Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,354
- 1,943
Haya yote yakiendelea, hali ya umeme inazidi kuwa mbaya. Soma hii habari ya Nipashe:
Mgao wa umeme hadi saa 4 usiku
2006-11-19 09:12:07
Na Joseph Mwendapole
Shirika la Umeme nchini (TANESCO), limetangaza hali mbaya ya umeme nchini na kwamba kuanzia kesho wateja watakuwa wanakatiwa umeme kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 4:00 usiku.
Meneja Uhusiano wa Shirika hilo, Bw. Daniel Mshana, alisema Shirika limelazimika kufanya hivyo kutokana na hali ya uzalishaji umeme kuzidi kushuka.
"Tofauti na siku zilizopita ambapo shirika lilikuwa na uwezo kidogo wa kukidhi mahitaji hayo ya wateja yanapoongezeka usiku, hivi sasa uwezo huo haupo tena kutokana na uzalishaji kuzidi kushuka, '' alisema Bw. Mshana.
Alisema ratiba hiyo mpya itawahusu wateja wote wa majumbani na viwandani na kwamba wateja wachache nyeti, zikiwemo hospitali za mikoa, viwanja vikubwa vya ndege, vituo vya jeshi na Ikulu, havitakuwa kwenye mgao huo.
Alisema Shirika hilo linashindwa kukidhi mahitaji ya matumizi ya umeme kutokana na maji ya kuzalisha umeme kwenye mabwawa makuu ya vituo vya nguvu za maji kupungua kwa kiasi kikubwa.
Alisema TANESCO imefikia hatua hiyo kwa sababu mitambo mingi ya dharura ya kukodi, haijaanza kuzalisha umeme kama ilivyotarajiwa.
Bw. Mshana alisema wateja wote walioko kwenye mikoa iliyounganishwa na Gridi ya Taifa imewekwa kwenye makundi matatu na kwamba kila kundi litakuwa likipata umeme baada ya siku tatu.
"Makundi haya yatakatiwa umeme kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 4:00 usiku, mbali na mgao unaofanyika mchana.
Kwa hiyo umeme utakatwa kwa kila kundi, kila baada ya siku tatu," alisema.
Alisema kwa kuwa mahitaji ya wateja wa umeme yamekuwa yakiongezeka hususan wakati wa usiku kati ya saa 12 na saa nne usiku, imekuwa vigumu kutosheleza mahitaji ya wakati huu.
Alisema mitambo ya kwanza ya dharura ya kukodisha ni ile iliyowekwa na kampuni ya Aggreko ya Uarabuni ambayo tayari inatoa megawat 40 za umeme, unaoingia kwenye mfumo wa Gridi ya Taifa.
Bw. Mshana alisema mitambo ya pili ya kukodi ya kampuni ya Richmond Development ya Marekani ambayo ina uwezo wa kuzalisha Megawat 100 za umeme haijawasili yote isipokuwa yenye uwezo wa kuzalisha megawat 22 tu.
Hata hivyo alisema hiyo iliyowasili haijaanza kuzalisha umeme na huenda ikaanza kabla ya mwezi Desemba mwaka huu.
Alisema mitambo iliyobaki ya megawat 80 itafungwa na kuanza kazi kabla ya mwisho wa mwezi wa kwanza mwakani.
Kwa mujibu wa Bw. Mshana, mitambio mingine italetwa na kampuni ya Alstom Power Rentals ya Marekani itakayokuwa na uwezo wa kuzalisha Megawat 40.
Alisema mitambo hiyo inatarajiwa kufungwa mkoani Mwanza na kuanza kazi kabla ya mwisho wa mwaka huu na kwamba mitambo ya awali ya megawat 20 inatarajiwa kuanza uzalishaji kabla ya Desemba mwaka huu.
Bw. Mshana alisema mitambo ya nne itakayojengwa na kampuni ya Wartsila ya Finland na baadae kumilikiwa na TANESCO, itakuwa na uwezo wa kuzalisha megawat 100 na itaanza kazi kabla ya mwezi Agosti mwakani.
SOURCE: Nipashe