Wapinzani/Ushindani), ama sivyo next election watakuwepo Chichiemu tu, maana wao ndio wanavyanzo vyote vya mapato, one ni Ruzuku kubwa, mirahaba ya madini na maliasili, kandarsasi za barabara, Ma RC na Ma-DC, to Permanent Secretaries etc etc
 
Sakata la umeme hewa wa Kampuni ya Richmond limeibuliwa tena kwenye Bunge letu tukufu na Mh. Wilbroad Slaa lakini linaelekea kuzimwa kiaina fulani na Waziri muhusika Mheshimiwa Philip Marmo.
Niwaulize wenzangu hivi kweli hatuhitaji majibu sahihi katika hili kama wananchi wa kawaida? Au hayo yaliyodaiwa na yanayoendelea kudaiwa kuwa ni moja ya kampuni za Mh. mkubwa sana EL ndio zinafichwa kiaina yake??
Mimi binafsi nadhani kuna haja ya waheshimiwa wabunge ambao ndio wawakilishi wetu kuelezwa ukweli wa jambo hilo.
Jamani nisaidieni!!
 
Shangilieni Stars ila msisahau Buzwagi, BoT na Richmond

Mwandishi Wetu
Kutoka Gazeti la Tanzania Daima

LEO timu yetu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, inajitupa uwanjani kumenyana na timu ngumu ya soka ya taifa ya Msumbiji kuwania tiketi ya kwenda Ghana, kushiriki fainali za Kombe la Mataifa Afrika, mwakani.

Kwa mtu anayejua maana ya uzalendo, hatakuwa na pingamizi kuwashajihisha Watanzania kuishangilia timu yao ya taifa.

Kwa vile Watanzania huwa hawana uhaba wa uzalendo japo kwa wengine ni juu juu, hili halina utata kuwa, wataishangilia timu yao, tena kwa nia safi, na wengine kwa nia chafu. Kuna msemo unaosema kwenye msafara wa mamba na kenge wamo.

Kadhalika, hata kwenye mashamsham na shamrashamra za kuishangilia Stars, ambao ndio msafara hasa wa mamba, kuna mikenge tena mingi itakayotaka kuutumia mwanya huu kuficha uchafu na aibu zao.

Hapa ndipo masuala mazito na muhimu kama kuendelea kuwashikia kidedea mafisadi wetu, yanaweza kusahaulika hata kupuuziwa. Hapa mikenge itafanya kila liwezekanalo ili kushangilia Stars kunoge, hata kuwa dili ili angalau yapumue kwa muda, hata kuwasahaulisha kabisa wananchi ambao si haba wanaonekana kuanza kutoka kwenye ukondoo na blanketi la kulishwa sifa uchwara.

Kwa siku nne zilizopita, hamasa ya Watanzania iko juu mno, idadi kubwa ya magari, hata ya daladala yanapeperusha bendera ya taifa. Kwa kifupi kila kona unayopita mazungumzo ni Stars, Stars, Stars.

Kwa wanaojua kuwa kwetu michezo haina umuhimu sana kwa wanasiasa, kuna kipindi hushangaa hata kuiona Stars au hata wakimbiaji wakikaribishwa bungeni hata Ikulu.

Mara nyingi hili linapotokea, ujue kuna lengo la kutaka kuipumbaza hadhira kama ilivyotokea siku za nyuma, baada ya Stars kuishinda Burkina Faso, ambapo kashfa ya Benki Kuu (BoT) ilikuwa imepamba moto.

Kutokana na ushindi huo, wanamichezo waliitwa bungeni, kanuni ikavunjwa kuwaruhusu wachezaji na walimu wao kuingia na kushangiliwa kiasi cha kupoteza kabisa hoja ya BoT iliyoshikiwa kidedea na Mbunge wa Karatu, Dk. Willibroad Slaa (CHADEMA).

Wakati hilo likiendelea, ulitokea msiba wa mbunge Amina Chifupa. Nao kwa namna yake, uliihamisha hadhira ya kashfa hiyo kwenda kwenye majonzi, huku mafisidi angalau wakipata ahueni kwa kutomeza dawa za shinikizo la moyo.

Hata ule moto wa kumtaka Gavana wa BoT, Daudi Balali kuwajibika, bahati mbaya ulizimika ghafla, huku naye akitukoga na kutusuta kuwa yuko ‘comfortable’, na ari yake ya kazi iko juu kwa madai kuwa tuhuma dhidi yake ni uzushi na kamwe hawezi kuachia ngazi kwa uzushi wa kwenye mtandao.

Tukirejea kwenye Taifa Stars, tuliwahi kuhoji kwanini timu hii inakuwa ya maana wakati wa matukio ya kashfa au hata inapopata ushindi baada ya kuhangaishwa kimalipo? Nani asiyejua kuwa Stars mara nyingi inachangiwa na wafanyabiashara wengi, lakini baadhi yao wachafu ambao kimsingi wanapenda kuitumia ama kutangazia biashara zao au kuwa karibu na mawaziri ili wafanikishe dili zao?

Tujiulize huku tukidurusu. Je, hii pesa inayoteketea kwa kuwasamehe kodi wafanyabiashara, kwanini isipewe Taifa Stars kama kweli tunaijali na kuipenda? Maana hawa wanaoichangia ili kuitumia na kupatia umaarufu, utakuta wengi wao ni wale wale wakwepa kodi, wafanya magendo, walanguzi hata wanaosamehewa kodi.

Kwanini tuwe na pesa ya kutumia kwenye sherehe na makongamano ya kipuuzi tukose ya kuiwezesha Taifa Stars? Kwa watu makini, uwekezaji kwenye michezo unalipa kuliko mambo mengine ya kisiasa. Kama vyama vinapewa ruzuku kujiendesha, kwanini Taifa Stars nayo isipewe? Maana ni kwa ajili ya taifa sawa na asasi nyingine.

Kama kuna mtoto yatima Tanzania, basi na Taifa Stars nayo ni miongoni mwao.

Taifa Stars wamepata nafasi hii ya kuungwa mkono na wananchi, piga ua wawape wananchi raha basi.

Lakini, wakati wananchi wakipewa raha, wasilewe kiasi cha kusahau wale manyang’au wanaowanyima raha kwa kuwaibia na kuwatumia kama mataahira.

Stars wapeni raha wananchi, lakini raha hiyo isiwafanye wasahau hoja nyeti kama ile iliyotolewa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, kuhusu kusainiwa mkataba wa Buzwagi.

Watanzania shangilieni Stars, lakini msilewe kiasi cha kusahau ununuzi wa rada tuliyoambiwa tutadai chenji yetu. Ununuzi wa ndege ya rais ambayo licha ya kununuliwa kwa zaidi ya sh bilioni 40, haifanyi kazi ipasavyo huku kukiwa na kashfa ya BoT, IPTL, Richmond na mauzauza mengine yenye utata.

Shangilieni Stars, lakini msisahahu usiri uliopo kwenye mikataba mingi ambayo wabunge wetu wameshindwa kuhoji, huku mkikumbuka suala la muafaka wa Zanzibar, ambao hadi sasa hakuna dalili za kufikiwa.

Stars wapeni raha Watanzania, lakini raha hiyo isiwafanye msahau umasikini unaozidi kila kukicha huku wananchi wakianikizwa kwa kauli ya ‘maisha bora kwa kila Mtanzania.’

Juzi juzi nchini Irak, imegundulika kuwa mpira unaweza kuwaunganisha watu hata wenye tofauti kubwa, ambazo zimewashinda wababe wa vita na wanadiplomasia. Nasi kwa Tanzania, tuitumie fursa hii kushikamana dhidi ya ufisadi ambao unaonekana kumshinda rais na serikali yake.

Ni michezo hii ilizaa vyama vya siasa kama TANU na ASP. Kadhalika ni michezo hii inaweza kuleta vuguvugu la kisiasa dhidi ya siasa babaishi na za kujuana na kulindana ambazo zimekuwa maafa kwa nchi yetu.

Wakati tukishangilia Taifa Stars, tujiweke sawa kuwazomea mafisadi tunaowajua, ambao wanajifanya hawasikii wala hawaoni kuwa tunajua na tunataka wawajibike bila mjadala.

Tunafahamu michezo ina mashabiki wengi kuliko siasa. Hivyo tutumie fursa hii kuzidi kuwahimiza wananchi wasilewe ushindi au fursa ya kufika tulipofika bali waamke na kudai haki ya kuwa na nchi isiyoendeshwa kimizengwe kutumiana na kudanganyana.

Tutumie fursa hii kukumbushia kurejeshwa kwa nyumba zetu, kutaja mali za maofisa wa serikali, kusuka upya na kupunguza Baraza la Mawaziri ambalo linaonekana wazi kupwaya na kukosa maana.

Wakati tukijiandalia tukio hili, tuwaambie tena wale wote wenye kashfa kuachia ngazi ili tupate watu wenye akili na adili, watuongoze badala ya kutuibia na kutufanya majuha.

Mungu ibariki Taifa Stars, Mungu ibariki Tanzania.

0713 260 071
 
Michezo Ni Siasa Pia , Na Watanzania Wengi Wanafikiri Kwamba Taifa Stars Ikishinda 1 Tu Wanapita Wakati Ni Uwongo Wanatakiwa Washinde Zaidi Ya Magori 4 Na Waombee Senegal Ifungwe Huko Kwao Na Hii Ni Ngumu Sana Kwa Sababu Kikosi Kinachocheza Na Senegal Leo Ni Kipya Kimeundwa Baada Ya Shirikisho La Mpira La Bukina Kuvunja Na Kuundwa Upya Kwahiyo Leo Ngoma Iko Huku

Inawezekana Watanzania Wengi Wamesahau Haya
 
SHY Nadhani TAnzania inahitaji sare tu kupita. Haihitaji magoli manne kama unavyodhani
 
Back
Top Bottom